From: 2023-09-04 to: 2023-09-11
( )
MLEZI WA WATOTO MSAIDIZI (CHILD CARE ASSISTANT) - 1 POST
MDAs & LGAs
Duties & Responsibilities

i. Kushiriki kutekeleza mpango jumui wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya watoto, (ECD integrated plan);

ii.Kuandaa na kutekeleza ratiba ya shughuli za kila siku katika kituo husika;

iii.Kubainisha na kutumia mazingira salama ya kujifunzia watoto;

iv.Kutoa rufaa ya masuala ya watoto yaliyo nje ya uwezo wake;

v.Kutambua watoto wenye mahitaji maalumu na kutoa huduma stahiki;

vi.Kushiriki katika uhamasishaji wa jamii katika kutoa huduma za malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto;

vii.Kutoa ushauri kwa wazazi/walezi kuhusu malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto katika eneo lake;

viii.Kuandaa na kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kila siku katika eneo husika;

ix.Kushiriki kwenye mchakato wa uendeshaji wa mashauri ya watoto katika ngazi husika (case management);

x.Kuandaa taarifa ya uanzishaji wa vituo vya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto katika maeneo husika; na

xi.Kufanya kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi kulingana na elimu na ujuzi wake.

Qualifications

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au kidato cha sita waliohitimu mafunzo ya Astashahada katika mojawapo ya fani zifuatazo:-  Elimu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, Ustawi wa Jamii, Saikolojia  kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.

Remuneration

TGS. B