i. Atafanya kazi chini ya uangalizi wa Mhandisi aliyesajiliwa na Bodi ya Usajili ya Wahandisi (Professional Engineer) ili kupata uzoefu unaotakiwa;
ii.Kufanya kazi kwa vitendo katika fani ya umeme ili kumuwezesha kupata sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi;
iii.Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu vifaa vya umeme na mitambo mbalimbali ndani na nje ya nchi;
iv.Kupitia mapendekezo ya miradi (project proposals) mbalimbali ya ufundi na umeme yanayowasilishwa Wizarani; na
v.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/ Stashahada ya Juu katika fani ya Uhandisi Umeme (Bachelor of Science in Electrical Engeneering) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na wawe wamesajiliwa na Bodi ya Usajili ya Wahandisi(ERB)
TGS.E