From: 2023-04-19 to: 2023-04-25
( )
MHANDISI MITAMBO DARAJA LA II (MECHANICAL ENGINEER II) - 20 POST
MDAs & LGAs
Duties & Responsibilities

i.Kufanya kazi chini ya uangalizi wa mhandisi aliyesajiliwa na bodi ya usajili wa wahandisi kama “Professional Engineer” ili kupata uzoefu unaotakiwa;

ii.Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu magari na mitambo mbalimbali, bei za magari na mitambo na vifaa vya umeme ndani na nje ya nchi;

iii.Kuhakikisha uthamani sahihi wa kazi ili kufikia thamani ya fedha;

iv.Kupanga, Kubuni na Kutengeneza Mitambo chini Mhandisi aliyesajiliwa (Professional Engineer);

v.Kufanya usanifu na kusimamia utekelezaji wa miradi ya Ufundi na Umeme (Electrical and Mechanical Projects);

vi.Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu katika kusimamia usanifu wa kazi na matengenezo ya mifumo ya magari/umeme na mitambo;

vii.Awe mchapakazi mwenye uwezo wa kupanga, kubaini na kusimamia uzalishaji;

viii.Kutunza vipuli na taarifa za matengenezo ya magari na mitambo;

ix.Kufanya ukaguzi na matengenezo ya kawaida na matengenezo kinga ya vifaa vya kazi, magari na mitambo;

x.Kusanifu, kuandaa gharama na kufanya matengenezo ya miradi ya umeme na ufundi (Electrical and Mechanica Projects);

xi.Kuandaa na kutunza kanzidata ya magari na mitambo pamoja na matengenezo yake; na

xii.Kufanya kazi atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

 

Qualifications

Awe na Shahada/Stashahada ya juu ya Uhandisi kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya Uhandisi Mitambo (Mechanical) na kusajiliwa na bodi ya uhandisi kama “Graduate Engineer”.

 

Remuneration

TGS.E