Ajali za majini zapungua Geita

Milard Ayo
Published: Feb 18, 2023 06:50:47 EAT   |  Educational

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeendelea kutoa elimu ya Usalama wa vyombo, abiria pamoja na mali zao wanapotumia usafiri majini. Akizungumza wakati akitoa elimu ya namna ya kujiokoa abiria pamoja na wavuvi katika mwalo wa Chato beach uliyopo wilayani Chato Mkoani Geita, Bw. Rashid Katonga ambaye ni Afisa Mfawidhi Tasac mkoa wa Geita […]

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeendelea kutoa elimu ya Usalama wa vyombo, abiria pamoja na mali zao wanapotumia usafiri majini.

Akizungumza wakati akitoa elimu ya namna ya kujiokoa abiria pamoja na wavuvi katika mwalo wa Chato beach uliyopo wilayani Chato Mkoani Geita, Bw. Rashid Katonga ambaye ni Afisa Mfawidhi Tasac mkoa wa Geita amesema mkakati uliowekwa na TASAC ni kuondokana na vifo ambavyo vimekuwa si vya lazima huku akisema atakaye kaidi kuvaa jaketi okozi “life jacket” sheria itachukua mkondo wake.

Aidha aliongeza kuwa TASAC wamesema vifo vingi ambavyo vimekuwa vikitokea majini vimekuwa vikisababishwa na ulevi kupindukia pamoja na watumiaji wa vyombo vya maji kutovaa life Jacket katika safari ambazo zimekuwa zikifanywa kila siku.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Chato Bw. Deusideth Katwale ameiomba TAKUKURU kuhakikisha wanakomesha vitendo vya rushwa katika mialo hiyo kwani pia imekuwa kichocheo cha ajali nyingi ndani ya ziwa.

TASAC inaendelea kuzunguka maeneo mbalimbali ya Mikoa pamoja na wilaya zake kwa lengo la kutoa elimu kwa abiria pamoja na wavuvi namna ya kujiokoa wawapo katika safari zao za kila siku.