From: 2022-03-31 to: 2022-04-13
(FARMING AND AGRIBUSINESS )
AFISA MIFUGO II - 2 POST
Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Duties & Responsibilities

i.Kuratibu mipango ya uzalishaji mifugo wilayani;

ii.Kuratibu uzalishaji wa mifugo katika mashamba makubwa ya mifugo;

iii.Kusaidia kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani;

iv.Kuratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji bora, usindikaji wa mazao ya mifugo kwa wataalam wa mifugo na wafugaji;

v.Kufanya mapitio na marekebisho ya miundo ya masoko ya mifugo wilayani kwake na mkoani;

vi.Kubuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani;

vii.Kufanya soroveya ya rasilimali (resource survey) kama vile mifugo, vyakula vya mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi;

viii.Kuendesha mafunzo kwa Mawakala, wauzaji na wataalam juu ya njia salama katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo;

ix.Kutafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali ;

x.Kufanya utafiti juu ya uharibifu wa mazingira katika wilaya;

xi.Kushiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa malisho;

xii.Kuandaa taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo;

xiii.Kufuatilia, kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo;

xiv.Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na fani yake kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.

 

Qualifications

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Mifugo (Animal Science) kutoka Chuo  Kikuu kinachotambuliwa na Serikali au sifa inayolingana nayo.

Remuneration

TGS D