Cardi B achora tattoo ya mwanae “Wave” usoni!

Milard Ayo
Published: Mar 04, 2023 04:00:22 EAT   |  Entertainment

Rapa wa Marekani na mtunzi wa nyimbo, Card B amechora tattoo yake ya kwanza ya jina la mwanae “WAVE” na kuipost kwa mara ya kwanza kwenye ukurasa wake wa twitter,hatua ambayo imezua hisia tofauti mtandaoni. Mama huyo wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 30 alichorwa na msanii wa tattoo Robinson De Los Santos, ambaye […]

Rapa wa Marekani na mtunzi wa nyimbo, Card B amechora tattoo yake ya kwanza ya jina la mwanae “WAVE” na kuipost kwa mara ya kwanza kwenye ukurasa wake wa twitter,hatua ambayo imezua hisia tofauti mtandaoni.

Mama huyo wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 30 alichorwa na msanii wa tattoo Robinson De Los Santos, ambaye alishiriki picha zake akifanya kazi kazi hiyo.

Kwenye picha aliyo post neno “Wave” limechorwa kwenye shavu lake ikionyesha neno hilo  wazi kwa mara ya kwanza tangu alipoifanya Agosti 2022 ambapo alipost picha hiyo bila kuona alichokichora.

Awali Cardi aliwaambia mashabiki zake kwamba alikuwa akifikiria kumchora tattoo mtoto wake wa miezi 11, jina la Wave usoni mwake lakini imepokelewa kwa hisia tofauti.

“We love it too maaaaa,”

“When you first said you’d do it I was acc scared. It came out real cute tbh. Simple and cute.”