i.Kuandaa Mpango wa mahitaji ya kiufundi na bajeti ya mradi husika;
ii.Kukagua eneo la mradi na kuandaa taarifa;
iii.Kushauri kuhusu uteuzi wa makandarasi na wataalamu wengine wa mradi;
iv.Kufanya upekuzi yakinifu wa mradi;
v.Kufanya tathmini ya athari za kimazingira ya mradi husika;
vi.Kuandaa michoro ya awali (outline proposals) na michoro yenye mahitaji kamili ya mradi (scheme designs);
vii.Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa eneo la miradi (Regular site visits);
viii.Kushauri kuhusiana na miliki ya majengo ya kale;
ix.Kukagua majengo ambayo yamekamilika kujengwa kwa madhumuni ya kutoa ushauri ili jingo liweze kupatiwa hati ya kutumika (Certificate of Occupancy); na
x.Kufanya kazi nyingine zinazoendana na fani yake kwa kadri atakavyopangiwa na mkkuu wake wa kazi
Kuajiriwa wenye Shahada / Stashahada ya Juu kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani zifuatazo: - Architecture, Building Design, Architectural and Building Engineering Technology, Landscape Architecture and Planning, Architectural Technology, Naval Architecture, Architectural Engineering, Construction Management, Conservation Architecture, na Interior Design awe amesajiliwa na Bodi ya Usajili ya Wasanifu Majengo (AQRB).
TGS.E.