From: 2023-04-21 to: 2023-05-04
( )
KATIBU MSAIDIZI WA BUNGE DARAJA LA II (USIMAMIZI WA MAZINGIRA) - 1 POST
Parliament of Tanzania
Duties & Responsibilities

i)Kuandaa na kuratibu vikao vya shughuli za Kamati na Mikutano ya Bunge;

ii)Kuandaa mihtasari ya vikao vya Kamati na Mikutano ya Bunge;

iii)Kuhakikisha wadau wanaohusika na shughuli za Kamati na Bunge wanapata ratiba kwa wakati;

iv)Kuainisha na kushauri kuhusu maeneo yanayohitaji utafiti zaidi katika masuala yanayoshughulikiwa na Kamati;

v)Kuainisha masuala yanayohitaji kutungiwa sheria au kufanyiwa marekebisho ya sheria;

vi)Kupokea na kuhariri maswali ya Wabunge; 

vii)Kuandaa na kusimamia usambazaji wa Orodha ya Shughuli za kila siku za Bunge kwa Wabunge na Wadau wakati wa Mikutano ya Bunge;

viii)Kuandaa na kuwasilisha Serikalini Orodha ya Maswali yatakayoulizwa Bungeni; na

ix)Kutekeleza majukumu mengine ya kiofisi atakayopangiwa na Msimamizi wake wa Kazi.

Qualifications

Mwombaji awe na Shahada kutoka Chuo Kikuu au Taasisi ya Elimu ya Juu inayotambuliwa na Serikali katika fani ya Usimamizi wa Mazingira (Environmental Management).

 

Remuneration

PSS D.