BRELA yawataka vijana na Wanawake kusajili majina ya biashara zao

Milard Ayo
Published: Mar 13, 2023 19:08:57 EAT   |  Business

Afisa Usajili Msaidizi wa Leseni wa Wakala wa biashara na Leseni BRELA Bethod Bangahanoze amewataka vijana na Wanawake kusajili majina ya biashara zao ili waweze kuongeza thamani ya kupewa tenda kubwa za serikali. Amesema hayo wakati wakitoa elimu ya Usajili wa kampuni na majina ya Leseni ya biashara kwa wateja waliofika kwenye Banda la Wakala […]

Afisa Usajili Msaidizi wa Leseni wa Wakala wa biashara na Leseni BRELA Bethod Bangahanoze amewataka vijana na Wanawake kusajili majina ya biashara zao ili waweze kuongeza thamani ya kupewa tenda kubwa za serikali.

Amesema hayo wakati wakitoa elimu ya Usajili wa kampuni na majina ya Leseni ya biashara kwa wateja waliofika kwenye Banda la Wakala wa Usajili wa biashara na Leseni BRELA katika maonyesho ya wajasiliamali na Wafanyabiashara katika Viwanja vya mlimani city jijini Dar es salaam.

Amesema makampuni wanayoanzisha wakisajili Leseni za kampuni zao na Usajili wa jina biashara itawapa sifa itakayowasaidia wasikose fursa ya kutambulika kisheria katika biashara zao kitaifa na kimataifa.

Alisema BRELA hutoka huduma za Usajili wa kampuni na Usajili wa jina la kampuni bure hivyo wafike katika Banda la maonyesho la hapo mlimani city au waingie kwenye mtandao wajisajili wenyewe popote walipo.

“Kuna fursa ambazo Mfanyabiashara anapata iwapo amesajili kampuni yake BRELA na hukosa fursa hizo iwapo hawajasaji Kampuni zao BRELA”

Aidha alizitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na kupata tenda kubwa za kiserikali, unakuwa unatambulika kisheria lakini pia inaongeza sifa ya kupata Mikopo katika taasisi mbalimbali za fedha.

Mariamu Masaninga ameshukuru Kwa elimu hiyo na kuahidi kufanya Usajili wa jina la biashara yake na kuwataka watu wote kufanya hima kusajili biashara zao ilikuongeza thamani katika soko la kitaifa na kimataifa na kuahidi kuongeza ubunifu katika biashara zao.

Kundi hilo la Vijana na wanawake limepata faida ya kujua misingi ya kuanzisha kampuni Kwa kusajiliwa kwani wengi wao wanafanya biashara katika bila kufanya usajili na hivyo inawanyima fursa ya kutambulika kisheria