DAR ES SALAAM: Msafara wa Baiskeli wa Nyerere Cycling Tour mwaka huu unatarajiwa kutoa madawati 1,000 kwa shule 10, kukarabati madarasa 40 na kujenga madarasa mapya 10, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi nchini. Msafara huo wenye urefu wa kilomita 1,500 hadi Butiama, utafanyika kuanzia Oktoba 5 hadi 14,…
HakiElimu Executive Director Mary Ndaro urged the fellows to use the programme to build the confidence, networks and skills needed to participate meaningfully in national affairs.
KUNYWA chai, kahawa au vinywaji vingine vikiwa moto sana kunaweza kuongeza hatari ya kupata saratani ya umio, kulingana na utafiti uliofanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza. Utafiti huo, uliochapishwa katika Jarida la International Journal of Cancer, ulihusisha watu 977,282 wenye umri wa juu na umeelezwa kuwa mojawapo ya tafiti kubwa zaidi kuchunguza uhusiano kati ya joto la vinywaji na saratani ya umio. Watafiti waligundua kuwa watu waliokunywa vinywaji vilivyo na joto la nyuzi 65 au zaidi walikuwa na hatari karibu mara tatu zaidi ya kupata saratani hiyo ikilinganishwa na waliokunywa vinywaji vya vuguvugu. Kulingana na watafiti, mvuke wenye joto kali unaweza kuharibu chembe zinazofunika umio wakati unapopita kuelekea tumboni. “Kunywa vikombe sita au zaidi vya vinywaji vya moto kwa siku kunaweza kuongeza hatari hiyo. Kuongezwa kwa maziwa kunaweza kupunguza joto kidogo, lakini chai au kahawa yenye maziwa bado inaweza kuwa moto kupita kiasi,” unasema utafiti huo. Chai inayotengenezwa mara tu baada ya maji kuchemka inaweza kuwa na joto la karibu nyuzijoto 100. Inapomiminwa kwenye kikombe, joto hilo hupungua hadi karibu nyuzi 90–95. Wataalamu wanashauri watu kusubiri kwa dakika chache kabla ya kunywa ili kinywaji kipoe hadi joto linalofaa. Mtaalamu wa Afya, Dk Keren Papier, alisema tafiti za awali Amerika Kusini, ambako watu wengi hunywa kinywaji cha mitishamba kikiwa moto sana, pia zilionyesha uhusiano wa kupata aina hiyo ya saratani. Hata hivyo, watafiti walisema hatari ya jumla ya kupata saratani ya umio bado ni ndogo hata kupitia unywaji wa vinywaji moto. Njia muhimu zaidi za kupunguza hatari ni kutovuta sigara na kupunguza unywaji wa pombe. Dalili za saratani ya umio zinaweza kujumuisha kiungulia, maumivu ya koo au kifua na kupungua uzani wa mwili.
DAR ES SALAAM: Wanafunzi 150 wenye uhitaji wanatarajiwa kunufaika na ufadhili wa masomo kupitia mbio za mbuzi za mwaka 2026 zinazoandaliwa na Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oyster Bay, huku klabu hiyo ikilenga kukusanya Sh milioni 250 kwa ajili ya kuwawezesha kuendelea na elimu ya juu. Tukio hilo la kila mwaka la kuchangisha…
ALIYEKUWA kasisi wa Kanisa Katoliki kutoka Italia, Sandro Ferretto, alimuoa Sharon Jepngok Kibet, 37, wikendi katika sherehe ya kitamaduni ya Tugen iliyofanyika Kasiela, Baringo Kusini. Ferretto, 53, aliwahi kuhudumu kama kasisi katika eneo hilo kwa karibu miaka 12 kabla ya kuacha ukuhani na kurejea Italia. Sherehe hiyo ilivutia maelfu ya wakazi waliokuwa wamekusanyika katika boma la babake Sharon, John Wendot, baada ya kusikia kuwa Mzungu alikuwa akimuoa binti wa eneo hilo. Hata hivyo, wengi walishangaa kumtambua bwana harusi kuwa kasisi wao wa zamani ambaye waliwahi kumwona akihudumu katika maeneo ya Kasiela, Chebinyiny, Sinoni, Embosos na Nyimbei. Bw Ferretto aliwasili Kenya mnamo 2008 na kwa miaka yake ya utumishi alitembelea familia, kuhudhuria shughuli za shule, kuwashauri vijana, kusaidia familia zilizohama makwao kutokana na ukosefu wa usalama na kuendesha misa. Sharon alilelewa Kasiela kabla ya kumaliza shule ya upili na kusomea udaktari wa kliniki. Baadaye alisafiri hadi Italia ambako uhusiano wake na Ferretto ulianza. Mnamo 2022, Bw Ferretto aliwasaidia Sharon na vijana wengine saba kutoka eneo hilo kupata ajira nchini Italia. Sharon alimweleza babake mnamo 2024 kuwa Bw Ferretto alikuwa ameacha ukuhani na alitaka kumuoa. “Binti yangu aliniambia kwamba Padre Sandro alikuwa amejiuzulu na alitaka kumuoa. Nilijiuliza, kasisi anawezaje kuoa?” akasema Bw Wendot. Alisema baadaye alikubali baada ya kufahamishwa kuwa Ferretto alikuwa amekamilisha taratibu zote za kuacha ukuhani na kupewa idhini ya kuoa. Wawili hao walifanya harusi ya kanisani nchini Italia Aprili mwaka huu kabla ya kurejea Kenya kwa sherehe ya koito. Bw Wendot alisema hakutaka kutumia uraia wa Bw Ferretto kama kisingizio cha kudai mahari ya kupita kiasi. “Niliozesha binti yangu kwa raia wa Italia kama mtu mwengine yeyote. Sikutarajia kumtendea kama mgeni na kumpunja pesa,” akasema. Bw Ferretto aliongozana na jamaa 12 kutoka Italia, marafiki na waliokuwa wafanyakazi wenzake katika Parokia ya Mochongoi. Sherehe hiyo ilijawa na nyimbo na ngoma za Kalenjin huku Bw Ferretto akicheza pamoja na wakwe na marafiki wake Wakenya. Raymond Cheboi, mdogo wa Sharon, alisema Bw Ferretto alikuwa rafiki wa familia na aliwahi kumsaidia mmoja wa ndugu zao kuwa katekista. Henry Cheburet, mkazi aliyemjua Ferretto tangu alipokuwa kasisi, alisema ndoa hiyo imekuwa gumzo kijijini. “Wengi walifika wakitarajia kumuona Mitalia akimuoa Sharon, lakini baadaye wakagundua kuwa alikuwa kasisi wao wa zamani,” alisema. Wendot alisema amewabariki walioana. “Nimewapa baraka zangu. Mungu awabariki katika ndoa yao,” alisema.
MBEYA: Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kupitia Chuo cha VETA Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza mkoani humo, imeanza mchakato wa kutambua, kutathmini na kurasimisha ujuzi wa ufundi stadi kwa wafungwa 100 walioupata wakati wakitumikia vifungo vyao. Mchakato huo ulianza Agosti 27, 2026, katika Chuo cha Ufundi cha…
SONGEA: Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Naomba, amesema hakuna taaluma inayoweza kujengwa bila msaada wa mwalimu. Profesa Naomba amesema hayo jana, alipokutana na walimu tarajali katika Chuo cha Ualimu Songea, mkoani Ruvuma . “Hakuna mtu anayeweza kuwa na ujuzi bila kupitia mikononi mwa mwalimu,” alisema. Alisema kuwa madaktari, wahandisi,…
KWA mwanafunzi aliye kijijini, kukosa intaneti humaanisha kukosa kuzama mtandaoni. Kwa mgonjwa, kunaweza kumaanisha kusubiri hadi afike hospitalini ili kupata ushauri wa daktari. Kwa mwananchi wa kawaida, huduma inayopatikana kwa simu au mtandao inaweza kumlazimu kusafiri kilomita kadhaa hadi mjini kwa sababu eneo analoishi halina intaneti. Hata hivyo, hali hiyo inaweza kubadilika kwa matumizi ya intaneti ya satelaiti, ambayo inalenga kufikisha mawasiliano katika maeneo ambayo minara na nyaya za kawaida za intaneti hazijafika. Kampuni ya Paratus Kenya, kwa ushirikiano na Starlink, imeanza kusambaza huduma hiyo katika maeneo ya mbali na ambayo hayajahudumiwa ipasavyo nchini. Teknolojia hiyo inajaribiwa katika sekta kama afya na elimu, ambako intaneti si anasa tena bali imekuwa sehemu muhimu ya kupata huduma. Akizungumza jijini Nairobi, Mkurugenzi Mkuu wa Paratus Kenya, Joseph Kibiwott, alisema kampuni hiyo inatafuta njia za kuhakikisha watu wanaoishi mbali na miji hawaachwi nyuma. “Tunatafuta namna ya kupanua muunganisho wa intaneti katika maeneo ambayo hayajahudumiwa ipasavyo nchini,” alisema Kibiwott. Kaunti ya Murang’a ni miongoni mwa maeneo ambayo teknolojia hiyo inafanyiwa majaribio. Gavana Irungu Kang’ata alisema intaneti ya satelaiti tayari imetumika katika huduma za afya, ikiwemo telemedicine, inayowawezesha wagonjwa kupata ushauri wa kimatibabu bila kulazimika kusafiri hadi vituoni. “Tumetumia teknolojia hii katika maeneo kama telemedicine na tunaangalia pia jinsi inavyoweza kutumika kwenye magari ya wagonjwa,” alisema. Hii ina maana kwamba ambulensi njiani, wahudumu wanaweza kuwa na uwezo wa kuwasiliana na wataalamu wa afya na kupata usaidizi kwa wakati unaofaa. Kang’ata pia alisema matumizi ya teknolojia hiyo yamesaidia baadhi ya idara za kaunti kupunguza gharama za intaneti. Hatua hiyo inakuja wakati huduma nyingi muhimu, kuanzia elimu na afya hadi huduma za serikali na biashara, zikihamia mtandaoni. Kampuni hiyo sasa inalenga kupanua mfumo huo katika nchi nyingine za Afrika Mashariki.
As the Tanzania Commission for Universities (TCU) wraps up the first round of undergraduate admissions for the 2026/2027 academic year, a massive logistical and financial bottleneck has emerged.
As the Tanzania Commission for Universities (TCU) wraps up the first round of undergraduate admissions for the 2026/2027 academic year, a massive logistical and financial bottleneck has emerged.
Thousands of students have another opportunity to secure university places after the Tanzania Commission for Universities (TCU) opened the second round of undergraduate admissions for the 2026/27 academic year.
ARUSHA: Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewakumbuka viongozi wakuu wa serikali pamoja na watu maarufu nchini waliosoma katika Shule ya Msingi Arusha, maarufu kama Arusha School, kwa kupanda miti ya matunda na kivuli katika eneo la shule hiyo. Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya kuwaenzi viongozi na watu mbalimbali waliopata elimu katika shule…
IRINGA: MABONANZA ya michezo kwa watumishi wa taasisi mbalimbali yameelezwa kuwa na nafasi muhimu katika kuimarisha afya ya mwili na akili, kupunguza msongo wa mawazo na kujenga mahusiano mazuri kazini. Akizungumza baada ya kuhitimishwa kwa bonanza lililofanyika Septemba 5, 2026 katika viwanja vya Chuo Kikuu Mkwawa (MUCE), Iringa, Mhandisi wa Bodi ya Maji Bonde la…
DAR ES SALAAM: MAMA na Baba lishe wa eneo la Kurasini lililopo Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam wamepatiwa elimu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutumia mkaa mbadala, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha matumizi ya nishati salama. Katika elimu hiyo, washiriki wameelekezwa namna ya kutumia mkaa mbadala ambao unauwezo wa…
TUME ya kuajiri walimu (TSC) imetangaza upya nyadhifa 1,631 za kuwapandisha cheo wasimamizi wa shule, na kuwapa fursa nyingine walimu wanaomezea mate nyadhifa za uongozi huku kukiwa na uhaba wa wasimamizi waliothibitishwa katika shule za umma. Nyadhifa hizo zinajumuisha nafasi 1,470 za Naibu Mwalimu mkuu, 132 Naibu Mwalimu Mkuu III na 29 za Mwalimu Mkuu II katika shule za msingi na sekondari. Tume imealika maombi kutoka kwa walimu wanaohudumu waliofuzu kujaza nafasi hizi za kupandishwa cheo kuambatana na Mwongozo wa Maendeleo Kitaaluma kwa Walimu. Maombi ni sharti yapokewe kufikia usiku wa manane Jumatatu Septemba 14, 2026, ilisema TSC katika notisi. Tangazo hilo jipya limejiri wiki chache tu baada ya Tume kuzindua mchakato wa kupandisha cheo uliojumuisha walimu 34,016 katika daraja zote, katika kile kilichotajwa kuwa moja kati ya shughuli kubwa zaidi za maendeleo kitaaluma katika miaka ya majuzi. Shughuli hiyo iliyotangazwa Julai, iliangazia nyadhifa kuanzia Mwalimu wa Ngazi ya Juu II hadi Mwalimu Mkuu na ilijumuisha nyadhifa za kufundisha, usimamizi wa shule, kuboresha mtaala na vyuo vya mafunzo ya walimu. Nyadhifa mpya zilizotangazwa ni muhimu, kwa sababu zinalenga nafasi za usimamizi wa shule wakati ambapo maelfu ya shule za umma zinaendeshwa bila wasimamizi waliothibitishwa. Mchakato huo wa kupandisha vyeo umejiri kukiwa na malalamishi kuhusu kukwama kitaaluma katika huduma ya kufundisha. TSC ilieleza Bunge kwamba walimu 178,871 wa shule za msingi na sekondari wamesalia katika daraja lile lile la kazi kutokana na upungufu kwenye bajeti, huku tume ikisema inahitaji mabilioni kushughulikia suala hilo. Tume ilisema sehemu kubwa ya walimu waliokwama kitaaluma ni kutoka gredi C3 kwa walimu wa sekondari na gredi C1 kwa walimu wa shule ya msingi ambapo waelimishaji wengi wamesalia kwa miaka mingi licha ya kutimiza viwango vya kufuzu kupandishwa cheo. “Tunaitaka TSC kutangaza mara moja nyadhifa za kuwapandisha vyeo walimu 135,000 ambao wamekwama katika daraja zao za kazi,” alisema Katibu Mkuu wa Kuppet, Bw Akello Misori.
KAGERA: Miradi sita yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 4.8 imepitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, ikiwa na lengo la kuboresha huduma za kijamii na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi. Miradi hiyo imejikita katika sekta za elimu, afya, maji, viwanda, utawala bora…
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma Mkomi, amesema ujenzi wa jengo jipya la ghorofa tatu lenye thamani ya dola za Marekani 750,000 katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Usimamizi cha Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI), ni utekelezaji wa maamuzi ya Bodi ya Taasisi hiyo yenye lengo…
KAGERA: Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang’onda, amemtunuku hati ya shukrani na tuzo Mzee Joseph Masabala, maarufu kama mzee mashuhuri wa Mkoa wa Kagera, kwa kutoa sehemu ya ardhi yake iliyopo Kata ya Kibeta, Manispaa ya Bukoba, kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa bweni la wanafunzi katika Shule ya…
MOROGORO; Wananchi mbalimbali wamejitokeza kwenye banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na kupewa elimu juu ya usimamizi wa shughuli za utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asiia. PURA ni sehemu ya taasisi mbalimbali zilizoshiriki kwenye Tamasha la Nne la Taifa la Utamaduni, Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro na lilikuwa…
WANANCHI wa Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera wamepata elimu kuhusu umuhimu wa uwekezaji kupitia mifuko ya pamoja, huku wahitimu wa Shule ya Msingi Rwambaizi waliomaliza masomo miaka 50 iliyopita wakirejea shuleni na kuchangia maendeleo ya taasisi hiyo. Wahitimu hao wameungana na wahitimu wa Darasa la Saba mwaka 2026 kufanya ibada ya pamoja na kuchangia maendeleo…
BAADHI ya maudhui katika mitandao ya kijamii hasa watoto wanapokaribia kufunga shule kwa likizo, huwa ni watu wakiulizana kuhusu bajeti zao za chakula. Mbali na kiwango cha chakula, kuna wale wanaozungumzia saa ambapo wana wao hutaka kula, wengine hata wakisaka chakula usiku wa manane. Hata hivyo, wataalamu wa lishe wanasema kuwa watoto hawa ambao pia wako katika umri ambao muda wao mwingi wanatumia katika masomo, asilimia ishirini ya kiwango cha chakula wanachokula kila mara hutumika na ubongo. Kulingana na Tom Wanjala, baba wa watoto watatu ambaye kifungua mimba wake ana umri wa miaka 16 na mchezaji wa mchezo wa raga, anasimulia jinsi alivyoshuhudia mabadiliko hayo kwa mwanawe. “Punde tu kifungua mimba wangu alipofikisha umri wa miaka 13, alianza kula chakula kingi zaidi. Hivi majuzi alipokuwa nyumbani kwenye likizo nilipokuwa nikimuangalia anavyokula sima maanake nilikuwa naye mezani, ndipo nilithibitisha kuwa katika umri wake na pia akiwa mtoto wa kiume anakula zaidi ya watu wengine katika familia,” anasema mzazi huyo. Baba huyo pia anasema kuwa mwanawe alipokuwa wa umri mdogo, hamu yake ya kula ilikuwa chini sana. Kulingana naye, kumuona mwanawe kuwa na hamu ya juu ya kula kunamdhihirishia jinsi anavyozidi kukua. Hamu ya kula imezidi “Hata mwanangu ambaye ana umri wa miaka 10 pia nimegundua kuwa hamu yake ya kula imezidi kuongezeka kinyume na alivyokuwa akila hapo awali. Miaka ya hapo awali haswa walipokuwa chini ya umri wa miaka saba, nilikuwa nikiwalazimisha wote wawili kula lakini kwa sasa wanataka chakula wenyewe tena kwa wingi,” anaongeza Tom. Mzazi huyo ambaye anaelewa sayansi ya matumizi ya lishe mwilini miongoni mwa watoto wanaobalehe, anasema kuwa kwa sasa jukumu lake ni kuhakikisha kuwa wanawe hawakosi chakula ilikuwasaidia kukua. “Huwa namruhusu mwanangu ale kwa sababu najua atafika katika umri ambapo hamu yake ya chakula itapunguka jinsi tu yangu ilivyopunguka. Nilipokuwa kwenye umri wa kubalehe nilikuwa nikila jinsi tu mwanangu anavyokula kwa sasa. Nafahamu kuwa anahitaji nguvu nyingi za kutembea, kucheza na pia kwenye shughuli tofauti maanake ni vigumu sana kumpata akiwa ameketi tu na kutulia sehemu moja akiwa nyumbani,” anasimulia. Alfrique Otieno Mwana, pia anashuhudia hali sawia kwake. “Kifungua mimba wangu yuko katika Gredi 10. Wakati alipokuwa nyumbani kwenye likizo na kuketi kwenye meza alikuwa akipakua chakula kingi ambacho alikuwa akila chote. Mwenzake mdogo ambaye pia ni mvulana wa umri wa miaka 10 pia hula kiwango cha juu cha chakula kinyume na hapo awali,” anasema mzazi huyo. Wakati uo huo, Alfrique anasema kuwa kifungua mimba wake ambaye yuko katika shule ya bweni huwa na hamu ya juu ya chakula kutokana na tamaa ya kukosa chakula cha nyumbani kwa muda. “Anapokuja nyumbani wakati wa likizo anataka sana kula chapati na akipewa moja au mbili hashibi. Unapata anakula tatu au nne ndiposa anashiba. Huwa namhimiza ale hadi ashibe kwa sababu hivyo ndivyo babangu alivyonifunza kula ilmradi siharibu chakula. Ninapomuona mwanangu anapokuwa na hamu ya juu ya kula chakula najua ni umri wake ambao ataupita siku za usoni,” anasema. Ishara ya kukua Kama tu Tom, mzazi Alfrique pia anakumbuka jinsi wanawe walipokuwa wachanga hawakuwa na hamu ya kula chakula. Kuwaona hamu yao ikiongezeka ni ishara kwake kuwa wanakua. “Wakati wakiwa kwenye likizo wanakula mara tatu kwa siku na pia wanakula vitafunio katikati. Kitinda mimba wangu wa umri wa miaka miwili angali hana hamu ya kula hivyo mara nyingi anakula kiamsha kinywa kuchelewa kisha anakula chajio mapema kwa sababu huwa anaamka kuchelewa na pia analala mapema,” anasema Alfrique. Kiwango cha lishe katika umri wa watoto wanaobalehe hutegemea na viwango vyao vya ukuaji. Haya ni kwa mujibu wa mtaalamu wa lishe ya kitabibu katika hospitali ya, Aga Khan University Hospital, Valentine Young Kwadha. Wakati uo huo, anaeleza kuwa mabadiliko yanayoendelea katika mwili wa mtoto kuanzia umri wa miaka 10 huhitaji ale chakula kingi zaidi ya alivyokuwa akila hapo awali. Hali hii anasema huchangia mtoto anayebalehe kula angalau asilimia 25 ya chakula zaidi ya kiwango ambacho mtu mzima katika familia hula. “Haistahili kuwa jambo la kushtua kuona mtoto anayebalehe akila chakula kingi kwa sababu hicho ndicho kiwango wanachohitaji kulingana na shughuli za kimwili..Mahitaji ya nguvu mwilini mwa watoto hawa kwa ujumla huanzia 2,000 hadi 3,000 kilokalori kila siku. Hii ni sawa na kusema kuwa mtoto anakula mara sita kwa siku kwa sababu wanakula mara nyingi na kiwango cha chakula wanachokula pia kinaongezeka,” anaeleza mtaalamu huyo. Kiwango cha mazoezi ya mwili Pia anasema kuwa kiwango cha chakula watoto hawa hula hutofautiana kulingana na urefu, jinsia na kiwango cha mazoezi miongoni mwao. Kwa mfano, mtoto wa umri wa miaka 13 aliye na urefu wa sentimita 120 atakula chakula zaidi ya mwenzake wa umri sawa lakini urefu wake ni sentimita 100. “Jinsi mwili unavyotumia nguvu na virutubisho kuanzia umri wa miaka 10 hadi 13 huwa juu miongoni mwa watoto wavulana ukilinganishwa na wasichana. Katika umri huu, miili ya wasichana huunda seli za mafuta zaidi huku miili ya wavulana ikiunda misuli. Misuli inahitaji nguvu na virutubisho zaidi,” anasema Valentine. Anawashauri wazazi wa watoto walio katika umri wa kubalehe kuwa watoto hao wanastahili kula kila baada ya saa 3-4. Kiamsha kinywa, chakula cha mchana na chajio anasema zinastahili kuwa sehemu kuu ya mlo wao. Katikati ya milo hiyo, anasema kuwa watoto hao wanastahili kula vitafunio kama vile matunda, njugu na sehemu ya kile walichobakisha wakati wa kiamsha kinywa kwa kuzingatia lishe bora. “Sahani ya mtoto anayebalehe inastahili kuwa na wanga, vitamini na protini. Katika umri huu, watoto wanahitaji protini zaidi. Kwa mfano, ikiwa aina ya chakula cha protini unaowalisha ni mayai, basi watahitaji mayai mawili wakati wa kiamsha kinywa, mayai mawili wakati wa chakula cha mchana na mayai mawili kwa chajio. Mayai hayo yatawapa kiwango cha protini wanayohitaji siku hiyo,” anaeleza Valentine. Vilevile, anawashauri wazazi kutowalisha watoto zaidi au kiwango cha chini cha chakula ili kuzuia watoto hao kukabiliwa na athari za utapiamlo. Hali hiyo huweza kubainishwa kupitia ushauri wa mtaalamu wa lishe kwa sababu kila mtoto huhitaji ushauri binafsi kulingana na kiwango cha lishe miili yao inahitaji. Kadhalika, anahimiza wazazi kuhakikisha kuwa watoto hawa wanapata usingizi wa kutosha wa kati ya saa nane hadi 10 mfululizo kila usiku, muda ambao pia hawastahili kuwa wanakula.
GEITA: TAASISI ya Mapung’o Foundation imetoa msaada wa magunia 30 ya mahindi na kilo 250 za sukari kwa Shule ya Msingi Bagaza iliyopo Kata ya Butobela wilayani Geita. Msaada huo unalenga kusaidia upatikanaji wa uji shuleni hapo kwa wanafunzi zaidi ya 1,700 na kuwatengenezea mazingira bora ya kujifunzia ili kuunga mkono juhudi za serikali za…
WAKUU wa shule za sekondari wameonya kuwa uhaba wa fedha unaathiri ubora wa elimu, huku wakitaka serikali iongeze kiwango cha fedha kinachotolewa kwa kila mwanafunzi. Wakuu hao wamesema gharama ya kuendesha shule imeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu kiwango cha ufadhili cha Sh22,244 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka kilipowekwa mwaka 2014. Onyo hilo linajiri shule zinapoanza muhula wa tatu, ambao ni muhimu kwa watahiniwa wa Kidato cha Nne wanaojiandaa kwa mitihani yao ya kitaifa (KCSE). Kwa mujibu wa uchanganuzi wa Chama cha Wakuu wa Shule za Sekondari (KESSHA), shule zimepokea Sh16,056.29 kwa kila mwanafunzi mwaka huu, dhidi ya Sh22,244 zinazotarajiwa. Hii inaacha pengo la Sh6,188 kwa kila mwanafunzi, sawa na asilimia 27.82 ya fedha zinazotarajiwa. KESSHA ilisema shule zilipokea Sh7,952.04 kwa kila mwanafunzi katika muhula wa kwanza, Sh4,766.49 muhula wa pili na Sh3,337.76 mwanzoni mwa muhula wa tatu. Mwenyekiti wa shule za kitaifa, Casper Maina, ambaye pia ni mkuu wa Nairobi School, alisema kiwango hicho hakikidhi mabadiliko ya gharama ya maisha. “Mgao hautoshi. Kiwango hiki kiliwekwa mwaka 2014, miaka 12 iliyopita. Mambo mengi yamebadilika tangu wakati huo. Kwa nini hakiongezwi upya?” alisema. KESSHA ilisema shule zilipokea Sh11,892.14 kwa kila mwanafunzi mwaka 2023, sawa na asilimia 53.46 ya kiwango kilichotarajiwa. Mwaka 2024, kiasi hicho kiliongezeka hadi Sh16,205.96, sawa na asilimia 72.86, kabla ya kushuka hadi Sh15,385.12 mwaka 2025. Mwaka huu, ingawa kiasi kilichotolewa kimeongezeka, bado shule hazijapokea fedha zote zinazotarajia. Wakuu wa shule walisema wanakabiliwa na gharama kubwa za chakula, umeme, maji, usafiri na vifaa vya masomo na mishahara ya wafanyakazi wasio walimu. “Tunatakiwa kutoa elimu bora kwa kutumia rasilimali ambazo hazijaongezeka kulingana na gharama. Mkuu wa shule analazimika kuamua ni jambo gani la kulipia sasa na lipi litasubiri,” alisema mkuu mmoja wa shule Nakuru. Shule pia zinakabiliwa na gharama ya maandalizi ya mtihani wa KCSE, ikiwemo ununuzi wa kemikali, vifaa vya maabara na uchapishaji wa mitihani ya marudio. Mkuu mwingine wa shule Nairobi alisema baadhi ya shule zimeanza kutegemea kukopa toka kwa wasambazaji. “Tunakopa na kuwaomba wasambazaji watupatie muda zaidi. Lakini huwezi kuendelea kukopa milele,” alisema. Wakati huo huo, Waziri wa Elimu, Bw Julius Ogamba amewataka wakuu wa shule kutumia fedha za umma kwa uangalifu na kuacha kuwatoza wazazi ada zisizoidhinishwa. “Serikali imejitolea kutekeleza wajibu wake kwa wanafunzi na taasisi za elimu,” alisema.
ARUSHA: Juhudi za wananchi wa Kitongoji cha Lailupa, Kijiji cha Meirugoi, Kata ya Gelai-Meirugoi wilayani Longido mkoani Arusha, za kujitolea kujenga darasa la shule ya awali (chekechea) lenye thamani ya Sh milioni 12, zimemgusa Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Steven Kiruswa, ambaye ameamua kugharamia hatua ya mwisho ya ukamilishaji wa jengo hilo kwa Sh milioni…
TANGA; Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na taasisi zake kuhakikisha bunifu zinazozalishwa na Watanzania haziishii kuoneshwa kwenye maonesho, bali zinaendelezwa, zinalindwa na kupelekwa sokoni, ili zitoe suluhisho kwa changamoto mbalimbali na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa. Waziri Mkuu ametoa maelekezo hayo leo, Jumatatu, Agosti 24, 2026,…
DAR ES SALAAM: Wanafunzi zaidi ya 95 kutoka Tanzania wameondoka nchini kwenda India kwa ajili ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali, ikiwa ni kundi la kwanza kati ya wanafunzi 198 wanaotarajiwa kusafiri kwenda India kupitia Global Education Link mwaka 2026. Wanafunzi hao wameondoka kupitia Kituo cha Ndege cha Kimataifa cha…
As universities increasingly turn to digital platforms to expand access to higher education, experts have warned that the rapid growth of online learning could undermine public confidence in academic qualifications unless institutions strengthen their internal quality assurance systems. The warning emerged during a Tanzania Commission for Universities (TCU) consultative workshop in Tanga on August 22, 2026. The meeting brought together vice-chancellors, deputy vice-chancellors, principals, and senior academic leaders from across the country to discuss emerging trends in higher education. Held alongside National Education, Skills and Innovation Week under the theme: Responding to Emerging Trends and Advancing Excellence in University Education, the forum highlighted online and transnational education as key areas requiring urgent intervention. Director of Academic and Institutional Audits at the Zimbabwe Council for Higher Education (ZIMCHE), Dr Hardson Kwandayi, noted that online learning is expanding rapidly across Africa, driven by digital transformation, internationalisation, and demand for flexible study modes. However, he warned that this rapid growth poses significant risks to universities and regulators, spanning academic integrity, inadequate infrastructure, degree recognition, and the proliferation of fraudulent providers. "Traditional quality assurance systems are no longer sufficient for online education, as they were designed mainly for campus-based institutions and often fail to evaluate digital learning environments adequately," said Dr Kwandayi. While online learning removes geographical barriers, supports self-paced study, and fosters international collaboration, Dr Kwandayi stressed that these benefits depend entirely on robust institutional frameworks. Unlike conventional contact learning, digital delivery exposes students to unstable internet connections, high data costs, limited peer interaction, and weak academic support. Universities also struggle to deliver practical laboratory training online, while digital assessments heighten risks of plagiarism, impersonation, contract cheating, and unauthorized AI tool usage. Unchecked poor-quality providers threaten to erode public trust across the entire higher education ecosystem. Dr Kwandayi urged institutions to collaborate closely with quality assurance agencies rather than relying solely on external regulation. TCU's regulatory response In response, the TCU is tightening frameworks governing internal quality standards. TCU executive secretary, Prof Charles Kihampa, told delegates that the regulator has adopted resolutions to strengthen institutional Quality Assurance Units, enforce regulatory compliance, and improve academic governance. Key measures include embedding quality assurance into strategic planning, acting on audit recommendations, and enforcing approved student intake limits through the Universities Information Management System. "The Commission already maintains specific guidelines covering online and blended delivery modes, alongside programme benchmarks and the University Qualifications Framework," said Prof Kihampa. He added that all programmes must undergo accreditation via the online Programme Management System, which also functions as a public database of accredited curricula. Beyond compliance Regional Project Coordinator for the East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP), Dr Cosam Joseph, argued that institutions must look beyond basic regulatory requirements. "Compliance alone is no longer sufficient to ensure institutions remain relevant, innovative, and globally competitive," said Dr Joseph, urging university leaders to reposition quality assurance as a driver of continuous improvement, evidence-based decision-making, and institutional excellence.
Portugal has enacted a law banning face coverings in public spaces, a measure that has been widely criticised as targeting Muslim women who wear full-face veils.
TANGA: Ubunifu wa wanafunzi na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) umeendelea kuibua matumaini kwa wananchi katika kutafuta suluhisho za changamoto mbalimbali za afya zinazowakabili katika maisha ya kila siku. Kupitia banda la MUHAS katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayofanyika katika Shule ya Sekondari Usagara, wananchi…
SHULE za jamii, zilizo katika kundi la C4, huenda zikanufaika pakubwa na mpango mpya wa usajili wa wanafunzi wa Gredi 10 unaopendekezwa kuanza Januari 2027. Wabunge wamepitisha kwa kauli moja hoja inayotaka Wizara ya Elimu, kwa ushirikiano na taasisi nyingine, kuweka idadi ya mikondo ambayo kila kundi la shule linaweza kuwa nayo. Chini ya pendekezo hilo, shule za kitaifa zilizo kundi la C1 zitakuwa na mikondo isiyozidi 10, za mikoa zilizo kundi la C2 mikondo minane, za kiwango cha kaunti katika kundi la C3 mikondo mitano na za kaunti ndogo na kijamii katika C4 mikondo mitatu. Kila mkondo hautaruhusiwa kuwa na zaidi ya wanafunzi 40. Hii ina maana kuwa shule ya kitaifa haitapokea zaidi ya wanafunzi 400. Mbunge wa Kitutu Masaba Clive Gisairo, aliyewasilisha hoja hiyo, alisema mpango huo utasaidia kupunguza msongamano katika shule za kitaifa na za mikoa huku ukiongeza idadi ya wanafunzi katika shule za kaunti na za kaunti ndogo.
ARUSHA: THE Executive Secretary of the National Examinations Council of Tanzania (NECTA), Prof Said Mohamed, has been elected the new President of the Association for Educational Assessment in Africa (AEAA) for the 2026/2027 term, pledging to strengthen unity, transparency and accountability within the organisation. Prof Mohamed said the challenges facing education systems across Africa require…
TANGA; Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) kimeendelea kujipambanua kama kitovu cha tafiti na bunifu zinazotoa majibu ya moja kwa moja kwa changamoto zinazoikabili jamii, huku kikisisitiza mfumo wa vitendo kwa wanafunzi wake kabla ya kuhitimu. Akizungumzia juhudi hizo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Evaristo Liwa, amesema chuo kimeimarisha mfumo ambapo kila muhula wanafunzi wanafanya…
TAKRIBAN thuluthi moja ya wanafunzi wanaojiunga na Sekondari Pevu kutoka Sekondari Msingi hawana ujuzi muhimu wa kusoma, kuandika na kuhesabu, ripoti mpya imefichua. Ripoti hiyo iliyotolewa na Usawa Agenda, shirika linalofanya utafiti kuhusu elimu ya msingi, pia imeonyesha kuwa wanafunzi katika shule za umma za maeneo ya mashambani ndio walioathirika zaidi. Utafiti huo uliofanywa katika kaunti zote 47 ulihusisha familia 41,156, shule 1,527 na wanafunzi 49,835. Pia ulihusisha jamii za wakimbizi katika kambi za Dadaab, Kakuma na Kalobeyei. Ripoti hiyo inasema asilimia 29 ya wanafunzi wa Gredi 9 hawana ujuzi wa msingi wa kusoma na kuhesabu. Mwanafunzi mmoja kati ya watano wa Gredi 9 hawezi kusoma hadithi ya Kiingereza ya kiwango cha Gredi 3. Hali hiyo pia inawakumba wanafunzi watatu kati ya 10 wa Gredi 7. Hata hivyo, pengo hilo huanza mapema zaidi. Asilimia 41 ya wanafunzi wa Gredi 7 hawana ujuzi wa msingi wa kusoma na kuhesabu. Ripoti hiyo ilisema shule za umma hufanya vibaya kuliko shule za kibinafsi katika kusoma na kuhesabu. “Ushahidi unaonyesha kuwa sera za serikali zimefanikiwa kuwadumisha wanafunzi madarasani, lakini bado hazijafanikiwa kuhakikisha wanajifunza au shule wanazojiunga nazo zina vifaa sawa vya kusoma,” ripoti hiyo ilisema. Ripoti hiyo ilibaini pia upungufu mkubwa wa vifaa shuleni. Ni asilimia 27.5 pekee ya shule za Sekondari Msingi zilizo na maabara za sayansi zinazofanya kazi, huku asilimia 27 zikiwa na maktaba. Ni asilimia 34.3 pekee zilizo na vifaa vya kutosha vya kusoma na asilimia 46.3 zilikuwa na kompyuta za wanafunzi. Tofauti za kikanda ni kubwa. Nairobi ina maabara zinazofanya kazi katika asilimia 98.7 ya shule za Sekondari Msingi, ikilinganishwa na asilimia 15.4 Kaskazini Mashariki na asilimia 13.8 Magharibi. Mkurugenzi wa Idara ya Sekondari Msingi katika Wizara ya Elimu Hellen Avisa, alisema changamoto ya ujuzi wa msingi inapaswa kushughulikiwa mapema. Alisema ushahidi uliowasilishwa unapaswa kuchochea hatua katika ngazi ya kitaifa, kaunti na shule. Ripoti hiyo inapendekeza wanafunzi wa Gredi 7 hadi 9 wapewe masomo maalum ya kurekebisha mapengo ya kusoma na kuhesabu. Pia inataka serikali kuongeza uwekezaji katika maabara, maktaba, vifaa vya kusoma na kuhakikisha fedha za shule zinatolewa kwa wakati. Ripoti hiyo ilisema ni asilimia 52.3 pekee ya shule za Sekondari Msingi zinazopokea fedha kwa wakati.
ARUSHA: KATIKA jitihada za kukuza ushirikiano kati ya taasisi za mafunzo na wenye viwanda na waajiri, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Hussein Mohamed Omar amehimiza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kushirikiana na wamiliki wa viwanda. Hususani Dk Omar aliiisisitiza VETA kuingia makubaliano na kampuni ya Hans…
GEITA; Taasisi ya Mapung’o Foundation iliyopo mkoani Geita imetoa msaada wa gunia 75 za mahindi ya chakula katika Shule ya Sekondari Nyakagwe, ili kuunga mkono upatikanaji wa chakula shuleni. Msaada huo unalenga kufanikisha utekelezaji wa sera ya serikali ya kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni wakati wa masomo na kutengeneza mazingira rafiki ya kujifunza. Mratibu wa…
DAR ES SALAAM: BALOZI wa Uturuki nchini Tanzania, Bekir Gezer, amesema uhusiano kati ya Tanzania na Uturuki unaendelea kukua na kuimarika katika maeneo mbalimbali, akisisitiza kuwa ushirikiano huo utaendelea kuleta fursa na manufaa kwa wananchi wa nchi hizo mbili. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam baada ya Chuo Kikuu cha Ankara na Chuo…
TANGA: Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kinashiriki katika Wiki ya Maadhimisho Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa kuonyesha bunifu zalishi nane zinazolenga kutoa suluhisho kwa changamoto katika afya, kilimo na ustawi wa jamii. Bunifu hizo ni pamoja na ROBOSPINE, inayosaidia watoto wenye spina bifida kusimama, kutembea na kufanya mazoezi; BILIMEASURE,…
TANGA: Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Buriani amepongeza na kuonesha kufurahishwa na bunifu zinazotengenezwa na wanafunzi na watafiti wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), zinazowasilishwa katika maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika katika Shule ya Sekondari Usagara, Mkoa wa Tanga. Akiwa katika banda…
DAR ES SALAAM: Meneja Mradi wa Taasisi ya Utamaduni na Maendeleo Afrika Mashariki (CDEA), Angela Kilusungu, amesema ujio wa mwanamuziki mkongwe kutoka Afrika, Yvonne Chakachaka, nchini Tanzania unalenga kutoa elimu na kuhamasisha wasanii kuhusu umuhimu wa kulinda na kunufaika na haki za kazi za muziki. Kilusungu amesema hayo leo Dar es Salaam, wakati akimpokea Chakachaka,…
RUVUMA; Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Wakili Mary Makondo, amezindua mradi wa MsingiTek unaolenga kujenga stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika Shule ya Msingi Humbaro, Kijiji…
ARUSHA; BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) limesema limejipanga kutumia teknolojia ya Akili Mnemba (AI) kuboresha mifumo ya utahini na tathmini ya elimu nchini, likisisitiza kuwa Tanzania haiwezi kubaki nyuma wakati teknolojia hiyo ikiendelea kubadili sekta mbalimbali duniani. Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohamed, amesema hayo leo jijini Arusha wakati wa Mkutano wa 42…
DAR ES SALAAM: FIFTY-FIVE years after Tanzania enacted its marriage law, and a decade after Rebeca Gyumi took the government to court over provisions allowing girls to marry before the age of 18, the legal question at the heart of the case remains unresolved. The 2016 lawsuit was widely seen as a turning point in…
ZANZIBAR: MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeahidi kuendeleza ushirikiano na Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar katika kutoa elimu na mafunzo ya ufundi stadi yenye ubora kwa kwa wananchi wa pande zote mbili za Tanzania bara na Zanzibar. Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore amesema hayo Agosti 14 alipotembelea mabanda…
BUKOBA, KAGERA: Kampuni ya Helios Towers imezindua rasmi maabara ya kisasa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika Shule ya Sekondari Katale iliyopo wilaya Bukoba mkoani Kagera, ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kurudisha fadhila kwa jamii kupitia uwekezaji katika sekta ya elimu na maendeleo ya kidijitali nchini Tanzania. Mradi huo umefadhiliwa na…
DODOMA: NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Denis Londo, amepongeza Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) kwa mpango wake wa kuwajengea watoto uelewa wa vipimo, akisema hatua hiyo imezaa mabalozi wanaoweza kueneza elimu hiyo kwa jamii. Londo alitoa pongezi hizo baada ya kupokea elimu kuhusu umuhimu wa kutumia vipimo sahihi kutoka kwa wanafunzi wa Klabu ya…
DAR ES SALAAM; MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Madenge, Temeke, Dar es Salaam, Khadija Mani ameishukuru Jubilee Group kwa kuwajengea ukuta kuzunguka shule hiyo kwa lengo la kuimarisha usalama na kuondoa changamoto ya usumbufu uliokuwa ukisababishwa na wapita njia na kuathiri mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Akizunguka katika hafla ya makabidhiano ya ukuta huo,…
Klabu ya Rotary imekabidhi madawati 150 kwa Shule ya Msingi Mwananyamala B, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya mchango wake wa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kujifunza kwa wanafunzi pamoja na kuunga mkono jitihada za Serikali za kuinua kiwango cha elimu nchini. Akizungumza katika makabidhiano hayo leo Aprili 29, Ofisa Elimu wa Kata…
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi, amewataka wahitimu wa Taasisi ya Teknolojia ya India Madras (IIT Madras) kutumia elimu, maarifa na ubunifu wao kama nyenzo za kutatua changamoto za jamii, kuboresha maisha ya wananchi na kuchangia maendeleo endelevu.
MOROGORO: Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimepongeza Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta ya Binafsi (PPPC) kwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya ubia (PPP) kama nyenzo ya kuharakisha maendeleo ya sekta ya kilimo na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa. Akizungumza leo Julai 17, 2026 wakati wa Mhadhara wa Wazi…
MOROGORO: Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimezindua programu mpya za Shahada ya Sayansi ya Ualimu katika mkondo wa Amali, hatua inayolenga kusaidia kutatua uhaba wa walimu wa masomo ya amali katika shule za sekondari nchini. Programu hizo zitawaandaa walimu watakaofundisha masomo ya uzalishaji wa mazao, ufugaji, viumbe maji, bustani pamoja na nguo na…