TAKRIBAN familia 603 zimefurushwa makwao na mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini, huku watu sita wakipoteza maisha kutokana na mvua kubwa inayonyesha wakati huu wa msimu wa mvua wa Oktoba, Novemba na Desemba.
Ripoti ya Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya inaonyesha kuwa jumla ya familia 1,141 zimeathiriwa na mafuriko, huku maji yakiharibu nyumba, mashamba, kukatiza barabara na kuhatarisha maisha ya wakazi wanaoishi karibu na mito na maeneo ya mabonde.
Kaunti za Tana River na Taita-Taveta ndizo zilizoathirika zaidi. Tana River imerekodi idadi kubwa zaidi ya familia zilizoathirika, huku familia 796 zikikumbwa na mafuriko na 525 zikilazimika kuhama makazi yao.
Katika Kaunti ya Taita-Taveta, familia kadhaa zimeachwa bila makazi baada ya mito kufurika katika mji wa Voi Jumatatu, na maji kuingia katika maeneo ya makazi.
Hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi kadri msimu wa mvua unavyozidi kushika kasi.
Idara ya Hali ya Hewa imetabiri kuwa mvua itaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini kati ya Novemba 17 na 23.
Watu sita wamefariki katika matukio tofauti. Watoto wawili walisombwa na maji ya mafuriko ya ghafla katika Kaunti ya Kajiado, huku wengine wawili wakizama Turkana.
Watu wengine wawili walifariki baada ya mashua kupinduka katika Kaunti ya Kitui, huku abiria wawili wakiendelea kutafutwa.
Katika Kaunti ya Tana River, maeneo ya Tana Kaskazini yameathirika zaidi baada ya maji ya Laga Wardesa kufurika na kuingia katika vijiji vya Eldera, Kono Ramadha na Mata Wardesa.
Zaidi ya familia 300 na mifugo zaidi ya 400 wameathirika.
Meneja wa kukabiliana na dharura wa Shirika la Msalaba Mwekundu, Anthony Muturi, alisema shirika hilo limesajili takriban watu 15,500 katika kaunti hiyo ili wapatiwe msaada wa kifedha wa kuwawezesha kuhamia maeneo salama kabla hali haijawa mbaya zaidi.
Mafuriko hayo pia yameathiri kilimo, huku takriban ekari 250 za mashamba zikifunikwa na maji. Ekari 100 ziko Manono na Lailoni, huku nyingine 150 zikiwa Bubu, Kipao na Tarasaa.
Vyanzo sita vya maji vinavyotumia pampu za mikono vimeharibika na vyoo 15 vya familia vimezama. Vyoo vingine 50, pampu 11 na baadhi ya shule ziko katika hatari ya kuathirika iwapo maji yataendelea kuongezeka.
Usafiri pia umeathirika, huku sehemu za Barabara Kuu ya Mombasa-Nairobi katika eneo la Maungu ikikosa kupitika.
Hali hiyo iliwaacha madereva wa magari na malori wakikwama kwa saa kadhaa Jumatatu. Barabara ya Kono Ramadha-Mlanjo pia imekatika na kufanya iwe vigumu kufikia baadhi ya jamii zilizoathirika.
Katika maeneo mengine, Barabara ya Kitui-Mwingi-Garissa imefurika katika Daraja la Mbakini, huku Barabara ya Doldol-Nanyuki katika Kaunti ya Laikipia ikikatika katika eneo la Daraja ya Mungu baada ya Mto Salama Ngororo kufurika.
Katika Kaunti ya Turkana, familia 39 zimeathirika na 38 zimefurushwa makwao, huku mifugo 382 wakipotea.
Mratibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu katika Tana River, Abubakar Rhoba, alisema shirika hilo, kwa usaidizi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), linapanga kutoa fedha kwa familia zilizo katika hatari ili ziweze kuhama maeneo yanayokumbwa na mafuriko.
Shirika hilo pia linatoa makazi ya dharura na vifaa mbalimbali vya matumizi ya nyumbani kwa familia zilizoathirika.
Ingawa mashirika ya kibinadamu hayajaripoti uhaba wa chakula au visa vya utapiamlo kufikia sasa, yameonya kuwa mafuriko yakidumu kwa muda mrefu yanaweza kuzidisha ukosefu wa chakula na kuongeza mahitaji ya msaada wa dharura.
Idara ya Hali ya Hewa pia imeonya kuwa mvua itaendelea kati ya Novemba 17 na 23, jambo linaloongeza hofu ya mafuriko zaidi, hasa katika maeneo ya karibu na mito na mabonde.
Mafuriko yaangamiza 6, zaidi ya 600 wafurushwa makwao mvua ikiendelea kunyesha

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…