Drake:Najuta kuwataja majina “Ex” katika nyimbo zangu!

Milard Ayo
Published: Mar 02, 2023 10:16:02 EAT   |  Entertainment

Wapenzi wa baadaye wa Drake huenda  hawataonekana wala kusikika majina yao kwenye muziki wake yaani hata kushirikishwa na drake kwenye ngoma yoyote, kulingana na rapper huyo kudai kuwa huenda amewaharibia maisha yao hasa kipindi  wakiachana na kuendelea na maisha yao binafsi na wapenzi wengine. Akiwa anazungumza na Lil Yachty kwenye “Moody Conversations” hivi majuzi, rapper […]

Wapenzi wa baadaye wa Drake huenda  hawataonekana wala kusikika majina yao kwenye muziki wake yaani hata kushirikishwa na drake kwenye ngoma yoyote, kulingana na rapper huyo kudai kuwa huenda amewaharibia maisha yao hasa kipindi  wakiachana na kuendelea na maisha yao binafsi na wapenzi wengine.

Akiwa anazungumza na Lil Yachty kwenye “Moody Conversations” hivi majuzi, rapper huyo alikiri kwamba ana majuto mawili linapokuja suala la kazi yake ya miongo kadhaa kwanza kuwataja wapenzi wake wa zamani katika nyimbo zake na kuwaita rappers wakubwa .

Ingawa alifafanua kwamba “mashairi hayana nia mbaya,” .

Katika albamu saba  za Drake, rapper huyo amewaita baadhi ya mastaa wakali wa Hollywood alio wahi kuwa na mahusiano nao kama vile Rihanna na SZA.

Katika wimbo wake wa 2021 “Mr.Right Now,” rapper huyo alidai kuwa alichumbiana kwa muda mfupi na mwimbaji wa “Kill Bill” SZA ndio mana alimtaja.

Mwaka huo huo, alirudi tena kwenye uhusiano wake na Jennifer Lopez na alimtaja katika ngoma  “Diplomatic immunity” na kusema 2010 alimpoteza J baada kupoteza halo/2017

Pia amemwita Keshia Chanté maarufu kwenye “In My Feelings” na mwanamke anayeitwa Kiki, ambaye watu wengi walidhani labda alikuwa Kim Kardashian lakini baadae ilisemekana  kuwa mwanamke huyo aliitwa  K’yanna Barber.

Licha ya kusema kwamba amejaribu awezavyo kuacha kufanya hivyo,wakati mwingine Drake anasema huingia tu katika hisia zake katika mashairi na yanayo taja wapenzi wake wa zamani na pia anaonesha hisia zake za kweli kwa mashabiki wanaosikiliza ngoma zake.