TAKRIBAN watu 49 wamefariki na wengine 182 wamelazwa hospitalini baada ya kushukiwa kuathiriwa na sumu kwenye pombe katika jimbo la Ondo, kusini-magharibi mwa Nigeria, Waziri wa Afya wa jimbo hilo alisema Ijumaa.
Suala hilo liliripotiwa kwa mara ya kwanza Septemba 5, wakati maafisa walisema watu 29 walikuwa wamefariki ndani ya wiki ya kwanza baada ya kunywa pombe hiyo.
Waziri wa Afya wa Ondo, Banji Ajaka, alisema idadi ya waliofariki ilikuwa imeongezeka hadi 49 kufikia Ijumaa.
Mamlaka za Ondo zinashuku kuwa vifo hivyo vilisababishwa na sumu ya methanol iliyokuwa kwenye pombe ya kienyeji inayotengenezwa kwa njia isiyodhibitiwa na inayojulikana kwa jina la “Monkey Tail”.
Tukio hilo limeangazia hatari za pombe zisizodhibitiwa ambazo bado hutumiwa kwa wingi katika baadhi ya maeneo ya Nigeria kutokana na bei yake ya chini na kupatikana kwa urahisi.
Bw Ajaka alisema tukio hilo lilifuatiliwa hadi kwenye sherehe mbili za kitamaduni katika eneo la Odigbo, ambapo wageni walikunywa pombe iliyotengenezwa nchini humo.
“Dalili za ugonjwa na taarifa kuhusu walichokunywa zimeibua tuhuma kubwa za kitabibu kwamba huenda waliathiriwa na pombe yenye sumu. Hata hivyo, bado hatujapata ushahidi wa maabara,” alisema Bw Ajaka katika taarifa.
Waathiriwa waliripoti dalili mbalimbali zikiwemo maumivu ya kichwa, maumivu ya mwili, matatizo ya kupumua, kupoteza fahamu.
Bw Ajaka alisema madhara hayo yalijitokeza kwa kasi baada ya watu kutumia pombe hiyo.
“Jambo hili lilitokea haraka. Unapokunywa, kutegemea kiwango ulichotumia, figo zinaweza kushindwa kufanya kazi, macho kupoteza uwezo wa kuona na ubongo kuharibika,” alisema.
Methanol ni aina ya sumu ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa mwilini inapomezwa.
Watu 49 wafariki Nigeria baada ya kunywa pombe yenye sumu

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsAfenifere demands prosecution of sponsors of campaign violence
…Raises alarm over rising attacks ahead of 2027 elections By Adeola Badru The pan-Yoruba socio-political organisation, Afenifere, has raised the alarm over increasing political violence ahead of the 2027 general elections, calling for the arrest and prosecution of perpetrators and their sponsors. The organisation warned that the growing incidents of thuggery, intimidation and inflammatory political […]
NewsPHOTOS: First Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsFirst Lady calls for continued investment in children at UNICEF anniversary
First Lady Jeannette Kagame has called for sustained investment in the education, healthcare opportunities for children to ensure no one is left behind due to poverty, disability,...
NewsObi woos Onitsha voters, promises jobs, better services
…Says Nigeria needs energetic president By Vincent Ujumadu The presidential candidate of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Peter Obi, on Friday drew a large crowd in Onitsha, Anambra State, as he led members of his campaign team on a roadshow and town hall meeting in the commercial city. Obi began his visit with a stop […]