Kushiriki katika maandalizi ya Mipngo na Bajeti ya Programu ili kuhaikisha Malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa;
ii.Kusimamia utengaji wa bajeti kwa fedha za Programu kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli na afua mbalimbali za Programu na kusimamia utekelezaji wa afua hizo;
iii.Kusimamia Rasilimali watu, Magari na Vifaa vya Programu, kwa kushirikiana na Timu ya Usimamizi wa Programu, ili kuhakikisha mafanikio yaliyokusudiwa yanafikiwa;
iv.Kushiriki katika ufuatiliaji na tathmini wa Programu ili kupima ufanisi na maendeleo ya utekelezaji wa shughuli na afua mbalimbali za Programu, kubaini changamoto na kuzipatia ufumbuzi ili programu iendelee kutekelezwa kwa ufanisi uliokusudiwa;
v.Kushirikiana na Timu ya Usimamizi wa Programu, kuhakikisha Programu inatekelezwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali, Taasisi na Miongozo inayosimamia utekelezaji wa Programu husuika;
vi.Kufuatiia na kusimamia ukusanyaji, uchakataji na uchambuzi wa taarifa za utekekezaji wa shughuli za Programu za mwezi, robo Mwaka na Mwaka na kuziwasilisha kwenye Timu ya Usimamizi wa Programu;
vii.Kuimarisha mawasiliano kati ya Taasisi na Wadau mbalimbali wa Programu, ikijumusha watumishi, Wahisani na Wadau wengine wa Programu;
viii.Kuhakikisha kuwa taarifa mbalimbali za Programu zinarekodiwa na kutunzwa vizuri na kwa usahihi, ikiwa ni pamoja na kuratibu utoaji wa machapisho ya programu;
ix.Kuratibu shughuli za ufuatiliji zitakazofanywa na Mdau Benki ya Dunia (World Bank Mission activities), na kuhakikisha kuwa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na Mdau wakati wa ufuatiliaji huo yanafanyiwa kazi kwa wakati; na
x.Kufanya kazi nyingine zozote za fani yake atakazoagizwa na kupangiwa na Mkuu wake.
2.5 NGAZI YA MSHAHARA: Kulingana na viwango vya Mradi.
3.0 MHASIBU- NAFASI 1
3.1 SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Shahada ya Kwanza ya Uhasibu, CPA na uzoefu kazini wa angalau Miaka 3. Shahada ya Uzamili ya Uhasibu itakuwa sifa ya ziada.
3.2 MAJUKUMU YA KAZI
i.Kushiriki katika utayarishaji wa bajeti ya Programu na kufanya ufuatiliaji na kusimamia mapato na matumizi ya fedha za Programu kwa kuzingatia Mpango na bajeti iliyoidhinishwa;
ii.Kutayarisha taarifa za kifedha na kibenki za kila mwezi, robo mwaka na mwaka za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Programu, na kuziwasilisha kwenye Timu ya Usimamizi wa Programu;
iii.Kufuatiia kwa ukaribu matumizi ya fedha za Programu na kuhakikisha kuwa matumizi hayo yanazingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia matumizi ya fedha za umma, miongozo ya Programu na Mpango na bajeti iliyoidhinishwa kwa mwaka wa fedha husika;
iv.Kutayarisha taarifa za hali ya kifedha (financial statements) za programu na kuziandaa kwa ajili ya ukaguzi wa ndani na nje ya taasisi kwa kuzingatia Miongozo ya Serikali na Programu;
v.Kuchambua taarifa za kifedha za Programu kwa lengo la kubaini changamoto za utekelezaji na kuishauri Timu ya Usimamizi wa Programu namna ya kutatua changamoto hizo;
vi.Kutoa ushauri kwenye Timu ya Usimamizi wa Programu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu udhibiti na usimamizi wa fedha za Programu ili kuongeza ufanisi wa usimamizi wa fedha hizo; na
vii.Kufanya kazi nyingine zozote za fani yake atakazoagizwa na kupangiwa na Mkuu wake.
Mwombaji awe na Shahada ya Uongozi wa Huduma za Afya (Health Services Administration) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali pamoja na Shahada ya Uzamili ya katika moja ya fani ya Mfumo wa Taarifa za Uendeshaji wa Huduma za Afya (Health System Management) au Ufuatiliaji na Tathmini katika Sekta ya Afya (Health Monitoring and Evaluation) na awe na uzoefu kazini wa angalau miaka mitatu. Mwombaji aliyefanya kazi kwenye Miradi/Programu, itakuwa sifa ya ziada.
Kulingana na viwango vya Mradi