Elon kuileta Starlink Tanzania?

Milard Ayo
Published: Feb 07, 2023 18:42:03 EAT   |  Technology

Boss wa SpaceX , Tesla na Twitter , Elon Musk (49) ambaye ni miongoni mwa Matajiri zaidi Duniani ameonesha nia ya kuuleta mradi wa Starlink nchini Tanzania ambapo amesema kinachosubiriwa kwa sasa ni Serikali ya Tanzania kutoa kibali . Kampuni ya SpaceX ya Elon imeendelea kuzindua satelaiti katika Nchi mbalimbali kama sehemu ya mradi wa […]

Boss wa SpaceX , Tesla na Twitter , Elon Musk (49) ambaye ni miongoni mwa Matajiri zaidi Duniani ameonesha nia ya kuuleta mradi wa Starlink nchini Tanzania ambapo amesema kinachosubiriwa kwa sasa ni Serikali ya Tanzania kutoa kibali .

Kampuni ya SpaceX ya Elon imeendelea kuzindua satelaiti katika Nchi mbalimbali kama sehemu ya mradi wa Starlink ambao unalenga kutoa huduma ya internet ya kasi ya juu zaidi kutoka anga za juu hadi maeneo ya mbali Duniani na huwasaidia hadi Watu wanaoishi maeneo ya mbali ambayo hayawezu kupata internet ya kasi ya juu zaidi.

Kupitia mtandao anaoumiliki wa Twitter Elon alikuwa anajibu comment ya Mwekezaji Mike Coudrey ambaye alimshauri Elon kuileta Starlink Afrika Mashariki hususani Tanzania ili Watu wawe na internet ya uhakika ya kuwawezesha kupata taarifa na kuwa na kesho iliyo bora ambapo Elon alinukuliwa akijibu “Tunasubiri kibali kutoka Tanzania”

Kwa upande wa Serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nape Nnauye ambaye Watanzania wengi walimtag kwenye tweet hizo ili kupata kauli yake alinukuliwa akisema “Walishajibiwa siku nyingi wana documents wanatakiwa kukamilisha ili mchakato uendelee, hawajakamilisha documents”