From: 2023-07-11 to: 2023-07-18
( )
MHAIDROLOJIA DARAJA LA II – (HYDROLOGIST II) - 16 POST
MDAs & LGAs
Duties & Responsibilities

i.Kusimamia ujenzi na ukarabati wa vituo vya hali ya hewa na vituo vya upimaji wa wingi wa maji kwenye mito, mabwawa na maziwa;

ii.Kufanya uhakiki wa takwimu (validation activities) wakati wa kuchakata takwimu;

iii.Kuandaa mipango na michoro mingine ya mtandao wa uchunguzi (observation networks) wa kihaidrolojia na kimetorolojia;

iv.Kuandaa mipango, kusanifu, kusimamia shughuli za ujenzi katika vituo vya uchunguzi (observation networks);

v.Kusimamia uchunguzi wa kihaidrolojia wa uhusiano kati ya kina cha maji na wingi wa maji (stage - discharge observations);

vi.Kutengeneza ramani za vidaka maji katika mabonde ya Maji kwa kutumia njia ya Geographical Information System (GIS);

vii.Kuandaa ramani zinazoonyesha maeneo yanayoathiriwa na mafuriko katika mabonde na kushiriki katika kutoa ushauri juu ya tahadhari;

viii.Kuhakiki ubora wa takwimu zote za kihaidrolojia na kimeteorolojia;

ix.Kuratibu na kufanya uchunguzi wa awali wa shughuli zinazohusu vituo vya kihaidrolojia; na

x.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

Qualifications

Awe na Elimu ya Kidato cha nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliyefuzu mafunzo ya Shahada ya kwanza ya Haidrolojia au Uhandisi wa Rasilimali maji kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

 

Remuneration

TGS E1