i. Kufanya kazi za kiuguzi za kuhudumia wateja katika jamii, hospitali na sehemu zote zinapotolewa huduma za afya;
ii. Kusimamia na kuratibu kazi zote za wahudumu wa afya katika
sehemu yake ya kazi;
iii. Kukusanya takwimu na kutayarisha taarifa za utendaji wake wa kazi;
iv. Kutoa huduma kwa wagonjwa majumbani;
v. Kutoa ushauri nasaha;
vi. Kutoa huduma za kinga na uzazi wa mpango;
vii. Kutoa huduma za uzazi na afya ya mtoto;
viii. Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya;
ix. Kufuatilia utunzaji wa vitendea kazi katika maeneo yake ya kazi; na
x. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi
zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
Kuajiriwa wenye cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kuandikishwa (Enrolled) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.
TGHS A