For much of the past three years, the global artificial intelligence race has been measured in models, chips and computing power. Technology companies have competed to build more capable systems, governments have rushed to establish AI strategies, and investors have poured billions of dollars into what many believe will become the defining technology of this generation.
Adhabu ya kaburi aijuaye maiti The Swahili expression “Adhabu ya kaburi aijuaye maiti” is a powerful proverb about suffering, hidden pain and personal experience. Its English equivalent would be:“Only the dead know the pain of the grave.” “Only the person going through it knows how painful it is.”“You never truly understand someone’s suffering until you…
IRINGA: Walemavu mkoani Iringa wameipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutoa elimu ya fedha inayowasaidia kuelewa utunzaji sahihi wa fedha, matumizi ya mikopo na namna ya kutambua alama za usalama zilizopo kwenye noti, huku wakiiomba benki hiyo kupanua wigo wa mafunzo hayo ili yawafikie walemavu wengi zaidi, hususan wanaoishi maeneo ya vijijini. Pongezi hizo…
A total of 34 Tanzanian operators named in the EU's latest published Air Safety List, including the national carrier Air Tanzania, Precision Air and several companies serving the country's tourism and domestic aviation markets.
MWANASPOTI limepata taarifa kuwa Swedy Mkwabi amechukua fomu kwa njia ya mtandao kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Simba SC katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Januari 30, 2027.
MDHIBITI wa Bajeti (CoB) Margaret Nyakang’o, amezua wasiwasi kuhusu hatua ya Kaunti ya Nairobi kukopa Sh1.5 bilioni kila mwezi kutoka Sidian Bank kulipa mishahara, licha ya serikali kuu kutoa mgao wa fedha kwa wakati. Ripoti iliyowasilishwa mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, inaonyesha kuwa kaunti hiyo ilikopa Sh1.56 bilioni Septemba na Sh1.49 bilioni Oktoba. Katika barua ya Novemba 16, 2026, Waziri wa Fedha wa Kaunti ya Nairobi Ibrahim Nyangoya Auma alithibitisha kuwa serikali ya kaunti ilitia saini makubaliano na Sidian Bank kuwezesha malipo ya mishahara. Hata hivyo, baadhi ya makato ya wafanyakazi yaliyopaswa kupelekwa kwa vyama vya akiba na mikopo (SACCO), hazina za pensheni na taasisi nyingine hayakulipwa kikamilifu. Benki hiyo ilionyesha kuwa Sh249.3 milioni za makato hayo Agosti bado hazijalipwa Septemba sawa na Sh254.5 milioni za Septemba zilizopaswa kulipwa Oktoba. Katika barua ya Novemba 16, 2026, Waziri wa Fedha wa Kaunti ya Nairobi Ibrahim Nyangoya Auma alithibitisha kuwa serikali ya kaunti ilitia saini makubaliano na Sidian Bank kuwezesha malipo ya mishahara. Alisema mpango huo ulilenga kushughulikia changamoto za haraka za kulipa wafanyakazi huku kaunti ikiimarisha mapato na usimamizi wa fedha. Hata hivyo, Nyakang’o alihoji sababu ya kaunti kukopa ilhali mgao wa fedha kutoka Serikali ya Kitaifa haukuwa umechelewa. “Hadi Oktoba, kaunti zilikuwa zimepokea mgao wao. Nairobi hata imepokea fedha za Novemba, lakini bado inakopa kutoka Sidian Bank,” alisema. Alisema ofisi yake iliitaka serikali ya Gavana Johnson Sakaja kueleza gharama ya riba inayolipwa kwa mkopo huo. Wasiwasi mwingine ni matumizi ya mfumo wa malipo ya mishahara nje ya Mfumo wa Taarifa za Rasilimali Watu (HRIS), ambao unaunganisha malipo ya mishahara na makato ya kisheria. Nyakang’o alisema utaratibu huo unaweza kusababisha wafanyakazi kulipwa mishahara huku michango ya pensheni, makato ya SACCO na marejesho ya mikopo yakikosa kuwasilishwa. “Hatari yake ni kuwa makato ya kisheria hayalipwi. Hili ni janga linalosubiri kutokea,” alisema. Aliongeza kuwa baadhi ya michango ya pensheni na malipo ya mikopo ya wafanyakazi hayakuwa yamewasilishwa kwa taasisi husika.
That goal has taken on greater importance as global competition in technology has intensified and international restrictions on access to some advanced technologies have tightened.
According to the report delivered at the 19th CPC National Congress in October 2017, China would relieve Beijing of functions nonessential to its role as the capital and use this effort to drive the coordinated development of the Beijing-Tianjin-Hebei region
CHAMA cha Wanafunzi wa Kiswahili katika Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (CHAWAKAMA-KENYA) kimezidisha juhudi za kukiendeleza Kiswahili na kukipa nafasi katika ulimwengu wa utandawazi kupitia makongamano yanayowaleta pamoja wanazuo, watafiti na wadau wa lugha hii adhimu. Mbali na kukuza Kiswahili, chama hiki kimekuwa jukwaa muhimu la kuwaunganisha wanafunzi wa vyuo vikuu, kuibua vipaji, kujenga mitandao ya kitaaluma na kuhamasisha ubunifu. Pia, kimechangia kuzalisha viongozi, waandishi, wahariri, watafiti na wakalimani watakaokipeperusha Kiswahili katika majukwaa ya kimataifa. Mwelekeo huo ulidhihirika Novemba 6–7 mwaka huu, wakati CHAWAKAMA-Kenya kilipoandaa kongamano la kikanda katika Chuo Kikuu cha Laikipia, lililoongozwa na kaulimbiu ya ‘Kiswahili na Utandawazi’. Kongamano hilo liliwakutanisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali, vikiwemo Rongo, Laikipia, Masinde Muliro, Kisii, Daystar, Kabianga, Murang’a, Turkana na Kaimosi. Washiriki walijadili nafasi ya Kiswahili katika kuzalisha maarifa, kuwasilisha uvumbuzi na kutatua changamoto za jamii. Kongamano lilifunguliwa rasmi na Prof Guyo Sarr Huka, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Laikipia anayesimamia masuala ya kitaaluma. Katika tukio hilo, kamati andalizi ikiongozwa na Mwenyekiti Clinton Ageta na mlezi wa chama Prof Sheila Wandera, ilizindua bidhaa zenye nembo ya CHAWAKAMA-Kenya, zikiwemo mashati-tao, chepeo, kalamu, bango na vitabu vilivyoandikwa na wanachama. Ubunifu wa wanachama ulijitokeza pia kupitia Kishazi TV, runinga ya mtandaoni iliyorusha matukio ya kongamano mubashara na kusambaza maudhui yake kupitia mitandao ya kijamii. Kongamano lilipambwa na michango ya wataalamu mashuhuri wa Kiswahili, akiwemo Dkt Moses Wasike (Mgeni Rasmi), Dkt Riro Matinde, Prof James Ontieri, Dkt Nixon Sangili na Dkt Sussy Nandama, miongoni mwa wengine. Mafanikio hayo yalitokana na ushirikiano wa CHAWAKAMA-Kenya, Idara ya Masomo ya Kibinadamu na Maendeleo, uongozi wa Chuo Kikuu cha Laikipia na Chama cha Kiswahili cha Laikipia (CHAKILA). Chama hicho kinaongozwa na Clinton Ageta (Mwenyekiti), Granton Mdogo (Naibu Mwenyekiti), Doreen Mukami (Katibu Mkuu), Griffin Amakala (Naibu Katibu Mkuu), Diana Mirriam (Mhazini), Velma Natang’a (Afisa wa Uhusiano Mwema), Micah Sikolia (Katibu Mtendaji) na Okimba Lester (Afisa Mwenezi). Wahariri ni Luke Shikoli, Kweyu Remjo, Augustine Wekesa, Winjoy Gacheri na Zdame Zuhura, huku Samson Nyamosi na Denis Chumo wakihudumu kama Maafisa wa Nidhamu. Kwa hakika, CHAWAKAMA-Kenya kinaendelea kuthibitisha kuwa mustakabali wa Kiswahili unategemea ubunifu, ushirikiano na juhudi za kizazi kipya.
Twenty-three American Peace Corps volunteers have been sworn in to begin a two-year assignment in Tanzania, where they will support secondary education and community health programmes.
MWANAMUME mwenye umri wa miaka 26 aliyetoweka mjini Mombasa mwezi uliopita aliwahi kushtakiwa kwa kosa la kusajili watu kujiunga na kundi la kigaidi, lakini baadaye akaachiliwa huru na mahakama, imebainika. Stakabadhi zilizowasilishwa katika Mahakama Kuu ya Mombasa zinaonyesha kuwa Ismail Yusuf Mohamed alikabiliwa na mashtaka yanayohusiana na ugaidi Januari 2022, miaka minne kabla ya kutoweka kwake. Mohamed alishtakiwa katika kesi ya uhalifu iliyokuwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Malindi. Hata hivyo, katika uamuzi uliotolewa Agosti 11, 2023, mahakama ilimuachilia huru baada ya kubaini kuwa upande wa mashtaka haukuthibitisha tuhuma zilizokuwa dhidi yake. Kesi hiyo ya awali imeibuka katika ombi lililowasilishwa na shirika la kutetea haki za binadamu la Vocal Africa, ambalo linaitaka polisi kueleza aliko Mohamed aliyetoweka kwake Oktoba 31 mwaka huu. Katika hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Bw Hussein Khalid, alisema Mohamed aliondoka nyumbani kwao eneo la Bondeni, Mombasa, kwenda kununua chakula cha jioni lakini hakurejea. Kwa mujibu wa hati hiyo, Mohamed alitekwa nyara mwendo wa saa tano usiku nje ya mgahawa wa Bondeni Carmel’s Joint, kando ya Barabara ya Abdel Nasser, na watu waliokuwa wakimfuatilia kwa gari aina ya pickup. Ombi hilo linadai kuwa, video za kamera za CCTV zinaonyesha wanaume hao wakishuka kwenye gari hilo, kumkamata Mohamed na kumwingiza kwa nguvu katika gari jeupe aina ya Toyota Land Cruiser kabla ya kuondoka naye. “Mahali alipo Mohamed na hali yake ya maisha hazijulikani, na pia hapatikani kwa simu yake ya mkononi,” alisema Bw Khalid katika hati ya kiapo. Shirika hilo linasema familia ya Mohamed iliripoti kutoweka kwake katika Kituo cha Polisi cha Mombasa Central, chini ya nambari ya OB 67/31/10/2026, lakini polisi hawajawafahamisha aliko wala hatua walizochukua katika uchunguzi. Aidha, juhudi za familia kumtafuta katika vituo mbalimbali vya polisi katika Kaunti ya Mombasa hazijazaa matunda. Vocal Africa iliomba mahakama kumwamuru Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kumfikisha Mohamed mahakamani, akiwa hai au mfu, mbali na kueleza aliko. Pia imeomba mahakama iwaite Bw Kanja, Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) Mohamed Amin na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Kitaifa (NIS) Noordin Haji kueleza kuhusu kutoweka kwake. “Utekaji na kutoweka kwa mtu bila kujulikana aliko ni mojawapo ya ukiukaji mkubwa zaidi wa haki ya mtu kuwa huru unaotambuliwa chini ya sheria za kimataifa,” anasema Bw Khalid. Shirika hilo linasisitiza kuwa kila mtu ana haki ya kusikilizwa kwa haki na kufanyiwa taratibu za kisheria, bila kujali kosa analotuhumiwa kutenda. Katika maagizo yaliyotolewa Novemba 17, Mahakama Kuu ilithibitisha kuwa ombi hilo lina dharura na kuwaamuru washtakiwa kuwasilisha majibu yao kufikia Novemba 18. Mahakama pia ilimwamuru Inspekta Mkuu wa polisi kuhakikisha Mohamed anafikishwa mbele ya Mahakama Kuu au Mahakamani Novemba 19 saa nne asubuhi. Inspekta Mkuu na DCI pia waliamriwa kuhifadhi na kuwasilisha rekodi za kamera za CCTV, mifumo ya kufuatilia magari, mawasiliano ya simu za mkononi, taarifa za mipakani, rekodi za vituo vya kulipia ushuru barabarani na taarifa za mfumo wa kutambua nambari za usajili wa magari, zinazohusiana na kutoweka kwa Mohamed kuanzia Oktoba 30, 2026.
MOROGORO: SERIKALI imewaelekeza watendaji wake kuhakikisha matumizi ya teknolojia ya Akili Unde (Artificial Intelligence – AI) yanapaswa kuzingatia uhakiki wa taarifa, usalama wa data, uadilifu na viwango vya kitaalamu. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu ,Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dk Jim Yonazi, wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya…
ARUSHA; Watetezi wa haki za wanawake na mitandao inayopinga ukatili wa kijinsia mkoani Arusha wameiomba Serikali kuunda kikosi maalumu ndani ya Jeshi la Polisi kitakachokuwa na jukumu la kufuatilia na kuchunguza matukio ya mauaji ya wanawake nchini. Watetezi hao wamesema lengo la kikosi hicho ni kuhakikisha wahusika wa mauaji hayo wanabainishwa haraka na kuchukuliwa hatua…
POLISI wamefanikiwa kumuokoa msichana wa miaka minne aliyetekwa nyara akicheza na watoto wengine katika uwanja wa wazi karibu na nyumbani kwao Malaa, Kaunti ya Machakos na kudaiwa kuuzwa kwa Sh150,000. Maafisa pia wamewakamata washukiwa wanne katika operesheni zilizofanyika Utawala, Nairobi na Meru kuhusiana na utekaji huo. Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), mwanamke aliyekuwa amejifunika kichwa kwa hijab alimshawishi mtoto huyo kuandamana naye kwa kisingizio cha kumpeleka dukani kununua sukari na chokoleti. Mama wa mtoto alipofika kumchukua, watoto wenzake walimweleza kuwa mwanamke huyo alikuwa amemchukua. Uchunguzi uliwawezesha wapelelezi kumkamata mshukiwa wa kwanza eneo la Tutua, kaunti ya Meru, kabla ya wengine watatu kunaswa Utawala karibu na duka la Quickmart. Kamanda wa Polisi wa Matungulu Peter Gichohi, alisema mtoto alipatikana akiwa katika hali nzuri na kupelekwa Kituo cha Afya cha Nguluni kufanyiwa uchunguzi kabla ya kuunganishwa na wazazi wake. Polisi wanachunguza madai kuwa mtoto huyo alikuwa ameuzwa kwa Sh150,000. Magari na pikipiki zinazoshukiwa kutumiwa katika uhalifu huo pia zilikamatwa.
TAKRIBAN familia 603 zimefurushwa makwao na mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini, huku watu sita wakipoteza maisha kutokana na mvua kubwa inayonyesha wakati huu wa msimu wa mvua wa Oktoba, Novemba na Desemba. Ripoti ya Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya inaonyesha kuwa jumla ya familia 1,141 zimeathiriwa na mafuriko, huku maji yakiharibu nyumba, mashamba, kukatiza barabara na kuhatarisha maisha ya wakazi wanaoishi karibu na mito na maeneo ya mabonde. Kaunti za Tana River na Taita-Taveta ndizo zilizoathirika zaidi. Tana River imerekodi idadi kubwa zaidi ya familia zilizoathirika, huku familia 796 zikikumbwa na mafuriko na 525 zikilazimika kuhama makazi yao. Katika Kaunti ya Taita-Taveta, familia kadhaa zimeachwa bila makazi baada ya mito kufurika katika mji wa Voi Jumatatu, na maji kuingia katika maeneo ya makazi. Hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi kadri msimu wa mvua unavyozidi kushika kasi. Idara ya Hali ya Hewa imetabiri kuwa mvua itaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini kati ya Novemba 17 na 23. Watu sita wamefariki katika matukio tofauti. Watoto wawili walisombwa na maji ya mafuriko ya ghafla katika Kaunti ya Kajiado, huku wengine wawili wakizama Turkana. Watu wengine wawili walifariki baada ya mashua kupinduka katika Kaunti ya Kitui, huku abiria wawili wakiendelea kutafutwa. Katika Kaunti ya Tana River, maeneo ya Tana Kaskazini yameathirika zaidi baada ya maji ya Laga Wardesa kufurika na kuingia katika vijiji vya Eldera, Kono Ramadha na Mata Wardesa. Zaidi ya familia 300 na mifugo zaidi ya 400 wameathirika. Meneja wa kukabiliana na dharura wa Shirika la Msalaba Mwekundu, Anthony Muturi, alisema shirika hilo limesajili takriban watu 15,500 katika kaunti hiyo ili wapatiwe msaada wa kifedha wa kuwawezesha kuhamia maeneo salama kabla hali haijawa mbaya zaidi. Mafuriko hayo pia yameathiri kilimo, huku takriban ekari 250 za mashamba zikifunikwa na maji. Ekari 100 ziko Manono na Lailoni, huku nyingine 150 zikiwa Bubu, Kipao na Tarasaa. Vyanzo sita vya maji vinavyotumia pampu za mikono vimeharibika na vyoo 15 vya familia vimezama. Vyoo vingine 50, pampu 11 na baadhi ya shule ziko katika hatari ya kuathirika iwapo maji yataendelea kuongezeka. Usafiri pia umeathirika, huku sehemu za Barabara Kuu ya Mombasa-Nairobi katika eneo la Maungu ikikosa kupitika. Hali hiyo iliwaacha madereva wa magari na malori wakikwama kwa saa kadhaa Jumatatu. Barabara ya Kono Ramadha-Mlanjo pia imekatika na kufanya iwe vigumu kufikia baadhi ya jamii zilizoathirika. Katika maeneo mengine, Barabara ya Kitui-Mwingi-Garissa imefurika katika Daraja la Mbakini, huku Barabara ya Doldol-Nanyuki katika Kaunti ya Laikipia ikikatika katika eneo la Daraja ya Mungu baada ya Mto Salama Ngororo kufurika. Katika Kaunti ya Turkana, familia 39 zimeathirika na 38 zimefurushwa makwao, huku mifugo 382 wakipotea. Mratibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu katika Tana River, Abubakar Rhoba, alisema shirika hilo, kwa usaidizi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), linapanga kutoa fedha kwa familia zilizo katika hatari ili ziweze kuhama maeneo yanayokumbwa na mafuriko. Shirika hilo pia linatoa makazi ya dharura na vifaa mbalimbali vya matumizi ya nyumbani kwa familia zilizoathirika. Ingawa mashirika ya kibinadamu hayajaripoti uhaba wa chakula au visa vya utapiamlo kufikia sasa, yameonya kuwa mafuriko yakidumu kwa muda mrefu yanaweza kuzidisha ukosefu wa chakula na kuongeza mahitaji ya msaada wa dharura. Idara ya Hali ya Hewa pia imeonya kuwa mvua itaendelea kati ya Novemba 17 na 23, jambo linaloongeza hofu ya mafuriko zaidi, hasa katika maeneo ya karibu na mito na mabonde.
KIONGOZI wa Linda Mwananchi Movement (LMM) Edwin Sifuna na washirika wake katika upinzani walisusia hotuba ya Hali ya Taifa ya Rais William Ruto bungeni, wakipinga visa vya utekaji nyara na vitisho dhidi ya wakosoaji wa serikali. Badala yake, walizindua rasmi mrengo wa wanawake wa chama hicho, ‘Dada za Sifuna’, katika makao makuu ya chama jijini Nairobi, hafla iliyohudhuriwa na viongozi kadhaa. Sifuna, ambaye pia ni Seneta wa Nairobi, alisema aliamua kususia kikao hicho kwa sababu kanuni za Bunge zinamtaka Rais asikilizwe kwa utulivu, hata anapotoa madai ambayo upinzani haukubaliani nayo. “Rais anaenda bungeni kudanganya tena. Kanuni za Bunge zinamtaka Rais asikilizwe kwa utulivu. Baadhi yetu hatuwezi kukaa kimya bila kumwambia kuwa anadanganya,” alisema. Alisema hotuba hiyo inapaswa kueleza hali halisi ya wananchi, uchumi na usalama nchini, badala ya Rais kujikita katika kutaja miradi ya maendeleo. Sifuna alirejelea Kifungu cha 132 cha Katiba kinachomtaka Rais kutoa hotuba kwa taifa kila mwaka kuhusu hatua zilizochukuliwa na maendeleo yaliyopatikana katika kutekeleza maadili ya kitaifa inavyofafanuliwa katika Kifungu cha 10. Alisema maadili hayo yanahusu haki za binadamu, demokrasia, utawala wa sheria, uhuru, ushirikishaji na haki, akidai visa vya utekaji nyara bado vinaripotiwa chini ya utawala wa Rais Ruto. LMM pia ilieleza wasiwasi kuhusu mashambulizi dhidi ya watu wanaotetea demokrasia, ikiwemo shambulizi la hivi karibuni dhidi ya Amos Boaz Masika, mfanyakazi katika Trans Nzoia. Chama hicho kilidai viongozi, wafanyakazi na wafuasi wake wamekuwa wakilengwa kwa mashambulizi, vitisho na kukamatwa kiholela, hasa katika kaunti za Trans Nzoia, Bungoma na Kakamega. Kililaumu serikali kwa kuzorotesha uchumi na kuongeza gharama ya maisha, kikisema vitisho na silaha haviwezi kupunguza bei ya bidhaa wala deni la taifa.
BUNGE jana liligeuka jukwaa la kwaya ya kaulimbiu za kisiasa wakati Rais William Ruto akitoa hotuba yake ya nne ya Hali ya Taifa, takriban miezi tisa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027. Usalama ulikuwa umeimarishwa katika majengo ya Bunge, huku barabara zilizo karibu zikifungwa na maafisa wa usalama kutoka vitengo mbalimbali. Mbwa maalumu wa kunusa vilipuzi pia walitumwa kukagua eneo hilo, huku watu waliokuwa na vitambulisho maalumu pekee wakiruhusiwa kuingia ndani ya Bunge. Rais aliwasili saa nane na dakika kumi mchana kupitia Barabara ya Uhuru na kuwasalimu maafisa waliokuwa wameandaa gwaride la heshima kabla ya kuingia katika majengo ya Bunge. Alipokelewa na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula na mwenzake wa Seneti Amason Kingi. Baadaye aliingia katika ukumbi wa Bunge saa nane na dakika thelathini na nane mchana, akiongozwa na maafisa waliobeba fimbo za mamlaka za mabunge hayo.
MISIMAMO mikali miongoni mwa wandani wa Kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka na Edwin Sifuna wa Linda Mwananchi inatishia kutatiza juhudi za upinzani kuwa na mwaniaji mmoja wa urais katika uchaguzi mkuu ujao. Licha ya viongozi hao wawili kuahidi kuunga mkono juhudi za ushirikiano kumkabili Rais William Ruto, wandani wao wanazidi kusukuma mbele azma zao za urais, kila upande ukisisitiza kuwa kiongozi wao ndiye mwenye nafasi nzuri ya kushinda. Washirika wa Bw Sifuna wanadai umaarufu wake unaoongezeka, hasa Magharibi mwa Kenya na miongoni mwa vijana, unamfanya kuwa mgombea anayefaa kupewa tiketi ya upinzani. Hata hivyo, wandani wa Bw Musyoka nao wanasisitiza kuwa uzoefu wake wa kisiasa na tajriba yake ya uongozi, inampa nafasi bora ya kuongoza upinzani. Mzozo huo pia umefichua mgawanyiko Magharibi mwa Kenya kuhusu ni nani anayefaa kuwakilisha eneo hilo katika mazungumzo ya kuunda muungano, huku washirika wa Bw Sifuna wakitilia shaka nafasi ya kiongozi wa DAP-Kenya Eugene Wamalwa. Katika kongamano la kitaifa la wajumbe wa Linda Mwananchi lililofanyika wiki iliyopita, wajumbe walimpa Bw Sifuna mamlaka ya kuongoza mazungumzo na vyama vinavyoshikilia msimamo kama wao kabla ya uchaguzi. Hata hivyo, washirika wake wanasisitiza kuwa mazungumzo hayo yanapaswa kuzingatia azma yake ya kuwania urais. Seneta wa Kakamega, Boni Khalwale aliambia Taifa Leo kuwa viongozi wa upinzani wanapaswa kuzingatia umaarufu wa Bw Sifuna wanapochagua mgombea wao, akisema atazungumza kwa niaba ya Linda Mwananchi wala si jamii ya Waluhya. “Hatutaingia kwenye mazungumzo tukiwa na masharti, lakini umaarufu mkubwa wa Sifuna unaonekana,” akasema Dkt Khalwale, akiongeza kuwa upinzani unahitaji mgombea maarufu anayeweza kuvutia wapigakura kote nchini. Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya alimshutumu Bw Wamalwa kwa kuhujumu azma ya Bw Sifuna ya kuwania urais, akisisitiza seneta huyo wa Nairobi ndiye anayepaswa kuwakilisha Magharibi kwenye mazungumzo. Mbunge wa Kabuchai Majimbo Kalasinga pia alipuuzilia mbali mapendekezo kuwa Bw Sifuna awe mgombea mwenza wa Bw Musyoka, akisema ana umaarufu kuliko vinara wa upinzani. “Sifuna atawania urais na hatuachia mtu mwengine nafasi hiyo, tuko naye mpaka debeni,” akasema Bw Kalasinga. Kwa upande mwingine, washirika wa Bw Musyoka wanapigania azma yake ya urais, wakionya dhidi ya mpango wowote utakaomlazimisha kumuunga mkono mgombea mwengine. Seneta wa Kitui, Enoch Wambua alisema kiongozi huyo wa Wiper hafai kukubali nafasi ya naibu rais, akisema alishawaunga mkono wagombea wengine katika chaguzi zilizopita. “Nilimwona akimsaidia Raila mara mbili na hata hakuwania urais katika uchaguzi uliopita. Binafsi, ningemshauri asikubali kuwa naibu wa Sifuna,” akasema Bw Wambua. Seneta wa Makueni Daniel Maanzo alisema upande wao utaunga mkono tiketi itakayompa Bw Musyoka nafasi ya kuwania urais, ingawa alipendekeza ushirikiano na Bw Sifuna. “Tiketi pekee tutakayokubali, na ambayo tunaamini inaweza kuunganisha upinzani na kushinda, ni ya Kalonzo-Sifuna,” akasema Bw Maanzo. Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko pia amemtaka Bw Musyoka aungwe mkono na upinzani, akimshauri afanye kazi na serikali iwapo hataungwa mkono. “Hii ndiyo risasi yake ya mwisho na nafasi yake ya mwisho. Ikiwa upinzani hautampa fursa ya kuwa mgombea wake wa urais, hafai kujaribu tena. Afadhali awe naibu rais wa Ruto au Waziri Mkuu,” akasema Bw Sonko. Bw Musyoka, hata hivyo, amesisitiza kuwa yuko tayari kujitolea kwa ajili ya umoja wa upinzani, akionya dhidi ya kuchochea mgawanyiko. “Ikiwa mimi ndiye sababu ya kuigawa nchi, basi afadhali nirudi nyumbani,” akasema.