‘Bwawa la Nyerere unalelewa na nchi zetu mbili ‘Misri na Tanzania,’ hauwezi kufeli’- Waziri Makamba

Milard Ayo
Published: Jun 01, 2023 17:07:04 EAT   |  News

Ni June 1, 2023 ambapo Waziri wa Nishati, January Makamba amehitimisha Mjadala wa Bajeti ya Wizaea ya Nishati. “Mradi huu (Bwawa la Nyerere) unalelewa na nchi zetu mbili (Tanzania na Misri), hauwezi kufeli. Na katika kushughulikia mradi huu lazima tuzingatie hilo. Ndio maana hakuna mambo ya mahakamani, haitatokea. Naomba waheshimiwa mtuamini, tumeweka sayansi ya usimamizi […]

Ni June 1, 2023 ambapo Waziri wa Nishati, January Makamba amehitimisha Mjadala wa Bajeti ya Wizaea ya Nishati.

“Mradi huu (Bwawa la Nyerere) unalelewa na nchi zetu mbili (Tanzania na Misri), hauwezi kufeli. Na katika kushughulikia mradi huu lazima tuzingatie hilo. Ndio maana hakuna mambo ya mahakamani, haitatokea. Naomba waheshimiwa mtuamini, tumeweka sayansi ya usimamizi wa miradi, tunaizingatia, tumefika pazuri sana. Mradi huu utakwisha salama kwa kibali cha Mwenyezi Mungu” Waziri wa Nishati, January Makamba.

“Siku moja hapa umeme umekatika Bungeni, kumetokea hitilafu. Ghafla bwana “fukuza Waziri, fukuza TANESCO”. Kumbe kuja kuchunguza waala!. Umeme umekatika kwenye uwanja wa mpira, “fukuza Waziri, fukuza TANESCO”. Kumbe ni mambo mengine. Jamani, sio wakati wote ni TANESCO, sio wakati wote ni Wizara. Sisi tutachukua wajibu wetu pale inapotokea” Waziri wa Nishati, January Makamba