Mrembo aua kikatili ili ajizushie kifo, amchoma visu mara 50 mwenzie waliekutana Instagram

Milard Ayo
Published: Feb 03, 2023 18:46:10 EAT   |  Technology

Mwanamke mmoja ajulikanae kwa jina la Shahraban K kutokea nchini Ujerumani ameshtakiwa kwa kosa la kumuua mtu aliyempata kupitia mtandao wa Instagram ili kuzusha kifo chake mwenyewe. Kwa mujibu wa ripoti ya Polisi wa nchini Ujerumani mshukiwa alidaiwa kumchoma  kisu Mwanamitindo  Khadija zaidi ya mara 50, na kumharibu kabisa sura yake baada ya kumshawishi kukutana […]

Mwanamke mmoja ajulikanae kwa jina la Shahraban K kutokea nchini Ujerumani ameshtakiwa kwa kosa la kumuua mtu aliyempata kupitia mtandao wa Instagram ili kuzusha kifo chake mwenyewe.

Kwa mujibu wa ripoti ya Polisi wa nchini Ujerumani mshukiwa alidaiwa kumchoma  kisu Mwanamitindo  Khadija zaidi ya mara 50, na kumharibu kabisa sura yake baada ya kumshawishi kukutana nae katika mji uliopo Bavaria uitwao Ingolstadt mnamo Agosti mwaka jana.

Mshukiwa huyo aliyetambulika kwa jina la Shahraban K mwanamke wa Kijerumani mwenye asili ya Iraq mwenye umri wa miaka 23 ambaye yeye pia ni mmiliki wa blog, inadaiwa alijaribu kufanya haya ili ionekane kama yeye ndiye aliyeuawa.

Kwa stori kamili unaweza ukabonyeza play kusikiliza makala hii iliyoandaliwa na Ayo TV & Millardayo.com