Gumzo;Mwanaume akatisha uhusiano na mpenzi wake kisa alimwomba pesa za kusuka

Milard Ayo
Published: Jul 28, 2023 10:43:01 EAT   |  Technology

Kijana mmoja ameingia kwenye mtandao  wa Twitter kueleza hali iliyompelekea kukatisha uhusiano wake na mpenzi wake kisa kuomba pesa ya akwenda kusuka.   Kijana huyo anayejulikana kwa jina la @ArtificialSteez kwenye Twitter,  alisema  kuwa gari lake lilipata ajali, hivyo alilazimika kulipia gari jingine kwa muda, huku akijaribu kurekebisha lililoharibika na alisema kuwa kampuni ya bima […]

Kijana mmoja ameingia kwenye mtandao  wa Twitter kueleza hali iliyompelekea kukatisha uhusiano wake na mpenzi wake kisa kuomba pesa ya akwenda kusuka.


Kijana huyo anayejulikana kwa jina la @ArtificialSteez kwenye Twitter,  alisema  kuwa gari lake lilipata ajali, hivyo alilazimika kulipia gari jingine kwa muda, huku akijaribu kurekebisha lililoharibika na alisema kuwa kampuni ya bima isingewezakugharamia matengenezo kwa sababu si yeye aliyekuwa akiendesha gari wakati ajali hiyo ilipotokea.


Hata hivyo, mpenzi wake alimwomba pesa kwa ajili ya nywele zake siku iliyofuata, lakini hakuweza kumpatia, kwa hiyo alikasirika na ulipotokea ugomvi aliamua kuachana  nae kwa sababu ya kile alicho dai kuwa mwanamke huyo hajali kwani aliwahi kumlalamikia kuwa alikuwa na msongo wa mawazo kutokana na kutafuta pesa za kurekebisha gari.


Aliandika, “Gari langu lilipata ajali, na ilinibidi kulipia gari la muda kisha nikamwambia nina stress na pesa za kurekebisha gari kwani bima haitanilipa kwa sababu rafiki yangu alikuwa akiiendesha. aliniomba pesa za nywele siku moja baadaye na nilikasirika sikuweza kwasababu sikuweza kumpa  ”