i.Atafanya kazi chini ya uangalizi wa Mhandisi aliyesajiliwa na Bodi ya Usajili ya Wahandisi (Professional Engineer) ili kupata uzoefu unaotakaiwa;
ii.Kufanya ukaguzi wa barabara na madaraja mbalimbali;
iii.Kuchunguza vyanzo vya ajali barabarani;
iv.Kufuatilia utekelezaji wa Sheria na Kanuni za ujenzi wa barabara;
v.Kutayarisha bajeti ya mwaka ya ujenzi na matengenezo ya barabara na madaraja;
vi.Kusimamia na kuratibu kazi za barabara na madaraja zinazotolewa na Makandarasi; na
vii.Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/Sita waliofuzu mafunzo ya Shahada/ Stashahada ya Juu katika fani ya Uhandisi Ujenzi waliojiimarisha katika Miundombinu na Uimara wa Majengo (Bachelor of Science in Civil Engeneering - Structural) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na wawe wamesajiliwa na Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB).
MHANDISI II UJENZI (STRUCTURAL)