From: 2023-07-11 to: 2023-07-18
( )
AFISA UGAVI DARAJA LA II (SUPPLIES OFFICER II). - 15 POST
MDAs & LGAs
Duties & Responsibilities

i. Kutayarisha makisio ya vifaa vinavyohitajika (Schedule of Requirements);

ii. Kuandaa utaratibu wa upokeaji wa vifaa;

iii. Kuandaa na kutunza takwimu za upokeaji, utunzaji na usambazaji wa vifaa;

iv. Kusimamia upokeaji, usambazaji na utunzaji wa vifaa (Phisical Distribution);

v. Kubuni mfumo wa uwekaji na utunzaji wa vifaa ghalani (Location Index Design);

vi. Kuandaa taarifa mbali mbali za vifaa;

vii. Kuhesabu na kutoa taarifa ya thamani ya vifaa vilivyomo ghalani kwa kufuata taratibu zilizopo;

viii. Kuandaa hati za kupokea vifaa

ix. Kutoa vifaa kwa watumiaji (Distribute goods to user Department and other users; na

xi.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

 

Qualifications

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza/Stashahada ya Juu ya Ununuzi au Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali au wenye "Professional level III" inayotolewa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini (Procurement and Supplies Professionals and Technicians Board - (PSPTB); au sifa nyingine inayotambuliwa na PSPTB na awe aliyesajiliwa na PSPTB kama "Graduate Procurement and Supplies Professional".

Remuneration

TGS.D