From: 2023-07-11 to: 2023-07-18
( )
MHAIDROJIOLOJIA DARAJA II (HYDROGEOLOGIST II) - 11 POST
MDAs & LGAs
Duties & Responsibilities

i.Kufanya na kusimamia utafiti wa maji chini ya ardhi wenye lengo la kubaini kiasi na ubora wa maji yaliyoko chini ya ardhi;

 

 

ii.Kufanya kazi za kihaidrojiolojia zinazohusiana na usalama wa mabwawa;

iii.Kukagua mitambo na vifaa vya makampuni yanayohitaji leseni za utafiti wa maji chini ya ardhi;

iv.Kukusanya, kuchambua na kuchakata takwimu na taarifa mbalimbali za kihaidrojiolojia kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ya Sekta ya Maji;

v.Kufanya matengenezo madogo ya vifaa vya utafiti wa maji chini ya ardhi;

vi.Kukusanya, kuchambua na kuchakata takwimu na taarifa mbalimbali za kihaidrojiolojia kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ya Sekta ya Maji;

vii.Kuratibu na kusimamia utafiti wa maji chini ya ardhi na kutoa ushauri unaohitajika na wataalam wa kada na fani zingine za Sekta ya Maji;

viii.Kuratibu na kusimamia uchimbaji wa visima na kuhakiki taarifa za kukamilika kwa uchimbaji;

ix.Kufanya usanifu wa ujenzi wa kisima (Design of well development); na

x.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

Qualifications

Awe na Elimu ya Kidato cha nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliyefuzu mafunzo ya Shahada ya kwanza ya Haidrojiolojia, Jiolojia, Uhandisi Jiolojia au Jiofizikia kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

 

Remuneration

TGS E1