From: 2023-07-11 to: 2023-07-18
( )
MHANDISI UMEME - MITAMBO (ELECTRO-MECHANICAL) - 4 POST
MDAs & LGAs
Duties & Responsibilities

i.Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu Umema na mitambo mbalimbali, bei za mitambo na vifaa vya umeme ndani na nje ya nchi;

ii.Kuhakikisha uthamani sahihi wa kazi ili kufikia thamani ya fedha;

iii.Kupanga, Kubuni na Kutengeneza Mitambo chini ya Mhandisi aliyesajiliwa (Professional Engineer)

iv.Kufanya Usanifu na kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Ufundi na Umeme (Electrical and Mechanical Projects);

v.Kufanya Ukaguzi na matengenezo ya kawaida na matengenezo kinga ya vifaa vya kazi, Ufundi na mitambo;

vi.Kusanifu, kuandaa gharama na kufanya matengenezo ya miradi ya Umeme na Ufundi (Electrical and Mechanical Projects);

vii.Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu vifaa vya umeme na mitambo mbalimbali ndani na nje ya nchi;

viii.Kuandaa na kutunza kanzidata ya mitambo pamoja na matengenezo yake; na

ix.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

Qualifications

Awe na Elimu ya Kidato cha nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliyefuzu mafunzo ya Shahada ya kwanza ya Uhandisi katika fani ya Umeme na Mitambo (Electro-Mechanical) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kutumia kompyuta na waliosajiliwa na Bodi ya Wahandisi kama Graduate Engineer (GE).

Remuneration

TGS E1