i) Kuandikisha na kudhibiti Amana (Securities) za Serikali;
ii) Kufuatilia hati za hisa;
iii) Kuwasiliana na watoaji mikopo/misaada kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa Miradi;
iv) Kuweka kumbukumbu za madeni ya nje;
v) Kuweka kumbukumbu za mikopo ya ndani;
vi) Kufuatilia na kusimamia matayarisho ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali;
vii) Kufuatilia utayarishaji na uchambuzi wa “Flash Reports” za kila mwezi; na
viii) Kutekeleza majukumu mengine ya kiofisi atakayopangiwa na Msimamizi wake wa Kazi.
Mwombaji awe na Shahada ya Sanaa yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya Uchumi na Mipango (Major in Economics) au Biashara au Uhasibu au Stashahada ya Juu ya Usimamizi wa Kodi kutoka Chuo/Taasisi inayotambuliwa na Serikali.
Waombaji wenye Cheti cha Taaluma ya Uhasibu CPA (T) au sifa nyingine inayolingana na hiyo inayotambuliwa na NBAA watafikiriwa kwanza.
PSS D