i.Kufanya ukaguzi wa ubora wa magari ya Serikali na kurekebisha ipasavyo;
ii.Kufanya upimaji wa Mitambo na Umeme kufuatana na maelekezo ya Mhandisi;
iii.Kufanya matengenezo ya mifumo ya umeme;
iv.Kufanya kazi za kutengeneza mitambo,magari na vifaa vya umeme; na
v.Kufanya usanifu wa miradi midogo midogo ya umeme (kusimamia jinsi ya kufunga mashine mpya zinazowekwa kwenye karakana za Ufundi na Umeme.
i.Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani ya Umeme
ii.Waliohitimu kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi wa miaka miwili kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za Umeme.
iii.Wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Hatua ya I katika mojawapo ya fani za Umeme kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali,
iv.Wenye Stashahada ya kawaida katika mojawapo ya fani za Umeme kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
TGS.C