i) Kusaidia kuandika na kukusanya ripoti za utafiti wa Kibunge;
ii) Kukusanya, kurekodi na kuchanganua takwimu za kazi za utafiti zinazoendelea;
iii) Kuhudhuria Mikutano ya Kanda ya kuhuisha programu za utafiti;
iv) Kutoa ripoti ya maendeleo ya utafiti na mapendekezo ya utafiti katika mikutano ya kanda ya kuihuisha programu za utafiti;
v) Kufanya shughuli za utafiti chini ya maelekezo na uangalizi wa Afisa Utafiti Mwandamizi;
vi) Kuandaa ripoti za Miradi ya utafiti kwa ajili ya kupitishwa na Afisa Utafiti Mwandamizi; na
vii) Kufanya kazi nyingine ya kiofisi atakayopangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
Mwombaji awe na Shahada ya Kilimo/Uchumi Kilimo/Uhandisi Kilimo (B.Sc. (Agric)/B.Sc (Agric.Economics and Agribusiness), au sifa inayolingana na hizo kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
PSS D.