“Mradi wa Morocco Square ukamilike June 30, 2022” Mabula

Milard Ayo
Published: Dec 13, 2021 12:05:11 EAT   |  News

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Angeline Mabula amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mkandarasi Kampuni ya Ujenzi ya Estim Construction kuhakikisha mradi wa ujenzi wa Morocco Square unakamilika kufikia Juni 30, 2022.

Kauli hiyo ya Dkt Mabula inafuatia uamuzi wa serikali kuiruhusu NHC kukopa fedha kwa ajili ya kumaliza mradi huo uliokuwa umesimama kwa takriban miaka mitatu sasa.

Kwa mujibu wa Msimamizi wa mradi huo kutoka shirika holi, Samuel Metili, mradi wa Morocco Square unaogharimu shilingi bilioni 137.5 ulisimama tangu mwaka 2017 kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya kifedha na mabadiliko ya baadhi ya maboresho kwenye maeneo ya majengo hayo.

Akizungumzia mradi wa Mji wa Kawe, Dkt Mabula alilitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuharakisha mazungumzo ya uwekezaji na Mwekezaji Mwenza Kampuni ya Al-Gurey-Dubai kuhusiana na mradi huo na kusisitiza kuwa, ni vizuri NHC ikawa mipango thabiti ya uendelezaji mji huo.

“Kuhusu mradi wa Kawe ni vizuri kujua future plan ya eneo na ni vizuri kila eneo la Shirika la Nyumba likafanyiwa maandalizi ya kitu kinachotaka kufanyika, yale maeneo ambayo ni ‘prime’ muyaainishe na kuyaendeleza maana hata NHC inaweza kunyang’anywa.” alisema Dkt Mabula.