
Category
Education policy, exam results and calendars, scholarships and opportunities for students, parents and teachers across the region.


MASWALI yameibuka kuhusu uwezo wa shule kuhudumia wanafunzi wapya wanaotarajiwa kujiunga na Sekondari Pevu mwakani. Haya yanajiri huku Waziri wa Elimu, Julius Ogamba akisema shule zina uwezo wa ziada na Wizara ya Elimu inatarajia asilimia 100 ya wanafunzi 1.13 milioni kujiunga na Sekondari Pevu. Hata hivyo, baadhi ya wakuu wa shule wanahisi hawako tayari kikamilifu. Wakuu wa shule waliozungumza na Taifa Leo wameelezea wasiwasi wao kuhusu mkondo wa Sayansi, Tekinolojia na Hisbati (STEM) kutokana na ukosefu wa miundombinu ya ICT na vifaa. “Tunasema wanafunzi 1.13 milioni watajiunga na shule za sekondari huku uwezo wa shule ukiwa 1.5 milioni, tuko sawa na tunatarajia asilimia 100 ya wanafunzi ambao matokeo yao tumeyatoa leo,” alisema Katibu wa Elimu ya Msingi, Julius Bitok, jana wakati wa uzinduzi wa matokeo ya KJSEA. Bw Ogamba alisema nafasi katika shule 9,540 za sekondari zitaongezeka wanafunzi 929,262 watakapomaliza shule za sekondari baada ya Mtihani wa (KCSE) mwaka huu. Wanafunzi watateuliwa katika shule za sekondari kulingana na Makundi- 1 hadi 4 -kulingana na utendaji wao na mkondo waliyochagua—STEM, Sanaa na Michezo, na Sayansi za Jamii. Hata hivyo, ukibaki mwezi mmoja tu kabla ya tarehe ya kuripoti ya Januari 12, 2026, vitabu vya Kiingereza pekee ndivyo vilivyofikishwa shule. Hii imesababishwa na deni la Sh10 bilioni wanazodai wachapishaji. Aidha, baadhi ya shule hazina maabara za kompyuta zinazofanya kazi na zinashindwa kulipa madeni ya vifaa vilivyonunuliwa. “Mbali na kutokuwa na kompyuta, tuna madeni ya vifaa vya maabara ikiwemo kemikali,” alisema mkuu wa shule ambaye hakutaka kutajwa jina. Mkuu mwingine wa shule anakadiria kuwa kubadilisha darasa moja kuwa maabara ya kompyuta kutagharimu takriban Sh700,000, pesa ambazo hawana.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameeleza mafanikio ya sekta ya elimu, ikiwemo ongezeko la bajeti ya wizara hiyo kwa asilimia 40 kutoka mwaka 2021/2022 hadi 2025/2026. Amesema chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, serikali imeongeza fedha za mikopo ya elimu ya juu kutoka Sh bilioni 464 hadi bilioni 916.7 zinazotolewa katika vyuo vikuu na vyuo vya kati. The post Bajeti ya elimu juu 40% miaka mitano first appeared on HabariLeo.

IRINGA: Chuo Kikuu cha Iringa (UoI) kimesema mageuzi yaliyofanywa na Mahakama Kuu Kanda ya Iringa katika miaka 20 ya uwepo wake yameleta mabadiliko makubwa katika namna wananchi wanavyofikiwa na huduma za haki. Akiwa mwenyeji wa ugeni wa viongozi wa Mahakama Kuu chuoni hapo, Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo, Kaleb Lameck Gamaya (Adv), alisema mafanikio … The post Mahakama Kuu Iringa yafungua mlango haki kwa wote first appeared on HabariLeo.

RAIS Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi awamu ya sita Dk Amani Abeid Karume pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Awamu ya Saba Dk Ali Mohamed Shein wameitaka Ofisi ya Makamu wa Rais kuendelea kutoa elimu ya kutosha ya Muungano ili misingi ya Muungano iliyowekwa na … The post Karume, Shein wataka elimu ya Muungano idumishwe first appeared on HabariLeo.

DAR ES SALAAM: Taasisi ya EMCA, inayojihusisha na utunzaji wa mazingira na utoaji wa elimu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo, imeendelea na kampeni yake ya “Tuelimishe Mazingira” kwa kutembelea Shule ya Msingi Mlimani Demonstration jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa EMCA, Zafarani Ramadhani, alisema … The post EMCA Yasistiza utunzaji mazingira first appeared on HabariLeo.

DAR ES SALAAM: MKUU wa Chuo Kikuu cha Mzumbe ambaye pia ni Rais mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, amewataka wahitimu wa chuo hicho pamoja na vijana nchini kujenga mitandao imara ya kitaaluma na kuendelea kulinda amani na mshikamano wa taifa, akisisitiza kuwa ndiyo msingi wa mafanikio … The post Dk Shein: Vijana jengeni mitandao ya kitaaluma first appeared on HabariLeo.

DAR ES SALAAM: CHUO KIKUU cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimesema kinatarajia kuongeza upanuzi wa uwezo wa udahili wa wanafunzi katika fani za afya, mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu mipya na ya kisasa kupitia Mradi wa Mageuzi ya Elimu ya Juu kwa Uchumi ( HEET). Mkuu wa MUHAS, Profesa David … The post Miundombinu mipya kuongeza masomo ya afya MUHAS first appeared on HabariLeo.

MBEYA: Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed, ametoa wito kwa wataalamu wa jiosayansi nchini kuanza mikakati madhubuti ya kutoa elimu na kuhamasisha wanafunzi kuifahamu na kuipenda fani hiyo ili kuongeza idadi ya wataalamu. Amesema licha ya umuhimu mkubwa wa jiosayansi katika maendeleo ya taifa, bado uelewa wake miongoni … The post ‘Wekeni mikakati wanafunzi waifahamu jiosayansi’ first appeared on HabariLeo.

CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) kimesema kimepata Sh bilioni 120 kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET). Mwenyekiti wa Baraza la MUHAS, Dk Harrison Mwakyembe amesema hayo wakati Mahafali ya 19 ya chuo hicho jijini Dar es Salaam. The post Bil 120/- mradi wa HEET zaineemesha MUHAS first appeared on HabariLeo.

WANAFUNZI watakaojiunga na Gredi 10 mwezi ujao watahitaji kufundishwa na walimu 58,590 zaidi kwa masomo spesheli chini ya Mtaala wa Umilisi na Utendaji (CBC). Masomo yaliyoathirika zaidi ni Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hesabu maarufu kama STEM japo mengine pia yameathirika kwa wastani. Hii ni kwa sababu wanafunzi 569,000, ambayo ni idadi ya juu zaidi, ndio walichagua masomo hayo yenye upungufu wa walimu 35,111. Masomo ya sayansi ya kijamii yanahitaji walimu 14,630 kisha yale ya sanaa na michezo yana upungufu wa walimu 8,778. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tume ya Kuwaajiri Walimu Nchini (TSC) anayesimamia ubora wa elimu Dkt Reuben Nthamburi, upungufu umepanda kutokana na mfumo mpya wa elimu. “STEM itakuwa na asilimia 60 ya wanafunzi ambao ni 677,144 kwenye madarasa 15,046. Tulifanya hesabu kwa kutumia darasa ambalo lina wanafunzi 45 ambako tunawahitaji walimu 35,111. Kwa sayansi ya kijamii tunawahitaji walimu 14,630 kisha sanaa na michezo inahitaji 8,778 ambapo idadi ya jumla ni 58,519,” akasema Dkt Nthamburi. TSC pia ilitoa wito kwa vyuo vikuu na vyuo vya ualimu kuhakikisha mafunzo yao yanaoana na hitaji jipya la soko hasa kwenye masomo ya sanaa na michezo. Dkt Nthamburi alisisitiza kuwa idadi ya walimu inastahili kuoana na wanafunzi hasa kwenye masomo ya STEM ambayo yamechukuliwa na wanafunzi 569,000 kati ya wanafunzi milioni 1.1 katika Gredi ya Nne. Wanafunzi hao wanahitaji walimu 35,111. Masomo ya sayansi nayo yalichaguliwa na wanafunzi 437,000 ambao watahitaji walimu 14,630 nao wanafunzi 124,000 wa Sanaa na Michezo wanahitaji wanafunzi 8,778. Afisa huyo wa TSC aliwaomba manaibu chansela wa vyuo vikuu na wakufunzi kwenye vyuo vya mafunzo wamakinikie vitengo muhimu katika kuwanoa walimu.
IDARA ya Afya katika kaunti ya Kisumu imeelezea hofu kuhusu mwenendo wa wanaume kuwaambukiza virusi vya HIV wake zao waja wazito. Mkurugenzi wa Afya ya Umma, Dkt Fredrick Oluoch alisema kuwa wamegundua visa ambapo akina mama huwa hawana virusi hivyo miezi ya kwanza kabla ya kupata uja uzito lakini hupatikana na HIV wanapokaribia kujifungua. Alisema hali hii huchangiwa na mwenendo wa wanaume kushiriki ngono na wapenzi wenye virusi hivyo kisha kuleta virusi hivyo kwa nyumbani kwa wake zao wenye uja uzito. “Tunaendelea kushuhudia hali inayotishia ambapo mama hupimwa na kutopatikana na virusi miezi mitatu ya kwanza ya uja uzito na katika miezi tatu ya mwisho kabla ya wao kujifungua, hupatikana na virusi hivyo. Hii ina maana kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba walipata virusi hivyo kutoka kwa waume zao wanaoshiriki mapenzi bila kinga nje ya ndoa,” akasema Dkt Oluoch. Afisa hiyo alisema hayo wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani zilizofanyika katika Shule ya Msingi ya Kisian, Kaunti Ndogo ya Kisumu Magharibi. Haya yanajiri wakati Baraza la Kitaifa la Kudhubiti Magonjwa Sugu (NSCC) imetoa ripoti inayoonyesha kwamba Kisumu ni miongoni mwa kaunti zilizoandikisha viwango vya juu vya maambukizi mapya ya HIV nchini mnamo 2024. Kiwango cha maambukizi ya HIV katika kaunti ya Kisumu ni asilimia 11 huku ikikadiriwa kuwa watu 111,367 wanaishi na virusi vya HIV vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi. Katika mwaka wa 2024, kaunti ya Kisumu iliandikisha maambukizi mapya 1, 341 ya virusi hivyo huku idadi ya wanawake ikiwa wengi (755) kuliko wanawake (361). Kwa upande mwingine, maambukizi mengine 225 yaliandikishwa katika watoto. Visa vya akina mama kuwaambukiza watoto wao (MTCT) vilipungua kutoka kima cha asilimia 9 mnamo 2019 hadi asilimia 5.97 mnamo 2024. Dkt Oluoch alisema Idara ya Afya katika Kaunti ya Kisumu inaazimia kupunguza kiwango hicho cha maambukizi hadi chini ya asilimia tano (5). Afisa huyo alisema japo visa vya maambukizi vimepungua kutokana na juhudi zinazoendeshwa kwa idara yake, juhudi hizo hata hivyo zinahujumiwa na mienendo ya wanaume kuwa na wapenzi wengi nje ya ndoa. “ Wanaume hawa wanafaa kuwalinda wake zao waja wazito kwa kukoma kujihusisha katika ngono bila kinga na wapenzi nje ya ndoa. Wanapaswa kuwa watulivu, wawalinde wake zao nyakati za uja uzito,” akasema Dkt Oluoch.
Shikamoo shangazi. Nimenaswa kimapenzi na msichana fulani. Juzi nilimtembelea kwao kwa mara ya kwanza. Mama yake hajaolewa tena ni mchanga na mrembo sana. Nimechanganyikiwa! Nishauri tafadhali. Ni wazi kwamba mama ya msichana huyo pia amenasa moyo wako kimapenzi. Sasa unashindwa utamchagua yeye ama ni binti yake. Jipe muda ufikirie kisha uamue. Ninaamini mama amekuzidi umri ingawa hiyo si hoja bora mapenzi. Nampenda tusiyeonana Nilijuana na mwanamume fulani kupitia kwa mtandoa na hatimaye tukapendana ingawa hatujawahi kuonana. Huu sasa ni mwezi wa sita tangu tulipojuana. Haya ni mapenzi ya kweli? Kuna visa kadhaa vya watu waliojuana na kupendana kupitia kwa mtandao na hatimaye wakaoana. Hata hivyo, hatimaye mtahitaji kukutana na kuwa pamoja kwa muda ndipo mjue ukweli wa mapenzi yenu. Eti ataacha tu mubaba iwapo nitaamua kumuoa Za kwako shangazi. Kuna mwanamke ninayemtaka lakini amekuwa akinizungusha tu. Hatimaye juzi alifungua moyo wake. Akaniambia ana uhusiano na mtu aliye na familia na atamuacha tu kama niko tayari kumuoa. Nishauri. Mwanamke huyo amekwambia anachotaka; mume wake mwenyewe. Na ndiyo sababu anataka kwanza umhakikishie kwamba nia yako kwake ni ndoa. Kama unaamini anatosha na uko tayari kwa ndoa, kazi kwako. Niko shule ya upili ila nimemfia jamaa fulani Shikamoo shangazi. Nina miaka 16 na ninasoma katika shule ya upili. Kuna mwanamume anayenitaka kimapenzi. Nampenda lakini nahofia mapenzi yataathiri vibaya masomo yangu. Nishauri. Msimamo wako hasa ndio ushauri wangu kwako. Wewe bado ni mwanamke mchanga na masomo ndiyo tegemeo lako maishani. Mwelezee msimamo wako huo. Kama kweli anakupenda atangojea.

IRINGA: Kijana wa kimasai, Lekishon Koipa, ameandika historia nyingine katika Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) baada ya kuibuka kinara wa ufaulu kwa kupata GPA ya juu kuliko wote chuoni 4.8. Kijana huyo mhitimu wa digrii ya awali ya elimu jamii na ualimu kwa mwaka 2025, ametangazwa kuwa mfano hai wa ushindi dhidi ya vikwazo … The post Kijana wa kimasai avunja rekodi chuo cha Mkwawa first appeared on HabariLeo.
IDARA ya Kuchunguza Uhalifu (DCI) katika Kaunti ya Mombasa inaendeleza upelelezi kuhusu kifo cha msichana mwenye umri wa miaka mitano aliyedaiwa kuanguka kutoka juu ya jengo la madrassa baada ya kufungiwa ndani kama adhabu. Tukio hilo lililotokea Novemba 18 asubuhi katika Madrassa Tul Nur eneo la Leisure, Nyali, limezua ghadhabu miongoni mwa wakazi na makundi ya kutetea haki za watoto, wanaotaka haki itendeke. Ripoti za awali za polisi zinaonyesha kuwa mtoto huyo alitenganishwa na wenzake na kufungiwa ndani kama adhabu. Watoto wengine walipokwenda kucheza, inadaiwa alijaribu kutoroka kupitia dirishani akaanguka na kupoteza maisha papo hapo. Afisa wa Upelelezi wa Kaunti Ndogo ya Nyali Mohamed Jillo, alisema maafisa wa DCI tayari wameandikisha taarifa kutoka kwa walimu, wanafunzi na uongozi wa madrassa. “Hili linaonekana kama suala la uzembe. Tunachunguza maelezo yote, kukusanya ushahidi na kubaini iwapo kuna mtu aliyekosa kutimiza wajibu wake,” akasema Bw Jillo katika mahojiano na Taifa Leo afisini mwake. Aliongeza kuwa, uchunguzi utabaini iwapo madrassa hiyo inafuata kanuni za ulinzi wa watoto zilizo katika sheria ya elimu ya msingi na sheria ya watoto. Mdokezi kutoka madrassa, ambae hakutaka kutajwa, alisema mama ya msichana huyo alikuwa amemuelekeza mwalimu amuadhibu binti yake kwa sababu alikataa kwenda madrassa asubuhi hiyo. Hivyo mwalimu akamzuia kuungana na wenzake wakati wa mapumziko ya saa nne asubuhi. Uongozi wa madrassa ulisema hautatoa taarifa kwa sasa hadi uchunguzi utakapokamilika. Kwa upande mwingine, familia ya msichana pia haikutaka kuhojiwa. Tukio hilo limezua mjadala mkali mitandaoni, watumiaji wakitaka maelezo ya kina kuhusu mazingira yaliyopelekea kifo hicho na kuwataka viongozi wa madrasa kuwajibika. Mashirika ya kutetea haki za watoto pia yametaka uchunguzi wa kina na kuchukuliwa hatua za haraka dhidi ya wahusika. Kuhusu madai kwamba wazazi wanashinikizwa kuacha kufuatilia kesi, maafisa wa DCI walisisitiza kuwa uchunguzi unaendelea kwa uwazi. Afisa wa watoto mjini Mombasa, Bw Gabriel Kitile, alisisitiza umuhimu wa kutumia mbinu salama kwa watoto katika taasisi zote za elimu, rasmi na za kidini. “Kilichotokea ni kielelezo kwamba hakuna mtoto anayepaswa kuwekwa hatarini kwa jina la adhabu. Kila kituo cha elimu lazima hakikishe watoto wanawekwa kwa uangalifu na wanalindwa kila wakati," akasema. Uchunguzi ukikamilika, faili itawasilishwa kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) ili kuamua hatua zinazofaa kuchukuliwa.

IRINGA;Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Kikwete, ameongoza mahafali ya 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) mjini Iringa leo, ambapo ametunuku shahada mbalimbali za umahiri na za awali kwa wahitimu. Katika ngazi ya umahiri, amewatunuku Digrii ya Umahiri wa Sayansi na Ualimu … The post JK aongoza mahafali ya 17 MUCE first appeared on HabariLeo.
WATOTO sita miongoni mwa 10 duniani kote hawajui kusoma sentensi rahisi wala kusuluhisha maswali ya kimsingi ya hesabu licha ya thuluthi yao kuwa shuleni kwa sasa. Haya ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na shirika linalofahamika kama People's Action for Learning (PAL) Network iliyotathmini matokeo ya masomo miongoni mwa watoto 89,870 wenye umri wa miaka mitano hadi 16 katika mataifa 12. Matokeo hayo yamezua wasiwasi mkubwa kuhusu ubora wa elimu katika mataifa mengi maskini kwa kufichua kwamba kuhudhuria shule pekee sio hakikisho la masomo halisi. Ripoti hiyo inaashiria kwamba Kenya inaongoza majirani zake barani Afrika Mashariki katika kufanikisha Viwango vya Chini zaidi vya Ufaafu (MPL) katika hisabati, licha ya changamoto zinazoendelea kama vile upungufu wa walimu, uhaba wa vifaa vya masomo na maswala yanayohusu vipimo. Kulingana na ripoti, asilimia 43 ya watoto wenye umri wa miaka 10 nchini wanatimiza kiwango kinachohitajika cha MPL ikilinganishwa na asilimia 33 Tanzania na asilimia 4 Uganda. MPL ni vipimo maalum vya kimataifa vinavyoonyesha kile ambacho mtoto anahitajika kujua mwishoni mwa elimu ya msingi ya chini. Vinajumuisha uelewa wa kimsingi wa kusoma na ujuzi wa kimsingi kuhusu tarakimu kama vile kutatua tarakimu kamilifu hadi 100 na kusuluhisha hesabu rahisi. Matokeo bora kwa kiasi fulani ya Kenya yanaashiria kupiga hatua katika elimu ya kimsingi, ingawa taifa hili bado linavuta mkia ikilinganishwa na nchi zilizoandikisha matokeo bora kama vile Mexico, Nicaragua, na Pakistan. “Pana haja ya kutathmini upya vifaa vya ufundishaji katika shule zetu kuhakikisha vinapiga jeki somo la tarakimu katika madarasa yetu,” alisema mkurugenzi wa Wizara ya Elimu, Martin Kungania, ripoti za kimataifa kuhusu mitihani ya kimsingi kwa tarakimu (ICAN) na kusoma (ICAR) zilipotolewa. Udadisi huu uliofanyika wiki ya kwanza ya Januari na wiki ya pili ya Agosti nchini Kenya, ulishirikisha watoto 6,669 na familia 4,459. Nchi zilizoshiriki udadisi huo ni pamoja na Kenya, Tanzania, Uganda, Senegal, Mali, Mozambique, Botswana, Bangladesh, Pakistan, Nepal, Mexico, na Nicaragua. Katika sehemu kubwa ya nchi zilizoshiriki, watoto wapatao tisa miongoni mwa 10 wamejiunga na shule, huku wengi wao wakihudhuria taasisi za umma, japo idadi kubwa wanasomea shule za kibinafsi. Kenya imejitokeza kuwa yenye idadi ndogo zaidi ya watoto wasioenda shule.Hii inaashiria kuwa juhudi za serikali za kufanikisha asilimia 100 ya watoto wanaojiunga na sekondari kutoka shule ya msingi, zinazaa matunda. Miongoni mwa watoto Wakenya wenye umri kati ya miaka 10 – 14, zaidi ya asilimia 80 wanahudhuria shule za umma, huku asilimia 16 wakihudhuria shule za kibinafsi na kuacha chini ya asilimia mbili ambao hawako shule. Duniani kote, Mexico inaongoza kwa idadi kubwa zaidi ya watoto waliojiunga na shule za umma kwa asilimia 90 ikifuatiwa na Tanzania asilimia 87 na Mozambique asilimia 85.
MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Meru ameshtakiwa kwa kuuza karatasi bandia za mtihani wa kidato cha nne (KCSE) mwaka 2025. Nasiuma Chrispinus Nambafu, mwenye umri wa miaka 22, alishtakiwa katika Mahakama ya Milimani. Nambafu alifika mbele ya Hakimu Benmark Ekhubi ambapo alikana mashtaka matano ya kuchapisha habari za uongo, kumiliki vifaa vya mtihani bandia vinavyodaiwa kutoka kwa Baraza la Mitihani la Kenya (KNEC), na kumiliki vitambulisho vya kitaifa vya watu wengine kinyume cha sheria. Kulingana na karatasi ya mashtaka iliyowasilishwa mahakamani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) kupitia kiongozi wa mashtaka Sonia Njoki, Nambafu alishtakiwa kwamba kati ya mwaka 2022 na Oktoba 11, 2025, alidai kuchapisha taarifa za uongo na kupotosha kupitia kundi la WhatsApp lililoitwa “Teachers KNEC Exams 2025”, akidai kwamba alikuwa na mitihani halali ya KCSE kutoka kwa KNEC. Katika mashtaka mengine matatu, Nambafu anakabiliwa na tuhuma za kupatikana na vitambulisho vya utaifa vya Lucy Muthoni Kimencu, Bosco Kioko Wambua, na Doris Kathini Kimencu, bila ruhusa ya kisheria, katika eneo la Kianjai, Kata ya Tigania Magharibi, Kaunti ya Meru. Anadaiwa kupatikana na vitambulisho hivyo vya utaifa katika nyumba yake mnamo Oktoba 11, 2025, wakati maafisa wa DCI walipomkamata. Mwanafunzi huyo aliiambia mahakama kuwa alikamilisha masomo katika Chuo Kikuu cha Meru cha Sayansi na Teknolojia (MUST) katika masomo ya Hisabati na Kemia na alikana mashtaka yote, akiomba mahakama impe dhamana inayofaa, akisema yeye anatoka katika familia maskini. Hakimu Ekhubi aliwachilia kwa dhamana ya Sh100,000 na wadhamini wawili wa kiasi sawa.Kesi hii itatajwa tena Novemba, 15 2025.

DAR ES SALAAM: Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimepiga hatua kubwa katika kuboresha elimu ya afya nchini kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), unaotekeleza ujenzi wa Ndaki ya Tiba katika Kampasi za Mloganzila na Kigoma. Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo, Makamu … The post Prof. Kamuhabwa: Mradi wa HEET umeleta mageuzi MUHAS first appeared on HabariLeo.
MITIHANI ya kitaifa kwa wanafunzi zaidi ya milioni 3.4 kutoka shule za umma na za kibinafsi ilianza jana kote nchini. Mitihani hiyo inajumuisha ya wanafunzi wa Gredi ya Sita (KPSEA), Gredi ya Tisa (KJSEA) pamoja na KILEA na KPLEA kwa wanaofuata mtaala wa hatua za kujifunza. Akisimamia usambazaji wa karatasi za mtihani katika Kaunti Ndogo ya Bureti, Kaunti ya Kericho, Waziri wa Elimu Julius Ogamba alihakikishia umma kuwa hatua madhubuti zimewekwa ili kulinda uadilifu wa mitihani. Mwaka huu, jumla ya wanafunzi 3,428,729 wanafanya mitihani katika vituo 68,546 wakiwemo 1,298,089 (KPSEA), 1,130,669 (KJSEA), 2,414 (KILEA) na 1,479 (KPLEA). KPSEA ni ya kuchagua majibu pekee, huku KJSEA ikiwa na maswali ya kuchagua na inayo hitaji majibu ya kuandikwa. Polisi watalinda tu mtihani wa KCSE, huku KPSEA na mitihani mingine ikisimamiwa na walimu na maafisa wa elimu. Katika Kaunti ya Trans Nzoia, baadhi ya vituo vikiwemo Matisi Friends, Central Primary School, St John’s Education Centre, Linta Academy na Royal Victor vilipata mkanganyiko wa karatasi za mtihani. Mkurugenzi wa Elimu wa kaunti hiyo, Pamela Akello, alithibitisha tukio hilo, lakini akasema lilitatuliwa bila kuathiri uadilifu wa mtihani. Aliongeza kuwa kuchelewa kuliathiri wanafunzi ambao hawakuhudhuria majaribio ya maandalizi. Trans Nzoia ina wanafunzi 24,312 wa KJSEA na 26,961 wa KPSEA katika shule za umma, na 23,097 wa KJSEA na 5,174 wa KPSEA katika shule binafsi. Shule za Kitale School na Mary Immaculate Primary ziliendelea vizuri na mitihani. Katika Kaunti za Uasin Gishu na Baringo, mitihani ilianza chini ya ulinzi mkali. Katika Kaunti ya Uasin Gishu, Mkurugenzi wa Elimu David Koech alisema wanafunzi 10 wanafanya mitihani hospitalini jijini Eldoret, akiwemo mama mchanga na wengine waliotoka kaunti jirani. Kamanda wa Polisi, Benjamin Mwanthi, alionya dhidi ya udanganyifu na kuwaonya polisi dhidi ya kubeba simu wakiwa kazini. Katika Kaunti ya Baringo, mitihani ilianza bila matatizo katika vituo 756, na vifaa vikitolewa kutoka kontena 19. Dkt Kipruto Kosgei, ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu wa kaunti hiyo, alisema kuna wanafunzi 15,672 wa KPSEA na 15,411 wa KJSEA. Hata shule zilizokuwa zimeathiriwa na mafuriko kama Noosukro na Loruk Primary, zimeshiriki mitihani hiyo. Ulinzi pia umeimarishwa kwa wadau wote. Katika Kisumu Central, kontena ya mitihani ilifunguliwa saa kumi na mbili asubuhi na Naibu Kamishna wa Kaunti Langat Bosek. Mwenyekiti wa Baraza La Kitaifa La Mitihani Kenya (KNEC) Profesa Julius Nyabundi alisisitiza mabadiliko kutoka neno “mitihani” kwenda “tathmini” na kupunguza uwepo wa polisi shuleni ili kujenga uaminifu. Katika Kaunti ya Kisii, mitihani ilianza vyema katika vituo vyote. Naibu Kamishna Joseph Mwangi anayesimamia Kisii Central na Nyaribari Chache, alisimamia usambazaji wa mitihani katika shule 78 za umma na 14 za binafsi. Katika Kaunti ya Homa Bay, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kitaifa ya Kukuza Mitaala (KICD) Prof Charles Ong’ondo alisema matokeo yatatangazwa kabla ya Sikukuu ya Krismasi. Alibainisha kuwa tathmini za mfumo wa CBE ni sehemu ya mabadiliko kutoka mfumo wa 8-4-4 na akawahimiza wazazi na walimu kuwa watulivu. Aliongeza kuwa polisi watasimamia tu mtihani wa KCSE. Kamishna wa Kaunti Ronald Muiwawi alikiri kuwepo kwa udanganyifu zamani kuliweka doa katika mitihani ya kitaifa miaka ile, huku Mkurugenzi wa Elimu Eunice Khaemba akisema kuna wanafunzi 39,436 wa KPSEA na 36,496 wa KJSEA. Katika Kaunti ya Siaya, kontena ilifunguliwa saa kumi na mbili asubuhi, na wakuu wa shule wakakusanya vifaa kwa wakati. Naibu Kamishna Robert Ngetich aliwataka wasimamizi na wanafunzi kuwa waadilifu, hasa ikizingatiwa kuwa huu ndio mtihani wa kwanza wa KJSEA. Katika kaunti zote Kericho, Trans Nzoia, Uasin Gishu, Baringo, Kisumu, Kisii, Homa Bay na Siaya, serikali imesisitiza uzingatiaji wa sheria, uadilifu na usalama katika kuhakikisha mitihani ya kitaifa inafanywa kwa haki na uaminifu.
MWANAFUNZI wa shule ya upili iliyo eneo la Lamu ya Kati, Kaunti ya Lamu, huenda akalazimika kufanya mitihani yake ya KCSE akiwa chini ya ulinzi wa polisi. Hii ni kutokana na kuwa, alikamatwa na kuwekwa rumande kwa sababu ambazo hazijabainika. Wanafunzi wa Kidato cha Nne walianza KCSE Jumanne iliyopita, kwa mitihani ya Utendaji. Wakati huo huo, mwanafunzi wa mtihani wa kitaifa wa Gredi ya Sita (KPSEA) kutoka Shule ya Faza Boys Comprehensive, Lamu Mashariki, alilazimika kufanya mtihani wake katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya King Fahd ambako amelazwa akipokea matibabu baada ya mkono wake kuvunjika. “Ninafahamu kuwa kuna mwanafunzi amelazwa katika Hospitali ya King Fahd na amefanyiwa upasuaji kwenye mkono uliovunjika. Tumeandaa mipango ili aweze kufanya mtihani wake huko. Pia kuna mwanafunzi mwingine aliye rumande lakini tumefanya mipango ya haraka na naye anafanya mtihani akiwa huko. Hadi sasa kila kitu kinaendelea vizuri,” alisema Mkurugenzi wa Elimu wa Kaunti ya Lamu, Bw Zachary Mutuiri. Mitihani ya KPSEA na KJSEA kitaifa ilianza jana (Jumatatu). Watahiniwa 36 wa KPSEA na KJSEA kutoka msitu wa Boni, Kaunti ya Lamu, walihamishiwa maeneo mengine kufanya mitihani hiyo. Kulingana na Bw Mutuiri, hatua hiyo ilichukuliwa sababu kuu ikiwa ni shule husika kukosa idadi kamili ya angalau watahiniwa 15 wa KPSEA au KJSEA wanaohitajika kuwezesha taasisi zao kuorodheshwa kuwa vituo vya kujisimamia kufanya mitihani hiyo. Kaunti hiyo ina watahiniwa 3,498 wa KPSEA ilhali wale wa KJSEA ni 4,432. Katika Kaunti ya Tana River, Naibu Kamishna, Bw Andrew Mutua, alisema ingawa baadhi ya wanafunzi waliripotiwa kutoweka katika baadhi ya maeneo, hakuna mwanafunzi aliyesajiliwa atakayefanya mtihani hospitalini au gerezani. “Hatutawaacha. Leo tunawatuma machifu kuhakikisha tunapata asilimia 100 ya wanafunzi wote kufanya mitihani,” alisema. Kwa mujibu wa maafisa wa elimu, zaidi ya wanafunzi 5,000 wanafanya mitihani katika maeneo mbalimbali ya Kaunti ya Tana River. Bw Mutua aliwahakikishia wazazi na wadau kuwa mitihani inaendelea kwa utulivu na serikali imejizatiti kuhakikisha mazingira ya haki na amani katika vituo vyote vya mitihani. Huko Mombasa, manyunyu madogo hayakuathiri morali ya walimu na watahiniwa. Mkurugenzi wa Elimu wa Kanda, Bi Anne Kiilu, aliwahimiza walimu kuendelea kuwahamasisha wanafunzi wote wakati wa kipindi hiki cha mitihani, akisema kuwa eneo hilo lina lengo la kuinua viwango vyake vya kitaaluma. Kaunti ya Mombasa ina vituo 573 vya KPSEA vyenye jumla ya watahiniwa 27,498, na vituo 273 vya KJSEA vyenye watahiniwa 21,677. Katika Kaunti ya Taita Taveta, Mkurugenzi wa Elimu wa Kaunti hiyo, Bw Khalif Hirey, alisema maandalizi yote yamekamilika kuhakikisha mitihani inafanyika kwa uwazi kote kaunti nzima. Kaunti hiyo ina vituo 205 vya KPSEA na 194 vya KJSEA ambapo jumla ya watahiniwa 7,546 na 6,867 mtawalia wanakalia mitihani hiyo. Ripoti za Kalume Kazungu, Stephen Oduor, Mishi Gongo na Lucy Mkanyika

DAR ES SALAAM: Mgombea urais kupitia chama cha UMD, Mwajuma Mirambo, ameendelea na kampeni zake za kunadi sera za chama hicho leo jijini Dar es Salaam, katika Wilaya ya Ilala, Jimbo la Segerea, kata ya Vingunguti, kwenye uwanja wa Msikate Tamaa. Akizungumza mbele ya wananchi waliojitokeza kwa wingi, Mirambo amesema serikali ya UMD ikipewa ridhaa … The post Mgombea urais UMD aahidi elimu, afya bora first appeared on HabariLeo.

WANAFUNZI 135,240 waelimu ya juu na ya kati wamepata udhamini wa masomo kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wa thamani ya Sh bilioni 426.5 kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dk Bill Kiwia kwenye mkutano wake na waandishi wa habari jijini Arusha. Dk … The post Wanafunzi 135,240 wapata mikopo first appeared on HabariLeo.

MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, ameahidi kuuenzi urithi wa Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad kwa kujenga Chuo Kikuu cha Maalim Seif Sharif Hamad katika mji wa Wete, Kaskazini Pemba. “ Chuo hichi kitakuwa ni ngome ya maarifa , uzalendo na maendeleo endelevu kwa vizazi vijavyo,” alisema Masoud. The post Othman aahidi Chuo Kikuu kumuenzi Maalim Seif first appeared on HabariLeo.

Na John Mhala,Arusha WANAFUNZI 135,240 wa vyuo vikuu na kati hapa nchini wenye sifa stahiki na waliodahiliwa na vyuo vyao wamefanikiwa kupata mikopo ya awamu ya kwanza ya Sh Bilioni 426.5. Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB), Dk Bill Kiwia mbele ya waandishi … The post HESLB yafafanua waliopata mikopo first appeared on HabariLeo.

WANAFUNZI kutoka shule za Msingi na Sekondari wameipongeza Serikali kwa ujenzi wa miundombinu bora na rafiki ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari, ambayo imechagiza ufundishaji na ujifunzaji. Hayo yamebainika leo Oktoba 24, 2025 jijini Dodoma, katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tathmini ya pamoja ya Sekta ya Elimu. Mwanafunzi mwenye mahitaji maalum, kutoka … The post Wanafunzi wapaza sauti katika tathmini ya elimu ya mwaka first appeared on HabariLeo.

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinaendelea kutekeleza kwa mafanikio Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET), unaolenga kuboresha miundombinu, kuimarisha mitaala, na kukuza mfumo wa kujifunza kidijitali. Mradi huu ni kiungo muhimu katika kuhakikisha elimu ya juu inachangia uchumi wa viwanda na maendeleo endelevu ya Taifa. The post HEET kuboresha miundombinu ya elimu UDSM first appeared on HabariLeo.

NI asubuhi yenye upepo mwanana katika viunga vya Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (RUCU) mkoani Iringa. Ndani ya ukumbi wa mikutano, wasomi, wachumi na wadau wa maendeleo wameketi kwa makini katika kongamano la kujadili mustakabali wa Tanzania kuelekea mwaka 2050. Kaulimbiu ya kongamano hilo lililoandaliwa kwa ushirikiano wa RUCU na Kituo cha Ubia kati ya … The post PPP nguzo ya utekelezaji Dira 2050 first appeared on HabariLeo.
SHULE zinapofungwa wiki hii kwa likizo ya muda wa miezi miwili, Wizara ya Elimu bado inakabiliwa na changamoto kufuatia mgao wa elimu kutotolewa kwa wakati kwa shule mbalimbali. Haya yanatokea huku Hazina Kuu ya Fedha na Wizara ya Elimu zikishirikiana kubadilisha kalenda ya ufadhili kutoka Januari – Disemba hadi Juni ili ioane na mwaka wa fedha wa serikali. Hadi sasa serikali imetoa Sh22.1 bilioni kama mgao wa kufadhili elimu kwa shule za msingi na zile za upili. Baadhi ya shule zilikosa ufadhili wakati ambapo mchakato wa kuhakiki na kuondoa shule feki zenye wanafunzi hewa ulikuwa ukiendelea. Kwa mujibu wa Katibu katika Wizara ya Elimu Julius Bitok, shule 18,000 kati ya zile 23,000 zimepokea mgao wao. Bado shule 5,000 zinahakikiwa. Kuna shule 97,800 za umma ambapo 47,666 ni za chekechea, 35,570 za msingi kisha 10,752 za sekondari. “Shule kadhaa hazijapata mgao kutokana na tofauti kwenye data walizowasilisha kuhakikiwa. Bado data zao zinaangaliwa kabla ya fedha kutolewa,” akasema Profesa Bitok. Profesa Bitok alifichua kuwa Wizara ya Elimu imetoa Sh10.4 bilioni kwa Wizara ya Elimu katika shule za sekondari ambapo Sh10.1 bilioni zimetumwa kwa shule. Kwa shule za sekondari za chini, hazina kuu imetoa Sh4.8 bilioni kati ya Sh5.6 bilioni huku Sh800 milioni ambazo zimesalia zikitarajiwa kutumwa kwa shule. “Ripoti itaandaliwa ambayo itaonyesha tofauti kwenye data iliyowasilishwa. Wakurugenzi wa elimu kwenye kaunti na kaunti ndogo wanafanya kazi na shule ili kushughulikia utata ambao umetokea,” akasema Profesa Bitok. “Imebainika kuwa baadhi ya shule zina wanafunzi chini ya idadi ya wastani ya wanafunzi 45 ambao wanahitajika katika kila darasa kwa mujibu wa Wizara ya Elimu,” akasema Profesa Bitok.
KAMATI ya Kitaifa ya Kuandaa Mazishi imetangaza kuwa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga itafanyika kuanzia saa tatu asubuhi Jumapili katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOUST), Bondo, Siaya. Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Oktoba 18, 2025 jioni, mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo Naibu Rais Kithure Kindiki alisema kuwa ibada hiyo itaendelea hadi saa saba mchana. “Baada ya hapo, kutafanyika shuhuda fupi, maombi na heshima za kijeshi kando mwa kaburi lake nyumbani kwa babake Kang’o Kajaramogi, kijiji cha Nyamira,” akaongeza. Profesa Kithure aliongeza kuwa kamati hiyo anayoongoza pamoja na kakake Raila, Oburu Oginga, itatoa maelezo kuhusu shughuli zitakazofuata “kwa heshima ya marehemu Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga baada ya mazishi ya kesho”. Awali, Katibu wa Usalama wa Ndani Raymond Omollo alitangaza mabadiliko mengine ya shughuli za kutoa heshima kwa mwendazake. Kwa mfano, Dkt Omollo alitangaza kusikitishwa kwa shughuli ya kutoa nafasi kwa wananchi kutaza mwili wa Raila katika Uwanja wa Michezo wa Jomo Kenyatta, eneo la Mamboleo, Kisumu mwendo wa saa tisa alasiri. “Mwili wa kiongozi wetu Raila Amollo Odinga utasafirishwa kwa helikopta hadi Bondo kutoa nafasi kwa wananchi wa eneo hilo kupata nafasi ya kuutazama,” akawaambia wanahabari katika uwanja huo. Kulingana na mipango ya awali, wakazi wa Kisumu wangepata nafasi ya kuutazama mwili hadi saa tisa alasiri kisha usafirishwe kwa barabara hadi Bondo. Shughuli ya kutazama mwili katika Opado Farm, Bondo ulikamilika dakika nne kabla ya saa moja za usiku, Jumamosi.

Ni wazi sasa — historia ya elimu ya juu nchini Tanzania inaandikwa upya katika ardhi ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE). Wakati majengo makubwa yakipanda kama ishara ya matumaini mapya, hewa ya mageuzi inahisiwa kila kona ya chuo hicho, shukrani kwa jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk … The post Dk Samia aandika historia DUCE first appeared on HabariLeo.

MOROGORO: CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA ) kimeeleza kuwa hadi kufikia Oktoba mwaka huu, miradi mipya ya utafiti 36 yenye thamani ya Sh bilioni 10.5 imepatikana. Kati ya miradi hiyo 10 inafadhiliwa na wafadhili wa nje, miradi miwili ya Serikali kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na miradi 24 inafadhiliwa na Chuo … The post SUA yapata miradi 36 ya bil 10.5/- first appeared on HabariLeo.

CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA ) kimeeleza kuwa hadi kufikia Oktoba mwaka huu miradi mipya ya utafiti 36 yenye thamani ya sh bilioni 10.5 imepatikana. Kati ya miradi hiyo 10 inafadhiliwa na wafadhili wa nje, miradi miwili ya Serikali kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na miradi 24 inafadhiliwa na Chuo Kikuu hicho kupitia mapato yake ya ndani. The post SUA yapata miradi 36 yenye thamani ya Bilioni10.5 first appeared on HabariLeo.

TAASISI ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imeendelea kutoa elimu kwa wananchi, wakulima na wadau wa sekta ya kilimo kuhusu utambuzi wa mbegu bora, taratibu za usajili wa wazalishaji wa mbegu, pamoja na namna ya kuepuka mbegu bandia sokoni. The post TOSCI yatoa elimu kutambua mbegu bandia first appeared on HabariLeo.

MTWARA: Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imeelekeza nguvu zake katika utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu miradi inayotarajiwa kutekelezwa kwa lengo la kuifanya kuwa na ufanisi kwa wazawa na taifa kwa ujumla. Mamlaka hiyo imetoa msisitizo huo Oktoba 15, 2025 katika Kijiji cha Ruvula, mkoani Mtwara, wakati wa zoezi la utoaji wa … The post PURA yaweka msisitizo elimu miradi kwa wananchi first appeared on HabariLeo.

IRINGA: Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Charles Nyagawa, amewataka wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Lugalo kutanguliza Mungu katika masomo na maisha yao, huku akiwahakikishia motisha ya kupata usafiri wa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha endapo watafanya vizuri katika mitihani yao ya taifa. Nyagawa aliyasema hayo … The post Nyagawa awapa motisha wahitimu wa Lugalo Sekondari first appeared on HabariLeo.

UBWABWA kwa wote, kilimo kwanza na nishati safi ndiyo baadhi ya ahadi zinazobeba ilani ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Katika kampeni zinazotarajiwa kuanza rasmi Agosti 28, mwaka huu chama hicho kimeweka mezani vipaumbele 10 vinavyoangazia uchumi jumuishi, ustawi wa wananchi, lishe bora, elimu bure yenye chakula…
MAMIA ya walimu wa shule za msingi waliotuma maombi ya kuteuliwa kufunza katika shule za Sekondari ya Msingi (JSS) wamezuiwa kufuatia tangazo la Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) iliyoweka masharti mapya ya uajiri. Kwa mujibu wa TSC, walimu waliohitimu na Digrii ya Elimu (Chaguo la Msingi) hawafai kufundisha wanafunzi wa JSS. Kenya ina zaidi ya walimu wa msingi 220,000, wengi wakiwa na diploma au digrii, huku wachache wakiwa na uzamili au hata uzamifu. Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa TSC, Bi Everleen Mutei, alifichua kuwa, tume hiyo ilipokea jumla ya maombi 3,718 kutoka kwa walimu wa shule za msingi waliotaka kuhamishwa hadi JSS. Hata hivyo, ni walimu 1,436 pekee waliohitimu kulingana na vigezo vilivyowekwa. “Pamoja na waraka huu ni orodha ya walimu 1,436. Mara baada ya kupokea, mnahitajika kuwachambua upya na kuwahamisha walimu waliotimiza masharti kufunza JSS kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa,” alisema Bi Mutei. Alisisitiza ni walimu waliohitimu kufundisha katika shule za upili pekee ndio wanaostahili kuhamishwa hadi JSS. Katika waraka uliotumwa kwa wakurugenzi wa elimu wa maeneo na kaunti ndogo, TSC ilieleza kuwa walimu wenye Digrii ya Elimu (Chaguo la Msingi) hawatimizi masharti ya kufundisha JSS.
WAPENZI wa Kiswahili nchini na kanda nzima ya Afrika Mashariki wanaomboleza kifo cha msomi na mwandishi Profesa John Hamu Habwe ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 62. Profesa Habwe alifariki akitibiwa hapo Jumapili katika hospitali moja jijini Nairobi baada ya kuugua kwa zaidi ya miaka mitatu. Alizaliwa na Mzee Hamu Jonah na mama Alice Apasi Hamu ameacha mjane Teresa Habwe na watoto. Profesa Habwe ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Ebukhaya, Emabuye kaunti ndogo ya Emuhaya mnamo mwaka wa 1963 ni Profesa wa kwanza katika kata ya Ebukhaya. Kwa muujibu wa kakake mdogo Astaricus Hamu ni kwamba marehemu alikuwa nguzo muhimu katika familia yao. “Profesa alikuwa nguzo muhimu katika jamii yetu hatujawahikuwa na mtu msomi mwenye kujali watu wake kama ndugu yangu. Mungu ailaze roho yake pema peponi.” alisema. Profesa Habwe alianzia masomo yake katika shule ya msingi ya Ebukhaya katika ilokuwa kata ya North Bunyore miaka ya sabini kabla ya kujiunga na shule ya upili ya Ebwali East Bunyore miaka ya themanini na hatimaye kujiunga na shule ya upili ya Kapkatet Boys kaunti ya Kericho kwa kidato cha sita. Mwishoni mwa miaka ya themanini. Alijiunga na chou kikuu cha Nairobi idara ya Lugha ya Kiswahili mapema miaka ya tisini kabla ya kufundisha katika shule mbalimbali eneo la Bunyore na hatimaye kuwa mkufunzi katika chuo kikuu cha Nairobi. Amefundisha katika chuo hicho kwa zaidi ya miaka 30 hadi mwaka wa 2016. Alipokuwa katika chuo kikuu cha Nairobi alipata kuhudumu kama mwenyekiti wa idara ya Kiswahili na lugha nyingine za kiafrika kwa miaka miwili . Mbali na kuwa mwalimu ameandika vitabu kadha na kushiriki warsha za Kiswahili na kutoa shauri kwa wataalam wa lugha ya Kiswahili kupitia kwa vipindi vya redio na runinga haswa KBC. Marehemu aliwahifundisha katika vyuo vingine ikiwa ni Pamoja vyuo vikuu vya Moi, Maseno na chuo kikuu cha Catholic University. Vile vile amefanyakazi katika mashirika ya kimataifa kama vile shirika la chakula na na killimo FAO, World Health Organization (WHO) na tume ya Afrika Mashariki yani Kiswahili Commission of East Africa kama mtafsiri. Ameandika vitabu vya watoto miongoni mwa vitabu vingine ikiwa ni Pamoja na kitabu chake cha Kwanza ‘Maumbile si huja’. Mipango ya mazishi inaendelea,marehemu atazikwa katika shamba lake Lugari katika kaunti ya Kakamega.

SERIKALI mkoani Kagera kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendea kuongeza vitendea kazi na kubuni technolojia wezeshi za kuwafikia wananchi wote ambao hawakubahatika kupata elimu kwa mfumo rasmi ili kutokomeza maadui watatu umasikini, maladhi na ujinga Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Muleba katika kilele cha maadhimisho ya juma la wiki ya elimu ya watu wazima…

MOROGORO: MKUU wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema amekuwa na mvuto maalum kwenye kilimo tangu awali kutokana na malengo ya Serikali yaliyowekwa juu ya kuondoa umaskini. Jaji Warioba alisema hayo wakati wa halfa ya mkutano maalum wa Baraza la Chuo la kuanga Baraza la Chuo…
Wasiwasi umetanda kwa maelfu ya wanafunzi wapya wa vyuo vikuu huku baadhi ya taasisi zikitarajia kufunguliwa Jumatatu ijayo, na wanafunzi wapya 194,372 wakikabiliwa na hali ngumu ya kuanza masomo. Baadhi wana hofu ya kuripoti chuoni bila hata senti ya matumizi, huku wengine wakifikiria kutofika kabisa siku ya ufunguzi. Vyuo vya Chuo Kikuu cha Nairobi, Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT), Chuo Kikuu cha Kenyatta, Chuo Kikuu cha Maseno, Multimedia, na Chuo Kikuu cha Kibabii vinatarajiwa kufunguliwa kati ya Agosti 18 hadi 25. Hata hivyo, zikiwa zimesalia siku chache tu, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB) na Hazina ya Vyuo Vikuu bado hazijathibitisha tarehe halisi ya kutoa fedha za ruzuku na za matumizi jambo linaloongeza wasiwasi kuhusu ikiwa wanafunzi wapya wataanza safari yao ya kitaaluma bila msaada wa kifedha wanaoutegemea sana. Lakini Mkurugenzi Mkuu wa HELB Geoffrey Monari alisisitiza kuwa mchakato wa utoaji fedha unaendelea kama ilivyopangwa. “Tuko katika njia sahihi. Pesa zitakuwa tayari watakaporipoti,” alisema. Licha ya hayo, baadhi ya wanafunzi waliohojiwa wanasema wako katika hali ya sintofahamu hawawezi kupanga usafiri au mahitaji ya msingi. Kwa Elvis Odhiambo, kupata nafasi ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Garissa imegeuka kuwa chanzo cha majonzi. Kijana huyo wa miaka 24 kutoka Kaunti ya Homa Bay alipata alama ya B– katika KCSE ya 2024, na hatimaye kupata nafasi ya kusomea Shahada ya Elimu ya Sayansi baada ya kujaribu mtihani huo mara tatu. “Siwezi kujiunga kwa sababu hakuna pesa. Niliomba HELB lakini sijapata kitu. Baba yangu amenambia nitafute kazi ya jua kali kwa sababu hatuwezi lipa Sh119,000 kwa mwaka, na hata nauli ni ghali mno. Nimejitahidi sana kufika hapa. Nilikuwa na matumaini kuwa mkopo ungekuja mapema kusaidia angalau nauli na mahitaji, lakini hakuna chochote,” alisema. Katika mfumo mpya wa ufadhili, wanafunzi wamegawanywa katika makundi matano ya mahitaji ya kifedha, yanayobainisha asilimia ya ufadhili wa serikali, mkopo, na mchango wa familia. “Nilifurahi sana nilipopokea barua ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Kaimosi Friends kusomea Shahada ya Elimu. Hii ilikuwa ndoto yangu – nafasi ya kujenga maisha, kuinua familia, na kutimiza malengo. Lakini sasa ndoto hiyo imejaa hofu. Karo ni zaidi ya Sh100,000 na siku zimekaribia, lakini fedha ambazo nilitegemea bado hazijatolewa. Sina uhakika kama nitaweza kujiandaa au hata kuripoti. Shinikizo ni kubwa mno. Nikiwaza jinsi familia yangu imejitolea, natetemeka kuona ndoto hii ikitoweka kwa sababu ya kuchelewa kwa fedha,” alisema Lidya Cherop. Velton Mboga, aliyepata nafasi katika Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki naye anasema hali ni ngumu: “Karo ni Sh55,000 kwa muhula, mzigo mkubwa kwa wazazi. Baba yangu ni mwalimu mstaafu. Tumeomba HELB lakini hatujui kama tutapata, au kiasi gani. Inatamausha kutojua kama fedha zitakuja kwa wakati,” alisema. Katika mitandao ya kijamii, Bw Monari alitetea mfumo mpya wa ufadhili, akiomba wadau wote kuuunga mkono, na kuonya kuwa kurejea kwa mfumo wa zamani ni hatari kwa elimu ya juu.

TANGA: MKUU wa mkoa wa Tanga, Dk Batlida Burian ameiomba Benki Kuu ya Tanzania kuendelea kuwajengea uwezo wananchi hususani wenye mahitaji maalum kuhusu utambuzi wa noti bandia . Kauli hiyo imetolewa kwa niaba yake na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Sebastian Masanja wakati akifungua mafunzo kuhusu utambuzi wa noti bandia kwa viziwi waliopo…
Wahasibu na maafisa wa fedha katika shule za umma watakaguliwa mtindo wa maisha na hata kuhamishwa baada ya kila miaka minne, iwapo Bunge la Taifa litaidhinisha mswada mpya wa marekebisho ya sheria unaoendelea kuzingatiwa. Mswada wa Marekebisho ya Elimu ya Msingi, 2025, unapendekeza kubadilisha Sheria ya Elimu ya Msingi, Sura ya 211, ili kukuza uwajibikaji na uwazi katika matumizi ya fedha za shule kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi wa Umma. Mswada huo, uliodhaminiwa na Mbunge wa Sirisia, John Waluke, unapendekeza kuwa taasisi zote za elimu ya msingi ziwasilishe maelezo ya mapato, mali na madeni ya wafanyakazi wasio walimu, wake au waume zao, na watoto wao wanaowategemea. “Kwa muda mrefu katika taasisi za elimu ya msingi, wahasibu ambao huajiriwa na bodi za usimamizi wamekuwa wakitumia fedha za shule kwa manufaa yao binafsi, jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Maadili ya Maafisa wa Umma,” Bw Waluke alieleza Kamati ya Elimu ya Bunge. Kwa mujibu wa mbunge huyo, ukaguzi huu unalingana na masharti ya Sheria ya Ukaguzi wa Umma, Sura ya 412B, na utaimarisha uwajibikaji katika taasisi za elimu ya msingi. “Hii itahakikisha matumizi bora ya fedha za umma na kutekeleza haki ya kupata elimu kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 53 (1)(b) ya Katiba ya Kenya,” akaongeza. Bw Waluke alisema kuwa kwa kuwa ni Bunge linaloidhinisha mishahara ya wahasibu hao, basi wanahesabiwa kuwa maafisa wa umma na hivyo wanapaswa kukaguliwa kikamilifu. “Mtu yeyote anayetumia afisi yake kujinufaisha au kunufaisha mwingine kinyume cha sheria, anatenda kosa la matumizi mabaya ya afisi kama inavyoelezwa katika Kifungu cha 46 cha Sheria ya Kupambana na Ufisadi na Uhalifu wa Kiuchumi,” alisema. Iwapo mswada huo utakubaliwa na kuchapishwa, Bw Waluke amesema atapendekeza mabadiliko zaidi ya kuhakikisha wahasibu wa shule za umma wanahamishwa kila baada ya miaka mitatu “Wahasibu ni kama watumishi wa umma; kwa nini wahudumu shule moja milele? Hapo ndipo rushwa huzaliwa na mali ya umma kutumiwa vibaya,” alisema. “Watu hawa wameharibu shule nyingi. Wamepata mali kila mahali na hauwezi hata kuelewa walizipataje,” aliongeza mbunge huyo.Kwa mujibu wa Bw Waluke, kuhusisha wake, waume na watoto katika ukaguzi huo ni njia ya kuzuia hali ambapo wahusika hutumia majina ya jamaa zao kuwekeza mali walizopata kwa njia za ufisadi. Hata hivyo, mbunge huyo atalazimika kusubiri hadi Kamati ya Elimu ikamilishe uchunguzi wa pendekezo hilo la sheria kabla ya kumweleza Spika ikiwa mswada unastahili kuchapishwa rasmi na kuwasilishwa bungeni kwa hatua zaidi. Iwapo kamati itapendekeza kuchapishwa, basi mswada utaanza safari rasmi ya kusomwa kwa mara ya kwanza bungeni, kabla ya kupelekwa kwa ushiriki wa umma, ambao utaongozwa na kamati hiyo ya elimu.

MTWARA: KUELEKEA Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025, waandishi wa habari mkoani Mtwara wametakiwa kuandika na kuripoti habari kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao. Rai hiyo imetolewa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk. Malima Zacharia ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa Year Book wakati wa mafunzo yaliyowakutanisha waandishi kutoka vyombo…
Mpenzi wangu anasoma chuo kikuu. Kuna jamaa nimewaona pamoja mara kadhaa na siku fulani nilimpata kwake. Nimemuuliza akasema wanasoma pamoja. Inawezekana ananicheza? Mwanawake na mwanamume wanaweza kutangamana bila uhusiano wa kimapenzi. Lakini pia ushirikiano huo unaweza kuzaa mapenzi. Huna sababu ya kumshuku mpenzi wako, lakini ni muhimu ufuatilie kwa karibu mienendo yao. Aliniweka presha tukala uroda sasa ninamchukia Mpenzi wangu alinilazimisha tushiriki mapenzi na baada ya hapo nikamchukia na kumuacha. Ameniomba msamaha akitaka turudiane lakini bado nina maumivu moyoni kutokana na alichonitendea. Nifanyeje? Mpenzi wako alifanya makosa makubwa kukulazimisha kufanya jambo ambalo hukutaka. Hatua yake ya kurudi kwako kuomba msamaha ni ishara kuwa anajuta. Kama bado unampenda, shauri moyo wako uone kama unaweza kumsamehe. Nilipekua simu yake nikakumbana na vituko Miezi miwili iliyopita nilipata ujumbe wa kimapenzi katika simu ya mpenzi wangu kutoka kwa mwanamke mwingine. Nimechunguza na hatimaye nimethibitisha huyo ni mpenzi wake. Uliamua kumchunguza mpenzi wako ili ujue ukweli kuhusu uhusiano wake na mwanamke huyo kwa sababu hutaki mpenzi asiye mwaminifu. Sasa umethibitisha, utaamua mwenyewe iwapo utajiondoa ama utaendelea. Ndoa yake ilivunjika ila nahofia mke atarudi Huu ni mwaka wangu wa pili katika uhusiano wa kimapenzi. Nimegundua mpenzi wangu alikuwa ameoa na wakaachana na mkewe. Nahofia mke wake anaweza kurudi baadaye. Ni kawaida kwa mtu na mkewe kuachana. Sielewi ni kwa nini mpenzi wako hakukwambia ukweli kuhusu maisha yake. Kwa sababu umejua, shauriana naye ili uhakikishe hakuna matumaini ya kurudiana ndipo muendelee na uhusiano wenu.

MOROGORO: WAKULIMA wameshauriwa kutumia mbinu bora za Kilimo ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo kilimo hifadhi kinacholinda mazingira na kuimarisha mavuno. Mtaalamu wa kilimo kutoka Kampuni ya Mzuri na Agram Afrika, Salimu Msuya amesema hayo wakati wa utoji elimu ya matumizi ya teknolojia za kisasa za Kilimo mjini Morogoro. Msuya amesema kilimo…

MOROGORO: CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeibuka kidedea kwa kuwa Mshindi wa Jumla na Mshindi wa Kwanza katika kundi la Taasisi za Mafunzo na Utafiti katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yamwaka huu ( 2025) yaliyofanyika mkoani Morogoro na unatokana na mchango wake mkubwa katika sekta ya kilimo nchini. Akizungumza mara baada…
Wanafunzi wa Gredi 10 ambao hawatachagua Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) lakini watachagua kusoma Hisabati ya Kawaida wataruhusiwa kufanya hivyo kulingana na matokeo yao ya tathmini ya Sekondari Msingi. Katibu wa Elimu ya Msingi, Profesa Julius Bitok, alisema kuwa wanafunzi hao watapewa nafasi ya kusoma Hisabati ya Kawaida iwapo wataonyesha uwezo kupitia matokeo yao ya awali. Katika waraka uliotumwa kwa wakurugenzi wote wa elimu wa kanda, kaunti na kaunti-ndogo, Wizara ya Elimu ilieleza mfumo wa utekelezaji wa awamu inayofuata ya Elimu ya Kuzingatia Umilisi (CBE), ambayo ni ngazi ya nne ya elimu ya msingi baada ya Chekechea, Shule ya Msingi na Sekondari Msingi. Mbali na masomo ya lazima, mwanafunzi atachagua masomo matatu zaidi. Profesa Bitok aliwashauri wanafunzi kuchukua angalau masomo mawili kutoka mkondo wa mtaala waliochagua. “Hii ina maana kwamba mwanafunzi anaweza kuchukua masomo matatu kutoka mkondo wa mtaala aliouchagua au masomo mawili kutoka humo na somo moja kutoka mkondo mwingine,” alisema Prof Bitok. Hata hivyo, alisema kuwa iwapo uchaguzi wa taaluma ya mwanafunzi unahitaji somo moja kutoka kila mkondo, basi ataruhusiwa kufanya hivyo. “Uchaguzi wa masomo utaongozwa na taaluma anayotazamia mwanafunzi, uwezo wake, nia na haiba, kwa msaada wa viongozi wa shule ya upili. Orodha ya masomo yote yanayotolewa katika shule ya upili chini ya CBC imetolewa na Taasi ya Kitaifa ya Ukuzaji wa Mitaala (KICD),” alisema. Serikali tayari imeanza maandalizi ya utekelezaji wa CBE katika Shule ya Upili, huku Wizara ya Elimu ikitoa miongozo kuhusu masomo yatakayofundishwa. Masomo manne ya lazima yatakuwa ni Kiingereza, Kiswahili, Hisabati ya Kawaida/Hisabati ya Msingi na Somo la Huduma kwa Jamii (CSL). “Ili kufafanua, wanafunzi wote watalazimika kusoma Kiingereza, Kiswahili na Huduma kwa Jamii (CSL). Wanafunzi watakaochagua STEM watasoma Hisabati ya Kawaida, ilhali wale wa mikondo mingine watasoma Hisabati ya Msingi,” alisema Prof Bitok.
MASHINDANO ya Kitaifa ya Tamasha za Muziki yanayoendelea katika Chuo cha Walimu cha Meru yanazidi kutia fora huku mawasilisho mbalimbali yakisisimua wadau. Mashindano ya mwaka huu yameonyesha ubunifu wa hali ya juu huku wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali wakizidi kuonyesha umarufu na vipaji vyao. Tazama mambo yanavyoendelea, kwa picha.... [caption id="attachment_176041" align="alignnone" width="1280"] Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Hill School kutoka Eldoret wapiga pozi katika Shule ya Upili ya Kaaga, Meru.[/caption] [caption id="attachment_176042" align="alignnone" width="1600"] Wanafunzi wa Chuo cha Walimu cha Kamwenja Jukwaani.[/caption] [caption id="attachment_176043" align="alignnone" width="1600"] Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Elegant Spur kutoka Ruiru.[/caption] [caption id="attachment_176046" align="alignnone" width="1280"] Wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi ya Damacrest kutoka Kiambu wakisherehekea tuzo baada ya ushindi.[/caption] [caption id="attachment_176047" align="alignnone" width="1204"] Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kivaywa jukwaani. [/caption] [caption id="attachment_176051" align="alignnone" width="1040"] Shule ya St Michael Shamusinjiri kutoka Ikolomani, Kakamega. PICHA ZOTE|TOBBIE WEKESA[/caption]