Gari ya magazeti yaua watu 9

Milard Ayo
Published: Dec 13, 2021 13:00:12 EAT   |  News

Watu tisa wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya hiace ya kubeba magazeti iliyokuwa ikitoka jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mbeya.

Watu tisa wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya hiace ya kubeba magazeti iliyokuwa ikitoka jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbiamesema ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Desemba 13, 2021 alfajiri katika kijiji cha Mahenge wilayani Kilolo mkoani Iringa.

Kamanda Bukumbi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo gari hilo lilimshinda dereva kwenye kona na kugonga mti uliokuwa pembezoni mwa barabara na kupinduka na kusababisha vifo vya watu 9.

“Watu 9 wamepoteza maisha katika ajali hiyo ambapo wanawake 4 wanaume 5 na majeruhi watatu wanaendelea kupewa matibabu katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa” Kamanda Bukumbi