Aga Khan wawapa mafunzo Walimu na Wanafunzi utunzaji mazingira

Milard Ayo
Published: Feb 22, 2023 09:29:28 EAT   |  Educational

Taasisi ya Elimu ya Aga Khan (AKES) Tanzania ikishirikiana na Taasisi ya Aga Khan Tanzania (AKF) imetoa mafunzo kwa walimu na wanafunzi juu ya namna bora ya kuhifadhi mazingira kwa maendeleo endelevu. Katika mafunzo hayo kwa vitendo, yaliyoshirikisha walimu na baadhi ya wanafunzi kutoka shule za awali, msingi na sekondari za Aga Khan zilizoko jijini Dar es Salaam, yaliwapa ujuzi wa […]

Taasisi ya Elimu ya Aga Khan (AKES) Tanzania ikishirikiana na Taasisi ya Aga Khan Tanzania (AKF) imetoa mafunzo kwa walimu na wanafunzi juu ya namna bora ya kuhifadhi mazingira kwa maendeleo endelevu.

Katika mafunzo hayo kwa vitendo, yaliyoshirikisha walimu na baadhi ya wanafunzi kutoka shule za awali, msingi na sekondari za Aga Khan zilizoko jijini Dar es Salaam, yaliwapa ujuzi wa kujenga “viwanda vya udongo” 60 katika eneo la Aga Khan Upanga, kwa kutumia malighafi rejereshi kama karatasi, boksi, mbolea na ndoo kubwa.

Katika mafunzo hayo, viwanda hivyo vidogo vidogo kwa ajili ya kutengeneza udongo wenye rutuba, pia vilijengwa na wanafunzi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Zanaki, ambayo ni jirani na Shule za Aga Khan.

Ujuzi huu wa kutengeneza udongo wenye madini muhimu ambayo ni sehemu muhimu ya ukuaji wa mimea, utasaidia kutunza na kuleta suluhisho la asili kwa ajili ya kilimo cha chakula kinachozingatia utunzaji wa mazingira kwa maendeleo endelevu.

Hii ni mara ya pili kwa taasisi ya Aga Khan kushirikisha wanafunzi na walimu wa Shule za taasisi hiyo katika kutunza na kuleta suluhu ya kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, ambapo walifanya kazi na Ismaili CIVIC kupanda zaidi ya miti zaidi ya 100 katika eneo dogo ili kukuza bioanuwai zinazotegemewa na атії.