Kampuni za Uber na Tigo watangaza ubia wa kampuni ya kuwazawadia wateja wao

Milard Ayo
Published: May 31, 2023 10:57:40 EAT   |  General

Leo Kampuni za Uber na Tigo zimetangaza ubia wa Mwaka mmoja wa Mfululizo wa kampeni za kuwazawadia madereva na wasafiri wanaotumia app ya Uber na Tigo Pesa. Kuanzia sasa, Madereva wanaotumia mfumo wa Uber wanaweza kujisajili kama wakala wa lipa kwa simu ya Tigo Pesa ambayo itawawezesha kupokea nauli kutoka kwa wasafiri wakaopenda kulipa nauli […]

Leo Kampuni za Uber na Tigo zimetangaza ubia wa Mwaka mmoja wa Mfululizo wa kampeni za kuwazawadia madereva na wasafiri wanaotumia app ya Uber na Tigo Pesa.

Kuanzia sasa, Madereva wanaotumia mfumo wa Uber wanaweza kujisajili kama wakala wa lipa kwa simu ya Tigo Pesa ambayo itawawezesha kupokea nauli kutoka kwa wasafiri wakaopenda kulipa nauli zao kupitia mitandao ya simu.

Madereva wanaotumia mfumo wa Uber wataweza kupata pesa zao kutoka kwenye akaunti za lipa kwa ismu bila makato yoyote kutoka kwenye mawakala wa Tigo Pesa kwa kiasi chochote chini ya Tshs, 500,000 kwa siku.

Abiria watakaotumia huduma ya Lipa kwa simu ya Tigo Pesa watarudishiwa 10% ya Nauli watakayolipa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa, sambamba na kampeni hi Uber itaendelea kufanya kampeni zingine kupitia app yao.

Madereva watakaotumia huduma ya lipa kwa simu kwa malipa yao ya nauli watarudishiwa 20% ya ada ya malipa kwa kila muamala unaofanywa kupitia lipa kwa simu.

Meneja wa Uber Afrika Mashabiki, Bw Imaran Manji anasema ‘Tuna furaha kubwa kuingia Ubia na kmapuni ya Tigo katika kufanikisha kampeni hii itakayowasaidia madereva kuongeza kipato na pia abiria kuokoa Pesa kila wanapotumia mfumo wa Uber.Ubia huu ni muhimu na una tija kubwa kwasababu inawafanyia wepesi abiria na maderve kufanya miamala wanapotumia mtandao wa Uber, Ikiwa ni pamoja na wateja ambao hawana akaunti za benki na wamepungukiwa na Pesa Taslimu’

Mkurungezi Mtendaji wa Tigo Pesa, Bi Angelica Pesha amesema..’ Ubia huu tunaoingia na kampuni ya Uber unaonesha waziwazi nia ya Tigo Pesa kufanikisha malengo yajke ya kusamba huduma za kifedha katika jamii ya Watanzania.Sasa Madereva wa Uber watapata huduma ya malipo ambayo inahakikisha abiria wao njia salama na rahisi ya kulipa nauli wanaposafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine’

‘Sambamba na hii ubia huu ni ushahidi kwamba huduma ya lipa kwa simu ni huduma yenye ufanisi mkubwa na tunategemea kwamba huduma hii itasaidia biashara ndogondogo kuendelea kukua’

‘Sekta ya usafiri wa teksi za mitandaoni imeleta mageuzi makubwa katika namna ambayo tunasafiri katika miji yetu na tangu walipofungua milango yao jijini Dar es Salaam mwaka 2016, Uber amekuwa mshirika mkubwa wa jiji hili kupitia huduma za Usafir, kuchangia katika Uchumi kwa kutoa fursa za kiuchumi sambamba na kuchangia katika mapato ya Serikali’- 

.
.
.
.
.
.