i.Kufanya doria ndani na nje ya eneo la hifadhi.
ii.Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi.
iii.Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha.
iv.Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori.
v.Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali.
vi.Kufanya usafi na ulinzi wa kambi.
vii.Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi.
viii.Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani.
ix.Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kukusanya takwimu zao.
x.Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na Nyara ndani na nje ya nchi.
xi.Kudhibiti wanyamapori waharibifu.
xii.Kudhibiti moto kwenye hifadhi na
xiii.Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa zinazoendana na taalima yake.
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au cha VI wenye Astashahada ya awali ya Uhifadhi wa Wanyamapori (Basic Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali au; Wahitimu wa Kidato cha Nne au kidato cha Sita wenye Astashahada ya Uhifadhi Wanyamapori (Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
TGS B