MKAGUZI WA NDANI DARAJA II (INTERNAL AUDITOR II) - 52 POST
MDAs & LGAs
Duties & Responsibilities
i.kuandaa program ya ukaguzi wa ndani;
ii.kufanya uchambuzi katika hatua za awali za ukaguzi;
iii.kufanya tathimini za udhibiti wa mifumo ya ndani katika hatua za awali (internal controls), uthibiti wa vihatarishi (risk management) na usimamizi wa mifumo ya uendeshaji (corporate governance);
iv.kuandaa mpango wa ukaguzi wa ndani wa kawaida au maalum;
v.kufanya ukaguzi wa kawaida, maalum, kiufundi na uchunguzi (Normal, Special Audit, Technical audit and Investigations);
vi.kufanya uhakiki wa hoja za ukaguzi zilizopokelewa;
vii.Kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya ukaguzi wa ndani;
viii.Kutoa ushauri wa kuimarisha utendaji wa taasisi; na
ix.Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
Qualifications
Kuajiriwa mwenye shahada ya biashara au Sanaa yenye muelekeo wa Uhasibu/Stashahada ya Juu ya Uhasibu/Ukaguzi hesabu wenye cheti cha taaluma ya uhasibu CPA(T) au sifa nyingine zinazotambulika na NBAA.