MOROGORO: SERIKALI imewaelekeza watendaji wake kuhakikisha matumizi ya teknolojia ya Akili Unde (Artificial Intelligence – AI) yanapaswa kuzingatia uhakiki wa taarifa, usalama wa data, uadilifu na viwango vya kitaalamu.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu ,Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dk Jim Yonazi, wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya kimkakati ya uongozi katika Ufuatiliaji na Tathmini kwa ajili ya utawala unaotegemea Ushahidi , mjini Morogoro.
Mafunzo hayo yanawashirikisha Wakurugenzi wa Mipango na wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara pamoja na wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Sekretarieti za Mikoa huku yakilenga kuongeza uwezo wa viongozi na wataalamu katika Ufuatiliaji, Tathmini, Utafiti na Ujifunzaji (MERL).
Dk Yonazi amesema kuwa teknolojia ya Akili Unde inapaswa kuwa nyenzo ya kuongeza uwezo wa kitaalamu , kurahisisha utendaji kazi, kuongeza ufanisi na kuboresha ubora wa huduma na si mbadala wa utaalamu wa watumishi kuwaondolea majukumu yao.
Amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha mfumo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini kwa kuweka miundo ya kitaasisi, kuandaa miongozo na kujenga uwezo wa watumishi wake .
Dk Yonazi amesema mafanikio ya mfumo huo hayatapimwa kwa wingi wa taarifa zinazokusanywa, bali kwa namna ushahidi unaozalishwa unavyotumika kuboresha maamuzi na utekelezaji wa majukumu ya Serikali.
“ Wataalamu hawapaswi kuishia kuandaa taarifa za utekelezaji kwa ajili ya kuripoti, bali wanapaswa kuwasaidia viongozi kubaini changamoto, kuelewa sababu za matokeo yaliyopatikana na kupendekeza hatua zinazofaa za kuboresha utendaji” amesema Dk Yonazi
Katibu Mkuu amesema kuwa taarifa zinazozalishwa zinapaswa kuwa sahihi, za kuaminika na kupatikana kwa wakati ili ziweze kusaidia viongozi kufanya maamuzi sahihi ya kisera na kiutendaji.
Dk Yonazi amewataka watendaji kutumia TEHAMA na mifumo ya kisasa kuimarisha usimamizi, uchambuzi na uwasilishaji wa taarifa, na kuboresha mwingiliano wa mifumo ya Serikali ili kupunguza mlolongo wa ukusanyaji wa taarifa.
Amesema mifumo ya Mipango na Ufuatiliaji na Tathmini katika taasisi za Serikali inapaswa kuendana na vipaumbele vya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ili kuwezesha kupima mchango wa kila taasisi katika kufikia malengo ya kitaifa, kubaini changamoto na kuweka hatua za ziada pale inapohitajika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa ufuatiliaji na tathimini ya utendaji wa serikali , kutoka katika ofisi hiyo ya Waziri mkuu , Sakina Mwinyimkuu amesema mafunzo hayo awamu inayofuata yatatolewa kwa makatibu wakuu, manaibu makatibu wakuu, makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa halmashauri nchini na waratibu wa mipango wa mikoa.
“Mafunzo haya yalikuwa yakifanyika kwa watumishi wa ngazi za chini kuanzia mwaka 2022 na sasa tumeamua kushirikisha viongozi wa ngazi za juu ili utekelezaji wake uwe rahisi ” amesema Mwinyimkuu.
‘AI isiwe mbadala ujuzi wa watumishi’

This story was originally published by Habari Leo.
Read the full story at Habari LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…