i. Kushirikisha jamii katika kubuni na kupanga miradi mbalimbali katika kata wanazofanyia kazi;
ii. Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango/miradi ya Mendeleo katika kata zao, kwa kushirikiana na Katibu Kata na Maafisa Maendeleo ya Jamii Wasaidizi.
iii. Kufanya utafiti na kutoka mapendekezo ya namna ya kukabiliana na matatizo mbalimbali ya maendeleo yanayorudisha nyuma maendeleo ya jamii kwa kushirikiana na watumishi wa sekta nyingine;
iv. Kuongoza na kusimamia utendaji kazi wa Maafisa Maendeleo ya Jamii Wasaidizi walioko katika vijiji/kata
v. Kuelimisha viongozi wa Serikali za vijiji, viongozi wa dini na viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu Sera mbalimbali za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto;
vi. Kuwawezesha na kushirikiana na wananchi na Maafisa Watendaji wa Kata; kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili kwa kuzingatia shughuli za sekta mbalimbali;
vii. Kuwawezesha viongozi wa viiji/kata kutengeneza ratiba za utekelezaji wa mipango/miradi;
viii. Kukusanya, kutunza, kutafsiri na kusambaza takwimu na kumbukumbu mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya jamii;
ix. Kusimamia na kuratibu shughuli za Maendeleo ya Wanawake, Watoto na Jinsia katika Kata;
x. Kuhamasisha wananchi kupambana na UKIMWI;
xi. Kuhimiza, kujenga na kuimarisha ari ya kufanya kazi za kujitegemea katika Kata
xii. Kutayarisha safari za kubadilishana uzoefu (exchange visits) kwa viongozi wa ngazi mbalimbali katika Kata au Wilaya na wananchi, ili kujifunza maendeleo ya sehemu zingine;
xiii. Kueneza Elimu ya Uraia mwema;
xiv. Kuhamasisha wananchi dhidi ya mila potofu kwa afya za wananchi na hasa wanawake na watoto wa kike; na
xv. Kueneza elimu ya Idadi ya watu na maisha ya familia.
Kuajiriwa wenye moja ya sifa zifuatazo:
§ Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au Kidato cha VI, wenye Stashahada ya Juu ya Maendeleo ya Jamii kutoka Chuo cha Mendeleo ya Jamii, Tangeru, au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
§ Kuajiriwa wahitimu wa Shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, SUA, au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya:
Maendeleo ya Jamii (Community Development), Elimu Jamii (Sociology), Maarifa ya Nyumbani (Home Economics), Maendeleo Vijijini (Rural Development), Mipango ya Maendeleo Vijijini (Rural Development Planning), Maendeleo ya Mazingira (Environment and Development), Uchumi na Maendeleo (Development Economics) au Maendeleo ya Jinsia (Gender in Development).
TGS D