Mtanzania atengeneza game za kutangaza Utalii

Milard Ayo
Published: Feb 09, 2023 10:47:56 EAT   |  Travel

Leo nakukutanisha na na Elias Patrick, Mtaalamu wa masuala ya Biashara na Teknolojia kutoka Tanzania ambaye katika juhudi za kuunga mkono Serikali katika kutangaza Utalii na vivutio vya Tanzania, Elias ametengeneza Mobile games tano ambazo zinapatikana Google Playstore ndani ya nchi 176 duniani. Games hizi zimepewa majina ya baadhi ya vivutio vya kitalii hapa Nchini […]

Leo nakukutanisha na na Elias Patrick, Mtaalamu wa masuala ya Biashara na Teknolojia kutoka Tanzania ambaye katika juhudi za kuunga mkono Serikali katika kutangaza Utalii na vivutio vya Tanzania, Elias ametengeneza Mobile games tano ambazo zinapatikana Google Playstore ndani ya nchi 176 duniani.

Games hizi zimepewa majina ya baadhi ya vivutio vya kitalii hapa Nchini ikiwemo Tanzanite Crush, Kilimanjaro Block Puzzle , Zanzibar Candy Blast , Serengeti Block Puzzle na Maasai: The Hunter .

Zaidi ya Watumiaji elfu 10 wamekwisha kupakua games hizi na Elias amesema ataendelea kutengeneza na kuboresha games hizi kwa vivutio vingine kwa kushirikiana na wadau watakaojitokeza ikiwemo serikali kwani zaidi ya asilimia 70 ya watumiaji wa simu Janja duniani wanacheza games.

Games hizi zinachangamsha ubungo na kupunguza stress kwani zimetengenezwa kukidhi standard za kimataifa ili zifikie watumiaji duniani kote, Elias amenukuliwa akisema “Kwa tushirikiane kutangaza Utalii wetu kimataifa ili kukuza pato la taifa huku jamii zetu zikinufaika na watalii wanaotutembelea”