MWANAMUME mwenye umri wa miaka 26 aliyetoweka mjini Mombasa mwezi uliopita aliwahi kushtakiwa kwa kosa la kusajili watu kujiunga na kundi la kigaidi, lakini baadaye akaachiliwa huru na mahakama, imebainika.
Stakabadhi zilizowasilishwa katika Mahakama Kuu ya Mombasa zinaonyesha kuwa Ismail Yusuf Mohamed alikabiliwa na mashtaka yanayohusiana na ugaidi Januari 2022, miaka minne kabla ya kutoweka kwake.
Mohamed alishtakiwa katika kesi ya uhalifu iliyokuwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Malindi.
Hata hivyo, katika uamuzi uliotolewa Agosti 11, 2023, mahakama ilimuachilia huru baada ya kubaini kuwa upande wa mashtaka haukuthibitisha tuhuma zilizokuwa dhidi yake.
Kesi hiyo ya awali imeibuka katika ombi lililowasilishwa na shirika la kutetea haki za binadamu la Vocal Africa, ambalo linaitaka polisi kueleza aliko Mohamed aliyetoweka kwake Oktoba 31 mwaka huu.
Katika hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Bw Hussein Khalid, alisema Mohamed aliondoka nyumbani kwao eneo la Bondeni, Mombasa, kwenda kununua chakula cha jioni lakini hakurejea.
Kwa mujibu wa hati hiyo, Mohamed alitekwa nyara mwendo wa saa tano usiku nje ya mgahawa wa Bondeni Carmel’s Joint, kando ya Barabara ya Abdel Nasser, na watu waliokuwa wakimfuatilia kwa gari aina ya pickup.
Ombi hilo linadai kuwa, video za kamera za CCTV zinaonyesha wanaume hao wakishuka kwenye gari hilo, kumkamata Mohamed na kumwingiza kwa nguvu katika gari jeupe aina ya Toyota Land Cruiser kabla ya kuondoka naye.
“Mahali alipo Mohamed na hali yake ya maisha hazijulikani, na pia hapatikani kwa simu yake ya mkononi,” alisema Bw Khalid katika hati ya kiapo.
Shirika hilo linasema familia ya Mohamed iliripoti kutoweka kwake katika Kituo cha Polisi cha Mombasa Central, chini ya nambari ya OB 67/31/10/2026, lakini polisi hawajawafahamisha aliko wala hatua walizochukua katika uchunguzi.
Aidha, juhudi za familia kumtafuta katika vituo mbalimbali vya polisi katika Kaunti ya Mombasa hazijazaa matunda.
Vocal Africa iliomba mahakama kumwamuru Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kumfikisha Mohamed mahakamani, akiwa hai au mfu, mbali na kueleza aliko.
Pia imeomba mahakama iwaite Bw Kanja, Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) Mohamed Amin na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Kitaifa (NIS) Noordin Haji kueleza kuhusu kutoweka kwake.
“Utekaji na kutoweka kwa mtu bila kujulikana aliko ni mojawapo ya ukiukaji mkubwa zaidi wa haki ya mtu kuwa huru unaotambuliwa chini ya sheria za kimataifa,” anasema Bw Khalid.
Shirika hilo linasisitiza kuwa kila mtu ana haki ya kusikilizwa kwa haki na kufanyiwa taratibu za kisheria, bila kujali kosa analotuhumiwa kutenda.
Katika maagizo yaliyotolewa Novemba 17, Mahakama Kuu ilithibitisha kuwa ombi hilo lina dharura na kuwaamuru washtakiwa kuwasilisha majibu yao kufikia Novemba 18.
Mahakama pia ilimwamuru Inspekta Mkuu wa polisi kuhakikisha Mohamed anafikishwa mbele ya Mahakama Kuu au Mahakamani Novemba 19 saa nne asubuhi.
Inspekta Mkuu na DCI pia waliamriwa kuhifadhi na kuwasilisha rekodi za kamera za CCTV, mifumo ya kufuatilia magari, mawasiliano ya simu za mkononi, taarifa za mipakani, rekodi za vituo vya kulipia ushuru barabarani na taarifa za mfumo wa kutambua nambari za usajili wa magari, zinazohusiana na kutoweka kwa Mohamed kuanzia Oktoba 30, 2026.
Korti yaambiwa aliyetoweka alionyesha dalili za ugaidi

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…