(i)Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida;
(ii)Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa;
(iii)Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika;
(iv)Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini;
(v)Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa Wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na Wasaidizi hao;
(vi)Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maafisa wali katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika; na
(vii)Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
Mwombaji awe amehitimu Kidato cha Nne na kuhudhuria Mafunzo ya Uhazili na Kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Awe amefaulu somo la Hati Mkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na awe amepata mafunzo ya Kompyuta kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
PSS B