INDIA: Sheria mpya, kutobadili imani ya kidini yazua gumzo.

Milard Ayo
Published: Mar 24, 2023 09:12:33 EAT   |  General

Makundi ya kihindu pamoja na chama tawala cha Hindu nationalist Bharatiya Janata, wanadai kwamba wamishonari wa kikristo wanabadili Imani za watu kote nchini kwa kutumia nguvu au ushawishi usiofaa. Katika miaka ya karibuni, wamedai kwamba waislamu wamekuwa wakivuta watu kwenye dini yao kupitia njia haramu na hadi sasa majimbo 12 kati ya 28 yaliopo nchini […]

Makundi ya kihindu pamoja na chama tawala cha Hindu nationalist Bharatiya Janata, wanadai kwamba wamishonari wa kikristo wanabadili Imani za watu kote nchini kwa kutumia nguvu au ushawishi usiofaa.

Katika miaka ya karibuni, wamedai kwamba waislamu wamekuwa wakivuta watu kwenye dini yao kupitia njia haramu na hadi sasa majimbo 12 kati ya 28 yaliopo nchini humo yamepitisha sheria hiyo, wakati baadhi ya yaliobaki yakitadhmini kufuata nyayo .

Hayo yamejiri wakati tume ya Marekani ya Uhuru wa kimataifa wa dini, USCRIF, ikieleza wasiwasi wake kutokana na sheria hiyo, na kuomba ibatilishwe.

USCRIF kupitia ripoti imesema kwamba sheria hiyo mpya inavuruga uhuru wa kidini nchini India, ambao tayari ulikuwa hatarini, na kwamba hatua hiyo ni kinyume na sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Viongozi ya makundi ya walio wachache nchini India wanasema kwamba sheria mpya ya kutobadili Imani iliyopitishwa katika baadhi ya majimbo inalenga kuadhibu na kukandamiza makundi ya wakristo na waislamu nchini humo.

Chanzo:VOA