Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.
RAIS SAMIA: "MKIKAZA HAKUNA PANYAROADI WALA MAKUNDI YA UASI" - ATUMA UJUMBE KWA POLISI JAMII... Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, azungumzia wajibu mkubwa wa…
MBEYA; SERIKALI imetoa vifaa vya ujenzi wa barabara kwa ajili ya maandalizi ya kukabiliana na mvua za El Niño mkoani Mbeya. Vifaa hivyo,ambavyo ni makaravati ya chuma vitatumika katika barabara kuu sita zinazounganisha Mkoa wa Mbeya na mikoa jirani. Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mbeya,…
KIGOMA: Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele amewahimiza vijana wa Kitanzania kutumia mitandao ya kijamii kwa uangalifu na kuwasilisha ujumbe wenye manufaa kwa jamii na taifa. Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Mujibu wa Sheria kupitia “Operesheni Linda Amani” na vijana…
KWA Said Faiz Khamis, 29, safari ya kawaida ya bodaboda usiku iligeuka kuwa jinamizi baada ya kushambuliwa kwa mapanga na kujeruhiwa kwenye kichwa na vidole. Mkazi huyo wa Maweni alisema mnamo Septemba 15, saa tano usiku, abiria mmoja alimuomba ampeleke nyumbani kwake eneo la Barsheba, Kisauni. Bw Khamis alimweleza abiria huyo kuwa angemfikisha steji na hangeingia kwenye kitongoji. Hata hivyo alipomfikisha kwenye steji, abiria alimuomba amfikishe nyumbani kwake, mita chache kutoka steji. Hata hivyo, alipomfikisha genge la majambazi waliokuwa na silaha walijitokeza na kumvamia. “Niligundua kuwa abiria alikuwa amepanga watu waliokuwa wanasubiri kunishambulia kwa mapanga. Niliponea chupu chupu na kutoroka lakini nilikuwa nimekatwa katwa kichwani na kwenye vidole. Nilihepa na funguo za pikipiki yangu kwa kutumia vichochoro,” alisema. Kupitia msaada wa waendesha bodaboda wenzake, alipata pikipiki hiyo katika kituo cha polisi cha Kiembeni mnamo Septemba 17. Hata hivyo, hii haikuwa mara yake ya kwanza kushambuliwa. Mapema mwaka huu, mwendo wa saa tisa usiku, Bw Khamis alisema alikuwa akimpeleka abiria katika Soko la Kongowea alipovamiwa na vijana waliokuwa kwenye pikipiki. “Walinipiga kichwani na kunikata kata na kuninyang’anya pikipiki yangu, simu na kila kitu nilichokuwa nacho kilienda. Walimuibia abiria wangu pesa zote ambazo alikuwa anaenda nazo Kongowea kununua bidhaa za biashara,” alisema. Baada ya kutafuta fedha na kununua pikipiki nyingine, alirejea kazini. Hata hivyo, baada ya kujeruhiwa kwa mara ya pili amemua kuacha kazi hiyo. “Sasa nimeamua kuacha hii kazi. Kichwa changu kimekatwa vibaya mara mbili. Hii kazi ni hatari sana na nina bahati niko hai,” alisema. Visa hivyo vimeibua hofu mpya kuhusu mashambulizi ya usiku katika maeneo ya Kisauni huku wakazi na wahudumu wa bodaboda wakidai magenge ya vijana wenye silaha butu yanaendelea kuwahangaisha wakazi. Mwenyekiti wa kamati ya usalama ya jamii ya Maweni na dereva wa bodaboda, Bw Samson Omondi, alidai kuwa magenge hayo wakati mwingine hutumia wanawake kama chambo. “Wanawake huwafuata waendesha bodaboda kwenye steji wakitaka huduma zetu. Wanapofikishwa waendako, abiria huchelewesha malipo kwa M-Pesa au kupiga simu, kumbe ni njama ya kuwapa muda washirika wao kujitokeza kutushambulia,” alisema. Bw Omondi aliwataka maafisa wa polisi kuimarisha operesheni na kuwakamata wanaohusika, akisema baadhi yao wanajulikana na jamii. Vikundi vya kutetea haki za binadamu pia vimeitaka serikali kuchukua hatua ya kuimarisha usalama. Mratibu wa Vocal Africa Pwani, Wild Sketty, alisema shirika hilo limeorodhesha watu wanane waliodaiwa kushambuliwa kwa mapanga kati ya saa nne usiku na saa kumi na mbili asubuhi ndani ya wiki moja Kisauni. Hata hivyo, Naibu Kamishna wa Kaunti ya Kisauni, Bw Jamleck Mbuba, aliwatuliza wakazi akisema polisi tayari wamewakamata baadhi ya washukiwa na wanaendelea kuwasaka wengine. “Tutawakamata wanaojificha. Tupeni muda, lakini mtusaidie kwa kutoa taarifa ili tuwatambue wahalifu walioko miongoni mwenu,” alisema.
TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeanza kupanga upya uongozi wake katika kaunti kwa kuwahamisha zaidi ya maafisa 20 wakuu wa uchaguzi katika maeneo mbalimbali nchini, huku maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2027 yakishika kasi. Uhamisho huo uliotangazwa katika barua iliyotiwa saini na Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa IEBC Ruth Kulundu. IEBC imesema mabadiliko hayo ni sehemu ya zoezi la kawaida la kiutawala la kujaza nafasi zilizo wazi, kuwaweka maafisa waliopandishwa vyeo katika vituo vipya na kuimarisha utendaji wa tume mashinani. Mabadiliko hayo yanajiri siku chache baada ya IEBC kutangaza Jumanne, Agosti 10, 2027 kuwa siku ya kupiga kura. Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon amepuuza madai kwamba uhamisho huo umechochewa na siasa au una uhusiano na uadilifu wa maafisa wanaohusika. Alisema ni utaratibu wa kawaida baada ya tume kuajiri maafisa wapya kuchukua nafasi za waliostaafu, waliofariki au walioondoka kazini. “Tumeajiri maafisa wapya wa uchaguzi wa kaunti. Hiyo inamaanisha lazima wapangwe upya na kupelekwa katika vituo vipya,” Bw Ethekon alisema katika mahojiano na Taifa Leo. Alisema takriban maafisa 17 wameajiriwa na kupandishwa vyeo, hivyo kuhitajika kupelekwa katika kaunti mbalimbali. “Kuna waliostaafu, wengine walifariki na wengine wakaondoka. Kwa hivyo wako takriban 17 ambao tumeajiri,” alisema. Baadhi ya maafisa waliohamishwa ni Beatrice Muli kutoka Kiambu hadi Taita-Taveta; Hudson Salenoi kutoka Vihiga hadi Turkana; Rebecca Abwaku kutoka Homa Bay hadi Trans Nzoia; Reuben Mbuu kutoka Makueni hadi Kitui na Amosi Chilai kutoka Nairobi hadi Kakamega. Wengine ni Japheth Lagat kutoka Trans Nzoia hadi Pokot Magharibi; Grace Anyang kutoka Migori hadi Kericho; Husna Hassa kutoka Mombasa hadi Kilifi; Zahara Hassan kutoka Mandera hadi Wajir na Sheikh Abdi kutoka Wajir hadi Garissa. Engor Emmanuel amehamishwa kutoka Turkana hadi Narok, Frank Boinet kutoka Elgeyo-Marakwet hadi Baringo, Sidney Namulungu kutoka Kericho hadi Marsabit, John Mwangi kutoka Baringo hadi Kirinyaga na Saumu Chirchir kutoka Murang’a hadi Bomet. Maafisa wa uchaguzi wa kaunti wana jukumu muhimu katika maandalizi ya uchaguzi, ikiwa ni pamoja na usajili wa wapigakura, mafunzo, usafirishaji wa vifaa na uendeshaji wa shughuli za kupiga kura. Bw Ethekon alisema zoezi hilo litaendelea huku nafasi zilizo wazi katika ngazi ya maeneo bunge zikijazwa. “Tunaendelea kuwapeleka katika vituo vyao. Hatua inayofuata ni kujaza nafasi zilizo wazi katika ngazi ya maeneo bunge,” alisema. IEBC pia imeweka ratiba ya shughuli kuelekea uchaguzi wa 2027. Vyama vya kisiasa vinatarajiwa kuwasilisha majina na saini za maafisa wao walioidhinishwa kufikia Oktoba 15, 2026. Sheria za uteuzi wa vyama zinatarajiwa kuthibitishwa na Msajili wa Vyama vya Kisiasa kufikia Oktoba 30 na kuwasilishwa kwa IEBC kufikia Novemba 6. Maafisa wa umma wanaonuia kugombea uchaguzi huo watahitajika kujiuzulu nyadhifa zao kufikia Februari 10, 2027. Kampeni rasmi zinatarajiwa kuanza Mei 29, 2027 na kumalizika Agosti 7, siku mbili kabla ya uchaguzi. Bw Ethekon alisema mabadiliko hayo yanalenga kuhakikisha kila kaunti ina afisa anayefaa kabla ya shughuli za uchaguzi kuingia katika hatua muhimu zaidi. Alisisitiza kuwa maafisa hawana haki ya kudumu katika kituo fulani. “Ukiambiwa uende kituo kipya, unaenda na kufanya kazi. Hauwezi kusema lazima ufanye kazi mahali pamoja,” alisema. Bi Kulundu aliteuliwa kuwa Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa IEBC Agosti 5, baada ya kumalizika kwa muda wa miezi sita wa Moses Ledama Sunkuli katika afisi hiyo.
GAVANA wa Kericho Dkt Eric Mutai ameshtakiwa mahakamani na mwanafunzi wa chuo kikuu akitaka aagize kumlipa Sh200,000 kila mwezi kwa matunzo ya mtoto wa mwaka mmoja anayesema alizaa naye. M.C, mwanafunzi wa mwaka wa nne katika Chuo Kikuu cha Kabianga, amemshutumu gavana huyo kwa kukwepa jukumu lake la mzazi kwa kukataa kutoa mahitaji ya mtoto huyo, ambaye anadai alizaliwa kutokana na uhusiano wao wa kimapenzi mwaka 2024. Bi M.C pia anataka Dkt Mutai ampe nakala ya kitambulisho chake cha kitaifa ili aweze kupata cheti cha kuzaliwa cha mtoto huyo. Katika stakabadhi zilizowasilishwa mahakamani, mwanafunzi huyo anasema yeye na Dkt Mutai walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi mwaka 2024, ambao ulisababisha kuzaliwa kwa mtoto huyo Julai mwaka huo huko Kericho. Anadai amekuwa akilea na kutunza mtoto tangu kuzaliwa kwake na ndiye amekuwa akigharamia mahitaji yake bila msaada wa maana kutoka kwa gavana. Bi M.C anasema hana ajira wala chanzo cha mapato kwa sababu bado ni mwanafunzi na kwa sasa anategemea ndugu zake kumsaidia yeye na mtoto. Anadai kwamba juhudi zake za mara kwa mara za kumshawishi Dkt Mutai achangie mahitaji ya mtoto hazijafua dafu. “Katika matukio kadhaa tangu mtoto azaliwe, mlalamishi amelazimika kuwasiliana na kumsihi mshtakiwa achangie mahitaji ya mtoto, lakini mara kadhaa simu na jumbe zake hupuuzwa,” inasema sehemu ya stakabadhi hizo. Kwa mujibu wa kesi hiyo, hali ilikuwa ngumu hadi Bi M.C akaondoka Kericho, ambako anaishi kwa kawaida, na kwenda kujisitiri nyumbani kwa dada yake huko Nakuru. Anasema dada yake amekuwa akimsaidia kupata mahali pa kuishi, chakula, matibabu na mahitaji mengine ya msingi akiwa na mtoto wake. Mwanafunzi huyo anadai pia kwamba kutokuwa na kitambulisho cha Dkt Mutai kumezuia mtoto kupata cheti cha kuzaliwa. Anasema hali hiyo imeathiri haki ya mtoto kupata uraia wa kutambuliwa nao. Kesi hiyo iliwasilishwa baada ya juhudi za wawili hao kufikia makubaliano kuhusu matunzo ya mtoto kushindikana. Bi M.C anasema baada ya kumtumia gavana barua ya kumtaka awajibike na kumjulisha kuhusu hatua za kisheria alizokuwa akizingatiwa, Dkt Mutai aliwasiliana naye akitaka suala hilo litatuliwe nje ya mahakama. Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, gavana alipendekeza kutoa Sh25,000 kila mwezi kwa matunzo ya mtoto. Hata hivyo, alikataa kiasi hicho akise ma hakitoshelezi mahitaji halisi ya mtoto. Kupitia mawakili wake, Bi M.C baadaye aliandaa makubaliano ya kugawana majukumu ya malezi na kuyawasilisha kwa mawakili wa gavana. Anasema Dkt Mutai aliwasilisha kesi katika mahakama ya hakimu Nakuru akimshutumu kwa kumzuia kumwona mtoto na kutofichua alikokuwa. Bi M.C amekanusha madai hayo. Anasema Dkt Mutai hajawahi kuonyesha nia ya kumwona mtoto tangu azaliwe wala kufanya juhudi za kupata taarifa kuhusu afya yake, alipo au hali yake kwa jumla. Anadai pia kuwa wakati mmoja alimpeleka mtoto katika makazi ya gavana akitarajia kupata msaada wa matunzo, lakini Dkt Mutai alikataa kumwona au kumshika mtoto huyo. Kulingana na madai yake, baadaye alikatazwa kurejea katika makazi hayo. Mwanafunzi huyo sasa anataka mahakama iamue kwamba haki za mtoto zimekiukwa na iamuru Dkt Mutai kulipa Sh200,000 kila mwezi kwa matunzo yake. Pia anataka gavana huyo awajibikie bima kamili ya matibabu ya mtoto. Katika uamuzi wa Septemba 14, mahakama iliagiza Dkt Mutai akabidhiwe karatasi za kesi ili ajibu madai yaliyowasilishwa dhidi yake. Kesi hiyo itatajwa tena Septemba 28.
RAIS mstaafu Uhuru Kenyatta jana alimkejeli Rais William Ruto kuhusu madai yake ya mara kwa mara kwamba anafadhili upinzani, kwa kujitaja mwenyewe kama “Sponyo”. Bw Kenyatta alikuwa akizungumza katika mazishi ya Christine Waruguru, mama wa aliyekuwa Naibu Mdhibiti wa Ikulu George Kariuki, katika Kaunti ya Murang’a. Aliandamana na Naibu Kiongozi wa Jubilee Party na mgombea urais, Dkt Fred Matiang’i, pamoja na Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro. Katika siku za hivi majuzi, Rais Ruto amekuwa akimtaja Bw Kenyatta kama mfadhili mkuu wa upinzani, wakati mwingine akimwita kiongozi wa waasi. Pia amekuwa akiita kundi la upinzani la Linda Mwananchi linaloongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuwa “Linda Uhuru Kenyatta”. Katika hafla hiyo ya mazishi, Bw Kenyatta alianza kutoa hotuba bila maandishi kabla ya kujizuia na kusema imekuwa hatari kwake kutoa mawazo yake hadharani bila maandalizi. “Imekuwa hatari kwangu kuzungumza,nisije nikatafsiriwa vibaya na vyombo vya habari, acha nifuate rambi rambi zangu nilizoandika,” alisema. Baada ya kumaliza kusoma ujumbe wake wa rambirambi, alimalizia kwa kauli ya mzaha iliyowafanya waliohudhuria kuangua kicheko. “Hayo ndiyo machache kutoka kwa Sponyo,” alisema. Hafla hiyo pia ilikuwa muhimu kisiasa kwa kuwa ilikuwa mara ya kwanza kwa Bw Kenyatta kushiriki jukwaa moja na Bw Nyoro tangu uhusiano wao wa kisiasa uvurugike mnamo 2018. Wakati huo, Bw Kenyatta alikuwa akimuunga mkono Raila Odinga kumrithi katika uchaguzi mkuu wa 2022, huku Bw Nyoro akiwa miongoni mwa viongozi wa Mlima Kenya waliomuunga mkono Dkt Ruto, ambaye wakati huo alikuwa Naibu Rais. Bw Nyoro alikuwa amechaguliwa kuwa Mbunge wa Kiharu mnamo 2017 kwa tiketi ya Jubilee akiwa mshirika wa karibu wa Bw Kenyatta. Lakini mnamo 2018, uhusiano wao ulianza kuvurugika. Wakati wa harusi ya aliyekuwa Seneta wa Murang’a Irungu Kang’ata, ambaye sasa ni gavana, Bw Kenyatta aliwashauri viongozi chipukizi, akiwemo Bw Nyoro, kutulia na kuanzisha familia. Muda mfupi baadaye, uhusiano wa kisiasa kati yao ulizidi kuwa mbaya, huku Bw Nyoro akikamatwa kwa madai ya kutofautiana kisiasa na baadaye akamjibu Bw Kenyatta vikali katika kampeni. Uwepo wa Bw Nyoro jana uliongeza hamu ya kisiasa katika hafla hiyo, hasa kutokana na ukaribu wake wa hivi majuzi na Dkt Matiang’i. Bw Kenyatta alimuidhinisha Dkt Matiang’i kuwa chaguo lake la urais kuelekea uchaguzi wa 2027 katika hafla iliyofanyika Murang’a Novemba 7, 2025. Tangu wakati huo, Bw Nyoro amekuwa akionyesha kumuunga mkono Dkt Matiang’i, hali ambayo imeibua mjadala kuhusu uwezekano wa wawili hao kushirikiana katika uchaguzi wa 2027. Hata hivyo, jana watatu hao hawakutoa tangazo lolote rasmi kuhusu mpango wa kisiasa au tiketi ya pamoja. Badala yake, Bw Kenyatta alizungumzia umuhimu wa taifa kuwaheshimu mashujaa wake, akisema Kenya ina historia ya kutowatambua ipasavyo waliotumikia taifa. Alisema wanawake na vijana ni miongoni mwa mashujaa ambao wamekuwa wakipuuzwa zaidi. Dkt Matiang’i naye alikosoa baadhi ya viongozi wa kitaifa ambao alisema wamekuwa wakiwatukana wengine, kuwadanganya wananchi na kutoa kauli zisizo na maana. Kwa upande wake, Bw Nyoro alimsifu Bw Kenyatta na kuhusisha baadhi ya miradi ya maendeleo katika Kiharu na uongozi wa rais huyo wa zamani. “Baadhi ya barabara mnazoona Kiharu zilitokana na uongozi wako mzuri, mkuu wangu,” alisema. Mbunge huyo pia alidokeza kuwa Bw Kenyatta bado ni mtu anayemshauri katika safari yake ya kisiasa. “Ninashukuru kwamba unatupa ushauri mzuri tunapokutafuta,” alisema. Bw Nyoro aliwaomba Wakenya kuelewa msimamo wake wa sasa wa kisiasa, akisema yuko katika hatua ya kujijenga mwenyewe.
By Samuel Oyadongha, Yenagoa Former President Goodluck Jonathan has called for the harmonisation of structures and salary scales across Nigeria’s federal and state civil services. Jonathan made the call in Yenagoa during the foundation-laying and fund-raising ceremony for the Bayelsa State Association of Retired Permanent Secretaries’ Secretariat Complex. The former President commended the retired permanent […]
By Udeme AkpanIkeja Electric Plc has warned customers against engaging unauthorised electricians to work on its network, following recent incidents involving fatalities linked to unsafe electrical activities.The company also provided updates on its Meter Asset Provider, MAP, refund process during its September Virtual Stakeholder Engagement, a monthly platform for customer education, operational updates and service-related […]
Watu watatu walifariki na wengine 23 kujeruhiwa, 11 kati yao wakalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), baada ya lori la mafuta kulipuka katika eneo la Juakali, Turbo, kando ya barabara kuu ya Eldoret-Webuye. Mkasa huo ulitokea baada ya umati wa wakazi kufurika katika eneo hilo kuchota mafuta yaliyokuwa yakivuja kutoka kwa lori lililokuwa limepata ajali. Walioshuhudia walisema lori hilo lilipinduka na muda mfupi baadaye likalipuka, na kusababisha moto mkubwa uliowapata watu waliokuwa wakichota mafuta. Waathiriwa walichomeka vibaya kiasi cha kutotambulika, huku majeruhi wakikimbizwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi (MTRH), Eldoret. Mkurugenzi wa Matibabu wa MTRH, Dk Andrew Wandera, alisema hospitali hiyo imepokea majeruhi 23 pamoja na miili miwili kabla ya manusura mmoja kufariki baadaye. “Tulipokea majeruhi 23 pamoja na miili miwili. Mwingine alifariki alipokuwa akipatiwa matibabu katika ICU,” alisema Dkt Wandera. Alisema majeruhi wengi walikuwa na majeraha makubwa ya kuchomeka, baadhi wakiungua zaidi ya asilimia 70 ya miili yao. Juhudi za waokoaji na maafisa wa kukabiliana na majanga ziliendelea katika eneo la mkasa huku baadhi ya miili ikidaiwa kunaswa chini ya mabaki ya lori hilo. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Uasin Gishu, Wilberforce Sicharani, alithibitisha mkasa huo na kuutaja kuwa wa kuhuzunisha. “Hii imekuwa ajali mbaya sana. Watu wamepoteza maisha kwa njia ya uchungu mkubwa,” alisema.N
MOROGORO: MKUU wa Mkoa wa Morogoro ,Queen Sendiga, amesema ataanza kufanya kazi kubwa ya kushughulika na baadhi ya viongozi wa vijiji ambao wanaonekana kuwa ni vyanzo vya kuchochea migogoro baina ya wakulima na wafugaji katika maeneo yao. Sendiga amesema hayo Septemba 17, 2026 wakati wa kikao chake na waandishi wa habari kilichofanyika ukumbi wa mikutano…
MOROGORO: Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Queen Sendiga, amesema atachukua hatua dhidi ya baadhi ya viongozi wa vijiji wanaodaiwa kuwa vyanzo vya kuchochea migogoro baina ya wakulima na wafugaji katika maeneo yao. Sendiga amesema hayo Septemba 17, 2026, wakati wa kikao chake cha kwanza na waandishi wa habari tangu alipokabidhiwa rasmi majukumu ya uongozi wa…
ZANZIBAR: RAIS na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi, amemteua Othman Masoud Othman kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Taarifa iliyotolewa leo Septemba 18, na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza leo. Aidha, Othman ataapishwa Septemba 22, saa 4:00 asubuhi Ikulu…
DAR ES SALAAM: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, anakusudia kuunda kamati ya kuchunguza mkataba wa mzabuni wa jezi za timu za taifa ili kubaini manufaa ya mkataba huo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Zaituni Mkwama, Kamati hiyo itachunguza mkataba huo pamoja na…
DODOMA: THE Bank of Tanzania (BoT) has urged the public to take greater care of their money, particularly banknotes, to ensure they remain in good condition and continue circulating for a longer period. The call was made yesterday by the central bank’s Manager for Banking and Currency Services-Dodoma Mr Nolasco Maluli during a financial education…
KIONGOZI wa Mashtaka ya Umma ameaomba mpelelezi wa zamani wa kitengo cha polisi cha Uingereza (Scotland Yard) azuiliwe kutoa ushahidi katika kesi ya ulanguzi wa dawa za kulevya aina ya methamphetamine yenye thamani ya Sh8.2 bilioni iliyowakabili raia sita wa Iran. Upande wa mashtaka ulisema mpelelezi huyo wa zamani, Bw Kevin Hurley, hakuhusika katika kukamatwa kwa dawa hizo wala uchunguzi wa kesi hiyo, hivyo hakuwa na msingi wa kutoa ushahidi kuhusu masuala yaliyohusiana na kesi hiyo. Bw Hurley alikuwa miongoni mwa mashahidi ambao washtakiwa hao walikuwa wamepanga kuwaita ili kupinga ushahidi wa upande wa mashtaka. Ushahidi wake ulitarajiwa kuangazia namna dawa hizo za kulevya zilizodaiwa kukamatwa katika Bahari Hindi zilivyopaswa kukusanywa, kuhifadhiwa, kutambuliwa, kuhamishwa, kupimwa, kuchunguzwa katika maabara na hatimaye kuwasilishwa mahakamani. Ushahidi wake pia ulilenga kuchunguza iwapo dawa hizo zilishughulikiwa ipasavyo tangu zilipokamatwa baharini, zilipokabidhiwa kwa mamlaka za Kenya, zilipohifadhiwa, kupimwa uzito, kuchukuliwa sampuli na hatimaye kuwasilishwa mahakamani. Upande wa mashtaka ulipinga vikali ushahidi wake, ukisema Bw Hurley hakuwa akiwasilishwa kama shahidi mtaalamu na akauliza msingi wake kutoa ushahidi kuhusu masuala yaliyohusiana na kesi hiyo. Hata hivyo, washtakiwa, kupitia kwa wakili wao, walipinga hoja hiyo wakisema upande wa mashtaka haukutoa sababu za msingi kisheria kumzuia Bw Hurley kutoa ushahidi kabla ya mahakama kumsikiliza. Wakili wa washtakiwa alisema Bw Hurley hatatoa ufasiri wa sheria za Kenya wala kusimulia kilichotokea wakati wa kukamatwa kwa dawa hizo. “Atatoa maoni yake ya kitaalamu kuhusu iwapo taratibu zilizotumika kushughulikia dawa hizo zinazodaiwa kuwa za kulevya zilifuata viwango vinavyotambulika vya utunzaji, uhifadhi na uwasilishaji wa ushahidi,” akaeleza. Mahakama itaamua wiki ijayo kama Bw Hurley atakubaliwa kutoa ushahidi wake au la. Jaseem Darzadeh Nia, Nadeem Jadgal, Hassan Baloch, Raheem Baksh, Imran Baloch na Imtiyaz Daryay wanakabiliwa na shtaka la kuhusika katika ulanguzi wa kilo 1,036.044 za methamphetamine zenye thamani ya takriban Sh8.2 bilioni. Wiki iliyopita, Mahakama ya Shanzu iliamua kuwa watu hao wana kesi ya kujibu baada ya kubaini kuwa upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi unaowataka washtakiwa hao kujitetea. Mahakama ilisema ushahidi huo ulihusisha operesheni iliyofanyika katika bahari kuu na ulihusisha meli iliyodaiwa kubeba zaidi ya tani moja ya methamphetamine. Upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi wa mashahidi 12, wakiwemo wanajeshi wa Jeshi la Wanamaji waliohusika katika kukamatwa kwa dawa hizo, wataalamu kutoka Maabara ya Serikali na nyaraka mbalimbali za ushahidi. Washtakiwa hao walikiri kosa walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza, lakini baadaye walikanusha shtaka hilo. Walidai kupitia mkalimani kuwa dawa hizo zilikuwa na uzito wa takriban kilo 800, wakisema wachunguzi walihesabu pia uzito wa vifungashio. Pia walidai kuwa methamphetamine ilikuwa halali nchini mwao na haikukusudiwa kutumiwa vibaya. Washtakiwa hao wamekuwa kizuizini tangu walipokamatwa mwaka jana baada ya kunyimwa dhamana.
RAIS William Ruto amemshambulia tena mtangulizi wake, Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, akimlaumu kwa kusaliti makubaliano ya kisiasa waliyofikia walipokuwa washirika na sasa kufadhili siasa za upinzani dhidi ya serikali yake. Dkt Ruto alisema yeye na Bw Kenyatta walikubaliana kuwa Rais huyo wa zamani angeongoza kwa miaka 10 kabla ya kumkabidhi yeye uongozi wa nchi kwa miaka mingine 10. Hata hivyo, alidai Bw Kenyatta alipuuza makubaliano hayo ulipofika wakati wake wa kugombea urais na badala yake akamuunga mkono aliyekuwa kiongozi wa ODM Raila Odinga katika uchaguzi wa 2022. “Hukutimiza. Badala yake, ulifanya kazi dhidi yangu,” Rais alisema alipokuwa akizungumza Sindo. Dkt Ruto alisema alimuunga mkono Bw Kenyatta katika chaguzi nne na kusimama naye alipohitaji msaada wa kisiasa. “Nilikuunga mkono katika chaguzi nne na nikakulinda. Ulipofika wakati wako wa kunisaidia, hukufanya hivyo hata kwa siku moja. Lakini baadaye Mungu alinisaidia kuwa Rais wa watu wa Kenya,” alisema. Hata hivyo, Rais alisema hamlaumu Bw Kenyatta kwa kutomuunga mkono, akisema ilikuwa haki yake ya kidemokrasia kumuunga mkono mgombea aliyemtaka. Lakini alimshutumu kwa kuhujumu serikali ya Kenya Kwanza na kufadhili siasa za upinzani. “Unashusha hadhi ya afisi ya Rais mstaafu. Unashusha hadhi yako mwenyewe kama mtu,” alisema. Kauli hizo zilitolewa muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kuunga mkono sheria inayowazuia marais wastaafu kushikilia nyadhifa za uongozi katika vyama vya kisiasa zaidi ya miezi sita baada ya kuondoka madarakani. Hata hivyo, mahakama haikuwazuia kuwa wanachama wa vyama au kushiriki shughuli za kisiasa. Bw Kenyatta ametangaza ataacha uongozi wa Jubilee kufuatia uamuzi huo. Dkt Ruto pia alikosoa rekodi ya kiuchumi ya serikali iliyotangulia, akidai serikali yake ilirithi uchumi uliokuwa katika hali mbaya. “Tumelipa sehemu kubwa ya madeni na kupunguza mfumuko wa bei. Pia tumeongeza mara mbili akiba yetu ya fedha za kigeni,” alisema. Alidai pia serikali yake imeajiri walimu 100,000, kujenga madarasa 23,000 na kufanya mabadiliko katika sekta ya afya. Kauli za Rais zilijiri akimaliza ziara ya siku tano Nyanza, ambapo alitembelea Siaya, Kisumu, Homa Bay na Migori, akizindua miradi na kutangaza mipango mingine ya thamani ya mabilioni ya pesa.
MUUNGANO wa Kenya Kwanza unaoongozwa na Rais William Ruto, umeanzisha kampeni kali ya kisiasa ya kuteka Kaunti ya Trans Nzoia kutoka kwa upinzani, hatua inayoongeza presha kwa Gavana George Natembeya huku makundi hasimu yakipambana kudhibiti kaunti hiyo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang’ula na msaidizi wa karibu wa Rais, Farouk Kibet, wamefika Kaunti hiyo kueneza ujumbe wa mafanikio ya serikali na wakati huohuo kuunga mkono wanaotajwa kuwa wapinzani wa gavana huyo. Tofauti na mwaka 2022 aliposhinda kwa kishindo, Bw Natembeya sasa anakabiliwa na mazingira mapya ya kisiasa. Gavana huyo wa chama cha DAP-K ametofautiana na kiongozi wa chama hicho, Eugene Wamalwa, na ameashiria kuondoka kwake. Tangu wakati huo amekuwa karibu na mrengo wa upinzani wa Linda Mwananchi unaohusishwa na Seneta wa Nairobi, Bw Edwin Sifuna. “Ninatafuta muhula wa pili kwa sababu bado nataka kukamilisha nilichoanzisha kubadilisha kaunti hii,” amesema mara kadhaa kwenye majukwaa yake ya kisiasa. Mabadiliko hayo ya kisiasa yametoa nafasi kwa Kenya Kwanza kuimarisha ushawishi wake Magharibi mwa Kenya na kutafuta mgombea mwenye uwezo wa kumpa changamoto gavana huyo. Wiki iliyopita, Mabw Wetang’ula na Kibet walizuru kaunti hiyo katika shughuli za kuwawezesha wanawake na waendesha bodaboda. Shughuli hizo ziliashiria ujumbe mmoja wa kisiasa: Kenya Kwanza inataka kuteka Trans Nzoia mwaka 2027. Katika mikutano hiyo, Bw Wetang’ula alimtangaza Balozi wa Kenya katika UN-Habitat, Bi Susan Nakhumicha, kama mgombea anayefaa kumpinga Bw Natembeya, huku Bw Kibet akimuunga mkono Mbunge wa Kiminini, Bw Maurice Kakai Bisau. Kuibuka kwa Bi Nakhumicha kumepatia siasa za ugavana sura mpya. Mnamo Juni 2026, Bw Wetang’ula alimuidhinisha waziwazi kuwania ugavana na kuwataka wanasiasa wengine wa Kenya Kwanza kumuunga mkono. “Nimewasiliana na wakazi wa wadi zote 25 na wengi wanatamani mabadiliko. Wanahisi wamevunjwa moyo na uongozi wa sasa na ninafahamu jinsi ya kuokoa kaunti hii nikichaguliwa gavana,” amesema Bi Nakhumicha. Hata hivyo, chama cha UDA kinakabiliwa na changamoto ya ndani kwa kuwa viongozi kadhaa wanawania tiketi hiyo. Mbali na Bi Nakhumicha, wanaowania ni Bw Maurice Bisau, aliyekuwa Mbunge wa Kiminini, Dkt Chris Wamalwa, na Bw Isaac Kogo. “Gavana wa sasa ameshindwa kuleta maendeleo. Amejikita zaidi katika kujenga taswira yake ya kisiasa badala ya kutimiza wajibu wake,” amesema Bw Bisau. Kwa upande wake, Dkt Wamalwa amesema: “Kaunti yetu imebaki nyuma kimaendeleo kutokana na uongozi mbovu. Rekodi yangu ya maendeleo tangu nikiwa Mbunge wa Kiminini inajieleza yenyewe.” Wakati huo huo, maendeleo yameibuka kuwa silaha kuu ya kisiasa. Viongozi wa Kenya Kwanza wanajivunia mradi wa nyumba za bei nafuu wa Sh15 bilioni, zaidi ya kilomita 300 za barabara za lami, masoko ya kisasa na mipango ya kuboresha Hospitali ya Kaunti ya Kitale kwa Sh1 bilioni. “Tunahakikisha hakuna eneo linaloachwa nyuma kimaendeleo, na hatutaacha kaunti hii isimamiwe vibaya,” alisema Bw Wetang’ula mjini Endebess. Ikiwa na wapiga kura karibu 400,000 waliosajiliwa, Trans Nzoia imekuwa muhimu kwa pande zote mbili. Kwa Rais Ruto, kushinda katika kaunti hiyo kutaimarisha nafasi yake ya kuchaguliwa tena. Kwa Bw Natembeya, kushinda muhula wa pili kutathibitisha kuwa ushawishi wake wa kisiasa umeendelea licha ya kutengana na DAP-K.
MWANAMUME anayedai alichangia Sh55 kwa kampeni ya Linda Mwananchi, amewasilisha kesi katika Mahakama Kuu akiomba itoe amri kumlazimisha Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, na vuguvugu hilo kutoa hesabu ya fedha zilizochangwa kwa mradi huo wa kisiasa. Bw Alan Masakhalia anataka mahakama iamuru Bw Sifuna na viongozi wa Linda Mwananchi kutoa taarifa kamili ya michango yote iliyotumwa kupitia nambari ya Paybill 3033049 pamoja na njia nyingine zozote zilizotumika kukusanya fedha. Bw Masakhalia anasema kuwa wananchi waliochanga fedha kwa hiari yao baada ya kualikwa hadharani kufanya hivyo wana haki ya kufahamu jinsi fedha hizo zinavyohifadhiwa, kusimamiwa na kutumiwa. Aidha, anataka mahakama kubaini ni hatua gani za kisheria zinazoweza kuchukuliwa iwapo mradi huo wa kisiasa utaachwa, kubadilishwa mwelekeo, kuhamishwa kwa mtu mwingine au kufanyiwa mabadiliko makubwa yanayokwenda kinyume na maelezo yaliyotolewa wakati fedha zilipoombwa. Bw Masakhalia anasema kuwa kesi hiyo haisukumi ajenda ya kibinafsi ya kisiasa kwamba Bw Sifuna anapaswa kugombea urais. Badala yake, anasema inalenga kupata ufafanuzi kuhusu wajibu wa kisheria unaohusishwa na fedha zinazochangwa na umma kwa madhumuni mahsusi ya kisiasa. Kulingana naye, baada ya kukusanya kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa Wakenya, Bw Sifuna anaweza kuamua kutowania urais, kuunga mgombea mwingine na kumhamishia miundombinu iliyoanzishwa kupitia mradi huo, au kutumia fedha hizo kwa madhumuni tofauti na yale yaliyoelezwa kwa waliochangia. “Hali kama hiyo itazua swali muhimu iwapo wananchi waliochangia fedha zao wana maslahi ya kikatiba na kisheria yanayoweza kutekelezwa kuhusu uhifadhi, uwajibikaji na matumizi halali ya fedha pamoja na mradi wa kisiasa waliofadhili,” alisema. Anataka mahakama kubaini iwapo Bw Sifuna anaweza kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa ajili ya azma ya urais, kisha baadaye kuachana na azma hiyo au kumuunga mkono mgombea mwingine baada ya fedha hizo kupatikana. Bw Masakhalia alikumbusha kuwa mnamo Julai 21, 2026, Bw Sifuna alizindua hadharani Paybill nambari 3033049 na kuwaalika Wakenya kutoa michango ya kifedha kusaidia vuguvugu la Linda Mwananchi. Anadai kuwa waandalizi walitangaza hadharani kwamba, watu 9,419 walichanga takriban Sh519,144 katika siku ya kwanza ya shughuli hiyo ya kuchangisha fedha. “Ndani ya takriban saa 36, jumla ya pesa zilizoripotiwa hadharani iliongezeka hadi karibu Sh2,210,836.82,” alisema. Mlalamishi huyo anasema kuwa sehemu kubwa ya michango ilikuwa ni michango midogo, mingine ikiwa ya chini hadi Sh10, jambo linaloonyesha kuwa mpango huo uliwasilishwa kama mradi wa kisiasa unaofadhiliwa na wananchi badala ya shughuli binafsi ya kifedha. Anasema kuwa alitoa mchango wake kwa hiari na kwa kutegemea maelezo yaliyotolewa hadharani kuhusu malengo ya mradi huo na sababu zilizowafanya wananchi waombwe kuchangia. “Sikutoa mchango huo kama zawadi binafsi kwa mshtakiwa wa Kwanza kwa matumizi yake mwenyewe. Wala sikuwa nikichangia harambee ya matibabu au elimu. Mchango wangu ulikuwa wazi kwa ajili ya hazina ya kampeni ya urais ya Mheshimiwa Sifuna,” alisema. Bw Masakhalia aliongeza kuwa ombi hilo la kuchangisha fedha lilivutia michango kutoka kwa Wakenya wengi wengine. Baadhi ya michango hiyo, alisema, ilikusanywa kupitia ndoo zilizowekwa katika masoko ya Naitiri, Butula, Kakamega na Kabuchai zikiwa na mabango ya Bw Sifuna ambayo waliochangia waliamini yalihusishwa na kampeni ya urais. “Ninaamini kuwa uhuru wa kikatiba wa kiongozi wa kisiasa kufanya maamuzi ya kisiasa hauondoi, kwa wenyewe, wajibu wa kisheria kuhusu fedha zilizoombwa na kupokelewa kutoka kwa wananchi kwa madhumuni ya kisiasa yaliyowasilishwa hadharani,” alisema. Mlalamishi huyo anataka mahakama ibaini iwapo wananchi waliochangia kifedha katika mradi huo wa kisiasa uliotangazwa hadharani walipata haki za kikatiba na kisheria zinazoweza kutekelezwa kuhusu matumizi, uwajibikaji na ufichuzi wa michango yao. Miongoni mwa maagizo anayotaka ni amri itakayomlazimisha Bw Sifuna na vuguvugu la Linda Mwananchi kutoa hesabu kamili na zilizothibitishwa za fedha zote zilizopokelewa kupitia Paybill nambari 3033049 pamoja na njia nyingine zozote. Pia anataka mahakama kuwaamuru washtakiwa kufichua matumizi yote ya fedha hizo, ikiwemo stakabadhi za malipo, kumbukumbu za malipo na stakabadhi nyingine zozote zinazothibitisha matumizi hayo.
TAKRIBAN watu 11 wamepoteza maisha katika ghasia na matukio mengine yanayohusishwa na mikutano ya kisiasa nchini tangu Februari, huku mikutano iliyokusudiwa kurai wapigakura ikigeuka kuwa hatari Kenya inapokaribia Uchaguzi Mkuu wa Agosti 10, 2027. Vifo hivyo vimetokea Nairobi, Homa Bay, Kisumu, Kisii, Vihiga, Kajiado na Embu, ambapo waathiriwa waliuawa au kujeruhiwa vibaya katika visa vya kupigwa risasi, kudungwa visu, kushambuliwa na makundi ya watu na mapigano kati ya polisi na raia. Mikutano ya kisiasa imezidi kuandamana na mapigano, uharibifu wa mali na madai ya kuwepo kwa vijana wanaotumiwa kufanya vurugu. Katika Kaunti ya Nairobi, miili mitatu ambayo haikuwa imetambuliwa awali ilipelekwa Nairobi Funeral Home na polisi baada ya mkutano wa Linda Mwananchi wa Jumapili iliyopita ulioanzia katikati ya jiji na kumalizikia Jacaranda Grounds. Familia za waathiriwa zimekanusha madai yaliyoenezwa mitandaoni kwamba waliuawa baada ya kukamatwa wakiiba simu katika Barabara ya Jogoo. “Kaka yangu, Joseph Omondi Shikuku, hajawahi kumwibia mtu yeyote. Yeye ni mtu mwema aliyekuwa akiendesha biashara ya kuuza nguo za mitumba Umoja 2. Kila kinachosemwa kwenye mitandao ya kijamii si kweli kabisa na sisi kama familia tumeumia,” alisema dadake, Mercy Awino Shikhukhu. Uchunguzi wa baada ya kifo ulionyesha kuwa Omondi alifariki kutokana na majeraha kwenye fuvu la kichwa. Familia inashuku huenda alisukumwa kutoka kwenye daraja la waenda kwa miguu na watu ambao hawakutambuliwa. Brandon Ong’or, 19, pia alifariki Jumapili. Mama yake, Hellen Ong’or, alisema mwanawe hakuwahi kuiba bali alituhumiwa kuwa mwizi na mfuasi wa kundi pinzani la kisiasa. Mkuu wa Polisi wa Buruburu, Boniface Lomuk, alithibitisha kupatikana kwa miili hiyo na kusema waathiriwa walidaiwa kushambuliwa na wakazi waliowalaumu kwa kuiba simu za waliohudhuria mkutano. Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, alilaani ghasia hizo na kusema siasa hazipaswi kuwa sababu ya watu kupoteza maisha. Vifo hivyo vilitokea siku chache baada ya watu wawili, Mike Macharia, 23, na Moses Munene, 30, kupigwa risasi wakati wa mapigano katika mkutano uliohutubiwa na Naibu Rais Kithure Kindiki katika Uwanja wa Nembure, Embu. Vijana waliokuwa nje ya uwanja walirusha mawe huku polisi wa kukabiliana na ghasia wakiwatawanya. Mapigano hayo yalidumu kwa saa kadhaa na magari sita yakachomwa moto. Kaunti ya Homa Bay pia ilirekodi vifo viwili Agosti 16 wakati wa ghasia zilizohusishwa na mkutano wa Linda Mwananchi. Konstebo Jim Richardson Onkundi, 36, alipigwa kichwani kwa jiwe, na gari lake likagonga jengo. Norine Nalangwa aligongwa na gari lililokuwa likienda kwa kasi alipokuwa akivuka barabara. Na Kaunti ya Kisumu, Dickson Oduor alifariki Julai 12 baada ya kudungwa visu wakati wa makabiliano kati ya wafuasi wa Linda Mwananchi na wanaounga mkono serikali. Katika kaunti ya Kisii, Vincent Osiemo, maarufu Mapinduzi, alifariki Julai 3 baada ya kuanguka kutoka kwa gari lililokuwa likitoroka mawe wakati wa mapigano. Katika kisa kingine huko Vihiga, mwendesha boda boda George Otobe aliuawa na kundi la watu Februari 21, huku Vincent Ayomo akipigwa risasi na kufariki Kitengela mwezi huo huo. Ghasia hizo zimeibua wasiwasi kuhusu usalama kuelekea uchaguzi wa 2027. Rais William Ruto, mwezi uliopita alikosoa washukiwa wa vurugu za kisiasa wanavyoshughulikiwa, akisema baadhi hupewa dhamana ndogo na kurejea kwenye mikutano. IEBC imesema itachukua hatua dhidi ya wanaokiuka sheria za uchaguzi. Mwenyekiti wake Erastus Ethekon, amesema tume hiyo, haina mamlaka ya kutekeleza usalama na inategemea idara za usalama. Kipindi rasmi cha kampeni kitaanza Mei 29, 2027 na kumalizika Agosti 7. Hata hivyo, miezi kadhaa kabla ya kampeni kuanza rasmi, mikutano ya kisiasa tayari imehusishwa na vifo.
The office of the Archbishop of Canterbury on Thursday withdrew an interfaith award given this September 11 to a Muslim cleric who praised Osama bin Laden, after the decision sparked backlash.
CHUOKikuu cha Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT) kimesema Mbunge wa Kimilili, Didmus Barasa, hakuwahi kuwa mwanafunzi chuoni humo wala hakikumtunuku shahada ya Uhandisi anayodai alihitimu mwaka 2008. Katika barua aliyoandika Septemba 14, 2026, Msajili wa Masuala ya Kitaaluma wa JKUAT, Dkt Aggrey Wanyama, alisema jina la mbunge huyo halipo katika rekodi zozote za chuo hicho. Chuo hicho pia kilipinga uhalali wa cheti kinachohusishwa na mbunge huyo, kikisema hakikufanya sherehe yoyote ya kuhitimu mwezi Mei 2008, tarehe iliyo kwenye cheti hicho. “Jina lake halipo katika rekodi za wahitimu wetu, na JKUAT haikuwa na sherehe ya kuhitimu mwezi Mei 2008. Kwa hivyo, cheti chake cha Shahada ya Uhandisi wa Umeme na Elektroniki si halisi,” alisema Dkt Wanyama. JKUAT ilieleza kuwa suala hilo liliwahi kuchunguzwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) pamoja na Bodi ya Wahandisi Kenya (EBK), na taasisi hizo zilipewa taarifa kuhusu uhalali wa sifa za kitaaluma zinazodaiwa na mbunge huyo. Chuo hicho kilisema matokeo ya uchunguzi wake yalitumwa kwa EACC na EBK ili yashughulikiwe na hatua zinazostahili kuchukuliwa. Hatua hiyo imefufua mjadala wa muda mrefu kuhusu historia ya elimu ya Barasa na vyeti ambavyo ametumia katika rekodi rasmi. Kwa mujibu wa wasifu wa zamani uliokuwa kwenye tovuti ya Bunge la Kitaifa, Barasa alidai kusomea Shahada ya Sayansi katika Uhandisi wa Umeme na Elektroniki JKUAT kati ya mwaka 2001 na 2005. Wasifu huo pia ulionyesha kuwa alisomea shahada ya uzamili nchini Australia. Hata hivyo, wasifu wa sasa wa Bunge unaonyesha historia tofauti ya masomo. Unaeleza kuwa alisomea Diploma ya Uhandisi wa Umeme na Elektroniki katika Chuo cha Mafunzo cha Kenya Power kati ya mwaka 2001 na 2004, kabla ya kupata Shahada ya Utawala wa Umma katika Chuo Kikuu cha Mount Kenya kati ya mwaka 2017 na 2021. Aidha, wasifu huo unaonyesha alisomea Shahada ya Uzamili ya Utawala na Usimamizi wa Umma katika chuo hicho kati ya mwaka 2021 na 2022. Mwaka huu, suala hilo lilirejea hadharani baada ya Shirikisho COFEK kuwasilisha kesi mahakamani likitaka kuthibitishwa kwa sifa za kitaaluma za mbunge huyo alipokuwa akijiandaa kuhitimu shahada ya uzamivu. Barasa alitunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Murang’a mwezi Agosti 2026, huku maswali yakiendelea kuulizwa kuhusu vyeti vyake vya awali. Katibu Mkuu wa COFEK, Stephen Mutoro, alisema taasisi za serikali zinapaswa kueleza hatua zilichukua baada ya kupewa taarifa na JKUAT. “Ikiwa EBK ilikuwa na taarifa hizi, ni kwa nini mbunge anaendelea kutambuliwa rasmi kama mhandisi kitaaluma? Wakenya wanastahili kujua ukweli,” alisema. Mbunge huyo hajatoa kauli rasmi kuhusu barua ya hivi punde kutoka JKUAT. Juhudi za kumtafuta ili kutoa maoni hazikufanikiwa.
GEITA: MKUU wa Mkoa wa Geita, Alexander Mnyeti, ameeleza kushangazwa na taarifa ya Zahanati ya Kijiji cha Kihula, wilayani Chato, kukosa dawa muhimu aina ya paracetamol na amoxicillin. Mnyeti ametoa kauli hiyo baada ya mzee mmoja, mkazi wa Kijiji cha Kihula, Kata ya Kasenga, kuwasilisha kero yake wakati wa mkutano wa hadhara, akidai kuwa zahanati…
HAKIKA, mnyonge hana haki. Hata ukimpa haki, anaweza kuikataa. Unyonge ninaorejelea hapa ni umaskini. Mtu wa kipato cha chini atakuwa radhi kudharauliwa iwapo kufanyiwa hivyo kutampa hela. Huwezi kunisadikisha vingine, hasa katika kisa ambapo mzazi ameuliwa mwana, halafu anaisihi mahakama imwonee imani muuaji kwa sababu muuaji mwenyewe, baada ya kuua, amemsaidia mzazi huyo kifedha. Kisa cha wazazi wa marehemu Sharon Otieno - msichana aliyeuawa na aliyekuwa gavana wa Migori, Bw Okoth Obado – kuiomba mahakama impe adhabu rahisi, isiyokuwa ya kifungo gerezani, kisa na maana aliwasaidia baada ya kuua mtoto wao, kinaatua moyo. Hakika, kinaudhi si haba unapozingatia kwamba msisitizo wa mahakama kuwa na imani unatarajiwa kumnufaisha Bw Obado pekee, si washtakiwa wenzake, Michael Oyamo na Caspal Obiero, ambao pia walikutwa na hatia ya kumuua Sharon. Kumbe, kwa hakika, pesa ni mvunja mlima? Tofauti ya Bw Obado na washtakiwa wenzake ni pesa tu. Bw Oyamo na Bw Obiero, waliokuwa watu wa mkono wa Bw Obado, wanalazimika kusubiri uamuzi wa mahakama, hata ikiwa ni wa kunyongwa, kwa sababu hawana pesa. Sina hakika Sharon mwenyewe angepewa fursa ya kuamua wanachopaswa kufanyiwa wauaji wake angesema aliye na pesa asazwe, maskini wasio na kitu waadhibiwe kwa vyovyote vile. Huko ni kuutia hatiani umaskini. Bila shaka watu watasema ni vyema kumsamehe aliyekukosea. Binafsi nakubaliana na mtazamo huo kwa asilimia zote. Msamaha unasisitizwa na imani na dini zote ninazojua. Hata hivyo, hakuna hata moja inayopendekeza kwamba aliye na pesa ahukumiwe tofauti na asiye nazo. Mtazamo wa aina hiyo, na naandika haya kwa huruma na heshima zote wanazostahili wazazi wa Sharon, unamsawiri anayeupendekeza kama mtu aliye na uroho wa pesa. Unamsadikisha tajiri kwamba, hata akimkosea maskini kwa kiasi gani, ilimradi ana uwezo wa kumfidia. hata nje ya mfumo wa mahakama, bado pesa zake zinaweza kumshawishi maskini akaghairi nia kuhusu adhabu kali anayostahili kupewa tajiri. Kwa maoni yangu, kesi dhidi ya Bw Obado na wenzake ilisikilizwa yote mpaka hatua ya kutoa adhabu kwa sababu walishtakiwa na serikali, si wazazi wa Sharon. Wazazi hao wangalipewa fursa ya kuiondoa, ili waelewane na wauaji hao nje ya mahakama, basi wangefidiwa kitambo sana mbali na macho yetu. Kando na kwamba nawapa pole zangu wazazi hao, naamini hawajamtendea haki binti yao, pamoja na kilenge aliyeuawa kwa kuchomwa kisu akiwa bado tumboni mwa Sharon! Unyama ulioje! Bila shaka, zamani jamii mbalimbali za Afrika zilikuwa na mifumo ya kuwapa haki waliotendewa unyama katika jamii. Baadhi zilipendekeza muuaji auawe, nyingine zikapendekeza alipe fidia ya ng’ombe, mbuzi, au kondoo wangapi …sijui! Aghalabu fidia ikilipwa na ukoo wa muuaji. Hata hivyo, mfumo wetu wa mahakama ni wa kileo, tena haumruhusu muuaji na mwathiriwa kuketi chini ya mti na kupiga bei kuhusu damu ya aliyeuawa, kwa hivyo ilikuwa lazima kesi dhidi ya wauaji hao watatu ifuate mkondo mzima wa sheria. Hali ingekuwa nyingine, wazazi wa Sharon wangalilaumiwa kwa kuipotezea mahakama muda na rasilmali muhimu ambazo zingetumika katika kesi nyingine kuwatafutia haki wanaostahili zaidi. Kesi hiyo inanikumbusha kisa cha mwanahabari maarufu wa Saudia, Bw Jamal Khashoggi, ambaye aliuawa na serikali ya nchi hiyo katika ubalozi wake nchini Uturuki miaka kadha iliyopita, baadaye serikali hiyo-hiyo iliyomuua ikafidia familia yake kwa mamilioni ya pesa. Familia hiyo ilichukiza wengi kwa kukubali hela hizo zinazoitwa ‘pesa za damu’ kutoka kwa serikali ambayo ilipanga mauaji ya mwenzao kwa kumchukulia kuwa mtu msumbufu, ikamuua kwa hakika, kisha ikaamua italipa fidia kiasi gani. Maoni yangu ni kwamba, katika kisa ambapo umwagikaji damu umetokea, waathiriwa hawapaswi kuonyesha kwamba wanataka fidia ya pesa. Mungu si maskini; hata ikiwa aliyeuawa ndiye aliyekukimu kifedha, kumbuka riziki hutoka kwa Mungu, hivyo atakupa kwa njia nyingine. - Douglas Mutua ni mwanahabari Mkenya anayeishi Amerika ([email protected])
Amnesty International has raised concerns over the arrest, detention and prosecution of journalists, activists and other Nigerians expressing dissent, saying such actions affected freedom of expression in the country.
The treason trial facing Chadema national chairman Tundu Lissu has hit a temporary hurdle after key defence witnesses, including Chief of Defence Forces (CDF) General Jacob Mkunda, failed to appear in court.
MKUTANO wa Linda Mwananchi ulioandaliwa katika uwanja wa Jacaranda, Nairobi ni kati ya mikutano mikubwa ambayo imetia wasiwasi serikali ya Rais William Ruto na Muungano wa upinzani unaojumuisha Kalonzo Musyoka, Rigathi Gachagua, Eugene Wamalwa, Dkt Fred Matiangi, Justin Muturi na Bi Martha Karua. Kundi la Seneta wa Nairobi Edwin Watenya Sifuna liliteka Nairobi kwa kishindo kikubwa. Magazeti yakapata masoko, redio zikawataja vinara bila ukomo na vijana wa mitandao ya kijamii wakachapisha matukio muhimu ya maeneo walikofika wanasiasa hao wakijumuisha Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, Gavana wa Siaya James Orengo, mwenzake wa Trans Nzoia George Natembeya kati ya wengine. Hata hivyo, katika chereko zote hizo, kuna vita vya chini kwa chini kuhusu ni nani anayestahili kuwa kiongozi wa Linda Mwananchi na pia mgombea Urais. Tofauti hizi kati ya Sifuna, Babu Owino na James Orengo huenda zikaliwacha vuguvugu hilo na majeraha makubwa kwa sababu jeshi kubwa la vijana lilikuwa nyuma yake. Nyufa katika ukuta huo pia zitagawanya hamu ya vijana kwa mapande tofauti na kumpa Rais Ruto nafasi rahisi kutwaa Urais kwa mara nyingine. Vivyo hivyo, kukiwa na mgawanyiko hapo katika Linda Mwananchi muungano wa United Opposition utaanza kujigamba kuwa huo ndio uliokuwa upinzani halisi wa kukabiliana na Rais Ruto. Ikumbukwe kuwa kundi hilo la vijana lina msukumo kiasi kwamba mabalozi wa nchi tofauti wanakutana na Sifuna kwa misingi kuwa athari zake zimekuwa kubwa katika jicho la diplomasia na uwezekano wa yeye kuwa Rais wa sita wa Jamhuri ya Kenya upo. Hoja nyingine inayojitokeza katika vurugumechi hii kati ya Sifuna, Orengo na Babu Owino ni kuwa walijitenga na chama cha ODM kwa kile walichodai kuwa ukosefu wa demokrasia. Je, vitendo vyao kwa sasa vinaakisi uzingativu wa demokrasia ama ni misuli ya masilahi? Waliosalia katika chama cha ODM kama mwenyekiti wake Gladys Wanga na kiongozi wa chama Oburu Oginga kwa sasa wanapiga sherehe kutokana na msukosuko huu ndani ya Linda Mwananchi. Kabla uchaguzi mkuu wa 2002, mizozo kama hii ilikuwa katika muungano wa NAK kwanza kati ya Mwai Kibaki, Wamalwa Kijana na Charity Ngilu. Kila mmoja alikuwa anataka kuwa Rais lakini wadau wakakubalia kuwa Kibaki apeperushe bendera, Wamalwa awe naibu wake. Hii iliwafanya kuaminika na hata Raila Odinga akajiunga nao bila masharti. Kundi la Sifuna litashawishi muungano wa upinzani kuliunga mkono tu endapo litakuwa na msimamo, vinginevyo safari ya kumpeleka Ruto Sugoi hatakuwa rahisi. Paul Nabiswa ni mhariri, NTV
RAIS William Ruto amewatahadharisha viongozi wa upinzani dhidi ya kutumiwa na watu aliowataja kuwa “wadhamini wa kisiasa”, akisema serikali jumuishi itashinda uchaguzi wa 2027 kwa kura nyingi zaidi. Rais Ruto alionekana kumlenga Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, akimlaumu kwa kushindwa kutekeleza mipango ya huduma ya afya kwa wote, nyumba za bei nafuu, maji na elimu alipokuwa madarakani. Alisema serikali yake imeanza kushughulikia changamoto zilizoachwa na utawala uliopita, kwa usaidizi wa viongozi wa ODM waliojiunga na serikali jumuishi. “Yule aliyewaajiri alishindwa na UHC, nyumba, maji na elimu. Sasa amekasirika kwa sababu mipango hiyo inaendelea,” alisema. Rais Ruto pia alikosoa upinzani kwa kile alichodai ni kampeni ya chuki na hujuma. “Tuliwashinda siku hiyo, na 2027 tutawashinda tena kwa tofauti kubwa zaidi!” alisema. Huko Migori, Rais Ruto aliahidi Sh124 milioni kukarabati daraja la Mto Migori linalounganisha Suna East na Suna West. Daraja hilo lilifungwa Februari baada ya sehemu yake kusombwa na mafuriko. Njia hiyo inaunganisha wasafiri kuelekea Sirare na Tanzania.
KINSHASA, DR Congo: POLISI nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Jumanne waliwatia nguvuni waandamanaji katika miji kadhaa waliokuwa wakipinga mabadiliko yanayopendekezwa ya Katiba. Wakosoaji wanahofia mabadiliko hayo yanaweza kumruhusu Rais Felix Tshisekedi kuwania muhula wa tatu. Katika jiji kuu la Kinshasa, polisi walitumia vitoza machozi na kufyatua risasi hewani wakati ambapo maandamano yalikuwa yamechacha. Maandamano hayo yaliitishwa na Muungano wa upinzani wa C64, unaohusishwa na waliokuwa wagombea urais Martin Fayulu, Moise Katumbi na Delly Sesanga. Mamia ya watu walishiriki maandamano hayo Kinshasa, kulingana na yaliyonakiliwa na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi. Maandamano hayo yalikuwa yameidhinishwa na yalianza kwa amani, lakini vurugu ziliibuka kati ya waandamanaji na wafuasi wa serikali. Pande zote zilitupiana mawe na baadhi ya waandamanaji wakaonekana wakiwa na mapanga, hali iliyosababisha polisi kuingilia kati. Katika miji ya Lubumbashi na Uvira, maandamano yalipigwa marufuku na serikali za mitaa, lakini waandamanaji walijibwaga barabarani kabla ya polisi kuwatawanya. Hii ni mara ya pili ndani ya miezi michache kwa C64 kuandaa maandamano dhidi ya mabadiliko ya Katiba. Maandamano ya awali yaliyofanyika Kinshasa mwezi Juni yalivunjwa kwa nguvu na vikosi vya usalama. Mvutano huo unatokea wiki tatu baada ya Rais Tshisekedi kutangaza mpango wa kuandaa mazungumzo ya kitaifa yatakayoleta pamoja vyama vya upinzani, mashirika ya kiraia na viongozi wa dini. Hata hivyo, waasi wanaodhibiti maeneo ya mashariki mwa nchi hawakujumuishwa. Tshisekedi amesema mazungumzo hayo yanalenga kushughulikia changamoto za kisiasa nchini humo. Hata hivyo, vyama vya upinzani na Kanisa Katoliki wamepinga mabadiliko yanayopendekezwa ya Katiba. Katiba ya DRC inasema mihula ya kuhudumu kwa rais huwa ni miwili ya miaka mitano kila mmoja. Hata hivyo, Bunge lilipitisha mswada mnamo Juni unaoruhusu mabadiliko ya Katiba kupigiwa kura ya maoni. Baadhi ya viongozi wa muungano unaounga mkono Tshisekedi wameunga mkono marekebisho ambayo yanaweza kumruhusu kuendelea kugombea urais. Hatua hiyo imezua wasiwasi miongoni mwa wapinzani na taasisi za kidini kuhusu mustakabali wa demokrasia na utulivu wa kisiasa nchini humo.
WANAOPINGA matokeo ya uchaguzi wa urais lazima wathibitishe zaidi ya kuwepo kwa ukiukaji wa sheria au kasoro katika upigaji kura ili matokeo yaliyotangazwa yabatilishwe, Jaji wa Mahakama ya Juu William Ouko amesema. Jaji Ouko alisema lazima wanaopinga matokeo hayo waonyeshe kuwa ukiukaji unaodaiwa uliathiri matokeo au uliharibu kwa kiwango kikubwa uadilifu wa uchaguzi kiasi kwamba mahakama haiwezi kwa njia yoyote ile kuunga mkono matokeo hayo. Alisema hayo Jumanne wakati wa mhadhara wa umma katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki. “Ni jukumu la mlalamishi kuthibitisha kuwa uchaguzi uliendeshwa vibaya sana na ukakumbwa na kasoro na ukiukaji wa sheria kiasi kwamba haijalishi nani alitangazwa mshindi. Yaani, uchaguzi ulikumbwa na kasoro nyingi ambazo kwa jumla ziliharibu kwa kiasi kikubwa uadilifu wa uchaguzi,” alisema. Aliongeza: “Si kila ukiukaji wa sheria unaosababisha uchaguzi kutangazwa batili.” Jaji Ouko alikumbusha kuwa kabla ya Katiba ya 2010, changamoto za matokeo ya urais zilikabiliwa na vikwazo vya kisheria na kiutaratibu. Katika kesi ya mwaka wa 1997, kesi ya aliyekuwa mgombea wa urais Mwai Kibaki kupinga ushindi wa Rais Daniel arap Moi lilitupiliwa mbali kwa sababu Kibaki hakumfikishia Moi stakabadhi za kesi binafsi. Kwa mujibu wa Jaji Ouko, uamuzi huo ulionyesha udhaifu wa mfumo uliokuwepo ambao haukuwezesha mzozo kuhusu uhalali wa mamlaka ya urais kushughulikiwa kikamilifu kwa misingi ya ushahidi. Hali hiyo ilizidi kuwa mbaya baada ya uchaguzi wenye utata wa mwaka 2007 na ghasia zilizofuata. Tume ya Kriegler ilieleza wasiwasi kuhusu imani ya wananchi katika taasisi za uchaguzi na mahakama. Jaji Ouko alisema mgogoro huo ulionyesha kuwa mizozo ya uchaguzi isipotatuliwa kupitia taasisi za kikatiba inaweza kuhamia uwanja wa kisiasa. Katiba ya 2010 ilijibu changamoto hizo kwa kupatia Mahakama ya Juu mamlaka ya kipekee ya kushughulikia kesi zinazopinga uchaguzi wa urais. Jaji Ouko alisema hatua hiyo ililenga kuhakikisha kuwa mzozo kuhusu kiti cha juu zaidi nchini unapata uamuzi wenye mamlaka na wa mwisho. Kisheria, kesi ya kupinga matokeo ya urais lazima liwasilishwe ndani ya siku saba baada ya kutangazwa kwa matokeo. Mahakama inapaswa kutoa uamuzi ndani ya siku 14, huku uchaguzi mpya ukifanyika ndani ya siku 60 endapo uchaguzi utabatilishwa. “Hata hivyo, kufanya mambo kwa haraka hakufai kuchanganywa na pupa,” alisema Jaji Ouko, akisisitiza umuhimu wa kusawazisha kasi na haki ya kila upande kusikilizwa. Alisema mzigo wa kisheria wa kuthibitisha madai hubaki kwa mlalamishi, ingawa mzigo wa kutoa ushahidi unaweza kuhamia upande mwingine pale mlalamishi anapowasilisha ushahidi wa kutosha unaohitaji majibu.
WAZAZI wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo aliyeuawa kinyama, Sharon Otieno, wameomba Mahakama Kuu imsamehe aliyekuwa Gavana wa Migori Okoth Obado na kumpa adhabu isiyohusisha kifungo gerezani. Douglas Zacharia Otieno na Melida Auma waliwasilisha ombi hilo mbele ya Jaji Cecilia Githua wakati wa hatua ya kumpa Obado adhabu baada ya kupatikana na hatia ya kumuua binti yao. Wazazi hao waliomba mahakama izingatie mazingira yote ya kesi hiyo, ikiwemo mambo yanayoweza kupunguza au kuongeza uzito wa adhabu, kabla ya kutoa uamuzi. Walisema licha ya maumivu makubwa yaliyosababishwa na kifo cha Sharon, wamechagua kumsamehe Obado na wanataka mahakama izingatie msamaha wao. “Familia inamshukuru sana Mheshimiwa Jaji kwa kuhakikisha haki imetendeka kupitia hukumu ya kumpata na hatia. Hata hivyo, katika hatua hii muhimu ya kutoa adhabu, familia inaomba mahakama itumie busara yake kusawazisha haki na ombi la familia ya mwathiriwa,” walisema. Sharon, aliyekuwa na umri wa miaka 26, alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Rongo. Alikuwa na ujauzito wa wiki 28 alipouawa kati ya Septemba 3 na 4, 2018, katika eneo la Owade, Homa Bay. Alikuwa ametekwa nyara pamoja na mwanahabari ambaye alifanikiwa kutoroka. Obado, aliyekuwa msaidizi wake wa kibinafsi Michael Oyamo na Caspal Obiero walipatikana na hatia ya kumuua Sharon mwezi Julai. Mahakama ilisema watatu hao walishirikiana na watu wengine ambao hawakufikishwa mahakamani kutekeleza mauaji hayo. Katika ombi lao, wazazi walisema Sharon alikuwa tegemeo muhimu la familia na kifo chake kiliwaacha wakiwa wamevunjika moyo na pia katika hali ngumu kifedha. Hata hivyo, walisema Obado alijitokeza baadaye kuwasaidia kifedha. “Baada ya msiba huu, mshtakiwa wa kwanza (Obado) alifanya jambo la kipekee; alijitokeza na kusaidia familia na nyumba yetu kifedha. Hakufanya hivyo kwa amri ya mahakama, bali kwa hiari yake, akiongozwa na huruma na nia ya kuboresha hali ya maisha ya familia,” walisema. Wazazi hao walisema msaada huo unafaa kuzingatiwa katika hatua ya kumwadhibu. Walieleza kuwa wanataka haki ya kurekebisha madhara yaliyosababishwa na uhalifu huo izingatiwe, badala ya adhabu pekee. “Tunaomba mahakama ikomeshe mzunguko wa maumivu. Tunaomba adhabu inayolenga kumrekebisha badala ya kulipiza kisasi pekee, na kumpa mshtakiwa wa kwanza nafasi ya kujirekebisha,” walisema. Pia waliomba mahakama itumie Kifungu cha 23 cha Sheria ya Kulinda Waathiriwa na kuamuru fidia kwa familia pamoja na adhabu isiyohusisha kifungo. Hata hivyo, waliomba uamuzi huo uzingatie maslahi ya umma, haja ya kuzuia uhalifu kama huo na miongozo ya kutoa adhabu. Wazazi hao walisema wameishi na maumivu makubwa tangu Sharon alipouawa, wakieleza miaka iliyojaa machozi, kukosa usingizi na ndoto mbaya. Walisema wanataka kufunga ukurasa wa tukio hilo na kuendelea na maisha baada ya miaka ya kupitia kile walichokiita kipindi kigumu zaidi katika maisha yao. Ingawa walikiri uzito wa kosa lililotendwa, wazazi hao walisema hakuna anayeelewa ukubwa wa hasara yao kuliko wao wenyewe.
MIVUTANO kuhusu madaraka na azma zinazokinzana za kisiasa miongoni mwa viongozi wakuu wa Linda Mwananchi imejitokeza hadharani, huku makundi tofauti yakionekana kuvutana kuhusu mwelekeo wa vuguvugu hilo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Kiini cha mzozo huo ni kutoaminiana na mvutano kuhusu chama kitakachotumiwa na viongozi hao waliotoka ODM. Uhasama huo mkali unashirikisha Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na wanasiasa ambao wapo katika kambi yao. Kambi moja inayomuunga mkono Bw Owino inataka Bw Sifuna agombee urais kupitia chama kipya cha Mwananchi Party, ambacho bado hakijazinduliwa rasmi. Kwa upande mwingine, Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya anataka Seneta huyo atumie Ukombozi People’s Party (UPP). Bw Owino anadaiwa kupata Muungano Party, chama cha aliyekuwa Gavana wa Kitui Kivutha Kibwana, kwa ajili ya kukibadilisha kuwa Mwananchi Party. Naye Gavana Natembeya anafanya mabadiliko katika United Democratic Party (UDP), iliyowahi kuhusishwa na marehemu Cyrus Jirongo, ili iwe UPP. Mvutano huo umechangiwa zaidi na maslahi ya kieneo kati ya viongozi wa Nyanza na Magharibi, pamoja na tangazo la Gavana wa Siaya James Orengo kwamba anataka kuwania tiketi ya urais ya Linda Mwananchi. Aidha, kuna swali kuhusu nani atakuwa kiongozi mkuu wa kisiasa wa vuguvugu hilo. Kuibuka kwa Bw Sifuna kama kiongozi maarufu zaidi kumeripotiwa kuwakwaza baadhi ya viongozi wakuu wanaohisi wanapaswa kuwa na nafasi na ushawishi sawa. Bw Owino alisema Jumanne kuwa mzozo huo unahusu zaidi chama cha kisiasa kitakachotumiwa katika uchaguzi wa 2027. Alisema alipata chama mapema mwaka huu na alikuwa akipanga kukitumia kuwania ugavana wa Nairobi kabla ya Linda Mwananchi kuanzishwa. Alisema awali yeye na wanachama wengine watatu walipewa jukumu la kutafuta chama. Mbunge wa Saboti Caleb Amisi alikuwa tayari ana chama, lakini baadaye alijiondoa baada ya kutofautiana na baadhi ya viongozi. Bw Owino alisema alipomweleza Bw Sifuna kuhusu vyama hivyo viwili, Seneta huyo alimwambia hakukuwa na tatizo mradi kuwe na muungano, huku kila mmoja akiwa kiongozi wa chama chake. Hata hivyo, alisema mvutano kuhusu chama cha kutumia bado unaendelea kuwatikisa. “Baada ya hapo kumekuwa na kuvutana kuhusu chama atakachotumia. Nimeamua kwamba tuwe na chama kimoja, lakini ikiwa hilo haliwezekani, basi tuwe na muungano kwa sababu ni miungano ambayo imeshinda chaguzi nchini,” alisema. Seneta wa Vihiga, Godfrey Osotsi, ambaye ni mshirika wa Bw Sifuna, alikutana na Bw Owino Jumatano katika juhudi za kusuluhisha tofauti hizo. Hata hivyo, Bw Osotsi alipuuza ripoti za tofauti kubwa, akidai kuwa kuna juhudi za Serikali kuigawanya vuguvugu hilo kupitia propaganda. Mbunge wa Funyula Oundo Midenyo alisema kuwa hakukuwa na makubaliano yoyote kuwa Bw Sifuna angetumia chama cha Owino. “Bado tunaendelea kuafikiana lakini hakukuwa na muafaka wowote kwamba Sifuna atumie chama cha Owino,” akasema Bw Oundo. Naye Mbunge wa Kabuchai Majimbo Kalasinga alihoji kwa nini Bw Owino hataki kumruhusu Bw Sifuna kuwa kiongozi wa chama chake ikiwa kweli anamuunga mkono katika azma ya urais. Mvutano huo pia umeonekana katika mikutano ya Linda Mwananchi ambao vinara hao walikwepo wikendi. Katika mkutano wa Jacaranda jijini Nairobi, maswali yaliibuka kuhusu itifaki baada ya Bw Owino kumwalika Bw Sifuna kuzungumza kwanza, badala ya kupewa nafasi ya mwisho kama kiongozi mkuu wa mkutano. Mvutano mwingine ulionekana katika mkutano wa Kitale mwezi mmoja uliopita, ambapo Mbunge wa Bumula Wanami Wamboka alichukua kipaza sauti kutoka kwa Bw Owino akiwa bado anazungumza. Aidha, kambi za Bw Orengo na Bw Sifuna zimeanza kutofautiana baada ya Gavana wa Siaya kutangaza azma yake ya kuwania urais, hatua ambayo iliwakasirisha baadhi ya wandani wa Bw Sifuna.
CHAMA cha Jubilee kimetumbukia katika vita vipya vya uongozi huku aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta akijiandaa kuacha rasmi uongozi wa chama hicho baada ya Mahakama Kuu kuamua kuwa marais wastaafu hawawezi kuendelea kushikilia nyadhifa za uongozi wa vyama zaidi ya miezi sita baada ya kuondoka Ikulu. Uamuzi huo umefungua mapambano mapya ya kumrithi Bw Kenyatta, huku Naibu Viongozi wa Jubilee Jeremiah Kioni na Fred Matiang’i wakiwa miongoni mwa wanachama muhimu katika mchuano huo. Kiini cha mzozo huo si kiti cha kiongozi pekee, bali pia udhibiti wa mtandao wa chama, mali, fedha na ushawishi wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Bw Kioni Jumanne alitangaza nia yake ya kuwania wadhifa wa Kiongozi wa Jubilee, siku moja tu baada ya Bw Kenyatta kutangaza atasalimisha uongozi wa chama. Katika taarifa yake, Bw Kenyatta alisema yuko tayari kukabidhi uongozi wa Jubilee kupitia mchakato unaozingatia katiba ya chama. Bw Kenyatta alikuwa amebaki katika uongozi wa Jubilee licha ya mzozo wa ndani uliochelewesha mabadiliko. Mnamo Machi 2025, alirejea kudhibiti chama hicho baada ya mapambano ya muda mrefu kati ya makundi hasimu. Hata hivyo, uamuzi wa Jaji Lawrence Mugambi sasa umefanya kuondoka kwake kuwa suala la kisheria badala ya uamuzi wa kisiasa. Jaji Mugambi alifafanua kuwa marais wastaafu hawazuiwi kuwa wanachama wa vyama au kushiriki shughuli za kisiasa. Kilichozuiwa ni kushikilia rasmi uongozi wa chama baada ya muda uliowekwa. Uamuzi huo umeacha Jubilee katika mchakato nyeti wa kutafuta atakayechukua nafasi ya Bw Kenyatta na kuamua mwelekeo wa chama kabla ya uchaguzi ujao. Bw Kioni sasa anataka uongozi huo upatikane kupitia Kongamano la Kitaifa la Wajumbe (NDC), akipinga uwezekano wa kiongozi mpya kupitia makubaliano ya ndani. “Jubilee ni chama cha kitaifa na kilikuwa chama tawala. Kwa hivyo, viongozi wetu hawateuliwi, wanachaguliwa na wajumbe katika Kongamano la Kitaifa la Wajumbe,” alisema. Kauli hiyo imeleta mtazamo tofauti kuhusu urithi wa chama, hasa ikizingatiwa kuwa Bw Matiang’i tayari ndiye mgombea urais wa Jubilee wa 2027. Baadhi ya wafuasi wa Bw Matiang’i walitarajia kuwa hadhi yake ya kisiasa pamoja na uteuzi wake kuwa mgombea urais ungemweka katika nafasi nzuri ya kurithi uongozi wa chama baada ya Bw Kenyatta. Lakini kuibuka kwa Bw Kioni kumefanya swali hilo kuwa tata zaidi. Mmoja wa watu wa karibu na chama alisema nafasi ya kiongozi wa chama na mgombea urais ni tofauti, na kwamba mmoja hawezi kumpisha mwingine moja kwa moja. “Uzuri wa Jubilee ni kwamba, kiongozi wa chama anapoondoka, manaibu wawili wana haki, nafasi na uwezo sawa wa kuwania nafasi hiyo. Hiyo ndiyo demokrasia,” alisema. Bw Kioni na Bw Matiang’i wote ni manaibu wa kiongozi wa Jubilee, jambo linaloweka msingi wa ushindani wa moja kwa moja kati ya makundi yanayowaunga mkono. Jubilee ni miongoni mwa vyama vilivyotawala siasa za Kenya wakati wa utawala wa Bw Kenyatta, ikiwa na wabunge na viongozi wengi wa kaunti. Nguvu zake zimepungua tangu Bw Kenyatta alipoondoka madarakani, lakini chama bado ni sehemu muhimu ya siasa za upinzani na mipango ya miungano kuelekea 2027. Pia kuna suala la fedha. Jubilee imewahi kuwa miongoni mwa wanufaika wakubwa wa Hazina ya Vyama vya Kisiasa, ikipokea takriban Sh240.4 milioni katika mwaka wa 2017/18, Sh434.6 milioni mwaka uliofuata, Sh564.2 milioni mwaka wa 2019/20, Sh515 milioni mwaka wa 2020/21 na Sh1.02 bilioni mwaka wa 2021/22. Kwa jumla, chama kilipokea zaidi ya Sh2.77 bilioni katika miaka hiyo mitano. Hata hivyo, mgao huo umepungua kutokana na kuporomoka kwa nguvu zake za kisiasa. Katika mwaka wa kifedha wa 2026/27, Jubilee imetengewa Sh128.86 milioni kutoka kwa Hazina ya Vyama vya Kisiasa. Mchanganuzi wa siasa Geoffrey Mboya alisema fedha ni sehemu tu ya mvuto wa chama hicho. Alisema udhibiti wa Jubilee pia unamaanisha kushikilia miundo ya wanachama, mtandao wa kitaifa, chapa ya chama na mamlaka ya kujadiliana kuhusu nafasi yake katika miungano ya kisiasa. Wakati huo huo, chama hicho kinakabiliwa na shinikizo la kurekebisha miundo yake kabla ya uchaguzi wa 2027.
The Independent National Electoral Commission (INEC)’s warning that abusive, inflammatory and threatening campaign language will attract severe sanctions under the Electoral Act 2026 is timely, but hardly novel. At the beginning of virtually every election season, INEC issues similar warnings to political parties, candidates and their supporters. The recurrence of such vices raises the question: […]
The Independent National Electoral Commission (INEC) has explained that its Chairman, Prof. Joash Amupitan, SAN, is currently away from Abuja on an official assignment, stressing that he has the authority to delegate his responsibilities to any National Commissioner. INEC Director, Voter Education and Publicity, Mrs Victoria Eta-Messi, gave the clarification in response to questions raised […]
By Musa Ubandawaki, Sokoto A fresh controversy has emerged over the 14-member advisory committee constituted by the Sokoto State Government to investigate the circumstances surrounding the attack on Sheikh Musa Ayuba Lukuwa and the subsequent death of his alleged attacker at the Lukuwa Jumu’at Mosque in Mabera, Sokoto metropolis. The controversy followed concerns raised by […]
PWANI; Mkoa wa Pwani kupitia timu za maafa umejiandaa kusaidia makundi maalumu wakiwemo watu wenye ulemavu, wazee na watoto wakati mvua za El Nino zitakapoanza kunyesha. Kauli hiyo imeteolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya kuchukua tahadhari juu ya mvua hizo zinazotarajiwa kuanza…
GAVANA wa Homa Bay Gladys Wanga amejikuta tena katikati ya gumzo la kisiasa baada ya kuonekana akisafiri kwa helikopta ya Jeshi la Anga pamoja na Rais William Ruto wakati wa ziara yake ya maendeleo katika Kaunti ya Siaya Jumanne. Video iliyosambaa mtandaoni ilimuonyesha Mwenyekiti huyo wa kitaifa wa ODM akishuka kutoka kwa helikopta hiyo pamoja na Rais Ruto baada ya wawili hao kusafiri pamoja kati ya maeneo mbalimbali aliyozuru kiongozi wa nchi. Mchanganuzi wa siasa Walter Opiyo alisema matumizi ya chombo hicho cha Rais ni ishara inayoweza kutafsiriwa kama ukaribu na mamlaka. Alisema helikopta za Rais kwa kawaida hutumiwa na Rais na kikosi chake cha usalama, hivyo kuruhusu kiongozi mwingine kuingia ndani yake kunaweza kuibua maswali kuhusu nafasi yake katika uongozi. “Helikopta ya Rais si matatu. Anayeingia ndani yake lazima afahamu itifaki kuhusu urais na awe mtu anayeaminika. Wanga anaposafiri na Rais, inaonyesha sasa yuko karibu na kitovu cha serikali jumuishi,” alisema Opiyo. Aliongeza kuwa safari hiyo ilimpa Wanga muda wa kuwa karibu na Rais bila hadhira. “Dakika hizo angani zinaweza kuwa muhimu zaidi kuliko saa nyingi jukwaani. Hapo ndipo mazungumzo muhimu ya kisiasa yanaweza kufanyika,” alisema. Mchanganuzi mwingine, Michael Kojo, alisema hatua hiyo ilikuwa na ujumbe wa kisiasa. “Akiwa mwenyekiti wa ODM, lazima aonyeshe kwamba ushirikiano wa chama na serikali unafanya kazi. Kusafiri na Rais na wote kuvaa kofia za ODM ni ujumbe kwamba ushirikiano huo unaendelea vizuri,” alisema. Wanga ana uwezo wa kukodi helikopta yake kama gavana na amewahi kufanya hivyo. Hata hivyo, mara kadhaa amekuwa akisafiri na Rais Ruto anapozuru eneo la Nyanza. Kojo alisema Wanga pia anaweza kuwa anasisitiza ushawishi wake wa kisiasa na kujiweka katika nafasi ya majukumu ya kitaifa siku zijazo. Katika ibada ya maombi katika kanisa la Voice of Salvation and Healing, Kisumu, Jumapili, Wanga aliketi upande wa kushoto wa Rais baada ya Gavana wa Kisumu Anyang’ Nyong’o. Katika miezi ya hivi karibuni, wafuasi wake wamekuwa wakimtaja kama mmoja wa wanaoweza kuwania wadhifa wa Naibu Rais, huku yeye akisema ODM haitakubali chochote chini ya kiti hicho katika mpango wowote wa kisiasa wa siku zijazo. Hata hivyo, Wanga pia analenga kuchaguliwa tena kuwa Gavana wa Homa Bay. Safari ya Jumanne haikuwa mara ya kwanza kwa Wanga kupanda helikopta ya Rais. Mapema mwaka huu, alinaswa kwenye video akikimbia kuingia kwenye helikopta hiyo pamoja na Mbunge wa Suna East Junet Mohamed. Kojo alisema kuonekana kwake mara kwa mara pamoja na Rais kunaashiria nafasi yake inayokua katika mawasiliano kati ya ODM na serikali. Wakati wa ziara hiyo, kulionekana alama za vyama tofauti katika mikutano, baadhi ya wananchi wakiwa wamevalia rangi za UDA, wengine za chungwa za ODM na wachache kofia za MDG. Rais na Wanga walionekana wakivalia kofia zinazofanana za ODM waliposhuka kutoka kwenye helikopta. Tukio hilo linakumbusha pia ziara ya Rais Ruto katika Kisiwa cha Rusinga, Homa Bay, Agosti 2024, ambapo Wanga alialikwa ndani ya gari rasmi la Rais na kuhutubia wananchi kupitia paa la gari.
KILIMANJARO; Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro wametakiwa kuchukua tahadhari na kujiandaa mapema kukabiliana na mvua kubwa El Nino kwa kuhakikisha mitaro na mifereji inakuwa wazi na mikondo ya maji inaachwa ipite kwa usalama. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boi Safi, ambaye amesema maandalizi ya mapema ni…
Chadema’s cadre Joseph Selasini said there is no political will for national reconciliation while freedom of expression remains absent due to abduction fears.
Chadema Vice Chairperson John Heche has strongly refused invitation letters from the Presidential Commission to Investigate Breaches of Peace During and After the October 29, 2025 General Election to be admitted by the High Court as physical exhibits in the ongoing treason trial facing party chairman Tundu Lissu.
DAR ES SALAAM: TANZANIA imekuwa miongoni mwa nchi zinazovutia wawekezaji, baada ya kufanikiwa kuvutia uwekezaji wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.7 ndani ya kipindi cha miaka mitano. Taarifa hiyo imetolewa leo, Septemba 16, 2026, na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dk Pius Chaya, katika uzinduzi wa Jukwaa la…
MUUNGANO unaoongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga umetaka mageuzi makubwa kufanyiwa mchakato wa uchaguzi kabla ya kura za mwaka ujao na ukatishia kuongoza Wakenya kwenye maandamano iwapo mabadiliko hayo hayatafanywa. Muungano huo, unaojulikana kama People’s Coalition on Electoral Reforms, umeibua mjadala mpya kuhusu maandalizi ya uchaguzi huku ukielekeza lawama kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Bunge na serikali. Miongoni mwa mageuzi unaopendekeza ni kufutwa kwa kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura za urais katika ukumbi wa Bomas, ukaguzi huru wa sajili ya wapigakura, kuongezwa kwa adhabu kali kwa makosa ya uchaguzi, kugatuliwa kwa matumizi ya mfumo wa teknolojia ya uchaguzi na mchakato wa wazi wa kuajiri maafisa wa IEBC. Muungano huo unawaleta pamoja Maraga, Mbunge wa Saboti Caleb Hamisi, Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi, kiongozi wa Thirdway Alliance Ekuru Aukot na aliyekuwa Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi. Akizungumza kwa niaba ya muungano huo, Maraga alisema mageuzi hayo lazima yatekelezwe kabla ya uchaguzi wa Agosti 2027 ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, wa haki, wenye uwazi na unaoaminika. “Kenya haiwezi kumudu uchaguzi mwingine ambao uaminifu wake ni wa kutiliwa shaka. Ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/2008 ni onyo la kitaifa ambalo hatuko tayari kulirudia,” alisema Maraga. Muungano huo unasema suala la uaminifu wa uchaguzi wa 2027 si la kisiasa pekee bali ni jambo la maslahi ya taifa linalohitaji wahusika wote-wapigakura, wagombeaji, serikali, upinzani na wananchi kwa jumla. Kwa mujibu wa Caroli Omondi, muungano huo unapinga kuwepo kwa kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura za urais, ukisema Katiba inahitaji kura zihesabiwe na kutangazwa katika vituo vya kupigia kura na katika ngazi ya eneo bunge. “Hakutakuwa na kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura za urais kinachoendeshwa na IEBC au mwenyekiti wake katika Bomas au mahali pengine popote,” alisema Omondi.
CHANGAMOTO ya upatikanaji wa maji safi na salama katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam imeendelea kuwaathiri wananchi kiuchumi kutokana na kutumia gharama kubwa ya kupata maji. Wananchi katika maeneo mbalimbali wanasema kutokuwa na uhakika wa kupata maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kumewalazimu kutafuta…
By Ediri Ejoh with Agency report The Federal Government (FG) has raised N728.9 billion in bonds as part of its funding process to offset the N4 trillion legacy debt it owed electricity Generation Companies, GENCOs. Speaking at the bond launch in Abuja, TaiwoOyedele, Minister of Finance and Coordinating Minister of the Economy, said the Series-2 […]
RIYADH, Saudi Arabia WAASI wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran wameanzisha wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Saudi Arabia, hatua ambayo imeongeza wasiwasi kuhusu usalama wa usafirishaji wa mafuta katika Mashariki ya Kati. Serikali ya Yemen ilisema kuwa Wahouthi wapo pwani ya magharibi ya Yemen, kando ya Bahari ya Shamu ambapo wamenogesha mikakati ya kushambulia Saudi Arabia. Wahouthi wenyewe walisema walirusha makombora kadhaa na ndege zisizo na rubani katika kituo cha kijeshi cha Khamis Mushait kusini mwa Saudi Arabia. Walisema walilenga ndege, uwanja wa ndege na maghala ya risasi, kulipiza kisasi mashambulizi ya anga ya Saudi Arabia nchini Yemen. Serikali ya Saudi Arabia imetoa tahadhari kwa wanaopanga kuzuru miji minne ya kusini. Saudi Arabia ilisema raia 13 walijeruhiwa katika mashambulizi hayo ya Wahouthi. Mashambulizi hayo yameongeza shinikizo kwa usafirishaji wa mafuta wa Saudi Arabia baada ya shambulizi la anga Alhamisi kusababisha bomba la mafuta linalounganisha mashariki na magharibi mwa nchi hiyo kusitisha shughuli. Saudia ililaumu wanamgambo hao wanaoungwa mkono na Iran kutokana na shambulizi hilo. Wafanyabiashara wa mafuta walisema kufungwa kwa muda mrefu kwa bomba hilo kunaweza kuathiri hadi asilimia nne ya usambazaji wa mafuta duniani, hasa wakati Mkondo wa kupitisha mafuta wa Hormuz ukiwa bado umefungwa na Iran. Wakati huo huo, matumaini ya diplomasia yalipungua baada ya nchi za Ghuba kuahirisha mazungumzo yaliyopangwa na Iran kuhusu kufunguliwa tena kwa Mlango wa Hormuz. Kabla ya vita kati ya Amerika-Israel dhidi ya Iran, Strait of Hormuz ilikuwa ikipitisha asilimia 20 ya mafuta yanayouzwa duniani. Oman, iliyokuwa imepanga kuandaa mkutano huo, ilitangaza kuwa umeahirishwa. Iran ilisema Saudi Arabia ndiyo iliyoomba kuahirishwa. Rais wa Amerika Donald Trump alisema Iran ilikuwa tayari kufanya makubaliano, lakini Mohsen Rezaei, katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, alikataa kauli hiyo na kusema hakuna mazungumzo hadi masharti ya Iran yatimizwe. Saudi Arabia imekuwa ikiongoza vita dhidi ya Wahouthi tangu 2015. Ingawa mapigano yalipungua baada ya pande zote kuafikia makubaliano ya kusitisha mapigano, vita vilianza tena mwezi huu. Kuendelea kwa mapigano na tishio kwa Mlango wa Hormuz kunazua hofu zaidi kwamba usambazaji wa mafuta duniani unaweza kuvurugika, hali ambayo huenda ikaendelea kuweka shinikizo la kupanda kwa bei ya mafuta.
Nigerian Guild of Editors, NGE, has raised concerns over the increasing harassment, intimidation and prosecution of journalists by security agencies, warning that such actions could undermine press freedom and legitimate journalistic practice.
KATIKA siku yake ya tatu ya ziara ya Nyanza, Rais William Ruto alipeleka mapambano yake ya kisiasa dhidi ya vuguvugu la Linda Mwananchi hadi Siaya, ngome ya Gavana James Orengo, akiwataka wapigakura kukataa vyama vipya ambavyo alisema havijathibitisha uwezo wao wa kuongoza nchi. Rais Ruto aliwataka wakazi kuunga mkono vyama vilivyo katika serikali jumuishi, akipuuza vyama vipya ambavyo bado havijasajiliwa rasmi. Alisema vyama hivyo havina uzoefu, mtandao wa kitaifa wala mipango thabiti ya kuongoza Kenya. Ziara yake Siaya ilikuwa na umuhimu wa kisiasa, hasa kwa kuwa viongozi wa Linda Mwananchi wanatarajiwa kuzuru eneo hilo siku chache zijazo. Rais Ruto pia alimshambulia Gavana Orengo kwa kuhusishwa na vuguvugu hilo, akimtaka badala yake kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo Siaya. “Namwambia Orengo aache kundi hilo linaloitwa Linda Sponsors au Linda Sponyo na ajiunge nami katika safari hii ya maendeleo na kujenga hospitali. Je, ninyi watu mlimchagua ajiunge na Linda Sponsors? Kwa nini anaruhusu kuwa kibaraka wa kisiasa na kutumiwa na rais mstaafu?” Rais Ruto alisema. Pia alimshambulia Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, akimlaumu kwa kuacha jukumu la kuwa kiongozi mstaafu na kuingia katika siasa za upinzani dhidi ya serikali yake. Rais Ruto alisema Bw Kenyatta alikuwa akiwafadhili wanasiasa wanaompinga baada ya kushindwa kutekeleza baadhi ya mipango aliyokuwa nayo katika sekta ya elimu na afya. Akizungumza alipokuwa akikagua ujenzi wa Daraja la Dhogoye, Siaya, Rais Ruto aliunganisha ujumbe wa maendeleo na siasa, akisema serikali jumuishi imefungua ukurasa mpya wa maendeleo katika Nyanza. “Serikali jumuishi ndiyo muungano pekee wenye uwezo wa kuunganisha taifa letu. Ndiyo yenye historia ya utekelezaji, maono ya kuaminika ya siku zijazo na mpango wa kushughulikia changamoto zinazokabili taifa,” alisema. Alionya wapigakura dhidi ya kuunga mkono vyama vipya, akisema Kenya haiwezi “kujaribu” viongozi wasio na historia ya utekelezaji. “Taifa letu halitajaribu watu wanaofanya majaribio. Msicheze kamari na watu ambao hawana mpango au historia ya wazi ya kuwafanyia kazi wananchi,” alisema. Rais Ruto pia alimwalika Mbunge wa Ugenya David Ochieng, ambaye anaongoza chama cha Movement for Democracy and Growth (MDG), kujiunga na serikali jumuishi. Bw Ochieng alikubali ombi hilo, lakini akaomba Rais Ruto kumuunga mkono katika azma yake ya kumrithi Bw Orengo kama Gavana wa Siaya. Aliahidi kumpa Rais Ruto asilimia 99.9 ya kura za Ugenya katika uchaguzi wa 2027 iwapo atapata uungwaji mkono huo. “Nimefurahia kufanya kazi nawe, Mheshimiwa Rais, kwa sababu umekuwa rafiki mzuri. Umetusaidia kuendeleza Ugenya... ndiyo maana tutakupa asilimia 99.9 ya kura zetu,” alisema Bw Ochieng. Viongozi walioandamana na Rais Ruto walitumia ziara hiyo kumshambulia Gavana Orengo, ambaye hakuwa kwenye ziara hiyo. Waziri wa Kawi na Petroli Opiyo Wandayi alisema viongozi wengi wa Siaya wameungana isipokuwa mmoja, akimtaja Bw Orengo. “Rais Ruto, tuachie Orengo sisi. Tutahakikisha anaenda nyumbani,” alisema Bw Wandayi. Gavana wa Homa Bay na Mwenyekiti wa ODM Gladys Wanga pia alimshambulia Bw Orengo, akimtaka aache kupotosha jamii ya Luo. Naibu Gavana wa Siaya William Oduol alijitangaza kuwa kaimu gavana kutokana na kutohudhuria kwa Bw Orengo. Rais Ruto alitaja miradi kadhaa ya maendeleo ambayo serikali imepanga kutekeleza Siaya. Alisema ujenzi wa barabara ya kilomita 500 inayozunguka Ziwa Victoria utaanza Novemba 2026, baada ya kusubiriwa kwa zaidi ya miaka 15. Barabara hiyo itaunganisha Busia na Muhuru Bay kaunti ya Migori kupitia Siaya, Kisumu na Homa Bay. Aidha, Sh32 bilioni zitatumika kujenga kilomita 400 za barabara mpya Siaya. Rais Ruto pia alisema Sh10 bilioni zimetengwa kwa uchumi wa baharini, ikiwemo utafiti na teknolojia ya uzalishaji wa samaki wachanga, gati nne, huduma za feri na vituo vya uokoaji.
MAHAKAMA Kuu imebatilisha uuzaji wa asilimia 15 ya hisa za Serikali ya Kenya katika kampuni ya Safaricom kwa Vodacom Group, ikisema shughuli hiyo ilifanyika kinyume na Katiba na sheria za nchi. Jopo la majaji watatu liliamuru hisa hizo zirudishwe serikalini, likibaini kuwa mchakato wa uuzaji ulikumbwa na dosari nyingi ikiwemo ukosefu wa ushiriki wa kutosha wa umma, kufichwa kwa taarifa muhimu, uwekaji wa bei usio na msingi wa wazi na kutoshughulikiwa kwa masuala ya usalama wa taifa yaliyotokana na kuhamishwa kwa udhibiti wa kampuni hiyo kwa wawekezaji wa kigeni. “Kwa kuzingatia hitimisho letu, tunashikilia kuwa hakukuwa na ushiriki wa umma wa maana na wa kutosha kuhusu uuzaji huo. Hivyo basi, Kifungu cha 10 na 118 cha Katiba kilikiukwa,” walisema Majaji Francis Gikonyo, Roselyne Aburili na Tabitha Ouya. Uamuzi huo ni pigo kubwa kwa mpango wa serikali wa kukusanya fedha za Hazina ya Kitaifa ya Miundombinu kupitia uuzaji wa mali ya umma. Serikali iliuza hisa hizo kwa Sh204.3 bilioni kwa bei ya Sh34 kwa kila hisa. Aidha, ilipata takriban Sh40.7 bilioni kutokana na kuuza haki zake za kupata mgao baadaye kutoka kwa asilimia 20 ya hisa ilizobaki. Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na mwanaharakati Tony Gachoka pamoja na wengine waliopinga uuzaji huo, wakisema Safaricom ni rasilimali muhimu ya kitaifa. Mahakama ilikataa hoja ya Vodacom Group kwamba, kesi hiyo ilikuwa imepitwa na wakati baada ya Bunge kuidhinisha muamala huo Machi 31, 2026. Majaji walisema kesi hizo zilipinga msingi wa kikatiba wa muamala wenyewe na kwamba, idhini ya baadaye ya Bunge isingeondoa ukiukaji uliodaiwa. Mahakama ilisema kuwa ingawa Bunge lilifanya mikutano ya ushirikishaji katika kaunti 30, stakabadhi muhimu kama mkataba wa ununuzi wa hisa na makubaliano kuhusu haki za mgao wa baadaye hazikuwekwa wazi kwa umma. “Tunakubaliana na walalamishi kwamba, taarifa na stakabadhi muhimu zilifichwa umma, Baraza la Mawaziri na Bunge la Taifa,” majaji walisema. Mahakama ilisisitiza kuwa ushiriki wa umma si suala la kufanya mikutano pekee bali lazima uwe wa kweli, wa wazi, wa maana na unaowezesha wananchi kushawishi maamuzi yanayofanywa. Majaji pia walibaini kuwa serikali iliwasilisha mpango huo kama uuzaji wa sehemu ya hisa, ilhali kwa hakika ulikuwa ni mchakato mpana zaidi wa marekebisho ya umiliki ambao ungeipa Vodacom udhibiti halisi wa Safaricom. Chini ya mpango huo, hisa za Vodafone Kenya katika Safaricom zingepanda kutoka asilimia 39.9 hadi asilimia 55, huku Vodacom Group ikimiliki kikamilifu Vodafone Kenya. Kwa mujibu wa mahakama, hatua hiyo ilifanana zaidi na unyakuzi wa kampuni kuliko uuzaji wa kawaida wa hisa za serikali. Mahakama pia ilikosoa serikali kwa kutofungua uwekezaji huo kupitia mchakato wa wazi wa kuchagua mwekezaji wa kimkakati. Kuhusu bei ya Sh34 kwa kila hisa, majaji walikubaliana kuwa mchakato uliotumika haukuwa wa kimantiki na ulikuwa wa kiholela. Zaidi, mahakama ilieleza kuwa muamala huo ulizua masuala mazito ya usalama wa taifa kwa kuwa Safaricom inaendesha miundombinu muhimu inayotumika katika uchaguzi, mifumo ya malipo ya serikali, huduma za fedha za simu na kuhifadhi data binafsi za mamilioni ya Wakenya. Majaji walisema kuhamisha udhibiti wa miundombinu hiyo kwa kampuni ya kigeni bila tathmini ya awali ya usalama wa taifa kulikiuka wajibu wa serikali wa kulinda maslahi ya nchi. Hivyo, mahakama ilitangaza uuzaji huo kuwa batili, ikafutilia mbali uamuzi wa Bunge uliouidhinisha pamoja na idhini yenyewe, mikataba na hatua zote zilizohusiana nao. Mahakama iliamuru asilimia 15 ya hisa za Safaricom zirudishwe chini ya umiliki wa Serikali ya Kenya kwa niaba ya wananchi. Pia ilikataa kusimamisha utekelezaji wa hukumu hiyo ili kuruhusu rufaa, na kuwaelekeza wahusika kuwasilisha ombi rasmi la kusitisha utekelezaji iwapo wanataka kufanya hivyo.