MISIMAMO mikali miongoni mwa wandani wa Kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka na Edwin Sifuna wa Linda Mwananchi inatishia kutatiza juhudi za upinzani kuwa na mwaniaji mmoja wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Licha ya viongozi hao wawili kuahidi kuunga mkono juhudi za ushirikiano kumkabili Rais William Ruto, wandani wao wanazidi kusukuma mbele azma zao za urais, kila upande ukisisitiza kuwa kiongozi wao ndiye mwenye nafasi nzuri ya kushinda.
Washirika wa Bw Sifuna wanadai umaarufu wake unaoongezeka, hasa Magharibi mwa Kenya na miongoni mwa vijana, unamfanya kuwa mgombea anayefaa kupewa tiketi ya upinzani.
Hata hivyo, wandani wa Bw Musyoka nao wanasisitiza kuwa uzoefu wake wa kisiasa na tajriba yake ya uongozi, inampa nafasi bora ya kuongoza upinzani.
Mzozo huo pia umefichua mgawanyiko Magharibi mwa Kenya kuhusu ni nani anayefaa kuwakilisha eneo hilo katika mazungumzo ya kuunda muungano, huku washirika wa Bw Sifuna wakitilia shaka nafasi ya kiongozi wa DAP-Kenya Eugene Wamalwa.
Katika kongamano la kitaifa la wajumbe wa Linda Mwananchi lililofanyika wiki iliyopita, wajumbe walimpa Bw Sifuna mamlaka ya kuongoza mazungumzo na vyama vinavyoshikilia msimamo kama wao kabla ya uchaguzi.
Hata hivyo, washirika wake wanasisitiza kuwa mazungumzo hayo yanapaswa kuzingatia azma yake ya kuwania urais.
Seneta wa Kakamega, Boni Khalwale aliambia Taifa Leo kuwa viongozi wa upinzani wanapaswa kuzingatia umaarufu wa Bw Sifuna wanapochagua mgombea wao, akisema atazungumza kwa niaba ya Linda Mwananchi wala si jamii ya Waluhya.
“Hatutaingia kwenye mazungumzo tukiwa na masharti, lakini umaarufu mkubwa wa Sifuna unaonekana,” akasema Dkt Khalwale, akiongeza kuwa upinzani unahitaji mgombea maarufu anayeweza kuvutia wapigakura kote nchini.
Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya alimshutumu Bw Wamalwa kwa kuhujumu azma ya Bw Sifuna ya kuwania urais, akisisitiza seneta huyo wa Nairobi ndiye anayepaswa kuwakilisha Magharibi kwenye mazungumzo.
Mbunge wa Kabuchai Majimbo Kalasinga pia alipuuzilia mbali mapendekezo kuwa Bw Sifuna awe mgombea mwenza wa Bw Musyoka, akisema ana umaarufu kuliko vinara wa upinzani.
“Sifuna atawania urais na hatuachia mtu mwengine nafasi hiyo, tuko naye mpaka debeni,” akasema Bw Kalasinga.
Kwa upande mwingine, washirika wa Bw Musyoka wanapigania azma yake ya urais, wakionya dhidi ya mpango wowote utakaomlazimisha kumuunga mkono mgombea mwengine.
Seneta wa Kitui, Enoch Wambua alisema kiongozi huyo wa Wiper hafai kukubali nafasi ya naibu rais, akisema alishawaunga mkono wagombea wengine katika chaguzi zilizopita.
“Nilimwona akimsaidia Raila mara mbili na hata hakuwania urais katika uchaguzi uliopita. Binafsi, ningemshauri asikubali kuwa naibu wa Sifuna,” akasema Bw Wambua.
Seneta wa Makueni Daniel Maanzo alisema upande wao utaunga mkono tiketi itakayompa Bw Musyoka nafasi ya kuwania urais, ingawa alipendekeza ushirikiano na Bw Sifuna.
“Tiketi pekee tutakayokubali, na ambayo tunaamini inaweza kuunganisha upinzani na kushinda, ni ya Kalonzo-Sifuna,” akasema Bw Maanzo.
Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko pia amemtaka Bw Musyoka aungwe mkono na upinzani, akimshauri afanye kazi na serikali iwapo hataungwa mkono.
“Hii ndiyo risasi yake ya mwisho na nafasi yake ya mwisho. Ikiwa upinzani hautampa fursa ya kuwa mgombea wake wa urais, hafai kujaribu tena. Afadhali awe naibu rais wa Ruto au Waziri Mkuu,” akasema Bw Sonko.
Bw Musyoka, hata hivyo, amesisitiza kuwa yuko tayari kujitolea kwa ajili ya umoja wa upinzani, akionya dhidi ya kuchochea mgawanyiko.
“Ikiwa mimi ndiye sababu ya kuigawa nchi, basi afadhali nirudi nyumbani,” akasema.
Misimamo mikali ya wandani wa Sifuna na Kalonzo yatishia kuvuruga upinzani

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…