Kuandaa Mpango Kazi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Programu kwa ili kupima maendeleo ya utekelezaji na athari za Programu ikijumuisha viashiria vya programu pamoja na mbinu mbalimbali zitakazotumika katika kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali za Programu;
ii.Kushiriki katika ukusanyaji wa takwimu na taarifa za programu zitokanazo na utekelezaji wa shughuli na matokeo ya Programu kwa kutumia njia mbalimbali kama vile utafiti, mahojiano na Mahojiano ya vikundi;
iii.Kushirikiana na Timu ya Usimamizi wa Programu, kwenye ufuatiliaji wa karibu wa utekelezaji wa shughuli zote za Programu, ili kuweza kupima ufanisi wa viashiria na vigezo vilivyowekwa na programu;
iv.Kushirikiana na Wadau wengine wa Programu katika kufanya tathmini ya athari ya Programu kwa wanufaika na Jamii kwa ujumla kwa kupima ufanisi wa viashiria vilivyowekwa;
v.Kusimamia utunzaji wa mifumo ya ukusanyaji na utumiaji wa takwimu za Programu kwa kuzingatia usahihi, usalama na upatikanaji wa takwimu husika;
vi.Kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Programu za mwezi, robo mwaka na mwaka na kuziwasilisha kwa Wadau wa Programu ikijumuisha Timu ya Usimaizi wa Programu, Wahisani na Wadau wengine, kwa kufuata utaratibu wa utoaji wa taarifa wa Taasisi;
vii.Kubainisha vihatarishi (Risk Identification) vinavyoweza kuzorotesha utekelezaji wa Programu na kufikiwa kwa malengo yaliyowekwa, ikiwa ni pamoja ana kupendekeza mbinu za kudhibiti/kuzuia kutokea kwa viashiria hivyo;
viii.Kuwajengea uwezo Timu ya Usimamizi wa Programu pamoja na Wadau wengine juu ya mbinu na kanuni mbalimbali za Ufuatiliaji na Tathmini ya Programu;
ix.Kuhahikisha kuwa programu inazingatia viwango, vigezo na maadili ya taaluma ya ufuatiliaji na tathmini ya Serikali na Benki ya Dunia kama vilivyoainishwa kwenye Miongozo ya Programu na Miongozo mingine ya Serikali;
x.Kuhakikisha bajeti ya utekelezaji wa shughuli za Ufuatiliaji na Tathmini inatengwa, kwa kushirikiana na Timu ya Usimamizi wa Programu;
xi.Kubuni mbinu za teknolojia mbalimbali ambazo zitarahisisha shughuli za ufuatiliaji na tathmini na ukusanyaji wa takwimu za Programu; na
xii.Kufanya kazi nyingine zozote za fani yake atakazoagizwa na kupangiwa na Mkuu wake.
Awe na Shahada ya Kwanza ya Ufuatiliaji na Tathimini (Monitoring and Evaluation) au Menejimenti ya Miradi (Project Management) na Shahada ya Uzamili ya Ufuatiliaji na Tathmini na awe na uzoefu kazini wa angalau miaka Mitatu. Mwombaji aliyewahi, kufanya kazi ya ufuatiliaji na tathmini wa miradi au program, itakuwa ni sifa ya ziada.
Kulingana na viwango vya Mradi