DAR ES SALAAM: WADAU wa sekta ya bima nchini wameendelea kutoa elimu kwa wanafunzi kupitia mashindano ya “Bima Debate” yaliyoandaliwa ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya Siku ya Bima yatakayofanyika kuanzia 26/06/2026 jijini Arusha. Mashindano hayo yamewakutanisha wanafunzi wa shule za sekondari pamoja na vyuo vikuu mbalimbali kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu umuhimu … The post Wanafunzi wapigwa msasa elimu matumizi ya bima first appeared on HabariLeo.
KWA muda mrefu, shule nyingi nchini Kenya zimekuwa zikitegemea kuni kuandaa chakula cha wanafunzi mfumo ambao hata ingawa ni maarufu umeendelea kuwa mzigo mkubwa kwa sababu ya gharama zake, changamoto za kiafya na uharibifu wa mazingira. Majiko mengi ya shule, moshi mzito ulikuwa sehemu ya maisha ya kila siku. Wapishi walilazimika kufanya kazi kwa saa nyingi katika mazingira yenye hewa chafu huku wanafunzi wakichelewa kupata chakula, hasa wakati wa mvua ambapo kuni huwa mbichi na vigumu kuwaka. Katika maeneo kame na nusu-kame (ASAL), changamoto hiyo imekuwa kubwa zaidi. Mahitaji ya kuni yameongeza ukataji miti, hali inayochochea athari za mabadiliko ya tabianchi kama vile ukame wa muda mrefu, mvua zisizotabirika na upungufu wa malisho kwa mifugo. Hata hivyo, hali hiyo inaanza kubadilika huku baadhi ya shule zikikumbatia matumizi ya majiko ya kisasa yanayotumia umeme na nishati ya jua (solar). Teknolojia hiyo mpya haipunguzi gharama za utendakazi, bali pia inalinda mazingira na kuboresha huduma ya lishe shuleni. Katika Shule ya Al-Huda Muslim iliyoko eneo la Majengo, Kaunti ya Kajiado, matumizi ya kuni yalikuwa yamekuwa changamoto kubwa kwa taasisi hiyo ya elimu hiyo yenye zaidi ya wanafunzi 820. Kwa mwezi, ilikuwa ikinunua magari mawili ya kuni kwa gharama ya karibu Sh20,000 kila mwezi, mbali na gharama nyingine za maji na shughuli za jikoni. Kwa jumla, zaidi ya Sh40,000 zilikuwa zikitumika kila mwezi kuendesha mpango wa chakula. [caption id="attachment_187993" align="aligncenter" width="300"] Joy Kwamboka kutoka EcoBora akielezea kuhusu majiko ya umeme na nishati ya jua. Picha|Sammy Waweru[/caption] Mwalimu anayesimamia mazingira na mpango wa lishe shuleni humo, Shaaban Iddi, anasema changamoto ya kuni ilikuwa kubwa zaidi ikikunbukwa kuwa Kajiado ni eneo lenye uhaba wa miti. “Wakati mwingine tulilazimika kuomba ruhusa kutoka kwa serikali ya kaunti kukata miti ili kuongeza kuni, jambo ambalo lilisababisha kuchelewa kwa maandalizi ya chakula,” anakumbuka. Mbali na gharama hizo, moshi kutoka jikoni uliathiri afya ya wafanyakazi. “Wapishi walifanya kazi kwa muda mrefu katika mazingira yenye moshi mwingi uliowaathiri kiafya,” Mwalimu Shaaban anaeleza. Lakini baada ya shule hiyo kuanza kutumia majiko yanayotumia umeme na nishati ya jua yaliyotengenezwa na kampuni ya EcoBora, hali ilianza kubadilika. Kwa sasa, chakula huiva kwa haraka, mazingira ya jikoni ni safi zaidi na wanafunzi hupata chakula kwa wakati unaofaa. “Masomo yanaendelea bila usumbufu kwa sababu chakula kinapatikana kwa wakati,” Shaaban anasema. Pia, anasema shule hiyo imeongeza juhudi za uhifadhi wa mazingira kwa kuhimiza upandaji miti hasa ya matunda kama vile maparachichi na karakara. “Klabu ya mazingira huwapa wanafunzi motisha ya kupanda na kutunza miti hadi wanapomaliza masomo yao,” anaongeza. Katika Kaunti ya Kiambu, PCEA Mama Ngina Primary and Junior Secondary School pia imeanza kutumia mfumo wa mapishi safi. Shule hiyo yenye karibu wanafunzi 2,500 ilikuwa ikikumbwa na changamoto ya moshi kutoka jikoni kutokana na madarasa mengi kuwa karibu na eneo la kupikia. Naibu mwalimu mkuu anayesimamia utawala, Rachael Ndune, anasema matumizi ya kuni yalikuwa yakichangia matatizo ya kiafya miongoni mwa wapishi. “Wafanyakazi wengi walikuwa wakiugua mara kwa mara kutokana na moshi na wakati mwingine walishindwa kufika kazini,” anasema. [caption id="attachment_187994" align="aligncenter" width="300"] Naibu mwalimu mkuu anayesimamia utawala, PCEA Mama Ngina Primary and Junior Secondary School, Kaunti ya Kiambu Rachael Ndune. Picha|Sammy Waweru[/caption] Kulingana na Ndune, shule hiyo ilikuwa ikitumia karibu Sh300,000 kwa muhula kununua kuni, huku zile mbichi zikisababisha chakula kuchukua muda mrefu kuiva. Kupitia matumizi ya majiko ya kisasa ya EcoBora, shule hiyo sasa inapunguza matumizi ya kuni na kuokoa muda wa maandalizi ya chakula. EcoBora ni kampuni yenye makao yake Nairobi na kiwanda cha kutengeneza majiko ya umeme na nishati ya jua katika Kaunti ya Kajiado. Mkufunzi wa wapishi kutoka EcoBora, Yvonne Nyambura, anasema taasisi zinazonunua majiko hayo hupatiwa mafunzo ya siku tatu hadi saba kuhusu matumizi bora ya nishati, usalama na utengenezaji vifaa. “Chakula kama githeri ambacho hapo awali kilikuwa kikichukua saa tano au sita kuiva kwa kutumia kuni, sasa huiva ndani ya saa mbili au tatu,” anasema. Kulingana na Joy Kwamboka kutoka EcoBora, Kenya ina zaidi ya taasisi 92,000 za elimu, zikiwemo shule na vyuo, na matumizi ya majiko safi yanaweza kuwa suluhisho muhimu katika kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Anasema shule moja inaweza kutoa hadi tani 700 za hewa ya kaboni kutokana na matumizi ya kuni. “Shule zikihamia matumizi ya umeme na nishati ya jua, zitapunguza ukataji miti, kupunguza uzalishaji wa hewa chafu na kuelekeza fedha zilizookolewa katika kuboresha lishe ya wanafunzi au miradi mingine ya maendeleo,” anaelezea. Kampuni hiyo hutengeneza majiko ya lita 20 hadi 2,000 kulingana na mahitaji ya wateja. Kadri Kenya inavyoendelea kushuhudia athari za mabadiliko ya tabianchi, shule zinaibuka kama sehemu muhimu katika juhudi za kulinda mazingira. Kupitia matumizi ya mapishi safi, taasisi za elimu zinaonyesha kuwa vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi vinaweza kuanzia shuleni huku watoto wakijifunza umuhimu wa kuhifadhi mazingira kwa kizazi cha sasa na kijacho.
SERIKALI imepuuzilia mbali madai kwamba hakuna masomo yanayoendelea katika Gredi ya 10 katika shule za upili baada ya kucheleweshwa kwa vitabu na changamoto nyingine zinazoshuhudiwa. Waziri wa Elimu Bw Julius Ogamba alisema licha ya kucheleweshwa kwa vitabu, shughuli za masomo zinaendelea madarasani kote nchini huku wizara ikijizatiti kuhakikisha wanafunzi wote wanapokea vitabu hivyo. Bw Ogamba alitoa ufafanuzi kuhusu kwa nini vitabu hivyo vilichelewa wiki moja sasa baada ya wanafunzi hao kujiunga na shule za upili. Kuwa mujibu wa wazazi na baadhi ya walimu waliohojiwa na Taifa Leo, kucheleweshwa kwa vitabu hivyo ulisababisha kusitishwa kwa masomo kwa wanafunzi wa Gredi ya 10. Hata hivyo, Bw Ogamba alihakikishia Wakenya kuwa masomo yanaendelea. Bw Ogamba alisisitiza kuwa shule nyingi zimeanza masomo hasa kuwaelekeza wanafunzi kuhusu masomo katika shule za upili ili kuwasaidia katika kuchagua taaluma wanazotaka. “Kwa sasa walimu wanawafafanulia kuhusu masomo waliyochagua na watakayosoma katika shule za upili. Huu ndio mchakato unaoendelea wakati huu. Kumbukeni hii ni mara ya kwanza kabisa kupokea wanafunzi wa Gredi ya 10. Kwa hivyo, haya ni masuala ambayo yanaweza kutokea,” alisema Waziri. Hata hivyo, alisema mpito ujao utakuwa laini kwani vitabu vitakuwa viko tayari. Mahojiano Akiongea kwenye mahojiano na runinga ya KTN, Bw Ogamba alisema kwamba wizara yake bado itazingatia sera ya kitabu kimoja kwa kila mwanafunzi katika kila somo ili kufanikisha elimu bila malipo. “Serikali ilikuwa ikidaiwa Sh11 bilioni na wachapishaji kutokana na madeni ya awali kuanzia Gredi ya 1 hadi Gredi ya 9. Wachapishaji walisimama kidete kwamba hawatatoa vitabu vya Gredi ya 10 hadi pale tutakapowalipa madeni yao. Wiki tatu zilizopita tuliwalipa Sh5.6 bilioni na tukakubaliana kwamba watasambaza vitabu hivyo shuleni,” akasema Bw Ogamba. Serikali imekuwa ikitumia NEMIS kusambaza vitabu katika shule za umma. Bw Ogamba alisema baada ya kulipa nusu ya deni hilo, wachapishaji hao walianza shughli za usambazaji Januari 16 na usambazaji huo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu. Waziri huyo alisema shule zote za upili za umma zitapokea vitabu vya Gredi 10 ifikiapo mwisho wa mwezi huu. Alibainisha kuwa kufikia sasa, asilimia 40 ya vitabu vimeshasambazwa, huku lengo likiwa ni kukamilisha zoezi hilo kufikia mwisho wa mwezi huu. Alisema vitabu hivyo vya Gredi ya 10 vina muda wa kudumu wa miaka minne. Serikali imekuwa ikisambaza vitabu kwa wanafunzi walioko shule za umma kote nchini kwa zaidi ya mwongo mmoja kupitia mpango wa elimu bila malipo huku ikitumia takwimu kutoka NEMIS kutathmini idadi ya wanafunzi. Kila mwanafunzi amekuwa akipokea kitabu cha kila somo. Waziri Ogamba, alifichua kuwa malimbikizi ya madeni hayo ndiyo yalisababisha hali hiyo, ambayo imeanza kutatuliwa na asilimia 40 ya vitabu tayari imesambazwa kwa shule za umma.
MATOKEO ya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) 2025 yamefichua shule ndogo ambazo hazikujulikana sana awali, baada ya kupata wastani alama bora na kushinda shule zilizokuwa zikichukuliwa kama mabingwa kitaifa. Shule za jadi kama Alliance High School, Kenya High School, Mang’u High School na Kapsabet Boys High School bado zinaendelea kutawala, lakini sasa zinakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa shule mpya, ndogo na za kibinafsi. Shule hizo ni kama Nova Pioneer Tatu Boys High School ya Kaunti ya Kiambu, iliyopata wastani wa alama 10.2 kutoka 8.3 mwaka 2024. Kati ya watahiniwa 82, wanafunzi 24 walipata A-, 49 B+, wanane B na mmoja B-. Asilimia 100 ya wanafunzi walifuzu kujiunga na vyuo vikuu, kulingana na Kaimu Mwalimu Mkuu Andrew Meraba. Shule ya Pangani Girls ilipata wastani wa 9.718 na kuimarisha sifa yake kama moja ya shule bora nchini. Ilikuwa na alama 39 za A, wanafunzi 92 wakipata A-, 101 B+, 69 B, 44 B-, 17 C+, wanane C, sita C- na mmoja D+. Katika Kaunti ya Kajiado, Shule ya Wasichana ya Ghanima El-Marzuq, Isinya, iliongoza miongoni mwa shule za kibinafsi.
JUMLA ya wanafunzi 232,281 waliofanya Mtihani wa Darasa la nane (KCPE) mwaka wa 2021 hawakufanya mtihani wa kidato cha nne (KCSE), kulingana na takwimu za hivi punde kutoka Wizara ya Elimu. Takwimu za Baraza la Kitaifa la Mitihani nchini (KNEC) zinaonyesha kuwa watahiniwa 1,225,507 walifanya mtihani wa KCPE mwaka wa 2021. Hata hivyo, ni wanafunzi 993,226 pekee waliofanya mtihani wa KCSE mwaka wa 2024, hali inayoangazia kiwango kikubwa cha wanafunzi wanaokatiza masomo katika ngazi ya sekondari. Takwimu zaidi kutoka KNEC zinaonyesha kuwa watahiniwa 2,634 walijisajili lakini hawakufanya mtihani wa KCSE mwaka wa 2025. Kwa jumla, watahiniwa 995,860 walikuwa wamejisajili kufanya mtihani wa kitaifa wa sekondari, lakini ni 993,226 pekee waliojitokeza kufanya mtihani. Takwimu hizi zinaonyesha ongezeko thabiti tangu mwaka wa 2021, ambapo watahiniwa 830,854 walisajiliwa na 826,807 wakafanya mtihani. Serikali imeendelea kutekeleza sera asilimia 100 ya wanafunzi kujiunga na sekondari, inayosisitiza kuwa kila mtoto ajiunge na shule ya msingi na kukamilisha masomo ya sekondari. Sera hii inatokana na Sheria ya Elimu ya Msingi, inayowalazimu wazazi wote raia wa Kenya au wale ambao watoto wao wanaishi nchini kuhakikisha watoto wao wanapata elimu ya sekondari. Ingawa sera hii ina nia njema, inahitaji kufanyiwa mabadiliko ili kushughulikia masuala halisi yanayoibuliwa na wazazi, wanafunzi wenyewe na wadau wa elimu. Sio wanafunzi wote wanaofaa mfumo rasmi na mgumu wa elimu ya sekondari, na wengi wangependelea, baada ya shule ya msingi, kufuata kozi za ufundi kama useremala, ushonaji, uashi na nyinginezo. Wanafunzi kama hao wanapaswa kuruhusiwa kufuata mkondo huo, huku wakiendelea kufundishwa masomo kama Kiingereza na Hisbati ili kuboresha ujuzi wao mawasiliano na ujasiriamali. Wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya KCSE 2025, shule za kitaifa ziliongoza kwa kutoa wanafunzi waliopata matokeo bora, na hivyo kudumisha sifa yao kama vituo bora kwa elimu. Kati ya watahiniwa 1,932 waliopata A kamili, wanafunzi 1,526 (asilimia 79) walitoka shule za kitaifa. Shule za mikoa zilifuata kwa wanafunzi 197, huku shule za kibinafsi zikiwa na 185 waliopata alama ya juu. Shule za kaunti ndogo zilifanya vyema kuliko shule za kaunti kwa kutoa wanafunzi 72,699 waliojiunga na vyuo vikuu ikilinganishwa na 36,600 wa shule kiwango cha kaunti, hali inayoonyesha uwezo mkubwa wa shule ndogo zilizo nje ya mfumo wa shule za kifahari.
DAR ES SALAAM: The National Examinations Council of Tanzania (NECTA) has announced the results of the National Assessment for Standard Four pupils, showing that the pass rate for Standard Four has increased by 2.67 percent, while the pass rate for Form Two rose by 1.52 percent. NECTA also noted that in 2026, Form Two students … The post NECTA sees rise in Std 4 pass by 2.67, Form Two by 1.52 percent first appeared on Daily News.
JAJI Njoki Ndung’u amechaguliwa kuwa mwakilishi wa Mahakama ya Juu katika tume ya kuajiri watumishi katika idara ya mahakama (JSC). Jaji Ndung’u alichaguliwa bila kupingwa mnamo Januari 9,2026 kutwaa mahala pa marehemu Jaji Mohammed Ibrahim aliyeaga Desemba 17,2025 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Jaji Ibrahim alihudumu kama mwanachama wa JSC tangu alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu 2011. Hadi kifo chake Jaji Ibrahim alikuwa Jaji wa Mahakama ya Juu na wakati huo huo mwakilishi wa korti hii ya upeo katika JSC. Majukumu hayo mawili yalimwezesha Jaji Ibrahim kuhakikisha ubora wa utekelezaji wa Katiba sawia na unyoofu wa utenda kazi katika idara ya mahakama kupitia JSC. Jaji Ndung’u alichaguliwa katika hafla iliyowajumuisha Jaji Mkuu (CJ) Martha Koome , Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu ,Jaji Smokin Wanjala Jaji Isack Lenaola na Jaji William Ouko. Zoezi hilo liliongozwa na Afisa wa Kusimamia Uchaguzi kutoka tume huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Dkt Swallah Yusuf. Jaji Ndung’u alichaguliwa kwa mujibu wa mwongozo na Sheria za JSC za 2011 zinazoitaka Idara ya Mahakama ya Juu kuwasilisha mwakilishi wake katika muda wa siku 21 baada ya mwanya kuimbuka. Jaji Ndung’u anayetwaa nafasi ya mwendazake Jaji Ibrahim ametambulika katika mchango wake wa kutetea haki za binadamu na masuala ya jinsia nchini. Mbali na wadhifa huo mpya , Jaji Ndung’u pia ndiye mwenyekiti wa kamati ya idara ya mahakama kuhusu uchaguzi na uteteaji wa haki za wafanyakazi katika idara ya mahakama. Katika hotuba yake baada ya kuchaguliwa Jaji Ndung’u aliahidi kutekeleza majukumu yake bila woga, upendeleo na kuhakikisha haki imetendeka. “Nitatekeleza majukumu yangu kwa uwazi, kuhakikisha haki imetendeka na kushinikiza uhuru wa idara ya mahakama katika utekelezaji wa kazi zake,” Jaji Ndung’u alisema. Akimpongeza Jaji Ndung’u kwa uteuzi wake Jaji Koome, aliyepia mwenyekiti wa JSC, alisema yuko na imani naye na kuongeza ,”mchango wako kutetea haki za jinsia na utekelezaji wa katiba umetambulikana kote.” Jaji Koome aliwataka wakenya wajitokeze kutetea haki zao na za wengine bila woga. Baada ya kifo cha Jaji Ibrahim, mahakama hii ya upeo imesalia na majaji sita ambao ni Jaji Koome, Jaji Mwilu, Jaji Wanjala, Jaji Ndung’u, Jaji Lenaola na Jaji Ouko. Zoezi la kuteuliwa kwa Jaji mwingine kutwaa wadhifa wa Jaji Ibrahim bado kutangazwa na JSC. Atakayeteuliwa sharti awe amehudumu kama Jaji wa Mahakama kuu , Mahakama ya Rufaa ama ametekeleza majukumu ya wakili kwa zaidi ya miaka 10 tangu ahitimu chuo kikuu kwa shahada ya digirii masuala ya sheria.
MABADILIKO katika kuhesabu alama za wastani kwa wanafunzi katika mtihani wa (KCSE yamesababisha ongezeko la wanafunzi waliopata alama bora, jambo linalofungua fursa zaidi za elimu ya juu na mafunzo ya kitaaluma. Kulingana na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Kitaifa (KNEC), Dkt David Njeng’ere, matokeo yaliyotolewa jana yamefanya Kenya kukaribia nchi ambazo wanafunzi wanaostahili kujiunga na vyuo vikuu kuwiana na idadi ya kawaida ya watu ambako hakuna majanga kama vita, njaa au janga la afya. Alieleza kuwa mafanikio haya yametokana na mabadiliko katika jinsi ya kuhesabu alama za wastani yaliyoanza mwaka 2023. Kwenye kigezo kipya, baraza huchambua wanafunzi kwa kutumia masomo saba badala ya masomo nane ya awali. Haya ni Hisabati, lugha bora zaidi kati ya Kiingereza, Kiswahili au Lugha ya Ishara ya Kenya, pamoja na masomo matano bora zaidi ya mtahiniwa. Tangu wakati huo, idadi ya wanafunzi wanaofunzu kujiunga na vyuo vikuu imekuwa ikiongezeka. Matokeo ya KCSE 2025 yameorodhesha idadi kubwa zaidi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu tangu marekebisho makali ya mitihani ya kitaifa yalipoanzishwa mwaka 2016. Wanafunzi 270,715 kati ya 993,226 waliofanya mtihani walipata kiwango cha C+ na juu, jambo linalowastahikishia kujiunga na vyuo vikuu. Kwa asilimia 27.18, kiwango cha wanaojiunga na vyuo vikuu kinazidi asilimia 25.53 ya mwaka 2024, asilimia 22.3 mwaka 2023, asilimia 19.03 mwaka 2022, na asilimia 11.3 mwaka 2017. “Kwa muda mrefu, tumekuwa chini ya asilimia 20. Kwa mfumo wa elimu kama huu, ina maana hauwezi kupata wafanyakazi wanaofunzwa kwenye vyuo ili kusaidia ukuaji wa uchumi,” alisema Dkt Njeng’ere. Alibainisha kuwa ongezeko la asilimia ya wanafunzi wanaofunzu kujiunga na vyuo vikuu linaashiria kuwa nchi iko kwenye mwelekeo sahihi, ikifuata mifano ya nchi kama Zambia (asilimia 50) na Korea Kusini (asilimia 70). Ingawa kimataifa hakuna kiwango kimoja kilichowekwa, miongozo ya sera za elimu na ripoti za Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) hutoa viwango vya jumla vya kati ya asilimia 30 hadi 40.
KWA mwaka wa pili mfululizo, idadi ya wasichana ilizidi wavulana katika Mtihani wa Kidato cha Nne (KCSE), jambo linaloonyesha mabadiliko ya kijamii na kielimu yanayoendelea kushuhudiwa nchini, hasa katika ushiriki wa wasichana katika elimu ya sekondari. Takwimu rasmi za Baraza la Kitaifa la Mitihani Kenya (KNEC) zinaonyesha kuwa jumla ya watahiniwa 993,226 walifanya mtihani wa KCSE mwaka 2025, ikilinganishwa na watahiniwa 962,512 mwaka 2024. Hii ni sawa na ongezeko la watahiniwa 30,714, au asilimia 3.19. Ongezeko hili linaashiria kuimarika kwa wanafunzi katika shule za upili pamoja na juhudi za serikali na wadau wa elimu kuhakikisha watoto wanabaki shuleni hadi kumaliza masomo ya sekondari. Kati ya watahiniwa wote wa mwaka 2025, wavulana walikuwa 492,012 (asilimia 49.54), huku wasichana wakiwa 501,214 (asilimia 50.46). Hii ni mara ya pili mfululizo tangu kuanzishwa kwa mtihani wa KCSE ambapo idadi ya wasichana imezidi ile ya wavulana, ishara kuwa juhudi za kuhimiza elimu ya mtoto wa kike zinaanza kuzaa matunda. Hata hivyo, hali hiyo haikuwa sawa kote nchini. Kaunti kumi zilirekodi idadi kubwa ya wavulana kuliko wasichana. Kaunti hizo ni pamoja na Garissa, ambako wavulana walikuwa asilimia 66.24 dhidi ya wasichana asilimia 33.76, Mandera (65.09 dhidi ya 34.91), Wajir (60.10 dhidi ya 39.90), Turkana (57.67 dhidi ya 42.33) na Narok (53.10 dhidi ya 46.90). Kaunti nyingine ni Samburu, Mombasa, Homa Bay, Nyamira na Pokot Magharibi. Hali hii imehusishwa na changamoto za kijamii, kiuchumi na kiutamaduni zinazoathiri elimu ya wasichana katika maeneo hayo. Kwa upande mwingine, kaunti 14 zilikuwa na idadi kubwa ya wasichana kuliko wavulana. Kaunti hizo ni pamoja na Vihiga, Elgeyo Marakwet, Kisumu, Kiambu, Kwale, Nairobi, Kakamega, Meru, Isiolo, Uasin Gishu, Machakos, Kitui, Busia na Tharaka Nithi. Wataalamu wa elimu wanasema hali hii inaonyesha mafanikio ya sera za elimu jumuishi na kampeni za kuzuia wasichana kuacha shule. Kaunti 23 zilirekodi uwiano wa karibu sawa wa kijinsia, zikionyesha usawa mkubwa kati ya wavulana na wasichana. Kaunti hizo ni pamoja na Lamu, Marsabit, Embu, Tana River, Laikipia, Kisii, Baringo, Migori, Trans Nzoia, Nandi, Kajiado, Taita Taveta, Kericho, Siaya, Kilifi, Bomet, Nyeri, Nyandarua, Murang’a, Nakuru, Kirinyaga, Bungoma na Makueni. Kuhusu umri wa watahiniwa, idadi ya wanafunzi wenye umri wa miaka 16 na chini iliongezeka kutoka 20,546 mwaka 2024 hadi 26,391 mwaka 2025, sawa na asilimia 2.65 ya watahiniwa wote. Hata hivyo, idadi kubwa zaidi ya watahiniwa, 716,048 (asilimia 72.02), walikuwa katika umri ufaao wa kati ya miaka 17 na 19. Uchambuzi wa kijinsia unaonyesha kuwa wasichana walifanya vyema zaidi kuliko wavulana katika masomo sita: Kiingereza, Kiswahili, Lugha ya Ishara ya Kenya, Sayansi ya Nyumbani, Elimu ya Dini ya Kikristo (CRE) na Sanaa na Ubunifu. Wavulana, kwa upande wao, waliongoza katika masomo 11, yakiwemo Hisabati, Baiolojia, Kemia, Sayansi ya Jumla, Historia na Serikali, Jiografia, Elimu ya Dini ya Kiislamu, Ujenzi na Masomo ya Biashara.
IDADI ya watahiniwa waliopata alama ‘A’ katika mtihani wa Kidato cha Nne Kenya (KCSE) mwaka 2025 imeongezeka, kulingana na takwimu zilizotolewa na Wizara ya Elimu Januari 9, 2026. Ongezeko hilo linaashiria mwelekeo chanya licha ya changamoto zinazokumba sekta ya elimu nchini.Kwa mujibu wa matokeo rasmi, jumla ya watahiniwa 1,932 walipata ‘A’ mwaka 2025, sawa na asilimia 0.19 ya watahiniwa wote 993,226 waliofanya mtihani huo. Hii ni ongezeko ikilinganishwa na 2024 ambapo watahiniwa 1,693 pekee, sawa na asilimia 0.18, walipata alama hiyo ya juu zaidi. Wizara ya Elimu inasema mabadiliko ya mfumo , ufuatiliaji mkali wa mitihani na kuimarika kwa mazingira shuleni ni miongoni mwa sababu zilizochangia hali hiyo. Shule za kitaifa ziliendelea kutawala katika kutoa wanafunzi waliopata A. Wakati huohuo, idadi ya wanafunzi waliopata alama za kujiunga moja kwa moja na vyuo vikuu pia imeongezeka. Jumla ya watahiniwa 270,715 walipata C+ na zaidi.
GEITA: HALMASHAURI ya Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita imeweka wazi kuwa imeandaa miundombinu inayotosheleza kupokea wanafunzi 3,056 wa kidato cha kwanza mwaka 2026. Ofisa Elimu Sekondari wilayani Nyang’hwale, Malemu Tito ametoa taarifa hiyo katika ziara ya mkuu wa wilaya kukagua miundombinu ya elimu kuelekea mwaka mpya wa masomo. Malemu amesema mpaka sasa tathimini inaonyesha kuwa … The post Nyang’hwale mguu sawa kupokea kidato cha kwanza first appeared on HabariLeo.
MTWARA; MANISPAA ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara imetoa zawadi kwa shule 15 za msingi zilizofanya vizuri matokeo ya darasa la saba mwaka 2025. Tukio hilo limefanyika wakati wa kikao kazi kwa wakuu wa shule, maofisa elimu kata pamoja na wataaluma wa manispaa kilichofanyika kwenye manispaa hiyo. Zawadi zilizotolewa ni fedha taslimu taslimu Sh milioni 6 … The post Mtwara Mikindani wazawadia Shule zilizong’ara 2025 first appeared on HabariLeo.
KUELEKEA kufunguliwa kwa muhula mpya wa masomo Januari 13, 2026, taswira ya elimu nchini inaonesha mafanikio makubwa yanayopaswa kupongezwa na kulindwa kwa vitendo. Serikali, kupitia jitihada za uongozi wake kuanzia ngazi ya kitaifa hadi mikoa na wilaya, imefanikiwa kutatua moja ya changamoto sugu katika sekta ya elimu ambayo ni uhaba wa madarasa. The post Wazazi, walimu wasimamieni wanafunzi wawe shuleni first appeared on HabariLeo.
GEITA; MKUU wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, Grace Kingalame ameagiza maofisa elimu kata kusimamia ubora wa madarasa ya awali ili kujenga mazingira rafiki kwa watoto kujifunza. Kingalame ametoa maagizo hayo wakati wa ziara maalumu ya kukagua miundombinu ya elimu kuelekea kuanza kwa mwaka mpya wa masomo 2026. Amesema shule zinapaswa kuzingatia muongozo wa sera … The post DC aagiza ubora madarasa ya awali first appeared on HabariLeo.
WALIMU wakuu wa shule za upili sasa wanataka Wizara ya Elimu kutelekeza mfumo wa kitaifa wa kuteua wanafunzi wa Gredi 10 na kukumbatia mfumo ambapo shule zilisimamia uteuzi huo. Walimu hao wanasema mfumo wa sasa unachanganya na kuondoa uwazi. Wakuu hao, chini ya chama chao (KESSHA), wanasema Mfumo wa Kusimamia Habari za Elimu Kenya (KEMIS) umewazuia kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uteuzi, huku shule zikikosa kujua wanafunzi wanaoteuliwa, historia zao za elimu, na uwiano wa maeneo wanayotoka. Haya yanajiri huku wazazi wakiendelea kulalamika kuwa baadhi ya wanafunzi wameteuliwa kujiunga na shule tofauti bila kuomba kuhamishwa. “Awali, tulijua wanafunzi tulioteua, matokeo yao na wanatoka wapi. Kwa mfano, mwanafunzi kutoka Kisauni angepelekwa Murang’a High School, kuhakikisha uwiano wa kitaifa. Sasa tunapata majina tu. Hatujui alama zao au historia zao,” alisema Mwenyekiti wa KESSHA, Willie Kuria. Alieleza kuwa mfumo wa awali, kupitia NEMIS, ulikuwa wenye uwazi na ushirikishaji, ulihakikisha uwiano wa kijiografia na haki sawa katika kaunti zote 47. Alisema wakuu wa shule hawapati matokeo ya Mtihani wa Gredi 9 (KJSEA) ya wanafunzi walioteuliwa kujiunga na shule zao. “Kama mwanafunzi aliye na alama za juu anateuliwa kujiunga na shule za mkoa– tunashangaa. Hatujui kama ufaafu kweli ulifuatwa,” alisema. KESSHA inapendekeza mfumo mseto ambapo wazazi wanaweza kuwasiliana na shule moja kwa moja kupata nafasi, kisha data hiyo iingizwe katika KEMIS kwa idhini ya Wizara ya Elimu. Vilevile, wakuu wanapaswa kupewa nafasi ya kujaza nafasi zinazobaki wanafunzi wakikosa kujiunga na shule walizoteuliwa. Bw Kuria alikanusha madai kuwa wakuu wanadai hongo ili kuteua wanafunzi katika shule bora, akisema pesa zozote zinazotozwa zinatokana na idhini ya Bodi ya Shule (BoM) na risiti rasmi huwa inatolewa.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inakusudia kuongeza bajeti ya sekta ya elimu kufi kia Sh trilioni moja ili sekta hiyo iwe kipaumbele kwa maendeleo ya nchi. The post SMZ kuongeza bajeti ya elimu tril 1/- first appeared on HabariLeo.
MWENYEKITI wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Mkoa wa Dodoma, Mchungaji Eliya Mathayo amewaomba wazazi na walezi kushirikiana na serikali kuhakikisha watoto wote walioandikishwa kuanza elimu ya msingi wanapelekwa kuanza masomo shule zikifunguliwa Januari mwakani. Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika kanisani hapo. Alisema … The post Baraza Makanisa Kipentekoste wataka watoto wapelekwe shule first appeared on HabariLeo.
MRADI wa Eco-School ni muhimu katika kuimarisha elimu ya mazingira na maendeleo endelevu kwa wanafunzi, jamii na taifa kwa ujumla. Mradi huu unawawezesha watoto kujifunza kwa vitendo, kukuza uongozi na kushiriki moja kwa moja katika uhifadhi wa mazingira na rasilimali asilia. The post Watoto wajifunze umuhimu wa mazingira first appeared on HabariLeo.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Mpango wa Elimu kwa Umma Kuhusu Muungano utakuwa endelevu ili kuhakikisha elimu hiyo inamfikia kila mmoja. Ameyasema hayo leo Desemba 19, 2025 wakati akizungumza katika kipindi cha Asubuhi Njema kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC). Amesema Waandishi wa … The post Masauni: Elimu kuhusu Muungano ni endelevu first appeared on HabariLeo.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amekutana na Balozi wa Saudi Arabia, Yahya Bin Ahmed Okeish, ambapo wamejadili kuimarisha ushirikiano katika sekta ya elimu pamoja na kuongeza fursa za skolashipu kwa vijana. Prof. Mkenda ameishukuru Saudi Arabia kwa kuongeza nafasi za ufadhili masomo ya jelimu ya juu kutoka 90 hadi 127 kwa … The post Tanzania, Saudi Arabia kuongeza fursa za elimu first appeared on HabariLeo.
MASWALI yameibuka kuhusu uwezo wa shule kuhudumia wanafunzi wapya wanaotarajiwa kujiunga na Sekondari Pevu mwakani. Haya yanajiri huku Waziri wa Elimu, Julius Ogamba akisema shule zina uwezo wa ziada na Wizara ya Elimu inatarajia asilimia 100 ya wanafunzi 1.13 milioni kujiunga na Sekondari Pevu. Hata hivyo, baadhi ya wakuu wa shule wanahisi hawako tayari kikamilifu. Wakuu wa shule waliozungumza na Taifa Leo wameelezea wasiwasi wao kuhusu mkondo wa Sayansi, Tekinolojia na Hisbati (STEM) kutokana na ukosefu wa miundombinu ya ICT na vifaa. “Tunasema wanafunzi 1.13 milioni watajiunga na shule za sekondari huku uwezo wa shule ukiwa 1.5 milioni, tuko sawa na tunatarajia asilimia 100 ya wanafunzi ambao matokeo yao tumeyatoa leo,” alisema Katibu wa Elimu ya Msingi, Julius Bitok, jana wakati wa uzinduzi wa matokeo ya KJSEA. Bw Ogamba alisema nafasi katika shule 9,540 za sekondari zitaongezeka wanafunzi 929,262 watakapomaliza shule za sekondari baada ya Mtihani wa (KCSE) mwaka huu. Wanafunzi watateuliwa katika shule za sekondari kulingana na Makundi- 1 hadi 4 -kulingana na utendaji wao na mkondo waliyochagua—STEM, Sanaa na Michezo, na Sayansi za Jamii. Hata hivyo, ukibaki mwezi mmoja tu kabla ya tarehe ya kuripoti ya Januari 12, 2026, vitabu vya Kiingereza pekee ndivyo vilivyofikishwa shule. Hii imesababishwa na deni la Sh10 bilioni wanazodai wachapishaji. Aidha, baadhi ya shule hazina maabara za kompyuta zinazofanya kazi na zinashindwa kulipa madeni ya vifaa vilivyonunuliwa. “Mbali na kutokuwa na kompyuta, tuna madeni ya vifaa vya maabara ikiwemo kemikali,” alisema mkuu wa shule ambaye hakutaka kutajwa jina. Mkuu mwingine wa shule anakadiria kuwa kubadilisha darasa moja kuwa maabara ya kompyuta kutagharimu takriban Sh700,000, pesa ambazo hawana.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameeleza mafanikio ya sekta ya elimu, ikiwemo ongezeko la bajeti ya wizara hiyo kwa asilimia 40 kutoka mwaka 2021/2022 hadi 2025/2026. Amesema chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, serikali imeongeza fedha za mikopo ya elimu ya juu kutoka Sh bilioni 464 hadi bilioni 916.7 zinazotolewa katika vyuo vikuu na vyuo vya kati. The post Bajeti ya elimu juu 40% miaka mitano first appeared on HabariLeo.
IRINGA: Chuo Kikuu cha Iringa (UoI) kimesema mageuzi yaliyofanywa na Mahakama Kuu Kanda ya Iringa katika miaka 20 ya uwepo wake yameleta mabadiliko makubwa katika namna wananchi wanavyofikiwa na huduma za haki. Akiwa mwenyeji wa ugeni wa viongozi wa Mahakama Kuu chuoni hapo, Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo, Kaleb Lameck Gamaya (Adv), alisema mafanikio … The post Mahakama Kuu Iringa yafungua mlango haki kwa wote first appeared on HabariLeo.
RAIS Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi awamu ya sita Dk Amani Abeid Karume pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Awamu ya Saba Dk Ali Mohamed Shein wameitaka Ofisi ya Makamu wa Rais kuendelea kutoa elimu ya kutosha ya Muungano ili misingi ya Muungano iliyowekwa na … The post Karume, Shein wataka elimu ya Muungano idumishwe first appeared on HabariLeo.
DAR ES SALAAM: Taasisi ya EMCA, inayojihusisha na utunzaji wa mazingira na utoaji wa elimu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo, imeendelea na kampeni yake ya “Tuelimishe Mazingira” kwa kutembelea Shule ya Msingi Mlimani Demonstration jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa EMCA, Zafarani Ramadhani, alisema … The post EMCA Yasistiza utunzaji mazingira first appeared on HabariLeo.
DAR ES SALAAM: MKUU wa Chuo Kikuu cha Mzumbe ambaye pia ni Rais mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, amewataka wahitimu wa chuo hicho pamoja na vijana nchini kujenga mitandao imara ya kitaaluma na kuendelea kulinda amani na mshikamano wa taifa, akisisitiza kuwa ndiyo msingi wa mafanikio … The post Dk Shein: Vijana jengeni mitandao ya kitaaluma first appeared on HabariLeo.
DAR ES SALAAM: CHUO KIKUU cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimesema kinatarajia kuongeza upanuzi wa uwezo wa udahili wa wanafunzi katika fani za afya, mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu mipya na ya kisasa kupitia Mradi wa Mageuzi ya Elimu ya Juu kwa Uchumi ( HEET). Mkuu wa MUHAS, Profesa David … The post Miundombinu mipya kuongeza masomo ya afya MUHAS first appeared on HabariLeo.
MBEYA: Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed, ametoa wito kwa wataalamu wa jiosayansi nchini kuanza mikakati madhubuti ya kutoa elimu na kuhamasisha wanafunzi kuifahamu na kuipenda fani hiyo ili kuongeza idadi ya wataalamu. Amesema licha ya umuhimu mkubwa wa jiosayansi katika maendeleo ya taifa, bado uelewa wake miongoni … The post ‘Wekeni mikakati wanafunzi waifahamu jiosayansi’ first appeared on HabariLeo.
CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) kimesema kimepata Sh bilioni 120 kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET). Mwenyekiti wa Baraza la MUHAS, Dk Harrison Mwakyembe amesema hayo wakati Mahafali ya 19 ya chuo hicho jijini Dar es Salaam. The post Bil 120/- mradi wa HEET zaineemesha MUHAS first appeared on HabariLeo.
WANAFUNZI watakaojiunga na Gredi 10 mwezi ujao watahitaji kufundishwa na walimu 58,590 zaidi kwa masomo spesheli chini ya Mtaala wa Umilisi na Utendaji (CBC). Masomo yaliyoathirika zaidi ni Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hesabu maarufu kama STEM japo mengine pia yameathirika kwa wastani. Hii ni kwa sababu wanafunzi 569,000, ambayo ni idadi ya juu zaidi, ndio walichagua masomo hayo yenye upungufu wa walimu 35,111. Masomo ya sayansi ya kijamii yanahitaji walimu 14,630 kisha yale ya sanaa na michezo yana upungufu wa walimu 8,778. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tume ya Kuwaajiri Walimu Nchini (TSC) anayesimamia ubora wa elimu Dkt Reuben Nthamburi, upungufu umepanda kutokana na mfumo mpya wa elimu. “STEM itakuwa na asilimia 60 ya wanafunzi ambao ni 677,144 kwenye madarasa 15,046. Tulifanya hesabu kwa kutumia darasa ambalo lina wanafunzi 45 ambako tunawahitaji walimu 35,111. Kwa sayansi ya kijamii tunawahitaji walimu 14,630 kisha sanaa na michezo inahitaji 8,778 ambapo idadi ya jumla ni 58,519,” akasema Dkt Nthamburi. TSC pia ilitoa wito kwa vyuo vikuu na vyuo vya ualimu kuhakikisha mafunzo yao yanaoana na hitaji jipya la soko hasa kwenye masomo ya sanaa na michezo. Dkt Nthamburi alisisitiza kuwa idadi ya walimu inastahili kuoana na wanafunzi hasa kwenye masomo ya STEM ambayo yamechukuliwa na wanafunzi 569,000 kati ya wanafunzi milioni 1.1 katika Gredi ya Nne. Wanafunzi hao wanahitaji walimu 35,111. Masomo ya sayansi nayo yalichaguliwa na wanafunzi 437,000 ambao watahitaji walimu 14,630 nao wanafunzi 124,000 wa Sanaa na Michezo wanahitaji wanafunzi 8,778. Afisa huyo wa TSC aliwaomba manaibu chansela wa vyuo vikuu na wakufunzi kwenye vyuo vya mafunzo wamakinikie vitengo muhimu katika kuwanoa walimu.
IDARA ya Afya katika kaunti ya Kisumu imeelezea hofu kuhusu mwenendo wa wanaume kuwaambukiza virusi vya HIV wake zao waja wazito. Mkurugenzi wa Afya ya Umma, Dkt Fredrick Oluoch alisema kuwa wamegundua visa ambapo akina mama huwa hawana virusi hivyo miezi ya kwanza kabla ya kupata uja uzito lakini hupatikana na HIV wanapokaribia kujifungua. Alisema hali hii huchangiwa na mwenendo wa wanaume kushiriki ngono na wapenzi wenye virusi hivyo kisha kuleta virusi hivyo kwa nyumbani kwa wake zao wenye uja uzito. “Tunaendelea kushuhudia hali inayotishia ambapo mama hupimwa na kutopatikana na virusi miezi mitatu ya kwanza ya uja uzito na katika miezi tatu ya mwisho kabla ya wao kujifungua, hupatikana na virusi hivyo. Hii ina maana kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba walipata virusi hivyo kutoka kwa waume zao wanaoshiriki mapenzi bila kinga nje ya ndoa,” akasema Dkt Oluoch. Afisa hiyo alisema hayo wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani zilizofanyika katika Shule ya Msingi ya Kisian, Kaunti Ndogo ya Kisumu Magharibi. Haya yanajiri wakati Baraza la Kitaifa la Kudhubiti Magonjwa Sugu (NSCC) imetoa ripoti inayoonyesha kwamba Kisumu ni miongoni mwa kaunti zilizoandikisha viwango vya juu vya maambukizi mapya ya HIV nchini mnamo 2024. Kiwango cha maambukizi ya HIV katika kaunti ya Kisumu ni asilimia 11 huku ikikadiriwa kuwa watu 111,367 wanaishi na virusi vya HIV vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi. Katika mwaka wa 2024, kaunti ya Kisumu iliandikisha maambukizi mapya 1, 341 ya virusi hivyo huku idadi ya wanawake ikiwa wengi (755) kuliko wanawake (361). Kwa upande mwingine, maambukizi mengine 225 yaliandikishwa katika watoto. Visa vya akina mama kuwaambukiza watoto wao (MTCT) vilipungua kutoka kima cha asilimia 9 mnamo 2019 hadi asilimia 5.97 mnamo 2024. Dkt Oluoch alisema Idara ya Afya katika Kaunti ya Kisumu inaazimia kupunguza kiwango hicho cha maambukizi hadi chini ya asilimia tano (5). Afisa huyo alisema japo visa vya maambukizi vimepungua kutokana na juhudi zinazoendeshwa kwa idara yake, juhudi hizo hata hivyo zinahujumiwa na mienendo ya wanaume kuwa na wapenzi wengi nje ya ndoa. “ Wanaume hawa wanafaa kuwalinda wake zao waja wazito kwa kukoma kujihusisha katika ngono bila kinga na wapenzi nje ya ndoa. Wanapaswa kuwa watulivu, wawalinde wake zao nyakati za uja uzito,” akasema Dkt Oluoch.
Shikamoo shangazi. Nimenaswa kimapenzi na msichana fulani. Juzi nilimtembelea kwao kwa mara ya kwanza. Mama yake hajaolewa tena ni mchanga na mrembo sana. Nimechanganyikiwa! Nishauri tafadhali. Ni wazi kwamba mama ya msichana huyo pia amenasa moyo wako kimapenzi. Sasa unashindwa utamchagua yeye ama ni binti yake. Jipe muda ufikirie kisha uamue. Ninaamini mama amekuzidi umri ingawa hiyo si hoja bora mapenzi. Nampenda tusiyeonana Nilijuana na mwanamume fulani kupitia kwa mtandoa na hatimaye tukapendana ingawa hatujawahi kuonana. Huu sasa ni mwezi wa sita tangu tulipojuana. Haya ni mapenzi ya kweli? Kuna visa kadhaa vya watu waliojuana na kupendana kupitia kwa mtandao na hatimaye wakaoana. Hata hivyo, hatimaye mtahitaji kukutana na kuwa pamoja kwa muda ndipo mjue ukweli wa mapenzi yenu. Eti ataacha tu mubaba iwapo nitaamua kumuoa Za kwako shangazi. Kuna mwanamke ninayemtaka lakini amekuwa akinizungusha tu. Hatimaye juzi alifungua moyo wake. Akaniambia ana uhusiano na mtu aliye na familia na atamuacha tu kama niko tayari kumuoa. Nishauri. Mwanamke huyo amekwambia anachotaka; mume wake mwenyewe. Na ndiyo sababu anataka kwanza umhakikishie kwamba nia yako kwake ni ndoa. Kama unaamini anatosha na uko tayari kwa ndoa, kazi kwako. Niko shule ya upili ila nimemfia jamaa fulani Shikamoo shangazi. Nina miaka 16 na ninasoma katika shule ya upili. Kuna mwanamume anayenitaka kimapenzi. Nampenda lakini nahofia mapenzi yataathiri vibaya masomo yangu. Nishauri. Msimamo wako hasa ndio ushauri wangu kwako. Wewe bado ni mwanamke mchanga na masomo ndiyo tegemeo lako maishani. Mwelezee msimamo wako huo. Kama kweli anakupenda atangojea.
IRINGA: Kijana wa kimasai, Lekishon Koipa, ameandika historia nyingine katika Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) baada ya kuibuka kinara wa ufaulu kwa kupata GPA ya juu kuliko wote chuoni 4.8. Kijana huyo mhitimu wa digrii ya awali ya elimu jamii na ualimu kwa mwaka 2025, ametangazwa kuwa mfano hai wa ushindi dhidi ya vikwazo … The post Kijana wa kimasai avunja rekodi chuo cha Mkwawa first appeared on HabariLeo.
IDARA ya Kuchunguza Uhalifu (DCI) katika Kaunti ya Mombasa inaendeleza upelelezi kuhusu kifo cha msichana mwenye umri wa miaka mitano aliyedaiwa kuanguka kutoka juu ya jengo la madrassa baada ya kufungiwa ndani kama adhabu. Tukio hilo lililotokea Novemba 18 asubuhi katika Madrassa Tul Nur eneo la Leisure, Nyali, limezua ghadhabu miongoni mwa wakazi na makundi ya kutetea haki za watoto, wanaotaka haki itendeke. Ripoti za awali za polisi zinaonyesha kuwa mtoto huyo alitenganishwa na wenzake na kufungiwa ndani kama adhabu. Watoto wengine walipokwenda kucheza, inadaiwa alijaribu kutoroka kupitia dirishani akaanguka na kupoteza maisha papo hapo. Afisa wa Upelelezi wa Kaunti Ndogo ya Nyali Mohamed Jillo, alisema maafisa wa DCI tayari wameandikisha taarifa kutoka kwa walimu, wanafunzi na uongozi wa madrassa. “Hili linaonekana kama suala la uzembe. Tunachunguza maelezo yote, kukusanya ushahidi na kubaini iwapo kuna mtu aliyekosa kutimiza wajibu wake,” akasema Bw Jillo katika mahojiano na Taifa Leo afisini mwake. Aliongeza kuwa, uchunguzi utabaini iwapo madrassa hiyo inafuata kanuni za ulinzi wa watoto zilizo katika sheria ya elimu ya msingi na sheria ya watoto. Mdokezi kutoka madrassa, ambae hakutaka kutajwa, alisema mama ya msichana huyo alikuwa amemuelekeza mwalimu amuadhibu binti yake kwa sababu alikataa kwenda madrassa asubuhi hiyo. Hivyo mwalimu akamzuia kuungana na wenzake wakati wa mapumziko ya saa nne asubuhi. Uongozi wa madrassa ulisema hautatoa taarifa kwa sasa hadi uchunguzi utakapokamilika. Kwa upande mwingine, familia ya msichana pia haikutaka kuhojiwa. Tukio hilo limezua mjadala mkali mitandaoni, watumiaji wakitaka maelezo ya kina kuhusu mazingira yaliyopelekea kifo hicho na kuwataka viongozi wa madrasa kuwajibika. Mashirika ya kutetea haki za watoto pia yametaka uchunguzi wa kina na kuchukuliwa hatua za haraka dhidi ya wahusika. Kuhusu madai kwamba wazazi wanashinikizwa kuacha kufuatilia kesi, maafisa wa DCI walisisitiza kuwa uchunguzi unaendelea kwa uwazi. Afisa wa watoto mjini Mombasa, Bw Gabriel Kitile, alisisitiza umuhimu wa kutumia mbinu salama kwa watoto katika taasisi zote za elimu, rasmi na za kidini. “Kilichotokea ni kielelezo kwamba hakuna mtoto anayepaswa kuwekwa hatarini kwa jina la adhabu. Kila kituo cha elimu lazima hakikishe watoto wanawekwa kwa uangalifu na wanalindwa kila wakati," akasema. Uchunguzi ukikamilika, faili itawasilishwa kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) ili kuamua hatua zinazofaa kuchukuliwa.
IRINGA;Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dk Jakaya Kikwete, ameongoza mahafali ya 17 ya Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) mjini Iringa leo, ambapo ametunuku shahada mbalimbali za umahiri na za awali kwa wahitimu. Katika ngazi ya umahiri, amewatunuku Digrii ya Umahiri wa Sayansi na Ualimu … The post JK aongoza mahafali ya 17 MUCE first appeared on HabariLeo.
WATOTO sita miongoni mwa 10 duniani kote hawajui kusoma sentensi rahisi wala kusuluhisha maswali ya kimsingi ya hesabu licha ya thuluthi yao kuwa shuleni kwa sasa. Haya ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na shirika linalofahamika kama People's Action for Learning (PAL) Network iliyotathmini matokeo ya masomo miongoni mwa watoto 89,870 wenye umri wa miaka mitano hadi 16 katika mataifa 12. Matokeo hayo yamezua wasiwasi mkubwa kuhusu ubora wa elimu katika mataifa mengi maskini kwa kufichua kwamba kuhudhuria shule pekee sio hakikisho la masomo halisi. Ripoti hiyo inaashiria kwamba Kenya inaongoza majirani zake barani Afrika Mashariki katika kufanikisha Viwango vya Chini zaidi vya Ufaafu (MPL) katika hisabati, licha ya changamoto zinazoendelea kama vile upungufu wa walimu, uhaba wa vifaa vya masomo na maswala yanayohusu vipimo. Kulingana na ripoti, asilimia 43 ya watoto wenye umri wa miaka 10 nchini wanatimiza kiwango kinachohitajika cha MPL ikilinganishwa na asilimia 33 Tanzania na asilimia 4 Uganda. MPL ni vipimo maalum vya kimataifa vinavyoonyesha kile ambacho mtoto anahitajika kujua mwishoni mwa elimu ya msingi ya chini. Vinajumuisha uelewa wa kimsingi wa kusoma na ujuzi wa kimsingi kuhusu tarakimu kama vile kutatua tarakimu kamilifu hadi 100 na kusuluhisha hesabu rahisi. Matokeo bora kwa kiasi fulani ya Kenya yanaashiria kupiga hatua katika elimu ya kimsingi, ingawa taifa hili bado linavuta mkia ikilinganishwa na nchi zilizoandikisha matokeo bora kama vile Mexico, Nicaragua, na Pakistan. “Pana haja ya kutathmini upya vifaa vya ufundishaji katika shule zetu kuhakikisha vinapiga jeki somo la tarakimu katika madarasa yetu,” alisema mkurugenzi wa Wizara ya Elimu, Martin Kungania, ripoti za kimataifa kuhusu mitihani ya kimsingi kwa tarakimu (ICAN) na kusoma (ICAR) zilipotolewa. Udadisi huu uliofanyika wiki ya kwanza ya Januari na wiki ya pili ya Agosti nchini Kenya, ulishirikisha watoto 6,669 na familia 4,459. Nchi zilizoshiriki udadisi huo ni pamoja na Kenya, Tanzania, Uganda, Senegal, Mali, Mozambique, Botswana, Bangladesh, Pakistan, Nepal, Mexico, na Nicaragua. Katika sehemu kubwa ya nchi zilizoshiriki, watoto wapatao tisa miongoni mwa 10 wamejiunga na shule, huku wengi wao wakihudhuria taasisi za umma, japo idadi kubwa wanasomea shule za kibinafsi. Kenya imejitokeza kuwa yenye idadi ndogo zaidi ya watoto wasioenda shule.Hii inaashiria kuwa juhudi za serikali za kufanikisha asilimia 100 ya watoto wanaojiunga na sekondari kutoka shule ya msingi, zinazaa matunda. Miongoni mwa watoto Wakenya wenye umri kati ya miaka 10 – 14, zaidi ya asilimia 80 wanahudhuria shule za umma, huku asilimia 16 wakihudhuria shule za kibinafsi na kuacha chini ya asilimia mbili ambao hawako shule. Duniani kote, Mexico inaongoza kwa idadi kubwa zaidi ya watoto waliojiunga na shule za umma kwa asilimia 90 ikifuatiwa na Tanzania asilimia 87 na Mozambique asilimia 85.
MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Meru ameshtakiwa kwa kuuza karatasi bandia za mtihani wa kidato cha nne (KCSE) mwaka 2025. Nasiuma Chrispinus Nambafu, mwenye umri wa miaka 22, alishtakiwa katika Mahakama ya Milimani. Nambafu alifika mbele ya Hakimu Benmark Ekhubi ambapo alikana mashtaka matano ya kuchapisha habari za uongo, kumiliki vifaa vya mtihani bandia vinavyodaiwa kutoka kwa Baraza la Mitihani la Kenya (KNEC), na kumiliki vitambulisho vya kitaifa vya watu wengine kinyume cha sheria. Kulingana na karatasi ya mashtaka iliyowasilishwa mahakamani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) kupitia kiongozi wa mashtaka Sonia Njoki, Nambafu alishtakiwa kwamba kati ya mwaka 2022 na Oktoba 11, 2025, alidai kuchapisha taarifa za uongo na kupotosha kupitia kundi la WhatsApp lililoitwa “Teachers KNEC Exams 2025”, akidai kwamba alikuwa na mitihani halali ya KCSE kutoka kwa KNEC. Katika mashtaka mengine matatu, Nambafu anakabiliwa na tuhuma za kupatikana na vitambulisho vya utaifa vya Lucy Muthoni Kimencu, Bosco Kioko Wambua, na Doris Kathini Kimencu, bila ruhusa ya kisheria, katika eneo la Kianjai, Kata ya Tigania Magharibi, Kaunti ya Meru. Anadaiwa kupatikana na vitambulisho hivyo vya utaifa katika nyumba yake mnamo Oktoba 11, 2025, wakati maafisa wa DCI walipomkamata. Mwanafunzi huyo aliiambia mahakama kuwa alikamilisha masomo katika Chuo Kikuu cha Meru cha Sayansi na Teknolojia (MUST) katika masomo ya Hisabati na Kemia na alikana mashtaka yote, akiomba mahakama impe dhamana inayofaa, akisema yeye anatoka katika familia maskini. Hakimu Ekhubi aliwachilia kwa dhamana ya Sh100,000 na wadhamini wawili wa kiasi sawa.Kesi hii itatajwa tena Novemba, 15 2025.
DAR ES SALAAM: Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimepiga hatua kubwa katika kuboresha elimu ya afya nchini kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), unaotekeleza ujenzi wa Ndaki ya Tiba katika Kampasi za Mloganzila na Kigoma. Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo, Makamu … The post Prof. Kamuhabwa: Mradi wa HEET umeleta mageuzi MUHAS first appeared on HabariLeo.
MITIHANI ya kitaifa kwa wanafunzi zaidi ya milioni 3.4 kutoka shule za umma na za kibinafsi ilianza jana kote nchini. Mitihani hiyo inajumuisha ya wanafunzi wa Gredi ya Sita (KPSEA), Gredi ya Tisa (KJSEA) pamoja na KILEA na KPLEA kwa wanaofuata mtaala wa hatua za kujifunza. Akisimamia usambazaji wa karatasi za mtihani katika Kaunti Ndogo ya Bureti, Kaunti ya Kericho, Waziri wa Elimu Julius Ogamba alihakikishia umma kuwa hatua madhubuti zimewekwa ili kulinda uadilifu wa mitihani. Mwaka huu, jumla ya wanafunzi 3,428,729 wanafanya mitihani katika vituo 68,546 wakiwemo 1,298,089 (KPSEA), 1,130,669 (KJSEA), 2,414 (KILEA) na 1,479 (KPLEA). KPSEA ni ya kuchagua majibu pekee, huku KJSEA ikiwa na maswali ya kuchagua na inayo hitaji majibu ya kuandikwa. Polisi watalinda tu mtihani wa KCSE, huku KPSEA na mitihani mingine ikisimamiwa na walimu na maafisa wa elimu. Katika Kaunti ya Trans Nzoia, baadhi ya vituo vikiwemo Matisi Friends, Central Primary School, St John’s Education Centre, Linta Academy na Royal Victor vilipata mkanganyiko wa karatasi za mtihani. Mkurugenzi wa Elimu wa kaunti hiyo, Pamela Akello, alithibitisha tukio hilo, lakini akasema lilitatuliwa bila kuathiri uadilifu wa mtihani. Aliongeza kuwa kuchelewa kuliathiri wanafunzi ambao hawakuhudhuria majaribio ya maandalizi. Trans Nzoia ina wanafunzi 24,312 wa KJSEA na 26,961 wa KPSEA katika shule za umma, na 23,097 wa KJSEA na 5,174 wa KPSEA katika shule binafsi. Shule za Kitale School na Mary Immaculate Primary ziliendelea vizuri na mitihani. Katika Kaunti za Uasin Gishu na Baringo, mitihani ilianza chini ya ulinzi mkali. Katika Kaunti ya Uasin Gishu, Mkurugenzi wa Elimu David Koech alisema wanafunzi 10 wanafanya mitihani hospitalini jijini Eldoret, akiwemo mama mchanga na wengine waliotoka kaunti jirani. Kamanda wa Polisi, Benjamin Mwanthi, alionya dhidi ya udanganyifu na kuwaonya polisi dhidi ya kubeba simu wakiwa kazini. Katika Kaunti ya Baringo, mitihani ilianza bila matatizo katika vituo 756, na vifaa vikitolewa kutoka kontena 19. Dkt Kipruto Kosgei, ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu wa kaunti hiyo, alisema kuna wanafunzi 15,672 wa KPSEA na 15,411 wa KJSEA. Hata shule zilizokuwa zimeathiriwa na mafuriko kama Noosukro na Loruk Primary, zimeshiriki mitihani hiyo. Ulinzi pia umeimarishwa kwa wadau wote. Katika Kisumu Central, kontena ya mitihani ilifunguliwa saa kumi na mbili asubuhi na Naibu Kamishna wa Kaunti Langat Bosek. Mwenyekiti wa Baraza La Kitaifa La Mitihani Kenya (KNEC) Profesa Julius Nyabundi alisisitiza mabadiliko kutoka neno “mitihani” kwenda “tathmini” na kupunguza uwepo wa polisi shuleni ili kujenga uaminifu. Katika Kaunti ya Kisii, mitihani ilianza vyema katika vituo vyote. Naibu Kamishna Joseph Mwangi anayesimamia Kisii Central na Nyaribari Chache, alisimamia usambazaji wa mitihani katika shule 78 za umma na 14 za binafsi. Katika Kaunti ya Homa Bay, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kitaifa ya Kukuza Mitaala (KICD) Prof Charles Ong’ondo alisema matokeo yatatangazwa kabla ya Sikukuu ya Krismasi. Alibainisha kuwa tathmini za mfumo wa CBE ni sehemu ya mabadiliko kutoka mfumo wa 8-4-4 na akawahimiza wazazi na walimu kuwa watulivu. Aliongeza kuwa polisi watasimamia tu mtihani wa KCSE. Kamishna wa Kaunti Ronald Muiwawi alikiri kuwepo kwa udanganyifu zamani kuliweka doa katika mitihani ya kitaifa miaka ile, huku Mkurugenzi wa Elimu Eunice Khaemba akisema kuna wanafunzi 39,436 wa KPSEA na 36,496 wa KJSEA. Katika Kaunti ya Siaya, kontena ilifunguliwa saa kumi na mbili asubuhi, na wakuu wa shule wakakusanya vifaa kwa wakati. Naibu Kamishna Robert Ngetich aliwataka wasimamizi na wanafunzi kuwa waadilifu, hasa ikizingatiwa kuwa huu ndio mtihani wa kwanza wa KJSEA. Katika kaunti zote Kericho, Trans Nzoia, Uasin Gishu, Baringo, Kisumu, Kisii, Homa Bay na Siaya, serikali imesisitiza uzingatiaji wa sheria, uadilifu na usalama katika kuhakikisha mitihani ya kitaifa inafanywa kwa haki na uaminifu.
MWANAFUNZI wa shule ya upili iliyo eneo la Lamu ya Kati, Kaunti ya Lamu, huenda akalazimika kufanya mitihani yake ya KCSE akiwa chini ya ulinzi wa polisi. Hii ni kutokana na kuwa, alikamatwa na kuwekwa rumande kwa sababu ambazo hazijabainika. Wanafunzi wa Kidato cha Nne walianza KCSE Jumanne iliyopita, kwa mitihani ya Utendaji. Wakati huo huo, mwanafunzi wa mtihani wa kitaifa wa Gredi ya Sita (KPSEA) kutoka Shule ya Faza Boys Comprehensive, Lamu Mashariki, alilazimika kufanya mtihani wake katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya King Fahd ambako amelazwa akipokea matibabu baada ya mkono wake kuvunjika. “Ninafahamu kuwa kuna mwanafunzi amelazwa katika Hospitali ya King Fahd na amefanyiwa upasuaji kwenye mkono uliovunjika. Tumeandaa mipango ili aweze kufanya mtihani wake huko. Pia kuna mwanafunzi mwingine aliye rumande lakini tumefanya mipango ya haraka na naye anafanya mtihani akiwa huko. Hadi sasa kila kitu kinaendelea vizuri,” alisema Mkurugenzi wa Elimu wa Kaunti ya Lamu, Bw Zachary Mutuiri. Mitihani ya KPSEA na KJSEA kitaifa ilianza jana (Jumatatu). Watahiniwa 36 wa KPSEA na KJSEA kutoka msitu wa Boni, Kaunti ya Lamu, walihamishiwa maeneo mengine kufanya mitihani hiyo. Kulingana na Bw Mutuiri, hatua hiyo ilichukuliwa sababu kuu ikiwa ni shule husika kukosa idadi kamili ya angalau watahiniwa 15 wa KPSEA au KJSEA wanaohitajika kuwezesha taasisi zao kuorodheshwa kuwa vituo vya kujisimamia kufanya mitihani hiyo. Kaunti hiyo ina watahiniwa 3,498 wa KPSEA ilhali wale wa KJSEA ni 4,432. Katika Kaunti ya Tana River, Naibu Kamishna, Bw Andrew Mutua, alisema ingawa baadhi ya wanafunzi waliripotiwa kutoweka katika baadhi ya maeneo, hakuna mwanafunzi aliyesajiliwa atakayefanya mtihani hospitalini au gerezani. “Hatutawaacha. Leo tunawatuma machifu kuhakikisha tunapata asilimia 100 ya wanafunzi wote kufanya mitihani,” alisema. Kwa mujibu wa maafisa wa elimu, zaidi ya wanafunzi 5,000 wanafanya mitihani katika maeneo mbalimbali ya Kaunti ya Tana River. Bw Mutua aliwahakikishia wazazi na wadau kuwa mitihani inaendelea kwa utulivu na serikali imejizatiti kuhakikisha mazingira ya haki na amani katika vituo vyote vya mitihani. Huko Mombasa, manyunyu madogo hayakuathiri morali ya walimu na watahiniwa. Mkurugenzi wa Elimu wa Kanda, Bi Anne Kiilu, aliwahimiza walimu kuendelea kuwahamasisha wanafunzi wote wakati wa kipindi hiki cha mitihani, akisema kuwa eneo hilo lina lengo la kuinua viwango vyake vya kitaaluma. Kaunti ya Mombasa ina vituo 573 vya KPSEA vyenye jumla ya watahiniwa 27,498, na vituo 273 vya KJSEA vyenye watahiniwa 21,677. Katika Kaunti ya Taita Taveta, Mkurugenzi wa Elimu wa Kaunti hiyo, Bw Khalif Hirey, alisema maandalizi yote yamekamilika kuhakikisha mitihani inafanyika kwa uwazi kote kaunti nzima. Kaunti hiyo ina vituo 205 vya KPSEA na 194 vya KJSEA ambapo jumla ya watahiniwa 7,546 na 6,867 mtawalia wanakalia mitihani hiyo. Ripoti za Kalume Kazungu, Stephen Oduor, Mishi Gongo na Lucy Mkanyika
DAR ES SALAAM: Mgombea urais kupitia chama cha UMD, Mwajuma Mirambo, ameendelea na kampeni zake za kunadi sera za chama hicho leo jijini Dar es Salaam, katika Wilaya ya Ilala, Jimbo la Segerea, kata ya Vingunguti, kwenye uwanja wa Msikate Tamaa. Akizungumza mbele ya wananchi waliojitokeza kwa wingi, Mirambo amesema serikali ya UMD ikipewa ridhaa … The post Mgombea urais UMD aahidi elimu, afya bora first appeared on HabariLeo.
WANAFUNZI 135,240 waelimu ya juu na ya kati wamepata udhamini wa masomo kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wa thamani ya Sh bilioni 426.5 kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dk Bill Kiwia kwenye mkutano wake na waandishi wa habari jijini Arusha. Dk … The post Wanafunzi 135,240 wapata mikopo first appeared on HabariLeo.
MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, ameahidi kuuenzi urithi wa Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad kwa kujenga Chuo Kikuu cha Maalim Seif Sharif Hamad katika mji wa Wete, Kaskazini Pemba. “ Chuo hichi kitakuwa ni ngome ya maarifa , uzalendo na maendeleo endelevu kwa vizazi vijavyo,” alisema Masoud. The post Othman aahidi Chuo Kikuu kumuenzi Maalim Seif first appeared on HabariLeo.
Na John Mhala,Arusha WANAFUNZI 135,240 wa vyuo vikuu na kati hapa nchini wenye sifa stahiki na waliodahiliwa na vyuo vyao wamefanikiwa kupata mikopo ya awamu ya kwanza ya Sh Bilioni 426.5. Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB), Dk Bill Kiwia mbele ya waandishi … The post HESLB yafafanua waliopata mikopo first appeared on HabariLeo.
WANAFUNZI kutoka shule za Msingi na Sekondari wameipongeza Serikali kwa ujenzi wa miundombinu bora na rafiki ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari, ambayo imechagiza ufundishaji na ujifunzaji. Hayo yamebainika leo Oktoba 24, 2025 jijini Dodoma, katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tathmini ya pamoja ya Sekta ya Elimu. Mwanafunzi mwenye mahitaji maalum, kutoka … The post Wanafunzi wapaza sauti katika tathmini ya elimu ya mwaka first appeared on HabariLeo.
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinaendelea kutekeleza kwa mafanikio Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET), unaolenga kuboresha miundombinu, kuimarisha mitaala, na kukuza mfumo wa kujifunza kidijitali. Mradi huu ni kiungo muhimu katika kuhakikisha elimu ya juu inachangia uchumi wa viwanda na maendeleo endelevu ya Taifa. The post HEET kuboresha miundombinu ya elimu UDSM first appeared on HabariLeo.
NI asubuhi yenye upepo mwanana katika viunga vya Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (RUCU) mkoani Iringa. Ndani ya ukumbi wa mikutano, wasomi, wachumi na wadau wa maendeleo wameketi kwa makini katika kongamano la kujadili mustakabali wa Tanzania kuelekea mwaka 2050. Kaulimbiu ya kongamano hilo lililoandaliwa kwa ushirikiano wa RUCU na Kituo cha Ubia kati ya … The post PPP nguzo ya utekelezaji Dira 2050 first appeared on HabariLeo.
SHULE zinapofungwa wiki hii kwa likizo ya muda wa miezi miwili, Wizara ya Elimu bado inakabiliwa na changamoto kufuatia mgao wa elimu kutotolewa kwa wakati kwa shule mbalimbali. Haya yanatokea huku Hazina Kuu ya Fedha na Wizara ya Elimu zikishirikiana kubadilisha kalenda ya ufadhili kutoka Januari – Disemba hadi Juni ili ioane na mwaka wa fedha wa serikali. Hadi sasa serikali imetoa Sh22.1 bilioni kama mgao wa kufadhili elimu kwa shule za msingi na zile za upili. Baadhi ya shule zilikosa ufadhili wakati ambapo mchakato wa kuhakiki na kuondoa shule feki zenye wanafunzi hewa ulikuwa ukiendelea. Kwa mujibu wa Katibu katika Wizara ya Elimu Julius Bitok, shule 18,000 kati ya zile 23,000 zimepokea mgao wao. Bado shule 5,000 zinahakikiwa. Kuna shule 97,800 za umma ambapo 47,666 ni za chekechea, 35,570 za msingi kisha 10,752 za sekondari. “Shule kadhaa hazijapata mgao kutokana na tofauti kwenye data walizowasilisha kuhakikiwa. Bado data zao zinaangaliwa kabla ya fedha kutolewa,” akasema Profesa Bitok. Profesa Bitok alifichua kuwa Wizara ya Elimu imetoa Sh10.4 bilioni kwa Wizara ya Elimu katika shule za sekondari ambapo Sh10.1 bilioni zimetumwa kwa shule. Kwa shule za sekondari za chini, hazina kuu imetoa Sh4.8 bilioni kati ya Sh5.6 bilioni huku Sh800 milioni ambazo zimesalia zikitarajiwa kutumwa kwa shule. “Ripoti itaandaliwa ambayo itaonyesha tofauti kwenye data iliyowasilishwa. Wakurugenzi wa elimu kwenye kaunti na kaunti ndogo wanafanya kazi na shule ili kushughulikia utata ambao umetokea,” akasema Profesa Bitok. “Imebainika kuwa baadhi ya shule zina wanafunzi chini ya idadi ya wastani ya wanafunzi 45 ambao wanahitajika katika kila darasa kwa mujibu wa Wizara ya Elimu,” akasema Profesa Bitok.
KAMATI ya Kitaifa ya Kuandaa Mazishi imetangaza kuwa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga itafanyika kuanzia saa tatu asubuhi Jumapili katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOUST), Bondo, Siaya. Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Oktoba 18, 2025 jioni, mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo Naibu Rais Kithure Kindiki alisema kuwa ibada hiyo itaendelea hadi saa saba mchana. “Baada ya hapo, kutafanyika shuhuda fupi, maombi na heshima za kijeshi kando mwa kaburi lake nyumbani kwa babake Kang’o Kajaramogi, kijiji cha Nyamira,” akaongeza. Profesa Kithure aliongeza kuwa kamati hiyo anayoongoza pamoja na kakake Raila, Oburu Oginga, itatoa maelezo kuhusu shughuli zitakazofuata “kwa heshima ya marehemu Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga baada ya mazishi ya kesho”. Awali, Katibu wa Usalama wa Ndani Raymond Omollo alitangaza mabadiliko mengine ya shughuli za kutoa heshima kwa mwendazake. Kwa mfano, Dkt Omollo alitangaza kusikitishwa kwa shughuli ya kutoa nafasi kwa wananchi kutaza mwili wa Raila katika Uwanja wa Michezo wa Jomo Kenyatta, eneo la Mamboleo, Kisumu mwendo wa saa tisa alasiri. “Mwili wa kiongozi wetu Raila Amollo Odinga utasafirishwa kwa helikopta hadi Bondo kutoa nafasi kwa wananchi wa eneo hilo kupata nafasi ya kuutazama,” akawaambia wanahabari katika uwanja huo. Kulingana na mipango ya awali, wakazi wa Kisumu wangepata nafasi ya kuutazama mwili hadi saa tisa alasiri kisha usafirishwe kwa barabara hadi Bondo. Shughuli ya kutazama mwili katika Opado Farm, Bondo ulikamilika dakika nne kabla ya saa moja za usiku, Jumamosi.
Ni wazi sasa — historia ya elimu ya juu nchini Tanzania inaandikwa upya katika ardhi ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE). Wakati majengo makubwa yakipanda kama ishara ya matumaini mapya, hewa ya mageuzi inahisiwa kila kona ya chuo hicho, shukrani kwa jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk … The post Dk Samia aandika historia DUCE first appeared on HabariLeo.