NAIBU Rais Kithure Kindiki amewataka viongozi wa Mlima Kenya kuwaheshimu wazee na kusikiza wito wao wa umoja, akisema tofauti za kisiasa hazifai kuruhusiwa kuvunja jamii ambayo imeshirikiana kwa miaka mingi.
Profesa Kindiki alisema amezingatia kwa uzito wito wa wazee wa kuongoza juhudi za maridhiano na umoja katika eneo hilo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Alisema ataheshimu mwongozo wa wazee anapozifikia jamii za Mlima Kenya Mashariki na Magharibi katika juhudi za kujenga umoja wa kisiasa.
Naibu Rais alisema hayo siku chache baada ya wazee wa Mlima Kenya kukutana katika Uwanja wa Kirigiti, Kaunti ya Kiambu, na kumtawaza kama kigogo wa siasa za eneo hilo.
Wazee hao walitoa wito wa umoja miongoni mwa jamii za Agikuyu, Embu, Ameru na Mbeere na kuwataka wakazi wa eneo hilo kubaki na umoja wa kisiasa kuelekea uchaguzi wa 2027.
Pia walionyesha kuunga mkono utawala wa Rais William Ruto, hivyo kumpa Profesa Kindiki jukwaa jipya la kuhakikisha eneo hilo linamuunga mkono Rais.
Profesa Kindiki alisema viongozi wanapaswa kuheshimu tofauti za kisiasa lakini wasizigeuze kuwa migawanyiko inayolemaza eneo hilo kimaendeleo.
Amekuwa akipinga juhudi za kugawanya Mlima Kenya kwa misingi ya Mashariki na Magharibi, akisema jamii hizo zina uhusiano mkubwa wa kihistoria, kitamaduni na kiuchumi kuliko tofauti zao za kisiasa.
Wito huo unakuja wakati siasa zikizidi kushika kasi katika eneo hilo, huku makundi hasimu yakitafuta kushawishi mwelekeo wa kisiasa wa eneo hilo kuelekea 2027.
Profesa Kindiki alisisitiza atatekeleza maagizo ya wazee kwa kupitia ziara za maendeleo katika Mlima Kenya Mashariki na Magharibi.
Baada ya mkutano wa Kirigiti, alikagua ujenzi wa Barabara ya Mukothima-Gaciongo-Gatunga katika eneobunge la Tharaka, Kaunti ya Tharaka Nithi, kabla ya kuhutubia wakazi katika Soko la Gaciongo wakati wa mkutano wa umma.
Naibu Rais ameweka barabara, miundombinu na utekelezaji wa mipango ya Serikali kuwa nguzo kuu za ziara zake, akisema uongozi wa kisiasa unapaswa kulenga kuboresha maisha ya wananchi.
Wazee wa Kirigiti waliwataka jamii za Mlima Kenya kuwa na msimamo wa pamoja kuhusu masuala yanayoligusa eneo hilo na kukataa juhudi za kuunda makundi tofauti ya kisiasa.
Mnafaa kuheshimu wazee walionitawaza, Kindiki aambia wakosoaji

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]