
POLISI FC VS YANGA SC-WANANCHI MLIKAA KINYONGE SANA-CHAMA LIPO DIMBANI LEO-UCHAMBUZI
🔴#LIVE:POLISI FC VS YANGA SC-WANANCHI MLIKAA KINYONGE SANA-CHAMA LIPO DIMBANI LEO-UCHAMBUZI ⚫️ OUR PLAYLISTS:
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.

🔴#LIVE:POLISI FC VS YANGA SC-WANANCHI MLIKAA KINYONGE SANA-CHAMA LIPO DIMBANI LEO-UCHAMBUZI ⚫️ OUR PLAYLISTS:

WASHINGTON, Amerika: TELEVISHENI Amerika Jumatatu zilisitisha kwa pamoja kurusha matangazo ya shughuli za Rais Donald Trump kutoka Ikulu ya White House, baada ya CNN, Politico na MS NOW kuzuiwa kuingia katika jengo hilo. Trump alitangaza marufuku hiyo Ijumaa, akishutumu mashirika hayo kwa 'kuandika habari za kutunga na uongo' kuhusu utawala wake. Vyombo hivyo vilisema waandishi wao walizuiwa kuingia White House mnamo Jumamosi. CNN, Politico na MS NOW baadaye zilitangaza kuwa zitawasilisha kesi dhidi ya utawala wa Trump ili kutetea kanuni kwamba serikali haiwezi kuamua kile ambacho vyombo vya habari vinaripoti. Kufuatia hatua hiyo, White House ilianzisha kituo chake cha matangazo mtandaoni, Trump TV, kinachorusha sehemu za video ya rais saa 24 kwa siku. Vyombo vingine vya habari pia vilisema havitashiriki katika mfumo wa pamoja wa kuripoti shughuli za rais. New York Times na Washington Post, kwa mfano, zilisema hazitachapisha picha za matukio ya Trump. Hatua hiyo ilisababisha kukosekana kwa picha za televisheni za Trump akipanda ndege ya Air Force One au akiwasili New York kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Trump pia alishiriki katika hafla ya kuzindua uwanja mpya wa helikopta ya Marine One katika bustani ya White House. Hafla hiyo ilikuwa mbashara kwenye tovuti ya White House, ingawa sauti ya hotuba yake haikusikika. Baadaye rais alionekana kwenye televisheni baada ya kukutana na Meya wa New York Zohran Mamdani. Mamdani alimweleza kuwa waandishi wote wa habari watakaribishwa katika mkutano na wanahabari. Trump alisema hakushtushwa na hatua hiyo, akisema vyombo vya habari vilivyodai vitamsusia havijawahi kufanya hivyo. Mfumo wa ushirikiano wa vyombo vya habari huyawezesha mashirika ya habari kushirikiana ili kupunguza gharama na matumizi ya nafasi wakati wa kuripoti shughuli za rais. Bryan Boughton, mkuu wa afisi ya Fox News Washington, alisema katika barua pepe kuwa mfumo huo hautaendelea kuripoti shughuli za Trump zinazowashirikisha vyombo vyote vya habari. Alisema hatua hiyo ilifuatia White House kuzuia CNN kutekeleza jukumu lake katika ziara ya Trump New York. Siku hiyo hiyo, CNN, Politico na MS NOW ziliwasilisha kesi Mahakamani jijini Washington, zikisema White House ilifuta vibali vya waandishi wao bila kuwapa taarifa wala nafasi ya kujitetea. Vyombo hivyo vilisema hatua hiyo inatishia uhuru wa vyombo vya habari na haki ya umma kupata habari huru bila kuingiliwa na serikali.

DAR ES SALAAM: SERIKALI imetoa Sh bilioni 20 kwa ajili ya kuendelea na malipo ya fidia kwa wananchi wa eneo la Kipunguni wanaopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), ambapo jumla ya Sh bilioni 86 kati ya Sh bilioni 114 zinazohitajika ikiwa tayari imelipwa. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja…

DAR ES SALAAM: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kinara wa Umoja wa Afrika wa Masuala ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Dk. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuwaongoza viongozi wakuu wa nchi za Afrika na wadau wa maendeleo katika kujadili na kuhamasisha uwekezaji katika afya ya uzazi, mama, mtoto mchanga na mtoto…

Wanajamii wa eneo la Oloitikosh katika Kaunti ya Kajiado wameanza kuweka ua kuzunguka ekari 60 za ardhi inayomilikiwa na Chuo cha Mafunzo ya Kiufundi cha Kajiado East (TVET), wiki mbili baada ya Rais William Ruto kuagiza ardhi hiyo ilindwe kwa ajili ya upanuzi wa taasisi hiyo. Shughuli ya kuweka ua Jumatatu iliongozwa na Naibu Chifu wa Oloitikosh, Moses Karaine, kwa ushirikiano na wakazi wa eneo hilo. Hatua hiyo imefuatia madai kwamba sehemu kubwa ya ardhi ya awali ya chuo hicho yenye ukubwa wa ekari 76 ilinyakuliwa na kugawanywa na watu binafsi kwa ushirikiano wa mabroka na baadhi ya wanasiasa. Inadaiwa kuwa chuo kilibaki na ekari saba pekee ambako majengo yake yamejengwa. Wakati wa ziara yake ya maendeleo katika eneo hilo wiki mbili zilizopita, Rais Ruto aliamuru ekari 60 zilizokuwa zikizozaniwa ziwekwe ua mara moja ili kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye ya chuo hicho. “Ardhi hii lazima ilindwe na kuwekwa ua. Nitarudi mwenyewe kukagua maendeleo. Baadaye TVET hii inaweza kukua na kuwa chuo kikuu,” alisema Rais wakati wa uzinduzi wa mabweni ya wanafunzi chini ya mpango wa Boma Yangu. Chuo hicho, ambacho kina umri wa miaka 10, kwa sasa kina takriban wanafunzi 800 wanaosomea kozi mbalimbali za kiufundi. Pia ndicho taasisi pekee ya serikali katika Kaunti ya Kajiado iliyo na kituo cha kidijitali cha Jitume Digital Hub. Mkuu wa chuo hicho, Watiri Kiragu, alisifu hatua ya rais akisema kurejeshwa kwa ardhi hiyo kutatoa nafasi muhimu kwa upanuzi wa taasisi hiyo siku zijazo. “Msingi wa upanuzi wa taasisi yoyote ni upatikanaji wa ardhi. Uamuzi huu ni wa manufaa makubwa kwa maendeleo ya chuo,” alisema. Mzee Daniel Lepatei, ambaye alipewa jukumu la kusimamia ujenzi wa ua huo, alisema jamii imejitolea kulinda ardhi hiyo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Kwa mujibu wake, mabroka wa ardhi walianza kugawa sehemu ya ardhi hiyo miaka mitano iliyopita na kupata barua za ugavi kwa njia isiyo halali. “Amri ya rais imeokoa mustakabali wa vijana wetu. Fedha za kujenga ua zimepatikana na taratibu za kurejesha ardhi zimekamilika,” alisema. Nao viongozi wa jamii walidai kuwa baadhi ya maafisa wa utawala, wanasiasa na maafisa wa ardhi walihusishwa na unyakuzi wa ardhi hiyo. Hata hivyo, Waziri wa Ardhi wa Kaunti ya Kajiado, Hamilton Parseina, alisema barua zote za ugavi zilizokuwa zimetolewa kwa watu binafsi tayari zimefutwa. “Ardhi hii ni mali ya chuo cha TVET. Barua zilizokuwa zimetolewa hapo awali zimebatilishwa ili kuruhusu upanuzi wa taasisi hiyo,” alisema. Hatua ya kuzungusha ua ardhi hiyo imepokelewa kwa furaha na wakazi, ambao wanasema italinda rasilimali ya umma wakati ambapo maeneo mengi ya Kitengela yanaendelea kukabiliwa na ongezeko la visa vya unyakuzi wa ardhi ya taasisi za umma.

MWANZA; MKUU wa Mkoa wa Mwanza, CP Salum Hamduni, amewataka wananchi wa Wilaya ya Ukerewe kushirikiana na Serikali katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili, ikiwemo upatikanaji wa maji, umeme na barabara. CP Hamduni ametoa kauli hiyo leo Septemba 22, wakati akizungumza na wananchi wa Ukerewe, ambapo amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wananchi, watumishi wa…

RAIS William Ruto anatarajiwa kutumia hotuba yake katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kuangazia masuala ambayo Kenya inayapa kipaumbele hasa yanayohusu amani na usalama. Masuala mengine yanahusu ufadhili wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, mageuzi ya UN, usimamizi wa Akili-Unde (AI) na diplomasia ya kiuchumi. Mkutano huo umeanza New York chini ya kaulimbiu “Kurejesha Imani, Kusimamia Mabadiliko: Umoja wa Mataifa Unaotekeleza kwa Wote.” Rais Ruto alifika New York Jumamosi na tayari amekutana na Wakenya wanaoishi Amerika akisisitiza wana wajibu muhimu katika maendeleo kupitia uwekezaji, utaalamu na mitandao ya kimataifa. Serikali pia ilizindua Jukwaa la Wakenya wanaoishi Ughaibuni, inayolenga kuwaunganisha Wakenya na kuongeza fursa za uwekezaji nchini. Katika hotuba yake, Ruto anatarajiwa pia kuunga mkono juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, maendeleo na haki za binadamu, huku akitoa msimamo wa Kenya kuhusu mageuzi ndani ya UN.

MAKANISA mawili yameingia katika mzozo wa kisheria kuhusu haki ya kutumia jina “Gospel of God Church”, huku rekodi zinazokinzana za usajili zikiwa kiini cha mgogoro wa zaidi ya miongo minne kuhusu utambulisho na mali ya kanisa. Mzozo huo unahusu ni upande upi una haki kisheria kutumia jina hilo na kudai mali zilizopatikana kwa jina hilo. Hii ni baada ya usajili wa mnamo 1968 kufutwa 1985, kisha usajili mpya wa 2004 kabla ya kurejeshewa jina la awali mnamo 2009. Upande mmoja umesajiliwa kama Gospel of God Church (SOC 7670), awali ikijulikana kama African Gospel Church, iliyotambuliwa kisheria mnamo 1968. Upande mwingine ni Gospel of God Church International (SOC 45700), awali ikijulikana kama Glorious Gospel of God Church, iliyosajiliwa mnamo 2004. Mzozo huo umepitia Afisi ya Msajili wa Mashirika, mahakama zinazoshughulikia ardhi na Mahakama Kuu, huku kila upande ukiwasilisha maelezo tofauti kuhusu taasisi ambayo kisheria iliendelea kuwepo baada ya mabadiliko hayo. Mzozo huo pia unahusu ardhi, majengo ya makanisa, magari na mali nyingine zilizopatikana kwa miongo kadhaa. Wiki iliyopita, Jaji Roseline Aburili alitupilia mbali ombi la kikatiba la Gospel of God Church International (SOC 45700), bila kuamua ni upande upi unaomiliki jina hilo au mali zinazobishaniwa. Mahakama ilisema waliowasilisha kesi walipuuza utaratibu wa kisheria wa kukata rufaa baada ya Msajili wa Mashirika kutoa maamuzi Agosti na Oktoba 2024, akiamuru SOC 45700 irejee kwa jina lake la awali, Glorious Gospel of God Church, ndani ya siku 30 au ifutiwe usajili. Chini ya Sheria ya Mashirika, taasisi isiyoridhishwa na uamuzi wa Msajili inapaswa kwanza kukata rufaa kwa Serikali kabla ya kuelekea Mahakama Kuu. “Kwa hivyo, ninapata kwamba ombi hili liliwasilishwa mapema na kupuuza kabisa masharti ya Sheria ya Mashirika,” alisema Jaji Aburili. Rekodi za mahakama zinaonyesha Gospel of God Church, SOC 7670, ilianzishwa Kenya 1968 na kupewa msamaha wa usajili Agosti 26 mwaka huo. Mnamo 1985, baada ya serikali kuingilia kati na viongozi wa kigeni kuondoka, wanachama wa Kenya walichagua viongozi wao. Naibu Msajili baadaye alifuta msamaha huo kupitia notisi ya gazeti rasmi. Waliowasilisha kesi walidai hatua hiyo ilimaliza uwepo wa kisheria wa kanisa hilo, na viongozi wa eneo hilo wakasajili Glorious Gospel of God Church of Kenya mnamo 2004. Msajili aliidhinisha mabadiliko ya jina kuwa Gospel of God Church International Machi 22, 2005. Hata hivyo, kundi la awali la Gospel of God Church, SOC 7670, lilirejeshwa katika usajili Novemba 11, 2009. Kundi hilo lilisema ndilo kanisa linalotambuliwa kisheria na lenye haki ya kumiliki mali yenye thamani ya mabilioni ya pesa. Jaji Aburili pia aligundua kuwa makanisa hayo hayakuwa na uwezo wa kufungua kesi kwa majina yao bila kutaja viongozi waliosajiliwa na kutoa idhini ya maandishi. Mahakama hivyo ilitupilia mbali ombi hilo na kuwaelekeza wahusika kufuata kwanza utaratibu wa rufaa.

DAR ES SALAAM: ARTIFICIAL Intelligence (AI) is rapidly changing how people learn, work, communicate and solve problems. In Tanzania, it presents an opportunity to transform education, improve productivity and prepare young people for an increasingly digital economy. However, AI adoption also raises concerns about independent thinking. The term “digital dementia”, although not an official medical…

NAIBU Rais Kithure Kindiki amewataka viongozi wa Mlima Kenya kuwaheshimu wazee na kusikiza wito wao wa umoja, akisema tofauti za kisiasa hazifai kuruhusiwa kuvunja jamii ambayo imeshirikiana kwa miaka mingi. Profesa Kindiki alisema amezingatia kwa uzito wito wa wazee wa kuongoza juhudi za maridhiano na umoja katika eneo hilo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Alisema ataheshimu mwongozo wa wazee anapozifikia jamii za Mlima Kenya Mashariki na Magharibi katika juhudi za kujenga umoja wa kisiasa. Naibu Rais alisema hayo siku chache baada ya wazee wa Mlima Kenya kukutana katika Uwanja wa Kirigiti, Kaunti ya Kiambu, na kumtawaza kama kigogo wa siasa za eneo hilo. Wazee hao walitoa wito wa umoja miongoni mwa jamii za Agikuyu, Embu, Ameru na Mbeere na kuwataka wakazi wa eneo hilo kubaki na umoja wa kisiasa kuelekea uchaguzi wa 2027. Pia walionyesha kuunga mkono utawala wa Rais William Ruto, hivyo kumpa Profesa Kindiki jukwaa jipya la kuhakikisha eneo hilo linamuunga mkono Rais. Profesa Kindiki alisema viongozi wanapaswa kuheshimu tofauti za kisiasa lakini wasizigeuze kuwa migawanyiko inayolemaza eneo hilo kimaendeleo. Amekuwa akipinga juhudi za kugawanya Mlima Kenya kwa misingi ya Mashariki na Magharibi, akisema jamii hizo zina uhusiano mkubwa wa kihistoria, kitamaduni na kiuchumi kuliko tofauti zao za kisiasa. Wito huo unakuja wakati siasa zikizidi kushika kasi katika eneo hilo, huku makundi hasimu yakitafuta kushawishi mwelekeo wa kisiasa wa eneo hilo kuelekea 2027. Profesa Kindiki alisisitiza atatekeleza maagizo ya wazee kwa kupitia ziara za maendeleo katika Mlima Kenya Mashariki na Magharibi. Baada ya mkutano wa Kirigiti, alikagua ujenzi wa Barabara ya Mukothima-Gaciongo-Gatunga katika eneobunge la Tharaka, Kaunti ya Tharaka Nithi, kabla ya kuhutubia wakazi katika Soko la Gaciongo wakati wa mkutano wa umma. Naibu Rais ameweka barabara, miundombinu na utekelezaji wa mipango ya Serikali kuwa nguzo kuu za ziara zake, akisema uongozi wa kisiasa unapaswa kulenga kuboresha maisha ya wananchi. Wazee wa Kirigiti waliwataka jamii za Mlima Kenya kuwa na msimamo wa pamoja kuhusu masuala yanayoligusa eneo hilo na kukataa juhudi za kuunda makundi tofauti ya kisiasa.

MWEKEZAJI na mwanasiasa Suleiman Shahbal anakabiliwa na changamoto ya kutenganisha mikataba yake ya mabilioni ya pesa katika miradi ya serikali na azma yake ya ugavana Mombasa, huku shinikizo ikizidi kwake ajiondoe kwenye kinyang’anyiro cha 2027. Shinikizo hizo zimezidi kujitokeza wiki chache baada ya kutia saini mkataba wa kuanzisha Eneo Maalum la Kiuchumi (SEZ) jijini Mombasa na kampuni ya kimataifa ya usafirishaji bandarini ya DP World katika Ikulu ya Nairobi. Rais William Ruto awali alikuwa amemshauri Bw Shahbal kuachana na siasa, lakini mfanyabiashara huyo akakataa. Katibu Mkuu wa chama cha United Democratic Alliance (UDA), Bw Omar Hassan, ambaye pia analenga kumng’oa Gavana Abdulswamad Nassir kitini, sasa amesema kuna hatari ya kutokea mgongano wa maslahi iwapo Bw Shahbal atakuwa gavana wa Mombasa huku akiendelea kuwa mshirika mkubwa katika sekta ya biashara ya kaunti hiyo. Mkataba huo wa Sh12 bilioni kati ya kampuni yake ya GulfCap Group na DP World unalenga kujenga Eneo Maalum la Kiuchumi (SEZ) lenye ukubwa wa ekari 535 Jomvu. Ardhi hiyo inamilikiwa na Serikali ya Kaunti ya Mombasa na hapo awali ilikodishwa kwa shirika la Kenya Meat Commission. Mbali na mradi wa SEZ, GulfCap pia inahusika katika ujenzi wa mradi wa nyumba za bei nafuu kwa ushirikiano na serikali ya kaunti mtaani Buxton. Mradi huo wa Sh6 bilioni ulianzishwa wakati wa utawala wa zamani wa kaunti chini ya gavana wa zamani Hassan Joho, ambaye sasa ni Waziri wa Madini na Uchumi wa Baharini, baada ya kubomolewa kwa nyumba za zamani za kaunti. Vilevile, GulfCap ina mradi mwingine kama huo jijini Nairobi. “Ukiwa mfanyabiashara, shikilia biashara na uwaachie wasimamizi wa serikali jukumu la kuweka mifumo na taratibu zinazostahili, kwa sababu una mgongano wa maslahi,” Bw Omar alisema. Huku akijipigia debe, Bw Omar alitaja uzoefu wake kama mwanaharakati wa haki za binadamu, seneta wa zamani wa Mombasa na Katibu Mkuu wa UDA kama sehemu ya sifa zake katika kinyang’anyiro cha ugavana. Alisema azma yake ya kisiasa imechochewa na hitaji la kuboresha utawala na kurejesha heshima, hadhi na uzingatiaji wa Katiba Mombasa. Mbunge wa Jomvu, Badi Twalib, pia alimkosoa Bw Shahbal kwa kumpinga Gavana Nassir katika uchaguzi wa 2027, licha ya serikali ya kaunti kumuunga mkono katika mpango wake wa kuendeleza SEZ. “Wale wanaomiliki SEZ wameanza kumpiga vita gavana hata kabla mradi haujaanza. Lakini leo tunawaambia kwamba gavana ataweka siasa kando. Huu sasa ni wakati wa maendeleo. Mtu mnayempiga vita ndiye huyo huyo atakayewanyooshea mkono na kuunga mkono mradi ili maendeleo yaje na watu wapate ajira,” alisema. Wakati wa kusainiwa kwa mkataba wa SEZ Septemba 8, Rais Ruto alisema Kenya inahitaji wawekezaji wakubwa, wawekezaji na wajasiriamali makini wenye uwezo wa kutekeleza miradi itakayochangia ukuaji wa uchumi. Hata hivyo, Bw Shahbal alikataa wito wa kuachana na siasa na ameendelea kusisitiza kuwa atawania kiti cha ugavana wa Mombasa mwaka 2027. Hivi majuzi, mbunge huyo wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) alieleza wasiwasi kwamba siasa za ugavana zinaweza kuathiri mradi wake na kuwataka wapinzani wake kuweka tofauti zao kando ili kuhakikisha mradi huo unafanikiwa. Bw Shahbal, ambaye ametangaza kuwa hatatafuta tiketi ya ODM kugombea mwaka wa 2027, alimuonya Rais Ruto dhidi ya mipango ya kisiasa ya kugawana maeneo kati ya ODM na UDA, almaarufu kama ‘zoning’. “Upuuzi huu wote wa kugawana maeneo umeandaliwa na watu wanaoogopa kuenda mashinani kukutana na watu. Ikiwa una imani na uongozi wako, nenda kwa wananchi uwaambie ulichofanya nao.

RAIS wa Uganda Yoweri Museveni amesema aligundua tu hivi majuzi kwamba aliyekuwa Mbunge wa Lugari, Cyrus Jirongo, alifariki katika ajali ya barabarani Disemba 13, 2025. Museveni alisema Jirongo ndiye aliyemjulisha mnamo 2019 kuhusu Uganda kununua mafuta kutoka Kenya kupitia madalali waliotoza bei ya juu, hali iliyosababisha serikali kupoteza mamilioni ya shilingi. Taarifa hiyo ilimfanya Museveni kumwagiza aliyekuwa Waziri wa Nishati Irene Muloni kuchunguza suala hilo. Siku tano baada ya kumtaja Jirongo na kumwita 'Seneta' ingawa mwanasiasa huyo hakuwahi kuhudumu kama seneta, Museveni alisema hakujua kuwa mwanasiasa huyo alikuwa amefariki. Alimsifu Jirongo kama kiongozi mzuri na mzalendo aliyeitumikia Kenya kwa kujitolea. “Tutamkosa,” Museveni alisema, akitoa rambirambi kwa familia, marafiki na wananchi wa Kenya.

MAHAKAMA Kuu imekataa ombi la dhamana la wanafunzi wanane wa Utumishi Girls Academy wanaokabiliwa na mashtaka ya mauaji ya wenzao 16 katika mkasa wa moto uliotokea shuleni Mei 28, 2026. Jaji Diana Kavedza-Mochache alisema kuwa kuwaachilia kwa sasa kunaweza kuhatarisha usalama wao, mashahidi na watu wengine wanaohusika katika kesi hiyo, pamoja na kuathiri mwenendo wa kesi. Mahakama ilisema ripoti zinaonyesha baadhi ya wanafunzi hao wamekumbwa na vitisho vya kushambuliwa wakiwa kizuizini, huku wengine wakinyanyaswa mtandaoni. Jaji alisema watoto wanaokabiliwa na sheria bado wana haki za kulindwa, licha ya uzito wa mashtaka. Aliagiza wapokezwe usaidizi wa kisaikolojia na ushauri nasaha.

Atiku, in a statement on Monday, raised questions over the status of presidential authority after the 21-day period elapsed, citing Section 145 of the 1999 Constitution.

By Udeme AkpanPresident and Chief Executive of Dangote Industries Limited, Aliko Dangote, has said the ongoing Dangote Petroleum Refinery Initial Public Offering, IPO, reflects the Group’s long-term commitment to Africa’s industrialisation, wealth creation and economic development.Speaking during an interview with Bloomberg Television, Dangote said the IPO was designed not only to raise capital but also […]

African Democratic Congress (ADC) has raised concern over alleged attacks on opposition political parties, political intimidation and threats to citizens ahead of the 2027 general elections.

MBEYA; JESHI la Polisi mkoa wa Mbeya limewakamata watu wawili kwa tuhuma za kupatikana na shehena ya mbegu za mahindi zilizoibwa,zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 56,mali ya Wakala wa Mbegu za Serikali(ASA). Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema watuhumiwa hao walikamatwa Septemba 20 jioni baada ya jeshi hilo…

A public transport driver who disappeared from his usual routes for nearly nine months has returned to find that colleagues had declared him dead and collected over Sh700,000 in what they described as funeral contributions.

MWANZA: THE Second Vice President of Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla has officially opened the Tanzania Military Sports Council (BAMMATA) competitions at the CCM Kirumba Stadium in Mwanza region today. The competitions, which involve military teams and defense and security agencies from seven regions, will be held for 10 days from today, September 21 to October…

CCM Deputy Secretary General (Zanzibar), Mr Abdi Mahamoud Abdi, has said the ruling party intends to seek permanent and lawful solutions to land challenges facing citizens through established decision-making platforms.

MWANZA; Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amefungua rasmi mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) leo Septemba 21, 2026 Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza. Mashindano hayo yanayoshirikisha timu za majeshi na vyombo vya ulinzi na usalama kutoka kanda saba, yataendelea hadi Oktoba 5,…

MWANZA: THE Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) has urged its Research, Planning and Investment (PRI) Department to accelerate the implementation of strategic plans and projects, emphasizing the use of technology, local expertise, and strict adherence to timelines and contractual obligations to improve project execution efficiency. The call was made by TANESCO Geita Regional Manager,…

DODOMA; Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) imesema sheria zimeboreshwa ili kuongeza kasi na tija katika utekelezaji wa Dira 2050. Wizara ya Katiba na Sheria imesema nguvu ya Taifa haipimwi tena kwa rasilimali zake za asili pekee bali kwa uimara wa taasisi zake; ufanisi wa mifumo ya utoaji haki na uwezo wa kusimamia sheria…

ZIKIWA zimesalia miezi 11 kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 10, 2027, vita vya kisheria kuhusu kuwepo kwa Kituo cha Kitaifa cha Kuhesabu Kura za Urais (NTC) vimeanza kushika kasi, huku macho yakielekezwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC). Mahakama Kuu inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa kikatiba wa NTC Septemba 22, 2026, kufuatia kesi zilizowasilishwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah pamoja na viongozi wa upinzani wakiongozwa na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na mwenzake wa DCP Rigathi Gachagua. Walalamishi wanataka mahakama itangaze kuwa kuanzishwa na kuendesha NTC kwa ajili ya kuthibitisha tena matokeo ya urais ni kinyume cha Katiba, na hivyo kubatilishwe. Wanadai kuwa katiba inaweka eneobunge kuwa kituo cha msingi na cha mwisho cha kuhesabu, kuthibitisha na kutangaza matokeo ya urais. Wanaopinga NTC pia wanataka IEBC izuiwe kuhesabu tena au kubadilisha matokeo yaliyotangazwa na maafisa wasimamizi wa uchaguzi wa maeneobunge. Aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga ameunga mkono wito wa kuondolewa kwa NTC. “Katiba haitoi nafasi kwa kituo cha kitaifa cha kuhesabia kura. Jukumu la IEBC ni kutangaza matokeo, wala si kuhesabu kura tena,” akasema Maraga. Hata hivyo, msimamo huo unatofautiana na uamuzi wa Mahakama ya Juu katika kesi ya uchaguzi wa urais wa 2017. Mahakama hiyo ilisema IEBC ina jukumu la kujumuisha na kuthibitisha kura kabla ya kutangaza mshindi, huku mchakato huo ukiendelea kutoka kituo cha kupigia kura hadi eneobunge na hatimaye NTC. Katika kesi ya 2022, Mahakama ya Juu ilifafanua kuwa jukumu la kuhesabu na kuthibitisha matokeo katika NTC ni la IEBC kama taasisi, huku mamlaka ya kutangaza mshindi yakiwa ya mwenyekiti wa tume. Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Justin Muturi na aliyekuwa rais wa Chama cha Mawakili (LSK) Nelson Havi pia wameunga mkono kuondolewa kwa NTC, wakisema matokeo yaliyohesabiwa na kutangazwa katika maeneobunge 290 yanapaswa kuwa ya mwisho. Kwa upande mwingine, aliyekuwa kamishIna wa IEBC Paul Kurgat anasema Katiba haijaweka jengo maalumu kuwa kituo cha kuhesabia kura, bali inasimamia mchakato. Anasema Kanuni za Uchaguzi zinahitaji kuhesabiwa kwa kura kikamilike katika kituo kilichotangazwa rasmi na IEBC. Mzozo huo sasa unahusu zaidi ya eneo la Bomas, kwani kesi hizo zinahoji iwapo IEBC ina mamlaka ya kikatiba na kisheria kuthibitisha matokeo ya urais katika ngazi ya kitaifa baada ya kutangazwa katika maeneo bunge. Kwa kuzingatia uwezekano wa suala hilo kufikishwa Mahakama ya Juu, uamuzi wa Mahakama Kuu unaweza kuwa hatua ya kwanza katika vita virefu vya kisheria kuhusu mfumo wa kuhesabu na kuthibitisha matokeo ya urais kuelekea uchaguzi wa 2027.

KILIMANJARO: THE inaugural Tanzania Infectious Diseases Institute (TIDI) Lung Health Half Marathon is targeting 3bn/- to support improvement of health services for patients requiring long-term treatment and care at the institute in Siha District of Kilimanjaro Region. Kilimanjaro Regional Commissioner (RC) Nurdin Babu announced the fundraising target on Friday while outlining plans for the race…

RAIS William Ruto aliondoka Nairobi kuelekea New York, Amerika, Jumamosi usiku ambako anatarajiwa kutumia Mkutano Mkuu wa 81 wa Umoja wa Mataifa (UNGA) kutangaza Kenya kama kitovu cha uwekezaji, teknolojia na fedha Afrika. Ziara yake ya siku tano itajikita katika kuvutia uwekezaji katika sekta za kawi, miundomsingi, kilimo, viwanda, afya, teknolojia na Akili-Unde (AI). Mradi unaotarajiwa kupewa uzito ni ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Sh2.2 trilioni ($17 bilioni) mjini Lamu. Serikali inasema kiwanda hicho chenye uwezo wa kusafisha mapipa 700,000 ya mafuta kwa siku kinaweza kuunda zaidi ya nafasi 60,000 za ajira na kusababisha Kenya na mataifa ya karibu kujitosheleza kwa kawi. Kulingana na Msemaji wa Ikulu, Hussein Mohamed, Rais Ruto atashirikiana na mfanyabiashara wa Nigeria, Aliko Dangote kuongoza mikutano ya uwekezaji iliyoandaliwa na kampuni za Africa Finance Corporation na Global Africa Business Initiative. Ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kuanza Septemba 30. Katika hotuba yake UNGA, Rais Ruto pia anatarajiwa kutetea mpango wa Afrika kujifadhili, maarufu kama “Africa-financing-Africa”, unaolenga kutumia zaidi akiba na mitaji ya Waafrika kufadhili maendeleo ya bara. Rais atatoa wito wa mageuzi na dhamana za kimataifa zitakazowezesha mtaji huu kutumika katika miundomsingi, biashara na vipaumbele vingine vya maendeleo,” alisema Bw Mohamed. Rais pia atatangaza Hazina ya Kitaifa ya Miundomsingi inayolenga kukusanya hadi $40 bilioni (Sh5.7 trilioni) kupitia wawekezaji binafsi na taasisi bila kuongeza deni la serikali. Teknolojia na Akiliunde pia zitakuwa sehemu muhimu ya ziara hiyo. Rais Ruto na Rais wa Finland Alexander Stubb wataongoza AI Middle Powers Initiative, inayolenga kuunganisha rasilimali za kompyuta, data na wataalamu ili mataifa yaendeleze uwezo wao wa AI.

ZANZIBAR: THE Chama Cha Mapinduzi (CCM)- Zanzibar has demanded stronger oversight and accountability in the implementation of government development projects, saying major public investments must deliver better services and economic opportunities for citizens. CCM Zanzibar Deputy SecretaryGeneral, Mr Abdi Mahmoud Abdi made the remarks during his tour of North Unguja yesterday, where he inspected development…

PWANI: ZAIDI ya tani 100 za mbaazi zilizokusanywa na wakulima wa Chalinze na Kibaha mkoani Pwani zimeuzwa zote katika mnada wa kwanza wa zao hilo, uliofanyika Kibaha kwenye ofisi za Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU). Meneja wa CORECU mkoani humo, Hamis Mantawela, amesema mnada huo umehusisha mbaazi kilo 101,346, ambapo Chalinze zilikusanywa…

MJADALA kuhusu mpango wa kugawana maeneo ya kisiasa unaendelea kuibua tofauti ndani ya ODM, huku Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya akipinga pendekezo hilo na kuunga mkono ushindani wa kirafiki kati ya ODM na UDA katika uchaguzi wa 2027. Mpango huo, ambao unalenga vyama washirika kukubaliana kutowasilisha wagombea dhidi ya wenzao katika maeneo fulani, ni miongoni mwa masuala tata katika mazungumzo ya makubaliano ya kabla ya uchaguzi kati ya ODM na UDA. Bw Oparanya, anayesemekana kuwa miongoni mwa wanaoweza kuchaguliwa kuwa mgombea mwenza wa Rais William Ruto, alisema ODM na UDA zinapaswa kuruhusu ushindani katika maeneo ya uchaguzi badala ya kuyagawana. “Tunataka vyama hivi viwili vikubwa viunde serikali imara mwaka ujao kwa sababu kila kimoja kinapaswa kuwa na nguvu. Tumekubaliana kuhusu kiongozi na tunataka ODM na UDA ziwe na nguvu hapa na kule tushindane kwa urafiki,” akasema Bw Oparanya katika uwanja wa Mayuba, Kaunti ya Bungoma mnamo Jumamosi. “Hatutaki ugawaji wa maeneo bali tushindane kwa urafiki kwa sababu sasa tuna baba mmoja. Mshindane huku mkijua kwamba tuna baba mmoja,” akaongeza. Msimamo wake unatofautiana na ule wa kiongozi wa ODM, Oburu Oginga, ambaye amekuwa akitaka maeneo yanayochukuliwa kuwa ngome za chama yalindwe katika makubaliano na UDA. “Baadhi ya watu wanasema hatutaki maeneo yatengwe. Ikiwa hamtaki, mnataka nini? Tunataka yatengwe kwa sababu Homa Bay ni eneo letu. Hatutaki UDA Homa Bay,” akasema Dkt Oginga. Amependekeza maeneo ambako chama kina magavana, wabunge na madiwani wake yahesabiwe kuwa ngome zake moja kwa moja. Msimamo huo umeungwa mkono na baadhi ya viongozi wa ODM, akiwemo Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga na Mbunge wa Homa Bay Mjini Peter Kaluma. Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa ODM wamepinga mpango huo wakisema unaweza kuzuia ushindani wa kisiasa na kupunguza nafasi ya wapiga kura kuchagua viongozi wanaowataka. Mnamo Aprili, wabunge Millie Odhiambo, Jared Okello, Onyango Koyoo, Phelix Jalang’o na Elisha Odhiambo walipinga ugawaji wa maeneo na kutaka uteuzi wa wagombea ufanywe kwa njia huru na ya haki. “Tunaihimiza chama chetu kufanya mchujo wa kuaminika kwa sababu tukifanya hivyo hatutahitaji kuwa na wasiwasi kuhusu ugawaji wa maeneo. ODM bado itashinda viti,” akasema Bw Odhiambo. Mjadala huo pia umeenea Magharibi, ambako Naibu Gavana wa Kakamega Ayub Savula amepinga mpango wa kuzuia vyama kuwasilisha wagombea katika maeneo fulani. Alisema makubaliano ya serikali pana hayapaswi kutumiwa kuzuia ushindani wa uchaguzi. “Makubaliano ya Serikali Jumuishi hayapaswi kutafsiriwa kuwa makubaliano ya kunyima vyama vya kisiasa nafasi ya kuwasilisha wagombea. Vyama vinapaswa kushindana” akasema Bw Savula. Katika ziara ya Rais Ruto Nyanza, suala hilo pia liliibua hisia tofauti. Mbunge wa Uriri Mark Nyamita alisema viongozi wa ODM wanapaswa kuruhusiwa kushindana katika viti vyao bila kuingiliwa na makubaliano ya vyama. Kwa upande mwingine, Naibu Kiongozi wa ODM Simba Arati alitaka UDA kuachwa nje ya Nyanza, akisema eneo hilo ni ngome ya ODM.

Washirika wa Rais William Ruto wanaonekana kuwa na nafasi muhimu katika juhudi za kumuinua Naibu Rais Kithure Kindiki kuwa msemaji wa kisiasa wa eneo la Mlima Kenya. Hafla ya Jumamosi katika Uwanja wa Kirigiti, Kiambu, ilifichua vita vipya vya kutafuta ushawishi wa kisiasa katika eneo hilo kuelekea uchaguzi wa 2027. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wazee kutoka jamii za Agikuyu, Embu na Meru ilimshuhudia Profesa Kindiki akivishwa mavazi ya kitamaduni na kutangazwa kuwa msemaji wa kisiasa wa Mlima Kenya. Wawakilishi wa mashirika sita ya wazee kutoka Mlima Kenya waliidhinisha uungaji mkono kwa Rais Ruto na Profesa Kindiki, huku wakipinga juhudi za kugawanya Mlima Kenya kisiasa. Waziri wa Utumishi wa Umma, Geoffrey Ruku, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika mjadala kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa eneo hilo, alitetea hafla hiyo. Bw Ruku aliitaja kama tamko rasmi la wazee wa Mlima Kenya kumtambua Profesa Kindiki kuwa msemaji na anayeshikilia mustakabali za kisiasa za eneo hilo. Hafla hiyo pia ilionekana kufunga mjadala wa Bw Ruku wa kugawanya Mlima Kenya Mashariki na Magharibi. Kwa wiki kadhaa, waziri huyo alikuwa akitumia shoka na msumeno kuashiria wazo la kugawanya maeneo hayo kisiasa. Hata hivyo, hafla hiyo ilizua upinzani kutoka kwa baadhi ya wazee na wanasiasa ambao walipinga uhalali wake. Mlezi wa Kiama Kia Ma, Kung’u Muigai, alipinga kutawazwa kwa Profesa Kindiki huku mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Agikuyu, Wachira Kiago, akisema kundi lake halikushiriki hafla hiyo. “Wakati mwingine inafikia mahali ambapo unapaswa kujiondoa na kuwa shahidi wa yanayotokea. Nadhani hiyo ilikuwa hafla ya Kiama Kia Ma na sisi hatukuhusika,” akasema Bw Muigai. Bw Muigai alisema baadhi ya wazee waliohudhuria hafla hiyo waliwahi kumtembelea aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua nyumbani kwake Wamunyoro na kumtambua kama kiongozi wa kisiasa wa Mlima Kenya. Alisema ushiriki wao katika hafla ya Profesa Kindiki ulizua maswali iwapo walikuwa wakiendeleza maslahi ya kibinafsi. Bw Gachagua, ambaye sasa anaongoza chama cha DCP , alijitenga na hafla hiyo na kukana kuhusishwa na wazee walioiandaa. Alidai baadhi ya waliohudhuria walilipwa Sh3,000 kila mmoja, ingawa madai hayajidhibitishwa. “Hizi ni njama za kisiasa zinazolenga kuwapatia nafasi salama mawakala wawili wa kugawanya mlima ambao ni Profesa Kindiki na Bw Ruku, kwa niaba ya Rais Ruto. Lakini kwa pamoja wanapaswa kujua kuwa kura ya 2027 itakuwa wakati wa kuwawajibisha,” akasema akiwa Kansas, Amerika. Profesa Kindiki aliteuliwa kuwa Naibu Rais Novemba 1, 2024 baada ya Bw Gachagua kuondolewa mamlakani. Tangu wakati huo, amekuwa akijitokeza kama kiungo kati ya serikali ya Kenya Kwanza na jamii za Mlima Kenya, huku akisisitiza kuwa atakuwa mgombea mwenza wa Rais Ruto 2027. Hata hivyo, uongozi wake wa kisiasa katika eneo hilo unapingwa na Bw Gachagua, Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Justin Muturi, Martha Karua na viongozi wengine wa kisiasa. Mbunge wa Juja, George Koimburi na mwenzake wa Ndia, George Kariuki, pia walizua maswali kuhusu kutawazwa kwa Profesa Kindiki, wakisema hafla hiyo haikuwa halali.

VIONGOZI wa DCP wamepinga kutawazwa kwa Naibu Rais Prof Kithure Kindiki kuwa msemaji wa eneo la Mlima Kenya, wakisisitiza kuwa uongozi wa kisiasa huamuliwa na wananchi wala si wazee. Wakiongozwa na Seneta wa Nyandarua, John Methu, viongozi hao walifika Embu na kusema Kiongozi wa DCP, Rigathi Gachagua, ndiye anayetambuliwa na wananchi wa eneo hilo kama kinara wao. “Ni wakazi wa eneo hili wanaoamua nani awe kinara wao, wala si wazee. “Kindiki anapaswa kuacha kufikiria kuwa yeye ndiye kinara wetu,” akasema Bw Methu akiwa Kianjokoma, Manyatta. Mbunge wa Manyatta Gitonga Mukunji alidai kuwa Sh60 bilioni zinatumika kugawanya Mlima Kenya kisiasa ili kura za eneo hilo zisiende ‘kapu’ moja kuelekea uchaguzi wa 2027. “Hatutaruhusu hili lifanyike. Eneo letu litaendelea kuwa kitu kimoja, iwe serikali ya Kenya Kwanza inapenda au la,” akasema Bw Mukunji. Kauli zao zilijiri baada ya wazee kutoka jamii za Kikuyu, Embu, Mbeere na Meru kumuidhinisha Prof Kindiki kuwa msemaji wa eneo hilo katika hafla iliyofanyika Kirigiti, Kiambu mnamo Jumamosi. Wazee hao walimkabidhi Prof Kindiki mamlaka ya kuwakilisha maslahi ya jamii zote za Mlima Kenya na wakasisitiza umuhimu wa umoja wa eneo hilo. Prof Kindiki aliwashukuru kwa kumuamini na kuahidi kutumikia jamii zote bila ubaguzi, huku akisema hataruhusu tofauti za kisiasa kugawanya eneo hilo. Viongozi wa DCP pia walikosoa serikali kuhusu kuuawa kwa vijana wawili katika uwanja wa Nembure, Embu, wakati wa mkutano wa kisiasa uliohudhuriwa na Prof Kindiki na Gavana Cecily Mbarire. Bw Methu alitaka waliohusika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

MIPANGO ya kuzindua Ukombozi People’s Party (UPP), chama kinachotarajiwa kutumiwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna katika azma yake ya kuwania urais mwakani, imeanza kushika kasi huku uzinduzi ukitarajiwa kufanyika mapema Oktoba. Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya na Seneta wa Vihiga, Godfrey Osotsi walisema wikendi kuwa chama hicho kitazinduliwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo, huku Oktoba 3 ikitajwa kuwa tarehe inayopendekezwa kwa uzinduzi huo. Hata hivyo, viongozi hao walikataa kutoa maelezo kuhusu mahali ambapo hafla hiyo itafanyika na maafisa watakaoshikilia nyadhifa katika chama hicho kipya. Bw Osotsi aliishutumu serikali kwa kuzuia juhudi za vuguvugu la Linda Mwananchi kusajili jina la kisiasa lililopendekezwa, akisema changamoto hizo hazijawazuia viongozi wake kutafuta chama mbadala. “Mmekuwa mkiuliza chama chetu ni kipi. Wamejaribu kuchukua jina la chama chetu na kuwaweka watu wao, lakini kesi hiyo itaamuliwa Septemba 30. Tulijaribu kupata chama lakini wakaweka vikwazo,” akasema Bw Osotsi. “Hata hivyo, sisi ni wajanja na tumepata chama. Ndani ya wiki mbili tutatangaza chama ambacho Edwin Sifuna atatumia kuwania urais,” akaongeza akiwa Vihiga. Mahakama ya Migogoro ya Vyama vya Kisiasa inatarajiwa kutoa uamuzi Septemba 30 kuhusu mzozo unaohusu jina la Linda Mwananchi. Bw Natembeya pia aliwaambia wafuasi wa Bw Sifuna kuwa muda wa kusubiri chombo cha kisiasa unaelekea ukingoni. “Katika wiki tatu zijazo, tarajieni moshi mweupe na hakuna mtu atakayetuchezea tena,” akasema. Uzinduzi huo unatarajiwa kuwakutanisha viongozi wa upinzani huku vuguvugu hilo likijaribu kujenga jukwaa imara kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Viongozi kadhaa waliozungumza na Taifa Leo walikataa kutoa maelezo kuhusu hafla hiyo na badala yake wakamtaka mwandishi awasiliane na Bw Sifuna. “Sina maelezo kuhusu mahali hafla hiyo itafanyika, lakini kuna bajeti na mambo mengine yanayohusika. Wasiliana na Sifuna mwenyewe,” akasema Mbunge wa Kabuchai Majimbo Kalasinga. Duru ndani ya kambi ya upinzani zilisema waandalizi wanapanga kuwaalika wageni mashuhuri, wakiwemo baadhi kutoka nje ya Kenya. Mipango ya uzinduzi huo inafanyika wakati kukiwa na tofauti ndani ya Linda Mwananchi kuhusu chama cha kisiasa kitakachotumika katika uchaguzi wa 2027. Bw Natembeya ameunga mkono Ukombozi kutumiwa na Bw Sifuna, huku Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino akisisitiza atatumia chama chake cha Mwananchi Party na kupendekeza muungano wa vyama hivyo. Akizungumza katika mazishi yaliyofanyika Nyakach, Kaunti ya Kisumu, Ijumaa, Bw Owino alisema ataendelea kuunga mkono azma ya Bw Sifuna ya kuwania urais licha ya tofauti hizo. “Tutamsimamisha Sifuna kuwa mgombea wa urais na kuunda muungano, huku Sifuna akiwa kiongozi wa Chama cha Ukombozi na Babu akiwa kiongozi wa Chama cha Mwananchi,” akasema. Hata hivyo, Mbunge wa Saboti Caleb Amisi ameonya kuwa Linda Mwananchi huenda ikasambaratika kabla ya uchaguzi wa 2027 iwapo viongozi wake hawatamaliza tofauti zao. Bw Amisi, ambaye ameondoka katika vuguvugu hilo, aliwashutumu baadhi ya viongozi kwa kufuata maslahi yao binafsi na kudhoofisha azma ya Bw Sifuna ya kujijenga kitaifa. “Babu Owino ana mapungufu yake kama binadamu, lakini bado ni kiongozi. Na kwa kuwa tunamhitaji Sifuna ashinde, lazima umpe nafasi kwa njia bora iwezekanavyo,” alisema akizungumzia tofauti kati ya Bw Owino na Bw Sifuna kuhusu chama cha kutumika katika uchaguzi wa mwaka ujao. Bw Amisi pia alijitolea kutoa chama chake cha People’s Renaissance Movement (PRM) kiwe chombo mbadala cha Seneta Sifuna, akisema yuko tayari kurejea Linda Mwananchi iwapo waanzilishi wa awali wa vuguvugu hilo watakutana na kutatua tofauti zao. “Ninaweza kurejea Linda Mwananchi, lakini kwanza tukutane kama waanzilishi wa awali na tutafute tulikosea wapi. Sifuna bado ni kiongozi wetu na chama kiko tayari. Suala la kutafuta chama halipaswi kuwepo kwa sababu chama hiki kilianzishwa hata kabla ya Linda Mwananchi,” akasema.

Chadema's decision regarding the Justice Lila Commission was resolved during a Central Committee meeting held on August 29, 2026, in Dar es Salaam, chaired by Chadema Vice Chairperson (Mainland) John Heche.

By Henry Umoru ABUJA — The Deputy President of the Senate, Senator Barau Jibrin, APC, Kano North, has congratulated First Lady Oluremi Tinubu on her 66th birthday, praising her contributions to national development and democratic governance. Barau, who is also the First Deputy Speaker of the ECOWAS Parliament, said the First Lady’s contributions to the […]

DAR ES SALAAM: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM ambaye pia ni Mlezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kenani Kihongosi, ameitaka TARURA na uongozi wa Wilaya ya Temeke kuchukua hatua dhidi ya mkandarasi Group Six International Limited, kutokana na kutoridhishwa na utendaji wake katika ujenzi wa barabara. Kihongosi ameyasema hayo wakati…

The CBK says banks keen on paying larger dividends than those allowed by the proposed rules can overcome the constraint by raising additional funds from other parties for purposes of enhancing their cash distributions.

ARUSHA: Wakati Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na mamlaka nyingine za Serikali zikiendelea kutoa tahadhari kuhusu msimu ujao wa mvua za vuli unaotarajiwa kunyesha kati ya Oktoba na Desemba 2026 na kuambatana na hali ya El Niño katika maeneo mbalimbali nchini, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limewataka waumini wake kuchukua hatua…

KARATASI zilizotumika, chupa za plastiki, makopo na vifungashio vingine vinavyotupwa kwa pamoja mara nyingi huonekana kama taka zisizo na thamani. Lakini yamkini usilojua ni kwamba iwapo taka hizo zitatenganishwa kwa usahihi, zinaweza kubadilika zikawa vifaa vipya kabisa kwa mwanadamu huku vikitoa fursa za kipato kwa maelfu ya watu wanaoshiriki katika sekta ya uchakataji upya wa vifaa vilivyotumika (recycling). Ni kwa msingi huo ambapo mpango mpya unaolenga kuwafundisha wanafunzi kutenganisha taka kisha kuiunda taka hiyo kuwa vifaa muhimu, ulibuniwa, ukiwalenga watoto kama washiriki muhimu katika kubadilisha namna taka zinavyokusanywa na kushughulikiwa nchini. Mpango huo unalenga kuifanya shule kuwa mahali ambapo tabia ya kutenganisha taka, kutambua vifaa vinavyoweza kuchakataliwa upya/kurejelewa na kuelewa thamani ya rasilimali zilizotumika inaanza mapema. Kupitia mpango huo, unaojulikana kama Tuwezeshe, kampuni ya PAKPRO (Packaging Producer Responsibility Organisation) na Kenya Scouts Association (KSA) zinalenga kuwapa wanafunzi maarifa na ujuzi wa vitendo kuhusu usimamiaji wa taka za vifaa vya kufungia bidhaa, kama vile plastiki, karatasi, makopo na vifaa vingine vinavyoweza kuchakatwa tena. Ushirikiano huo ulizinduliwa katika Kambi ya Maskauti ya Rowallan, Nairobi, ukiwalenga watoto wenye umri wa kati ya miaka sita na 24. Sehemu muhimu ya mpango huo ni usambazaji wa mapipa 600 katika shule 150, ambapo wanafunzi watafundishwa kutenganisha taka badala ya kuzichanganya zote katika pipa moja. Lengo ni kuhakikisha kuwa vifaa vinavyoweza kurejelewa vinakusanywa kwa njia inayowezesha kupelekwa kwa wakusanyaji, vituo vya ununuzi wa taka na wachakataji walio katika sekta rasmi ya urejeleaji. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mkuu Mtendaji wa PAKPRO, Joyce Gachugi-Waweru, alisema mabadiliko ya kweli katika usimamizi wa taka yanahitaji kuanza na elimu na tabia zinazojengwa mapema. Alisema watoto wa leo ndio watakaokuwa viongozi na wafanyaji wa maamuzi katika kipindi cha miaka 20 ijayo, hivyo ni muhimu kuwafunza namna taka zinavyoweza kuwa rasilimali badala ya mzigo. “Tunataka kizazi kitakachoelewa kuwa taka si kitu cha kutupwa tu. Kuna vifaa vinavyoweza kurejelewa na kuendelea kuwa na thamani katika uchumi, ikiwa vitatenganishwa na kushughulikiwa ipasavyo,” alisema. Kwa mujibu wa PAKPRO, uchanganyaji wa taka bado ni changamoto kubwa inayopunguza ufanisi wa urejeleaji. Vifaa vinavyoweza kuchakatwa vinapochanganywa na mabaki ya chakula na taka nyingine, huwa vigumu zaidi kutenganishwa na mara nyingi hupoteza thamani yake. Mpango wa Tuwezeshe unalenga kushughulikia changamoto hiyo kuanzia katika chanzo cha taka - shuleni- kwa kuwapa wanafunzi uwezo wa kutambua, kutenganisha na kuhifadhi vifaa vinavyoweza kurejelewa. Kamishna Mkuu wa KSA, Victor Radido, alisema ushirikiano huo utawezesha maskauti kutumia mtandao wao wa shule na vikundi vya vijana kueneza maarifa kuhusu usimamizi bora wa taka. Alisema elimu hiyo haitakiwi kubaki darasani pekee, bali inapaswa kuwafikia wazazi na jamii kupitia tabia ambazo wanafunzi wataendelea nazo wakiwa nyumbani. “Tunataka watoto wetu waelewe kwamba usimamiaji taka unaanza na hatua rahisi kama kuweka karatasi, plastiki na taka nyingine katika mapipa yanayofaa. Hii ni tabia watakayoweza kuendeleza shuleni, nyumbani na katika jamii,” alisema. Washirika hao wanasema mpango huo hautahusu kuweka mapipa pekee, bali pia kuwasaidia wanafunzi kuelewa kinachotokea baada ya taka kuwekwa kwenye pipa. Hii ni pamoja na kufahamu safari ya chupa ya plastiki, karatasi au makopo kutoka shuleni hadi kwa mkusanyaji na hatimaye kwa mchakataji anayezigeuza kuwa malighafi au bidhaa mpya. Walimu pia watapewa nafasi ya kuongoza shughuli za vitendo, ikiwemo mashindano ya usafi, mafunzo ya ubunifu wa kutumia tena vifaa na ufuatiliaji wa kiasi cha taka kinachokusanywa. Hatua hizi zitasaidia shule kupima maendeleo na kudumisha mpango kwa muda mrefu zaidi. PAKPRO imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali kuimarisha mifumo ya ukusanyaji na urejeleaji wa taka za vifungashio. Shirika hilo linasema zaidi ya chupa bilioni moja za plastiki zimekusanywa kupitia mifumo ya urejeleaji inayohusishwa na juhudi zake, huku zaidi ya Sh100 milioni zikiwa zimeelekezwa katika kukuza shughuli za urejeleaji na kuwawezesha wahusika katika sekta hiyo. Sekta ya urejeleaji inahusisha maelfu ya watu, wakiwemo wakusanyaji taka, waendeshaji wa vituo vya ununuzi wa taka, wasafirishaji, waunganishaji na wachakataji. Kwao, taka zilizotenganishwa vizuri ni malighafi yenye thamani. Kwa kuwafundisha wanafunzi kutenganisha taka, mpango huo unalenga pia kuwaonyesha uhusiano kati ya tabia za kila siku na fursa za kiuchumi zinazotokana na urejeleaji. Wanafunzi watakapojifunza kutenganisha taka shuleni, wanatarajiwa kupeleka maarifa hayo nyumbani na kuwahamasisha familia zao kufuata utaratibu huo. Ushirikiano huo unatekelezwa wakati Kenya ikiendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi endelevu wa taka chini ya sheria na kanuni zinazosisitiza kupunguza taka, kutumia tena na kurejeleza vifaa vinavyoweza kurejeshwa. PAKPRO na KSA zinasema mpango wa Tuwezeshe ni hatua ya kujenga kizazi kitakachotambua kuwa thamani ya taka haimaliziki zinapotumiwa mara ya kwanza. Badala yake, kupitia utenganishaji sahihi, vifaa hivyo vinaweza kurejea katika uzalishaji, kusaidia biashara za urejeleaji na kupunguza kiasi cha taka kinachoishia kwenye jalala kama Dandora, Kayole na vingenevyo.

Russian visitors have, meanwhile, praised Zanzibar for its hospitality, safety and improving infrastructure, with some comparing the islands to the Maldives.

TAKRIBAN watu 49 wamefariki na wengine 182 wamelazwa hospitalini baada ya kushukiwa kuathiriwa na sumu kwenye pombe katika jimbo la Ondo, kusini-magharibi mwa Nigeria, Waziri wa Afya wa jimbo hilo alisema Ijumaa. Suala hilo liliripotiwa kwa mara ya kwanza Septemba 5, wakati maafisa walisema watu 29 walikuwa wamefariki ndani ya wiki ya kwanza baada ya kunywa pombe hiyo. Waziri wa Afya wa Ondo, Banji Ajaka, alisema idadi ya waliofariki ilikuwa imeongezeka hadi 49 kufikia Ijumaa. Mamlaka za Ondo zinashuku kuwa vifo hivyo vilisababishwa na sumu ya methanol iliyokuwa kwenye pombe ya kienyeji inayotengenezwa kwa njia isiyodhibitiwa na inayojulikana kwa jina la “Monkey Tail”. Tukio hilo limeangazia hatari za pombe zisizodhibitiwa ambazo bado hutumiwa kwa wingi katika baadhi ya maeneo ya Nigeria kutokana na bei yake ya chini na kupatikana kwa urahisi. Bw Ajaka alisema tukio hilo lilifuatiliwa hadi kwenye sherehe mbili za kitamaduni katika eneo la Odigbo, ambapo wageni walikunywa pombe iliyotengenezwa nchini humo. “Dalili za ugonjwa na taarifa kuhusu walichokunywa zimeibua tuhuma kubwa za kitabibu kwamba huenda waliathiriwa na pombe yenye sumu. Hata hivyo, bado hatujapata ushahidi wa maabara,” alisema Bw Ajaka katika taarifa. Waathiriwa waliripoti dalili mbalimbali zikiwemo maumivu ya kichwa, maumivu ya mwili, matatizo ya kupumua, kupoteza fahamu. Bw Ajaka alisema madhara hayo yalijitokeza kwa kasi baada ya watu kutumia pombe hiyo. “Jambo hili lilitokea haraka. Unapokunywa, kutegemea kiwango ulichotumia, figo zinaweza kushindwa kufanya kazi, macho kupoteza uwezo wa kuona na ubongo kuharibika,” alisema. Methanol ni aina ya sumu ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa mwilini inapomezwa.

WADAU wa elimu pamoja na viongozi wa utawala katika Kaunti Ndogo ya Webuye Mashariki, Kaunti ya Bungoma, juzi walifanya mkutano wa dharura kufuatia ongezeko kubwa la mimba za mapema katika shule moja ya eneo hilo. Wanafunzi wasiopungua 36 wa Shule ya Sekondari ya Bakisa wamekuwa wajawazito au wameacha masomo mwaka huu baada ya kupata watoto. Kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa na uongozi wa shule hiyo, wanafunzi 10 kwa sasa ni wajawazito na bado wanaendelea na masomo yao huku wakikabiliana na changamoto za ujauzito. Wengine 13 walijifungua majuzi, huku wanafunzi 13 zaidi wakiacha shule kabisa baada ya kupata mimba. Mkutano huo uliofanyika Ndivisi uliwaleta pamoja maafisa wa usalama, viongozi wa elimu, wazazi, viongozi wa kidini na wanasiasa ili kutafuta suluhu za haraka za kukabili tatizo hilo. Akizungumza katika mkutano huo, Naibu Kamishna wa Kaunti wa Ndivisi, Emmanuel Kenga, alisema umaskini uliokithiri na uzembe wa baadhi ya wazazi ni miongoni mwa sababu kuu zinazochangia kuongezeka kwa mimba za mapema. Alisema kuna wanaume wanaowalenga wasichana wadogo kwa kuwapa chakula, zawadi ndogo na fedha ili kushawishi kushiriki ngono. “Umaskini unachangia sana tatizo hili. Baadhi ya wanaume wanatumia udhaifu wa wasichana wetu kwa kuwavutia kwa pesa na mahitaji ya msingi,” alisema Kenga. Aidha, alitaja matumizi yasiyodhibitiwa ya simu za mkononi na teknolojia kama sababu nyingine inayowafanya watoto kukumbana na maudhui yasiyofaa katika umri mdogo. Baadhi ya wazazi waliodhuria mkutano huo walidai kwamba wasichana wengi hushawishiwa na wanaume wanapokuwa njiani kuelekea au wakitoka shuleni. Wengine walilaumu hali ya watoto kulelewa na babu na nyanya huku wazazi wao wakitafuta ajira mijini. Viongozi wa utawala walifichua kuwa baadhi ya familia hukubali fidia kutoka kwa wanaodaiwa kuwapa mimba watoto wao badala ya kuripoti kesi hizo ili hatua za kisheria zichukuliwe. Inadaiwa kwamba kesi nyingi hutatuliwa kupitia mikutano ya kijamii au baraza za wazee kwa makubaliano ya kifedha. Mwalimu Margaret Muindi aliwataka wazazi kukoma kupokea zawadi au fedha kutoka kwa wahusika wa vitendo hivyo kwa kuwa hatua hiyo huathiri juhudi za kupata haki kwa waathiriwa. Naye Nancy Chibeu, alionyesha masikitiko yake akisema kuwa licha ya wanafunzi 36 kuathiriwa, ni kesi moja pekee ambayo imeripotiwa rasmi. Alitoa wito kwa wananchi kuwafichua wahusika ili wachukuliwe hatua za kisheria na wasichana walindwe dhidi ya unyanyasaji wa kingono.

BAADA ya chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP) kinachoongozwa na Rigathi Gachagua kushinda uchaguzi mdogo wa Ol Kalou mnamo Julai 2026, viongozi wengi waliokuwa wakimuunga mkono Rais William Ruto walianza kuonyesha nia ya kuhamia upande wa Gachagua. Katika uchaguzi huo, mgombea wa DCP Kamau Ngotho alipata kura 35,440 dhidi ya kura 5,450 za mgombea wa UDA Muchina Nyagah. Ushindi huo mkubwa ulitafsiriwa kama ishara kwamba eneo la Mlima Kenya lilikuwa likibadili msimamo wake wa kisiasa. Kutokana na wimbi hilo la viongozi waliotaka kuhamia DCP, Gachagua alitangaza kuwa chama chake kingepokea wanachama wapya lakini wale waliokuwa washirika wa karibu wa Rais Ruto wangepitia mchujo mkali kabla ya kukubaliwa. Hatua hiyo ilifuatia shinikizo kutoka kwa viongozi wa DCP waliokuwa na wasiwasi kuwa baadhi ya wanasiasa hao walitaka kuingia chamani ili kukidhoofisha kutoka ndani. Viongozi hao walikumbushwa jinsi baadhi yao walivyoshiriki kampeni dhidi ya Gachagua na DCP. Mnamo Agosti 2, 2026, Gachagua alitangaza kuundwa kwa kamati ya watu saba kuchunguza maombi ya viongozi waliotaka kuhama kutoka UDA kwenda DCP. Kamati hiyo ilijumuisha Maseneta John Methu, Joe Nyutu na Karungo Thang’wa pamoja na wabunge na viongozi wengine wa chama. Hata hivyo, mpango huo haukudumu. Wanachama wa DCP waliibua malalamiko wakitaka wanaotaka kujiunga na chama wapimwe hadharani katika mikutano ya kisiasa badala ya kuhojiwa kwa siri. Hali hiyo ilifanya kamati ya uchunguzi ishindwe kuanza kazi rasmi. Mbunge wa Gatundu Kusini Gabriel Kagombe alikuwa miongoni mwa walioathiriwa na mfumo huo mpya. Alimuomba Gachagua msamaha hadharani na kutangaza kwamba amechoka na Rais Ruto. Lakini aliporuhusiwa kuhutubia mikutano ya DCP katika maeneo mbalimbali, wananchi walimzomea na kukataa kumpokea. Kilichompata Kagombe kilituma ujumbe kwa viongozi wengine waliotaka kuhama. Wengi waliogopa aibu ya kukataliwa mbele ya umma na hivyo wakaamua kubaki katika UDA au kutafuta vyama vingine. Aliyekuwa mwenyekiti wa Kampuni ya Mbegu Kenya, Wangui Ngirichi, pia alikabiliwa na hali ngumu alipojaribu kujiunga na DCP. Mikutano aliyohudhuria iligeuka kuwa ya vurugu huku wafuasi wake wakikabiliana na wale wa DCP, hali iliyosababisha majeraha na kifo cha mtu mmoja. Kwa sasa, viongozi wa DCP wanasema kanuni za uchunguzi bado zipo, lakini hakuna aliyewasilisha rasmi ombi la kuchunguzwa. Hivyo basi, kamati iliyoundwa na Gachagua imebaki bila kazi. Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa mpango wa kuwachuja wafuasi wa Rais Ruto uliporomoka kutokana na upinzani wa wanachama wa DCP wenyewe. Badala ya mchakato rasmi wa uchunguzi, wanachama waliamua kuwa wapiga kura katika mikutano ya hadhara ndio wawe waamuzi wa mwisho kuhusu nani anafaa kupokelewa katika chama hicho. Matokeo yake ni kwamba viongozi wengi waliokuwa wakipanga kuhamia DCP wameendelea kusalia katika UDA au wanasaka majukwaa mengine ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

KIONGOZI wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM), Dkt Oburu Oginga, bado yuko nchini Uingereza akipokea matibabu huku familia yake ikisema hali yake imeimarika lakini bado hajaruhusiwa na madaktari kurejea nchini. Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Kisumu, Ruth Odinga, ambaye ni dadake mdogo, alisema mwanasiasa huyo mkongwe anaendelea kufuatiliwa na madaktari na familia haijafanya mipango yoyote ya haraka ya kumrejesha nyumbani. Kwa mujibu wa Bi Odinga, jambo la msingi kwa sasa ni kuruhusu madaktari kukamilisha kukagua afya yake kabla ya uamuzi wowote kufanywa kuhusu safari yake ya kurejea Kenya. “Ameimarika sana, lakini hatujapanga kurejea kwake Kenya kwa sasa,” alisema Bi Odinga akiwa Uingereza. Aliongeza kuwa familia haina haraka ya kumrejesha nchini kwa kuwa bado ana miadi kadhaa ya matabibu ambayo lazima ahudhurie. Bi Odinga alifafanua kuwa Dkt Oginga hajalazwa hospitalini kwa sasa. Badala yake, anaishi karibu na hospitali anayohudumiwa ili iwe rahisi kuhudhuria ukaguzi na miadi ya madaktari. “Hajalazwa. Tunaishi karibu na hospitali, kwa hivyo ni rahisi kwake kuonana na madaktari wakati wowote anapohitajika,” alisema. Familia hiyo imesisitiza kuwa afya ya mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 83 ni muhimu zaidi kuliko majukumu yake ya kisiasa. Kwa sababu hiyo, hawataki kuharakisha kurejea kwake kabla madaktari kuthibitisha kuwa yuko katika hali nzuri. Habari hizo zinajiri huku Dkt Oginga akiendelea kushiriki shughuli mbalimbali kwa njia ya mtandao akiwa Uingereza. Wiki hii alichapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii akieleza kuwa yeye na mkewe, Mama Judy, walimpokea Balozi wa Kenya nchini Uingereza, Maurice Makoloo, katika makazi yao. Alisema walijadili jinsi ya kuimarisha uhusiano kati ya Kenya na Uingereza, kusaidia Wakenya wanaoishi ughaibuni pamoja na kuchangia maendeleo ya taifa kupitia uwekezaji na ujuzi wao.

Tension that had simmered for months within the All Progressives Congress, APC, and the immediate circle of President Bola Tinubu has finally spilled into full public view, setting the Minister of the Federal Capital Territory FCT, Nyesom Wike, against a bloc of governors elected on the party’s ticket, and raising hard questions about how the president plans to keep his disciples intact heading into the 2027 election. Where each side stands

NYOTA ya kisiasa inaonekana imeanza kumng’aria Raila Jnr, mwanawe marehemu Waziri Mkuu Raila Odinga akionekana kujitosa kwenye siasa mzimamzima kwa kuungana na Rais William Ruto katika ziara ya siku tano eneo la Nyanza. Raila Jnr aliandamana na Rais Ruto alipoanza ziara yake Kaunti ya Kisumu, akaenda naye katika Kaunti ya Siaya kisha akafululiza na kiongozi wa nchi hadi Kaunti ya Migori. Ni mkutano wa Kaunti ya Homa Bay, siku ya mwisho ya ziara ya Rais mnamo Alhamisi ndiyo alikosa kwa sababu familia ilikuwa ikizindua kamati ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha ‘Baba’ Nairobi. Hadhi ya Raila Jnr ilionekana kuwa juu wakati wa mkutano wa viongozi waliochaguliwa katika eneo la Luo Nyanza mnamo Jumapili kwenye ikulu ya Kisumu. Baada ya wabunge na maseneta kutoka kaunti zote nne kutambulishwa, Kiongozi wa wachache Junet Mohamed alimwalika Raila Jnr ahutubu. Hii inaweza kufasiriwa kuwa huenda alipewa hadhi ya juu kwa kuwa baada ya kumaliza hotuba yake, Bw Mohamed aliwaalika magavana kisha Rais akapewa nafasi ya kuongea. “Mheshimiwa karibu sana Kisumu na mimi kama kijana wa baba nasema kuwa mlikuwa na ndoto sawa na Raila si kwa eneo la Nyanza pekee bali pia Kenya mzima,” akasema Jnr huku akishangiliwa na umati ambao ulisikika ukisema ‘wewe ndiye baba aliyebaki’. “Watu wetu kile ningependa kuwaambia ni kwamba Baba alituambia tukae pamoja na tufanye hivyo kwa kusalia ndani ya ODM,” akaongeza akiwa ameandamana na shangazi yake Tabby Osewe. Mnamo Jumatatu, Jnr aliandamana na Rais Ruto katika kufungua miradi mbalimbali katika Kaunti ya Kisumu ikiwemo barabara ya Chiga-Rabuor na miradi mingine katika eneobunge la Muhoroni. Familia ya Baba yaunga Ruto Mnamo Jumanne, Junior aliandamana na Rais katika kutathmini na kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo daraja la Dho Goye, kukagua uwanja wa Jaramogi mjini Siaya miongoni mwa miradi mingine. “Mheshimiwa Rais nakukaribisha hapa Siaya na nina kuku ambaye Mama Ida amenipa nikupee. Hapa sisi tunakuunga mkono kupitia chama cha ODM na kama familia ya baba tuko nawe hadi 2027,” akasema. “Huku ni nyumbani, mimi na ami yangu Dkt Oburu Oginga tunakuunga. Kama watu wa Siaya endelea kutuhudumia na miradi ijae huku kwa sababu tuko nawe hadi mwisho,” akasema baada ya kualikwa na Rais. Ziara ya Migori nayo ilionekana kusisimua zaidi kwa sababu Jnr alishangiliwa huku akisema ana ndoto ya kisiasa ya babake ambayo lazima ayatimize. “Mimi pia ni Raila na baba aliacha chama kikubwa na si cha wazee pekee bali watu wote. Kwa sasa tuko ndani ya Serikali Jumuishi na hata eneo letu pia nalo lazima liendelee,” akasema akiwa Migori. Kwenye mahojiano na Taifa Leo baada ya ziara hiyo ya Nyanza, Jnr alisema kuwa analenga kutia bidii katika siasa na kujitafutia umaarufu badala ya kutumia jina la familia. “Siwezi kuketi tu kwa sababu mimi ni mwana wa Raila, lazima pia nionyeshe juhudi na kujifunza kutoka kwa wanasiasa wazoefu ambao watanishika mkono. Mimi pia sasa ni mwanasiasa,” akasema akisisitiza kuwa pia ataendeleza kampeni yake katika eneobunge la Kibra. Analenga kumbandua mbunge wa sasa Peter Orero ambaye alikuwa mwandani wa marehemu babake na anahudumu muhula wake wa kwanza. Aliyekuwa mbunge Imran Okoth pia anasaka kiti hicho Jnr, 46, akiingia bungeni mwaka ujao, atakuwa anafanya hivyo kwa umri sawa na alivyofanya babake mnamo 1992. Marehemu Raila alichaguliwa mbunge wa Langata kupitia Ford Kenya huku babake akiwahi nafasi kama hiyo kule Bondo. Kwa mujibu wa mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Javas Bigambo, ni wazi Rais Ruto ameamua kumshika Jnr mkono na kumtambisha baada ya dadake Winnie kutoonekana kujihusisha sana na masuala ya uongozi. “Winnie ni mbunge wa EALA na hata mwanzoni alionekana kujihusisha sana kisiasa kuliko Jnr. Hata hivyo, Jnr ameonyesha wazi yuko tayari kushikwa mikono na kufanya kazi na Rais,’’ akasema Bigambo “Baada ya kuidhinishwa na Mama Ida awanie kiti cha ubunge wa Kibra, inaonekana ameamua kujitosa mzimamzima katika siasa na kupigania nafasi yake. Yupo pazuri kuwa mrithi wa siasa za ufalme wa Jaramogi,” akaongeza.

RAIS wa Uganda Yoweri Museveni amesema nchi yake ilisitisha ununuzi wa mafuta kupitia Kenya baada ya kugundua kile alichokitaja kuwa udanganyifu uliokuwa ukiigharimu mabilioni ya shilingi kupitia mabroka. Akizungumza nchini Uganda, Museveni alisema mpango uliokuwa ukitumika haukuwa wa serikali kwa serikali (G2G) kama ulivyowasilishwa, bali ulikuwa mpango wa “serikali kwa mabroka”, ambapo Uganda ilinunua bidhaa za petroli kupitia mawakala waliokuwa wakinufaika kwa gharama ya walipa ushuru. Uganda, ambayo haina bandari ya bahari, kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea Bandari ya Mombasa na mtandao wa mabomba ya mafuta wa Kenya kuagiza mafuta yake. “Kulikuwa na mawakala nchini Kenya waliokuwa wakiuzia Uganda mafuta. Hii ilikuwa janga kubwa. Sikujua hadi nilipoelezwa na seneta mmoja kutoka Kenya,” alisema Museveni. Kulingana na rais huyo, alipopewa taarifa hizo aliwaagiza maafisa wake wa nishati kuchunguza suala hilo lakini hatua za haraka hazikuchukuliwa. Hata hivyo, baada ya uchunguzi zaidi, Uganda ilibadili mfumo wake wa ununuzi wa mafuta. Kwa sasa Uganda inaagiza mafuta kupitia ushirikiano kati ya Kampuni ya Kitaifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na kampuni ya Vitol, kufuatia mabadiliko ya sera yaliyofanywa mnamo 2023. Museveni alisema hatua hiyo imepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za mafuta. Kulingana na takwimu zilizotolewa na Katibu wa Wizara ya Nishati nchini Uganda, Irene Batebe, Uganda ilikuwa ikilipa wastani wa Sh15,340 kwa tani moja ya dizeli chini ya mfumo wa zamani, ikilinganishwa na Sh10,790 chini ya mfumo wa sasa. Kwa petroli, gharama ilishuka kutoka Sh12,675 kwa tani moja hadi Sh7,995, huku gharama ya mafuta ya ndege ikishuka kutoka Sh14,853 hadi Sh10,303 kwa tani moja. Aidha, serikali ya Rais William Ruto ilieleza kuwa mpango wa serikali kwa serikali (G2G) ulianzishwa mnamo 2023 ili kupunguza shinikizo la fedha za kigeni nchini. Serikali ilisema sekta ya mafuta ilikuwa ikihitaji karibu Sh64.7 bilioni kwa mwezi fedha za kigeni kwa ajili ya uagizaji wa mafuta, hali ambayo ilikuwa ikitishia akiba ya fedha za kigeni na usalama wa nishati nchini. “Sitasahau takwimu hizo. Zinathibitisha jinsi tulivyokuwa tukipunjwa kwa miaka mingi,” alisema Museveni. Kauli yake imezua mjadala mkubwa nchini Kenya, hasa kutokana na jinsi serikali ya Rais William Ruto ilivyokuwa imewasilisha mpango wa G2G kama suluhu ya kupunguza shinikizo la fedha za kigeni na kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini. Hata hivyo, msemaji wa serikali ya Kenya Charles Owino alijibu kwa njia ya kidiplomasia akisema uhusiano kati ya Kenya na Uganda unaendelea kuwa mzuri. “Tuna uhusiano mzuri wa kikazi na Uganda. Tunaendelea kushirikiana katika miradi mbalimbali ya miundombinu ya mafuta,” alisema Owino. Wakati huo huo, aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ameunga mkono madai ya Museveni akisisitiza kuwa mpango huo uliwanufaisha watu binafsi badala ya serikali ya Kenya. Akizungumza katika mkutano nchini Amerika, Gachagua alidai kuwa biashara ya mafuta ni ya thamani ya mabilioni ya pesa na kwamba wanaonufaika ni watu walio ndani ya utawala wa Kenya Kwanza. Kwa upande wake, mshauri wa rais wa masuala ya uchumi David Ndii alipinga madai hayo kupitia mtandao wa X, akisema kampuni zinazouzia Kenya mafuta zinamilikiwa na serikali husika, huku kampuni inayouzia Uganda ikiwa ya kibinafsi. Mjadala huo umeendelea kuibua maswali kuhusu uwazi katika biashara ya mafuta na iwapo mfumo wa G2G uliokuwa ukitumika uliwanufaisha wananchi au mawakala. Licha ya mvutano huo wa kisiasa, Kenya na Uganda zinaendelea kutegemeana kiuchumi, hasa katika sekta za biashara, usafirishaji na nishati, huku wadadisi wakisubiri kuona iwapo madai ya Museveni yatachochea uchunguzi zaidi kuhusu biashara ya mafuta katika eneo la Afrika Mashariki.

Managing Director/Chief Executive Officer of JustOne Homes Ltd, Taiwo Idowu, has warned that fraud, inadequate property verification and the activities of unqualified operators are threatening confidence in the country’s real estate sector. Idowu raised the concern at the unveiling ceremony of the company’s latest initiative, which was attended by industry stakeholders. He said the increasing […]

Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula ameongeza juhudi za kuimarisha uungwaji mkono kwa Rais William Ruto huku akimtaka kiongozi wa chama cha Democratic Action Party of Kenya (DAP-K), Eugene Wamalwa, kuondoka katika muungano wa upinzani na kujiunga na serikali ya Kenya Kwanza. Akizungumza katika mikutano tofauti Magharibi mwa Kenya, Wetang’ula alisema Wamalwa anafaa kutathmini upya msimamo wake wa kisiasa na kushirikiana na serikali kwa maslahi ya wananchi. Alidai kuwa viongozi wa muungano anaouunga mkono kwa sasa wanaweza kumsaliti kisiasa. “Muungano ambao ndugu yangu mdogo Eugene Wamalwa anaunga mkono kwa sasa utamwangusha kisiasa. Nafasi yake ni kufanya kazi pamoja na serikali kwa maendeleo ya wananchi,” alisema Wetang’ula. Wakati huohuo, Spika huyo alimkosoa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, akimtaka kuheshimu hadhi yake ya kiongozi mstaafu na kupatia serikali ya Rais Ruto nafasi ya kuongoza nchi bila kuingiliwa. Akizungumza katika hafla ya kuwawezesha waendesha bodaboda katika shule ya Ojaamong’ Comprehensive, Kaunti ya Busia, Wetang’ula alisema marais waliostaafu nchini wamekuwa wakitoa nafasi kwa warithi wao kuongoza bila kuwakosoa hadharani. “Nimehudumu serikalini tangu enzi za Rais Moi na baadaye Rais Kibaki, lakini sijawahi kuona rais mstaafu akimshambulia hadharani aliye mamlakani,” alisema. Wetang’ula alimtaka Kenyatta kujikita katika majukumu yake kama rais mstaafu na mwakilishi wa Kenya katika Muungano wa Afrika (AU), akisema nafasi hiyo inahitaji uzalendo na ushirikiano na serikali iliyoko madarakani. Aidha, Spika huyo alitetea azma ya Rais Ruto kutafuta muhula wa pili mwaka 2027, akisema uchaguzi huo unapaswa kuamuliwa kwa msingi wa maendeleo yaliyotekelezwa na serikali. Alitaja miradi ya barabara, nyumba za bei nafuu, kilimo, umeme na unyunyuzaji kama baadhi ya mafanikio ambayo wapigakura wanapaswa kuzingatia. Katika Kaunti ya Busia, Wetang’ula alisifia miradi kama Eneo la Kuchakata Bidhaa za Mauzo ya Nje la Busibwabo na Mradi wa Unyunyuzaji wa Bunyala, akisema itatoa nafasi za ajira na kuchochea uchumi wa eneo hilo. Akiwa katika mazishi katika Eneo Bunge la Saboti, Kaunti ya Trans Nzoia, Spika huyo aliendelea kutetea juhudi za Rais Ruto za kutaka muhula wa pili, akisema viongozi waliomtangulia walihudumu kwa zaidi ya muhula mmoja bila kuzuiwa kisiasa. Pia aliwataka viongozi kuachana na siasa za matusi na badala yake kuzingatia maendeleo ya wananchi, akisisitiza kuwa tofauti za kisiasa hazipaswi kuzuia utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Kauli za Wetang’ula zinajiri viongozi wa Kenya Kwanza wakizidisha kampeni za kuimarisha uungwaji mkono wa Rais Ruto katika maeneo mbalimbali nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Before the Court of Appeal, Dr Kajigili raised 10 grounds challenging the High Court decision, arguing that there were errors in the process used to take disciplinary action against him.

DAR ES SALAAM; Wadau wa michezo nchini wametakiwa kusubiri ripoti ya Kamati ya Uchunguzi itakayoundwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, kuhusu mkataba wa jezi za timu za Taifa, badala ya kuanza kuzua taharuki kwamba hatua hiyo ni kuingilia shughuli za uendeshaji mpira wa miguu. Akizungumza na DailyNews Digital, kiongozi wa…