Alichokifanya Prof. Katundu kwa watumishi ofisi ya Waziri Mkuu, atoa kauli

Milard Ayo
Published: Mar 02, 2023 14:56:25 EAT   |  Jobs and Career

Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu na taasisi zake ikiwemo OSHA, wameshiriki katika mbio za Kimataifa za Kili Marathon Mkoani Kilimanjaro wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Adam Katundu katika mbio za Kilomita 21 na Kilomita 5. Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali […]

Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu na taasisi zake ikiwemo OSHA, wameshiriki katika mbio za Kimataifa za Kili Marathon Mkoani Kilimanjaro wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Adam Katundu katika mbio za Kilomita 21 na Kilomita 5.

Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu Bi. Edith Kisanji Simtengu amesema lengo kubwa la kushiriki katika mbio hizo ni kutekeleza sera ya kupambana na magonjwa sugu yasiyoyakuambukiza hivyo kuwafanya wafanyakazi wawe na afya njema na kuhamasika katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa OSHA, Bi Netiwe Mhando ambaye pia alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa mbio za Km 21 amesema kuwa ushiriki wa mbio hizo unatokana na majukumu ya msingi yanayosimamiwa na taasisi ya OSHA ikiwemo kuimarisha usalama na afya za wafanyakazi.

“Tunaposhiriki katika michezo kama hii maana yake tunahimiza wafanyakazi kujiweka katika hali nzuri ya kiafya hivyo kuilinda nguvu kazi ya taifa nashauri taasisi zingine kuhamasika katika kushiriki michezo na mazoezi mengine ili kuwasaidia wafanyakazi kujiweka imara, kuhamasisha ushirikiano na pia kuleta ari ya kufanya kazi katika maeneo yao ya kazi” alisema Bi Mhando.

.