From: 2023-09-04 to: 2023-09-11
( )
AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA LA II... - 2 POST
MDAs & LGAs
Duties & Responsibilities

i. Kuwezesha jamii kushiriki katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kusimamia na kutathmini mipango/miradi ya maendeleo; 

ii.Kutoa na kuwezesha upatikanaji wa mafunzo kwa viongozi wa Kijiji/mtaa na vikundi mbalimbali vya maendeleo kijijini/mtaa kuhusu utawala bora na uongozi, ujasiriamali. mbinu shirikishi jamii na kazi za kujitegemea; 

iii.Kuwa kiungo kati ya wananchi, viongozi na watumishi wengine wa Serikali katika kutekeleza shughuli za maendeleo; 

iv.Kuwawezesha wananchi kupanga na kutekeleza kazi za kujitegemea katika ngazi ya Kijiji/mtaa; 

v.Kuandaa na kutoa taarifa za kazi za maendeleo ya jamii kila mwezi kwa uongozi wa kijiji na kwa Msimamizi wake wa kazi; 

vi.Kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na vya kimaendeleo; 

vii.Kutambua na kuwezesha kaya masikini kuinua uchumi wao kupitia fursa na rasilimali zinazowazunguka; 

viii.Kuwezesha utekelezaji wa afua za kuzuia ukatili wa jinsia; 

ix.Kuwezesha utekelezaji wa program za uwezeshaji wanawake; 

x.Kuwezesha program za haki na malezi katika ngazi ya familia; 

xi.Kuwezesha utekelezaji wa afua za kuzuia ukatili wa jinsia; na 

xii.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi. 

Qualifications

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au kidato cha sita, wenye Stashahada (Diploma) katika moja ya fani zifuatazo:- Maendeleo ya Jamii (Community Development), sayansi ya Jamii (Sociology), masomo ya Maendeleo (Development Studies), Mipango na Usimamizi wa Miradi (Project Planning and Management), Jinsia na Maendeleo (Gender and Development), Rural Development kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

Remuneration

TGS.C