i.Kukunja karatasi ngumu na kutengeneza ‘covers’ za vitabu, majarida, madaftari katika mahitaji mbalimbali kwa kugandisha, kuweka pamoja au kushona katika hali mbalimbali za ubora;
ii.Kukarabati vitabu, kumbukumbu mbalimbali au majarida kwa kuyawekea gamba jipya au kurudisha katika hali yake ya mwanzo kutegemea na kifaa hicho kilivyoharibika;
iii.Kupanga vifaa vilivyotengenezwa katika makasha kwa vipimo vyake au katika seti;
iv.Kuendesha mashine ya kukata karatasi/kupiga chapa/mashine za composing, kushona au kugandisha vitabu, majarida, madaftari na vifaa vingine vinavyokuwa vimetakiwa kwa mtindo na ubora wake; na
v.Kupanga karatasi zitakazochapwa kwa hesabu ya kila kitabu, jarida, daftari na vinginevyo kwa kushonwa au kugandishwa pamoja.
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne au sita katika masomo ya sayansi au Sanaa wenye cheti cha majaribio ya ufundi daraja la I (Trade Test Grade I or Level III) katika lithography/composing/binding/machine binding au waliohitimu mafunzo ya miaka miwili ya kupiga chapa.
TGS B.